Friday, September 30, 2016

TUMALIZE MWEZI HUU WA TISA NA BURUDANI YA NGOMA YA ASILI YA MGANDA KUTOKA LUDEWA


Wiki, mwezi ndo unaisha  sasa hivi utastukia mwaka pia umeisha. Nahisi wote mwezi huu unaisha mkiwa na afaya njema. Binafsi nipo salama...Haya tuendelee na hiyo ngoma stepu yako wee moja mbili tatu....usisahau mkia na kipenenga.... mwisho wa juma pia mwezi uwe mwenye amani na upendo...Kapulya

Thursday, September 29, 2016

SEHEMU FULANI AFRIKA/TANZANIA ....JE? UNAJUA NI WAPI?

Kuna sehemu  katika nchi yetu ukipita huwezi kupita tu unatamani ushinde hapo  angalao tu kwa masaaa kadhaa...Je? wajua hapa ni wapi ?:-)

Tuesday, September 27, 2016

UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU!!!

Sio wakati wote mtu mwenye furaha huwa mwema. Lakini kila wakati, mtu mwema mara zote huwa na furaha.
Kila la kheri. UPENDO DAIMA!

Monday, September 26, 2016

WIKI HII TUANZE NA MAPISHI AMBAYO WENGI TUMEPIKA NA KUKULIA....NIMEKUMBUKA SANA MAPISHI HAYA YA KUTUMIA MAFIGA MATATU...

Kwenye chungu ni makande, wakati ukisubiri makande yaive  basi ni mtindo mmoja tu kuchoma mahindi....Na ujuavyo chakula cha kupikia  kwenye chungu kinavyokuwakitamu.....

Saturday, September 24, 2016

JUMAMOSI NJEMA ....KARIBUNI CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA...............!!

Nimeukumbuka LUNDO -NYASA kwetu kule Mbamba bay ugali wa muhogo na dagaa  na ukikosa dagaa samaki ....mmmhhhh naweza kusema ndicho chakula nikipendachona kilichonikuza....
JUMAMOSI NJEMA.

Thursday, September 22, 2016

SWALI... UNADHANI HUYO KWENYE PICHA NI NANI NA YUPO WAPI?


TUTAONANA TENA MAJALIWA NA KAMA BASI NIWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...



Tuesday, September 20, 2016

PALE MTU UNAPOPATA ZAWADI AMBAZO NI MAALUMU NA NI AMBAZO ZIMETENGENEZWA KWA UMAKINI

 ZAWADI HII NILIPATA MWAKA JUZI TOKA KWA KAKA MASAWE...
NA JUZI TU NIMEPATA HII KWA KAKA MDOGO BATHOLOMEW  TOKA UMASAINI:-) Ni furaha ilioje kupata zawadi hizi. Hii ya pili imetengenezwa na mikono ya mama yake Batholomew mwenyewe. Vitu vya kitamaduni safi sana...Ahsante mama.

Monday, September 19, 2016

TUANZE JUMATATU HII NA PICHA HII..KWELI HUU NI UUNGWANA?

Hebu angalia huyo mama, yaani sasa badala ya kubeba mtoto mgongoni  amebeba kuni na mtoto tumboni. Halafu huo mzigo wa kuni ni bonge la mzigo na ukiangalia kwa pembeni kabania na mboga majani ....Ila mimi nina swali kwa nini asingebeba hizo kuni kichawani ?Na hapo nadhani akifika nyumbani ni kwenda kuteka maji au kutwanga pia. Hakika hapa ndio pale tunapotakia kuwa na usawa....tujadili pamoja

Sunday, September 18, 2016

SALA YANGU YA JUMAPILI YA LEO...TUSALI KWA PAMOJA...

Ee Mwenyezi Mungu, mikononi mwako niguse kama ulivyo waguse vipofu wakaona. Bariki familia yangu,  nyumba yetu, rafiki zangu, kazi yangu. Utupe riziki, wepesi wa maisha ya hapa duniani. Ee Mungu usikie maombi yetu. AMINA. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA!!

Thursday, September 15, 2016

VITU VYA ASILI NI VIZURI SANA ANGALIA HIKI KITANDA...PICHA YA WIKI HII...

Napata raha sana nionapo vitu kama hivi...Kitanda hiki kimetengenezwa kwa miti ya asili angalia mwenyewe..kazi ya mikono ya mtu fulani....
TUPO PAMOJA DAIMA.....KAPULYA

Wednesday, September 14, 2016

LEO TUTEMBELEE KWETU MBINGA... KWA NDUGU ZETU WAMATENGO


Mbinga ,  Ni Wilaya  moja kati  ya wilaya tano za Mkoa wa Ruvuma wa Tanzania Ambayo upande wa kaskazini umepakana na Mkoa wa Njombe, upande wa mashariki na wilaya ya Songea Vijijini na Wilaya ya Songea Mjini, upande wa kusini na Msumbiji na wa magharibi na Ziwa Nyasa

Tuesday, September 13, 2016

CHAGUO LAKO UGALI KWA CHAINIZI NA DAGAA AU MLANDE PORI....

 BONGE LA UGALI KWA DAGAA NA CHAINIZI
 UGALI KWA MLENDA PORI
Hapa ni mtihani kwangu sijui wenzangu kwani hizi mboga zote kwangu ni bonge la kitoweo..kaaazi kwelikweli hapa. Je wewe unachagua mlo upi hapa?

Monday, September 12, 2016

JUMATATU YA LEO TUANZENA UJUMBE HUU...KAMWE USISAHAU HIZO AINA TATU (3) ZA WATU MAISHANI MWAKO

1. Mtu ambaye ame/alikusaidia katika /ulipokuwa na wakati mgumu.

2. Mtu aliyekuacha ukiwa na wakati mgumu.

3. Mtu aliyekuweka katika wakati mgumu.
DAIMA  PAMOJA ....KAPULYA WENU!!



Sunday, September 11, 2016

Saturday, September 10, 2016

MALEZI YA WATOTO YANA CHANGAMOTO ZAKE/ KILA UMRI UNA SHUGHULI ZAKE. MAMA NA KIJANA WAKE!

Nadhani wazazi/walezi wengi wanajua jinsi ilivyo. Watoto wakiwa wadogo umri wa miaka 1 mpaka 5-6 wakati wote ni mama na baba...hasa na mama, na wafikiapo miaka 6-10 marafiki huwa pia na baada ya hapo marafiki huongezeka na ule utegemezi sana wa mama na baba hupungua. Hap nilipata wasaa kuongea na kijana  Erik...maana sio kila siku unaweza ukapata ule muda wa kubadilisha mawazo. Ilikuwa safi sana nadhani mnaweza kuona katika picha maana sura zinasema kila kitu.
JUMAMOSI NJEMA!!

Thursday, September 8, 2016

ELIMU:- WIZARA YA ELIMU MPO...WANAFUNZI WANASOMA KATIKA WAKATI MGUMU NA WALIMU KUFUNDISHA KATIKA MAZING MAZINGIRA MAGUMU...

Hao ni wanafunzi ambao wanasoma katika wakati Mgumu na kwenye mazingira Magumu Je? Wizara ya Elimu inafikiriaje hili swala?. Ni jabu kwa nchi kama Tanzania ambayo ina umri zaidi ya  Miaka 50 sasa wanafunzi kusomea chini ya miti na walimu kufundisha katika mazingira magumu kama hayo.
Je unategemea wanafunzi hao wataelewa? na Je? hii ndio Elimu Bora au Bora Elimu? kama kawaida palipo na wengi pana Majibu au Mjadala haya  Wasomaji wenzangu karibuni tutafakari kwa pamoja na  ikiwezekana tuchukue hatua........Kapulya wenu....PAMOJA DAIMA

Wednesday, September 7, 2016

NJIA NZURI YA KUWEZA KUTAFAKARI PALE UNAPOPUMZIKA NI KWENDA MSTUNI ...KAPULYA WENU HUTUMIA MUDA HUO KUTAFUTA UYOGA NA KUTAFAKARI....

Leo ni siku yagu ya mapumziko, na siku kama hii napendakuitumia kwa kwenda mstuni kutafuta uyoga. Ndiyo natafuta uyoga, lakini la muhimu zaidi kwangu ni  kunyoosha viungo na bila kusahau kuwa mstuni peke yako ingawa hujui kama upo peke yako ni njia moja ya kufikiri mambo mengine katika maisha. Ila pia  kama leo nimepata kitoweo:-)
JIFUNZE KUTAFAKARI KWA KWENDA MSTUNI:-)  KWANI NI SEHEMU TULIVU SANA...

Sunday, September 4, 2016

TUANZE JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TISA NA MLO HUU KARIBUNI TUJUMUIKE ....JUMAPILI NJEMA...

Ni jumapili  ya kwanza ya mwezi wa tisa nami napenda  kuanza na mlo huu....karibuni tujumuike. JUMAPILI NJEMA

Friday, September 2, 2016

UJUMBE WA IJUMAA YA LEO KUTOKA KWA NAMCHUNGA KOMBA AIDS IMALA VANDUGHA KWA LUGHA YA KINGONI IKIWA NA MAANA AIDS INAMALIZA WATU...


Wimbo unasema hivi...Sema haraka tutakutwa na watu maana tupo njian. tembea haraka haraka ni njiani tutakutwa na watu. Fanya haraka haraka tutakutwa. Aids inamaliza watu, wengine wanafuta mali, wengine wanafuata pesa, wengine wanakufa wanaacha watoto, wengine wanakufa wanaacha magofu,wengine wanakufa wanaacha mama, wengine wanakufa wanaacha baba. Wengine wanapata wanakocheza ngoma, wengine wanapata wanakokunywa pombe/komoni, wengine wanapata wanakotafuta kazi, wengine wanapata wanakotafuta samaki. Aids inamaliza watu.

Thursday, September 1, 2016

KUPATWA KWA JUA HUKU MBEYA/REJEWA-TANZANIA......

Hapa ilikuwa kama nne na robo  ilionekana hivi
Na baada ya muda kama saa nne na dakika orobaini na mbili ilionekana hivi. Yaani mwezi ulionekana mdogo sana. Jua limeishiwa nguvu kabisa na kamwezi kanaonekana kwa pembeni kama kifaranga kinatengenezwa

 
Na sasa jua limeanza kujiachia, lilikuwa limeshukwa kabisa. Baada ya hapo ghafla hali ya hewa imebadilika na kuwa na baridi kali sana. Picha zaidi zitakuja maana tukio lasemekana litakamilika saa nane....