Wednesday, October 2, 2013

TUBAKI HAPA TANZANIA.......NA KWINGINE TENA BALI NI MKOANI RUVUMA KWETU!!!


MKOA WA RUVUMA -TANZANIA
MKOA WA RUVUMA:- Ni kati ya mikoa 26 ya nchi yetu Tanzania.
Mkoa wa Ruvuma umepewa jina kutokana na mto RUVUMA ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Mkoa wa Ruvuma unapakana na Ziwa la Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa Mashariki. Kuna mikoa mitano ambayo ni (idadi ya wakazi katika mabano) Songea Mjini (131,336), Songea Vijijini (147924), Tunduru (247,976), Mbinga 404,799), na Namtumbo ni (185,131). Makao makuu ya mkoa ndipo Songea. Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002).
Makabila makuu katika Mkoa huu wa Ruvuma ni Wangoni, Wanyao, Wamatengo, Wandendeule na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri/Seminari kubwa ya Peramiho ya watawa wa Wabenedikto kama wengi mjuavyo.
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ipo katika hali mbaya..
YATAKUJA MENGI KUHUSU MKOA HUU WA RUVUMA WENYE KUVUMA:-)
NA KAPULYA WENGU YUPO KINAMNA  ....MCHANA/JIONI NJEMA KWA WOTE.

6 comments:

ray njau said...

Ruvuma inavuma na itazidi kuvuma kwa kuwa ina wenyewe na wenyewe wa kuivumisha ili izidi kuma ni hawa wafuatao:-
Wangoni, Wanyao, Wamatengo, Wandendeule na Wandengereko.
===================================
Mkoa wa Ruvuma uko kusini mwa Tanzania kati ya latitude 9’35’ na 11°
45°Kusini mwa Ikweta na kati ya longitude 34° na 38’ na 38°10’ Mashariki mwa
mstari wa meridiani. Upande wa kusini Mkoa huu umepakana na nchi ya
Msumbiji, Mashariki unapakana na Mikoa ya Lindi na Mtwara, Kaskazini
unapakana na Mkoa wa Morogoro, Kaskazini Magharibi unapakana na Mkoa
wa Iringa na upande wa magharibi Mkoa huu unapakana na nchi ya Malawi.
Mwinuko wa Ardhi:
Sehemu kubwa ya Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa mashariki ni tambarare
ambayo ipo kwenye mwinuko wa kati ya mita 300 hadi 2000 kutoka usawa wa
bahari.
Hali ya hewa:
Mkoa una joto la wastani wa nyuzi joto 23oC. Joto hili huongezeka hasa mwezi
Oktoba hadi kufikia nyuzi joto 30oC na kupungua wakati wa baridi hasa mwezi
Julai kufikia nyuzi joto 13oC.
Mkoa huu ni kati ya Mikoa michache nchini yenye bahati ya kupata mvua za
kutosha ambazo hunyesha kuanzia mwezi Novemba hadi Mei kila mwaka.
Wastani wa kiasi cha mvua inayonyesha kwa mwaka ni mm.1100. Kiasi cha juu
ni mm.1600 ambacho hupatikana katika Wilaya ya Mbinga kwenye miinuko ya
milima ya Umatengo na kiasi cha chini ni mm.802.8 ambacho hupatikana katika
sehemu kubwa ya wilaya ya Tunduru.
Katika msimu wa 2010/2011 mvua zilianza mwezi Novemba, 2010 kwa maeneo
mengi. Mvua hizo ziliambatana na kuanza kwa kilimo rasmi. Kufikia mwezi
Februari 2011 wastani wa mm 1,062.4 zilikuwa zimenyesha kwa siku 72
ikilinganishwa na mm 633 zilizonyesha kwa siku 50 kipindi kama hicho msimu
wa 2009/2010.
Eneo la Mkoa:
Eneo la Mkoa huu ni kilometa za mraba 64,233 na kati ya hizi, kilometa za
mraba 2,978 (sawa na asilimia 5) zimefunikwa na maji katika ziwa Nyasa,
kilometa za mraba 6,958 sawa na asilimia 11, ni eneo la Hifadhi ya misitu ya
Taifa na kilometa za mraba 50,673 ni eneo linalofaa kwa kilimo, sawa na
asilimia 79 ya eneo lote. Aidha, eneo la kilomita za mraba 3,624 ni eneo lisilofaa
kwa kilimo, sawa na asilimia 6 ya eneo lote la Mkoa.
5
Idadi ya watu:
Kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2002 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na watu
1, 117,166 (wanawake 571,619 na wanaume 545,547). Kutokana na maoteo ya
Takwimu za sensa za kitaifa za mwaka 2002 Mkoa wa Ruvuma unakadiriwa
kuwa na watu wapatao 1,375,017 (wanaume 672,692 na wanawake 702,325)
kufikia Desemba 2010.
Utawala:
Mkoa una wilaya tano (5) ambazo ni Tunduru, Songea, Mbinga, Namtumbo na
Nyasa (Wilaya mpya ambayo itaanza rasmi mwaka wa fedha 2011/2012).
Aidha, Mkoa una Halmashauri sita (6) ambazo ni Songea, Tunduru, Mbinga,
Namtumbo, Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Nyasa (Halmashauri
mpya ambayo itaanza rasmi mwaka wa fedha 2011/2012). Idadi ya Tarafa ni
24, Kata 140, Vijiji 476 na Mitaa 98.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ushukuruwe kwa kuipanua Jiografia yangu kwa vile mie niliandika kwa kifupi sana Ahsante sana...Na yeyeto anayejua kuhua Ruvua zaidi KARIBU SANA.-:)

sam mbogo said...

Inaonekana wewe sasa umekumbuka nyumbani? Dada Yasinta pole saniii!! Mkoa wako unakotoka inaonekakana si mchezo haya endelea kutupasha. wangoni bwanaa! acha tu fujo nyingi.kaka s

ray njau said...

Asili ya Jina la Ruvuma
==========================
Jina limetokana na mto Ruvuma ambao umeanzia katika milima ya Matogoro
iliyoko Songea, ambayo kwa kingoni Kuvuma maana yake Kuunguruma yaani
maji yaliyokuwa yana bubujika na kuporomoka kutoka katika chanzo cha Mto
huo, baada ya Waanzilishi wa Utawala wa Kikoloni Wajerumani kushindwa
kutamka Kuvuma wakaita Ruvuma.
Kabla ya kuanzishwa kwa Utawala wa Kikoloni mwaka 1897 eneo zima la Mkoa
lilikuwa limegawanyika katika vi-nchi kulingana na Koo au kabila kama vile
Ngoni Mshope, Ngoni Njeru, Ndonde, Matengo, n.k. baada ya kuimarika kwa
Utawala wa Kikoloni katika eneo la Ungoni na Baada ya Vita vya Maji Maji vya
mwaka 1905 -1907 eneo la Ungoni ambalo lilikuwa linajulikana kama Nchi ya
Undonde lilibadilishwa jina na Wajerumani na kuitwa Songea, jina la kiongozi
maarufu wa kabila la wangoni aliye ongoza Mapambano dhidi ya Wakoloni-
Wajerumani kipindi hicho ikiwa ni wilaya zilizokuwa zinaunda Mkoa wa kusini
yaani Southern Province Makao Makuu yake yakiwa Lindi. Hata baada ya vita
vya kwanza vya dunia Utawala wa Wajerumani kukoma, eneo liliendelea kuwa
chini ya Mkoa wa Lindi ikijumuisha Wilaya tatu yaani Tunduru, Songea na
Mbinga. Baada ya uhuru mwaka 1963 ndipo ulipoanzishwa Mkoa wa Ruvuma.

Kabla ya Uhuru, Mkoa wa Ruvuma ulikuwa ni sehemu ya jimbo la Kusini
ambalo lilijumuisha mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi, hadi mwaka 1963
ulipoanzishwa rasmi na kuwa na wilaya za Songea, Mbinga na Tunduru.
Mwaka 2002 Mkoa ulikuwa na Wilaya nne baada ua kuanzishwa kwa Wilaya
mpya na Namtumbo.
Kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1982 Serikali ya Mkoa ilikuwa katika mfumo
wa Madaraka mikoani ambapo Serikali za Mitaa zilifutwa.
Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo
wa Mkoa RDD (Regional Development Director) na Afisa Tawala wa Mkoa
ambaye alisimamia wakuu wa idara mbalimbali.
Wakati huo shughuli zote za maendeleo ya Mkoa zilikuwa chini ya Afisa
Mipango wa Mkoa ambaye pia alikuwa na Maafisa Mipango wengine chini yake.
Pia kulikua na wakuu wa Idara wengine kama Afisa Utamaduni wa mkoa, Afisa
Kilimo wa Mkoa.
Muundo huu wa madaraka mikoani ulidumu kwa muda wa miaka kumi yaani
mwaka 1972 hadi 1982 ambapo muundo wa serikali za mitaa ulianzishwa na
kuanza kutekelezwa rasmi. Kwa sasa Sekretarieti ya Mkoa inaongozwa na
Mkuu wa Mkoa akisaidiwa na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na mamlaka za
Halmashauri zilizo chini ya Wakurugenzi wakiongozwa na Wakuu wa Wilaya.

ray njau said...

KAMPUNI YA SONGEA NETWORK YAPANIA MAKUBWA KATIKA KILIMO NA ELIMU
KAMPUNI ya Songea Network Centre na Valongo Network Centre za Mkoani Ruvuma zimeazimia kuimarisha kilimo cha Kahawa,ulezi na Jetropa katika Mkoa wa Ruvuma ili kuwakomboa wananchi wa kipato cha chini kwa kilimo hicho.
Kampuni hizo zimetambulishwa jana rasmi mbele ya Serikali ya Mkoa na kutaja malengo yao katika kuendeleza mazao hayo matatu kwa ustawi wa jamii za watanzania ambao zaidi ya asilimia 80 wanategemea kilimo.
Mkurugenzi wa Kampuni hizo Xaveri Kazimoto Komba ameyataja malengo yao kuwa ni kuendeleza elimu katika Mkoa,kuimarisha kilimo cha ulezi,kahawa na Jetropa,kukuza utamaduni na kuimarisha hali ya Mkoa kwa mazingira ili uoto wa asili usitoweke.
Komba alisema katika kuimarisha kilimo cha kahawa Mkoani Ruvuma tayari ameisha unganisha Mkoa na watafiti wa zao hilo toka Ujerumani ambao kwa kutumia teknolojia za kisasa wataliendeleza zao hilo na kuleta uzalishaji wenye tija ili kukuza kipato cha wakulima wa kahawa Mkoani Ruvuma.
Akiongelea hatua zingine za kuboresha uzalishaji wa zao hilo na mazao mengine yaliyo tajwa amesema hapata kuwepo na tatizo la soko kwani utaratibu umeisha andaliwa wa kununua mazao hayo iwapo yatazalishwa kwa kasi na kutunza ubora wake na soko limeandaliwa.
Akitambulisha mradi wa kuboresha elimu Kazimoto amesema tayari wameisha anzisha Sekondari ya St.Sapiensia ambayo ina kidato cha nne sasa na kuchukua wanafunzi wa dini zote wa kike na wa kiume,shule ambayo iko Parokia ya Mjimwema manispaa ya Songea.
Katika hatua nyingine tayari Songea Network Centre imeisha panda miti zaidi ya 500 ya kivuli matunda na mbao kwa hatua ya kulinda na kuboresha mazingira,miti ambayo imepandwa Songea mjini na Kijiji cha Mbinga Mhalule Tarafa ya Muhukuru.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Vestina Nguruse ambaye kwa cheo chake ni mshauri wa mipango Mkoa amesema mradi wa kilimo kinachojali watu unaoanzishwa na Songea Network Centre uwe endelevu kwa kuwa mipango yake ni ukombozi kwa watu wa Ruvuma.
Amesema shida kubwa ni soko kwa mazao ya wakulima na bei zisizo za uhakika ambazo hubadilishwa mara kwa mara kutokana na soko la dunia linavyoendelea lakini kutokana na utafiti wa kina uliofanywa na Songea Network Centre bila wasiwasi suala la soko litadhibitiwa kikamilifu.
Nguruse amefafanua kuwa fursa za kuendeleza mazao haya katika Mkoa zipo za kutosha akataja uwepo wa ardhi safi kwa kilimo cha kahawa,ulezi na Jetropa ni nguvu kazi ya kutosha yaani wakulima uwepo wa Bandari ya Mtwara na ujenzi wa barabara inayoendelea toka Mtwara Mbamba bay pia mito na mabonde yenye maji wakati wote kwa kilimo cha umwagiliaji.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Nguruse aliwaasa viongozi wa mradi kusimamia mradi huo uwe endelevu na utimize azima yake ya kumkomboa mkulima wa Mkoa wa Ruvuma
Wakati huo huo imefahamika kuwa jitihada za kupata soko la uhakika kwa mazao hayo matatu zimeletwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Ahamad Ngemara ambaye amefanya jitihada kubwa kwa suala la masoko nchini Ujerumani.{Chanzo:Thomas Lipuka,Songea}

===============================
Menejimenti za kampuni hizo zinaweza kuwasiliana na Tanzania Exporters Association (www.tanexa.com) kwa mashauriano ya pamoja na usaidizi wenye manufaa kijamii.
===================================

ray njau said...

Kampuni kufundisha wakulima 100,000 shamba darasa

KAMPUNI ya Lutukira Mixed Farm Project yenye makao yake jijini Dar es Salaam imepanga kutoa mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima 100,000 watakaozunguka eneo la mradi wa uwekezaji wa kilimo cha karanga,ufuta na alizeti wilayani Songea.

Mradi huo tayari umepata eneo la ekari 20,000 za kulima mazao ya kibiashara na kujenga kiwanda cha kukamua mafuta ya mbegu. Wakulima watakaofundishwa watalima mazao mbalimbali na kuyauza kwenye kampuni hiyo ambayo itayakamua na kuyaunza nje ya nchi.

Mwenyekiti ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Alhaji Said Kilahama alisema hayo jana jijini hapa alipozungumzia mkakati ya kutekeleza mradi wa kilimo Lutukira Mixed Farm Project.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa katika kipindi cha miaka 10 ijayo kwa njia ya vitendo.

Kilahama alisema kampuni yake itatekeleza mpango huo katika Kijiji cha Lutukira ambako imepata ekari 50,000 za mradi wa kilimo cha kibiashara kwa mazao ya karanga, ufuta na alizeti na kwamba kwa sasa tayari ekari 300 zimelimwa.

“Ndugu waandishi, kampuni yangu kwa ushirikiano na Kampuni ya Montara Land Limited iliyoandikishwa Seychelles ilianza mradi kwa kutenga Dola 3 milioni za Marekani ili kupata eneo la kilimo cha kibiashara ikiwa ni kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania kuboresha kilimo nchini’’ alisema.

Alisema mradi huo utaajiri wafanyakazi 61 wa kudumu na wengine 100 watakuwa wakiajiriwa wakati wa kipindi maalumu cha kazi nyingi.

Mwenyekiti huyo alipongeza ushirikiano mzuri alioanza kuupata kutoka kwa wananchi wa Lutukira ,viongozi wa Wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla katka kutekeleza mpango huo.

Kuhusu huduma za jamii, Kilahama alisema mradi huo utashirikiana kwa karibu na wananchi ambapo sasa inawapatia trekta wananchi ili walitumie katika kilimo na kwamba pia itashirikiana na Serikali katika kupunguza kero za jamii hususan masuala ya afya, elimu, maji na kuondoa njaa nchini.

Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa kulima mazao ya alizeti na karanga ambayo yatakuwa na soko la uhakika katika kampuni yake.Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ,Said Mwambungu alinukuliwa akiwataka wakazi wa mkoa huo kushirikiana vizuri na wawekezaji.
{Chanzo: Mwananchi}