Thursday, October 31, 2013

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUUFUNGE MWEZI HUU WA KUMI KWA UBUNIFU WA MCHEZO HUU!!!

Napenda kuwatakieni wote mwisho wa mwezi huu wa kumi. Naamini umekuwa mwezi mzuri kwa wengi na kwa wale walikuwa na majukumu kupita kiasi basi nawaombeeni mwezi uanzao kesho uwe mzuri. NAWATAKIENI WOTE MWENZI MPYA WA KUMI NA MOJA UWE MZURI NA WENYE AMANI NA FURAHA. MWAPENDWA WOTE....KAPULYA

Tuesday, October 29, 2013

NIMETAMANI SANA CHAKULA HIKI MIHOGO KWA SAMAKI

Nimetumiwa picha hii na mdogo wangu Sarah Mgaya sasa hivi ni mihogo na samaki ni chakula ambacho nimekula sana nawaza kusema ndicho kilichonikuza. Kama si hivyo basi ugali wa muhogo na samaki...nimetamani mno...ahsante

Monday, October 28, 2013

TUANZA JUMATATU HII NA ENZI HIZOOO JE MNAKUMBUKA???

Binafsi nimekumbuka sana maana ndo nilikuwa kadala/kachiki tu ...Muwe na jumatatu njema wote!!

Sunday, October 27, 2013

NAPENDA KUWATAKIENI DOMINIKA HII YA WATAKATIFU WOTE IWE NJEMA KWA WOTE...

 
Napenda kuwatakieni wote jumapili njema sana na Furaha na upendo zitawale ndani ya  mioyo na nyumba zenu. Ujumbe wa leo:NINAMPENDA  MUNGU NA   NDIO MAANA MOYO WANGU UNAMTUKUZA NA KUMSHANGILA UKISEMA: Ee Bwana na Mungu wangu, Uliye mwanzo na mwisho wangu, Kuanzia sasa najiweka mikononi mwako, unitumie kulingana na mapenzi yako. Kisha unifundishe njia ya kuipanda ngazi ya kufikia. AMINA....KAPULYA
 

Friday, October 25, 2013

IJUMAA YA LEO NA KAZI YA MIKONO YA KAPULYA...KUOKA MIKATE!!

Nimechoka kununua mikata, nikaamua kuoka mwenyewe leo. Halafu ni mitamu zaidi kwa kweli. Ni rahisi sana. Maji lita moja, unga wa ngano lita moja na nusu, chumvi kijiko cha mezani cha chakula, Sukari vijiko 2 vya mezani, mafuta ya kula kikombe kimoja kidogo cha chai(1dl) na hamira pkt moja (50g) au kama ya unga ni vijiko 2 vya chai. Unachanganya vyote na moja kwa moja unakanda unga mpaka unaona umekuwa laini. Unafunika na kitambaaa kizuri kwa dakika 30 ili uumuke. Baadaye unatengeneza utakavyo na kuumua tena dakika 30. Baada ya hapo unapaka maji au maziwa na kuingiza kwenye oven kwa dakika 8-10 na hapo mikate tayari. NAWATAKIENI IJUMAA PIA MWANZO MZURI WA MWISHO WA JUMA HILI. IJUMAA NJEMA!!!

Wednesday, October 23, 2013

JUMATANO YA LEO NIMEAMUA KUTEMBELEA IRINGA-ISMILA!!!

Ismila ni mojawapo wa vivutio vya utalii ambao upo ndani ya mkoa wa IRINGA yetu...karibuni wote kutembelea sehemu hii ya kumbukumbu. JUMATANO  NJEMA KWA WOTE.

Tuesday, October 22, 2013

UJUMBE MZURI KWA WOTE WALIOOA NA WASIOOA NA KUOLEWA PIA WASICHANA NA WANAUME!!

Habari za leo ni matumaini yangu kuwa wote mna afya njema...Nimetumiwa ujumbe huu na msomaji wa Maisha na Mafanikio nikaona si vibaya kuweka hapa ili nanyi wenzangu mfaidike...haya karibu kusoma
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
Very Touching Story....
A poor boy was in love with a rich man’s daughter….One day the boy proposed to her and the girl
said…”Hey! Listen, your monthly salary is my daily hand expenses..
How can I be involved with you..?
How could you have thought of that?
I can never love you, so forget about
me and get engaged to someone else
at your level”
But somehow the boy could not
forget her so easily…..Sometime 10
years later they stumbled into each
other in a shopping mall.
The lady again said….,”Hey.. ! You!
How are you? Now I’m married and
do you know how much my husband’s
salary is..? $15,700 per month! Can
you beat that? And he is also very smart”
The guy’s eyes got wet with tears on
hearing those words from the same
lady….

A few seconds later, her husband
came around but before the lady
could say a word her husband seeing
the guy, said……
“Sir you’re here and you’ve met my
wife..” Then he said to his wife,”This
is my boss, I’m also one of those
working on his $100 million project!
And do you know a fact my dear? My
boss loved a lady but he couldn’t win
her heart….That’s why he has
remained unmarried since.

How lucky would that lady have been,
if she had married this my boss now?
These days, who would love someone
that much?"
He said all these to his wife.
The lady looked in total shock but
couldn’t utter a word….
————— ————— ————— ——-
Life is so short and it’s just like a
mirror.
You can only see as much as it
reflects. So don’t be too arrogant or
proud by looking down on others
because of their current situations.
Things get changed with time just
like the weather..! Don’t under
estimate anyone because everyone
has a great future!
Where you have been rejected before,
you will be celebrated soon in Jesus name.

Shout a big AMEN if U're A believer
God bless you !

Sunday, October 20, 2013

JUMAPILI NJEMA ...ZILIPENDWA!!!

Napenda kuwatakieni wote JUMAPILI NJEMA .....na tukumbukane ....LEO NI JUMAPILI/DOMNIKA YA 29 YA MWAKA C....

Friday, October 18, 2013

IJUMAA YA LEO NA UJUMBE HUU MWANZO WA MAISHA NI MGUMU LAKINI UVUMULIVU NDIO KINGA!!!


Uvumilivu ni Msingi wa maisha ya kila binadamu..Mwanzo ni mgumu...IJIMAA NJEMA KWA KILA ATAKAYEPITA HAPA.....KAPULYA WENU.

Wednesday, October 16, 2013

KAMA MVI NI KIPIMO CHA BUSARA, NI KWA NINI ZIFICHWE??


Mbona Profesa Mbele anazo mvi lakini hazifichi?

Habari zenu wasomaji/wandugu na wengine wote. Ni Jumatano nyingine .Basi mwenzenu nimeamka nikiwa na wazo hili la MVI au niseme nimeota nina mvi kichwa chote. Ndo nikakumbuka kuwa mwaka juzi niliandika makala na nimeona niiweke tena hapa. Kwani mimi naamini mtu unaporudia kusoma aidha kitabu au habari fulani ndipo unapozidi kujifunza haya karibu sana......
Mvi ni dalili ya uzee au ni kitu gani? Kwa zamani ingekuwa ni muhali mkubwa mtu kuuliza swali la aina hii, kwa sababu mvi zinahesabiwa kama dalili ya busara, bila shaka zikihusianishwa na kuona mengi ambayo ni wenye umri mkubwa tu waliokuwa na nafasi hiyo.
Lakini leo, mvi ni kisirani na karibu kila mtu anajaribu kuzikimbia, kwani kuendalea kuwa kijana ni sifa kubwa. Kwa sasa uzee unanuka na kila mmoja anajaribu kuukimbia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kukana umri na kujirudisha nyuma kimatendo. Kwa kifupi hii ndiyo historia ya mvi, usiziogope bure!
Karibu rangi zote asilia za nywele zinatoka kwenye kitu kiitwacho melanin, ambacho huzalishwa na mwili kutokana na seli zinazofahamika kama melenocytes. Nywele zinapobadilika na kuwa nyeupe ina maana kwamba, melenocytes haizalishi tena melanin. Mabadiliko haya ya nywele kutoka rangi nyeusi na kukosa rangi (mvi) siyo hatua ya siku moja bali mwaka na miaka, kwani nywele moja hubadilika baada ya muda mrefu na nyingine na nyingine. Siyo hatua ya siku moja tu.
Kwa kadiri mtu anavyozeeka ndivyo ambavyo uwezo wa mwili kuzalisha melanin unavyopungua. Uwezo huu huanza kupungua mtu anapofikia umri wa miaka 35 au 40. Lakini watu wengine huanza kuota mvi wakiwa na umri wa miaka hata 20 tu. Je, hii nayo inatokana na nini?
Hili kusema kwali siyo jambo la ajabu. Ingawa kuna watu ambao huwa wanalishangaa. hata hivyo wana sayansi wanasema kwamba hawajaweza hasa kujua ni kwa sababu zipi uwezo wa mwili kuzalisha melanin huwa unashuka. Lakini wana uhakika kwamba wale wanaoanza kuota mvi kabla hawajafikisha umri wa miaka 35, kwa sehemu kubwa wanaathiriwa na urithi au kizalia.
Kama mtu ataona kwamba anaanza kupata mvi mapema sana ni dhahiri kwamba akiangalia kwenye familia yao atakuta kuna mtu ambaye naye alianza mapema kuwa na mvi. Hii itasaidia kumuonyesha kwamba mvi zake ni matokeo ya kizalia.
Pengine ni jambo la ajabu kwamba kuvuta sigara kunatajwa kama sababu ya kuchochea mtu kupata mvi akiwa na umri mdogo. Ukiwachunguza wavuta wazuri, utagundua kwamba wameanza kuota mvi mapema kuliko umri wa miaka 35 au 40.
Matatizo kwenye kiungo kinachodhibiti ukuaji mwilini, yaani thyroid huweza pia kusababisha mtu kupata mvi kabla ya kufikisha umri wa miaka 35. Pia ukosefu wa vitamin B12 unatajwa kwa sababu nyingine.
Kuna watu ambao hata kama wana umri wa miaka 60 bado hawataki kuona nywele nyeupe vichwani mwao . Watu hawa huangaika huku na kule kutafuta dawa kuondoa mvi na pengine kutumia rangi ya nywele ili kufanya rangi ya nywele nyeupe zisionekane. Huu ni kama mwendawazimu kwa kiasi fulani. Kwanini?
Kwanza kuna ukweli kwamba nyingi kati ya hizo zinazodaiwa kuwa rangi za kuondoa mvi, zina athari katika mwili wa mtumiaji. Lakini wendewazimu mkubwa zaidi ni kitendo chao cha kukataa ukweli ambao inabidi waujivunie.
Mvi bado ni dalili ya busara. Kama umefikia umri wa kuota mvi na hujafanya jambo lolote la maana na hujatoa mchango wowote wa maana kwa familia yako au jamii unamoishi ni lazima utaficha mvi zako. Kwanini?Kwa sababu utaona haya sana kuonekana kwamba umri wako ni mkubwa lakini hujafanya lolote. Tunaposema mchango wa maana hatuna maana ya fedha au mali, bali zaidi tuna maana ya mawazo ya kujenga na pengine kuandaa misingi ya kujenga kwa nia ya kuleta maendeleo baadaye.
Hebu chunguza kwa makini, utagundua kwamba watu wote wanaojaribu kuficha mvi ni wale watu ambao wametawaliwa sana na vionjo na tamaa ya miili yao kuliko maendeleo ya binadamu. Ni wale watu ambao hata kama wana fedha, hawajajua hasa wako hapa duniani kwa sababu gani. Hivi ndivyo ilivyo kwa sababu watu wa aina hii huhofia sana umri, huhofia sana kufa kwa sababu hawajakamilisha walichokuja kukifanya duniani kwasababu hawajajua bado.
Kukosa kujiamini na kujikubali kwamba wewe ni fulani na uko katika hali fulani na kiwango fulani hupelekea watu wengi kubadili majina, kuchukua makabila yasiyo yao, kujiita maarufu au kuongopa kuhusu maisha yao kwa ujumla. Mtu anayejaribu kuficha mvi ili asijulikane kwamba ana umri mkubwa hana tofauti na watu hawa.
Mtu ambaye anajiamini hawezi kuogopa kutaja umri wala kuonyesha kwamba ana umri mkubwa. Na mtu hawezi kujiamini kama hajijui yeye ni nani na kujijua kunataka mtu asiishi kwa kutazama wengine watamuonaje, bali anajionaje.
Kuficha mvi inaweza kuwa ni dalili ya mtu kuvuka kipindi fulani bila kufanya mambo ambayo kisaikolojia alitakiwa kuyafanya wakati huo. Kama mtu alitakiwa kufanya mambo hayo katika umri wa miaka 20 hadi 25 na hakufanya, kuna kawaida ya mtu kama huyo kuja kutaka kuyafanya akiwa na umri wa juu zaidi.
Kwa kuwa wakati huu mvi ni dalili kwamba ameshapita umri wa kufanya mambo hayo, atahakikisha kwamba dalili hii inafunikwa au kufutwa ili isimfedheheshe. Wengi wetu tunawajua wa waficha mvi na vituko vyao huko mitaani kwetu. Habari hii chanzo ni Jitambue.......Ukitaka kusoma maoni ya mwaka juzi bazi unaweza kuingia KAPULYA. NAWATAKIENI JUMATANO YENYE AMANI NA UPENDO PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA.....KAPULYA

Monday, October 14, 2013

JUMATATU HII TUANZE NA ZILIPENDWA!!!

Je? Kuna unayemtambua katika picha hii. Jumatatu iwe njema kwa wote.

Friday, October 11, 2013

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA MWEMA NA PIA IJUMAA NJEMA SANA!!!

Leo nasema tu Ijumaa iwe njema sana maana ndio mwanzo wa mwisho wa juma hili. Walio na familia basi wajaribu kuwa na familia, na pia ni safi ukawa na rafiki , jirani ni muhimu katika maisha kubadilisha mawazo.

Ujumbe mdogo wa Ijumaa:- Dunia ni kama kitabu, na wale ambao hawasafiri, wanasoma ukurasa mmoja tu.
IJUMAA NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!

Wednesday, October 9, 2013

KARIBUNI UTAANZA MSIMU WA MATUNDA HAYA YA PORI KWA JINA LA MASUKU/MAPOTOPOTO

 

Kama mnakumbuka kuna mada niliwahi kuiweka hapa kwa kuwakumbusha basi gongeni kapulya. Matunda haya ni maarufu sana katika Mkoa wa Ruvuma  nasi huyaita masuku na wangoni wanasema Mapotopoto ni matamu sana. Na kwa kujipatia hela ni rahisi sana masuku kumi ni shilingi 100 kwa hiyo ukiwa nayo mia moja  uongo mbaya...NAWATAKIENI JUMATANO NJEMA SANA WOTE NA PANAPO MAJALIWA TUTAGONGANA TU....



Tuesday, October 8, 2013

HIVI NDIVYO MAPISHI YA NANGONYANI YALIVYOKUWA JANA JIONI SAMAKI WA KIHINDI!!!

 Hapa samaki anaandaliwa, ni samaki wa kihindi inaitwa KHARI MACHLEE  ulikuwa mlo wangu wa jana jioni unaweza kula na wali, ugali na mikate pia.
Na hapa ndo tayari ameiva na tayari kwa kuliwa ni mlo mzuri kwa kweli ...nilipitiwa kwa utamu nikasahau kupiga picha ilivyokuwa kwenye sahani yangu ilivyoonekana...:-) Kapulya

Monday, October 7, 2013

TUANZA JUMATATU HII NA MDADA HUYU:- HUYU NDIYO YASINTA /KAPULYA NAMBA 2...

Leo katika pita pita nimekutana na hii.. nimependa jinsi alivyoandika na alichoandika. Na zaidi ni kwamba huwa napenda sana kumwambia mtu vitu kama hivi wakati yupo hai ..kwa hiyo nachukua nafasi hii na KUMSHUKURU SANA KAKA RAY...Kwa kumsoma zaidi kaka huyu ingia hapa

Yasinta ni mzaliwa wa Lundo -Nyasa Songea mkoani Ruvuma na hatumii soda, pafyumu, wala mafuta makali, haweki dawa nywele zake daima na rasta ndiyo chaguo lake la kudumu. Mazoezi ya kukimbia kila fursa inapojitokeza imefanya awe na muonekano wa ujana hadi wakati huu.
Ni mkarimu, mtulivu, mkali, mwenye upendo, msikivu, mdadisi na hapa nampachika jina la dada wa Maswali magumu na pasua bongo .
Ni mpenzi wa lugha ya nyumbani na ana kipaji cha kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... Kibena… nk. Ukitaka kufikia maisha na mafanikio ni lazima uupende na kuutambua utamaduni wako na kuuheshimu ule wa wengine .
Hana majivunao na hupenda kubadilishana mawazo na watu mbali mbali, na pia anapenda kufuatilia habari za nyumbani kwake alikotoka na haoni haya kuongea lugha yake ya kingoni chenye ladha ya kimanda na kuhanikizwa na ghani ya kindendeule.
Daima anajitambulisha kwa jina la asili ya kwao na huona fahari kutumia jina hilo.
Makazi yake ya sasa ni ughaibuni katika ardhi ya waswidi na hajafunga milango kwa uzao wake kutambua na kuenzi asili ya mama yao ijapokuwa wao ni wazawa wa ughaibuni, amekuwa msitari wa mbele katika malezi ya wanae ili kuhakikisha watoto wako hawajitengi na asili ya alikotoka.
Hana uchoyo katika kutoa mashauri na kupitia makala zake anazotundika kibarazani kwake na anaendelea kutoa usaidizi kwa wengi, amekuwa mstari wa mbele katika kuilemisha jamii bila kujali rika. Anajitolea kufundisha kile akijuacho juu ya malezi na matatizo mbali mbali anayoweka Kibarazani kwake (Maisha na Mafanikio) ambacho ni kitovu chenye kukutanisha wadau mbali mbali wenye fikra pevu, na kuibua mijadala yenye kuelimisha, kufundisha, kuburudisha na kuhuzunisha pia.kabili wanandoa na malezi ya watoto.
Kamwe hafuniki hisia zake kwa blanketi na siku zote anaweka wazi hisia zake kwa mume Wave na kwa jamii yake, lakini yeye ni makini sana ili kuepuka kumuumiza mtu mwingine kihisia, na kama kwa kusema huko kutamkera mtu mwingine, ni mwepesi kuweka sawa maelezo yake ili kuondoa mgongano wa mawazo katika jamii yake.
NAWATAKIENI WOTE JUMATATU NJEMA SANA !!!


Sunday, October 6, 2013

NI JUMAPILI YA MWAKA C:LEO TUTEMBELE KIJIJINI KWETU LITUMBANDYÓSI/PAROKIANI

Kanisa hili nimesali mara nyingi sana ni KANISA LETU LA PAROKIA YA LITUMBANDYÓSI . NAWATAKIENI JUMAPILI NJMA SANA WOTE MTAKAOPITA HAPA.


Thursday, October 3, 2013

ZILIPENDWA...UNAWAFAHAMU WATU HAWA AU UNAJUA HAPA NI WAPI?



Wametulia hapo bila wasiwasi inaonekana ni mahali pazuri na penye utulivu...Haya karibuni kufumbua fumbo la leo....:-) Sijui itakuwa mwaka gani hapa????

Wednesday, October 2, 2013

TUBAKI HAPA TANZANIA.......NA KWINGINE TENA BALI NI MKOANI RUVUMA KWETU!!!


MKOA WA RUVUMA -TANZANIA
MKOA WA RUVUMA:- Ni kati ya mikoa 26 ya nchi yetu Tanzania.
Mkoa wa Ruvuma umepewa jina kutokana na mto RUVUMA ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Mkoa wa Ruvuma unapakana na Ziwa la Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa Mashariki. Kuna mikoa mitano ambayo ni (idadi ya wakazi katika mabano) Songea Mjini (131,336), Songea Vijijini (147924), Tunduru (247,976), Mbinga 404,799), na Namtumbo ni (185,131). Makao makuu ya mkoa ndipo Songea. Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002).
Makabila makuu katika Mkoa huu wa Ruvuma ni Wangoni, Wanyao, Wamatengo, Wandendeule na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri/Seminari kubwa ya Peramiho ya watawa wa Wabenedikto kama wengi mjuavyo.
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ipo katika hali mbaya..
YATAKUJA MENGI KUHUSU MKOA HUU WA RUVUMA WENYE KUVUMA:-)
NA KAPULYA WENGU YUPO KINAMNA  ....MCHANA/JIONI NJEMA KWA WOTE.