Hizi ni nyanya zangu ambazo zilikuwa bado kuiva kama mnavyoona ...nimeamka leo asubuhi nimeshikwa na butwaa nyasi zote zilikuwa nyeupe theruji kabisa kitu ambacho zikutarajia kwa haraka hivi. Kwa hiyo imenibidi kuzivuna kabla hazijaharibika sana na kuzihifadhi. Vipi SIJUI kwa kweli..Je nikizihifadhi kwenye boxi zitaiva? Maana hapa ni nusu ya tulizokula....
Hahahaaa:-) na nikaamua nivune tu na vitunguu vilivyobakia ...mkulima wa ajabu anaanza kula kabla hajavuna na sasa vimebaki sita (6) tu....KARIBUNI KUNISAIDIA KULA NYANYA HIZO!!!
8 comments:
Kaazi kwelikweli,mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotarajiwa yanamlazimisha mkulima kula mbegu na kuuza jembe.
Yasinta kazi ya mikono yako ni nzuri na sana na wala usikate tamaa kwa kuwa kule kusini wanasema:"MADENGO NTIMA."
Mie ntakuja kula kachumbari mana una nyanya hapo na kitunguu, nitengenezee ili nyanya zipungue. Ukiziweka kwenye box zitaiva haraka halafu zote kwa wakati mmoja! ila huna jinsi uzitoe kabla hazijaiva sana sana, ivisha taratibu ukiweza. Haya mkulima Yasinta kila la heri.
tushakaribia dada. We andaa pilau na kachumbari..
Kaka Ray! Nashukuru kwa kunitia moyo...ila "MADENDO NTIMA" hiyo kama nimeelewa.
Usiye na jina! Kachumbali utaishindwa mwenyewe....na ahsante kwa ushauri . Ntaweka baadhi kwanza nione kama zitaiva.
Kaka wa mimi Mrope....karibu sana tena sana....na wala usikonde vyote utapata:-D
Pole KADALA.lakini si haba tumekula mwaka huu..
Wauzie watu wa hoteli na migahawa utapata hela. By Salumu.
Ah ah ah hoteli na migahawa, kibongo bongo! Sijui kama ni rahisi hivyo kwa ulaya, embu dada yetu Yasinta atuambie. Mana walivyo strict na kujua zimelimwaje nk!!!Si unajua mambo ya afya kwa nje wenzetu makini. Ila sijui kwa Sweden, Ujerumani hauzi kirahisi hivyo. siku njema.
KACHIKI..Ahsante alo..Ni kweli ila hata hivyo nasikitika..njoo chukua nawe:-)
Kaka Salumu! :-) Hapa hakuna mambo hayo labda niwape majirani
Usiye na jina! kumbe unaishi Ujerumani mwenzangu..Basi kanuni/sheri ni hizo hizo..Na kwanza kama una kazi nyingine huwezi tu kuanza kuuza kitu bila kuripoti na kupata kibali na mambo mengine mengiiii.
Post a Comment