Kuondokana na hisia za mapenzi dhidi ya mpenzi uliyetokea kumpenda sana lakini mkaachana katika mazingira ambayo hukuyatarajia, si jambo rahisi na hasa kama wewe ndiye uliyeachwa. Unaweza kujiambia kwamba amekosea sana kukuacha na kamwe hatoweza kumpata mwanamke atakayempenda kama ulivyompenda wewe. Lakini kiukweli ndani ya moyo wako unampenda na kitendo cha kukuacha bado kinakuumiza na kukutesa. Inawezekana pia ukawa unatamani sana akurudie kwa sababu ulimpenda sana na unahisi upweke moyoni. Kwa mwanamke aliyeachwa, kuwaza hivyo ni jambo la kawaida kabisa, labda kama hukutokea kumpenda mwanaume huyo. Lakini kama miezi na miaka inapita na bado unaendelea kuwa na mawazo ya aina hiyo, basi hilo litakuwa ni tatizo, na hapa chini nitajaribu kueleza namna ya kuondokana na mawazo ya aina hiyo na kuendelea na maisha, kwani kuachwa na mpenzi sio mwisho wa dunia.
1.Unamuwaza muda wote Hili ni jambo la kawaida, lakini duh, kama unajikuta unamuwaza mpenzi aliyekuacha muda wote na kujikuta unashindwa kufanya mambo yako ya msingi kwa ustawi wa maisha yako, basi hilo ni tatizo ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi. Ingawa waswahili husema “lisilo machoni, halipo moyoni,” lakini mimi nasema sio kila lisilo machoni halipo moyoni, kwa swala la mapenzi nadhani iko hivyo. Ukweli ni kwamba hujui yuko wapi, anafanya nini au yuko na nani na hapo ndipo utakapojikuta ukitafuta picha mlizopiga mkiwa pamoja wakati wa kilele cha mapenzi yenu, na wakati mwingine unaweza kusikia wimbo fulani ambao aliupenda sana ukakukumbusha tukio lililowakuta mkiwa pamoja ambalo linahusiana na wimbo huo. Kwa kifupi ni kwamba, ni jambo la kawaida sana kumkumbuka mpenzi mliyeachana mara kwa mara baada ya kuachana. Lakini kama mawazo hayo yanaonekana kukuumiza na kukupotezea muda basi jua kwamba, jambo hilo linaweza kukuletea matatizo makubwa sana kiafya. Namna gani utaondokana na tatizo hili: Muda ni nyenzo muhimu sana katika kuponya. Kama unashindwa kupata suluhu ya namna ya kuondokana na mawazo ya huyo mpenzi mliyeachana naye, basi jipe muda, kwani kwa kujipa muda zaidi unajipa nafasi ya kuponya majeraha ambayo yanaonekana kukutesa. Kwa jinsi muda unavyochukua nafasi ndivyo unavyomudu kusahau na ndio maana waswahili husema yaliyopita si ndwele tugange yajayo Endelea kusoma zaidi HAPAhttp://kaluse.blogspot.se/2013/07/mwanamke-je-bado-una-hisia-za-kumpenda.html JUMATANO NJEMA SANA WOTE!!!
Wednesday, July 31, 2013
NADHANI MNAKUMBUKA KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO MAREDIO YA MADA, PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI LEO KATIKA PITA PITA ZANGU NIMEKUTANA NA HII...EBU SOMA....
Ndugu zangu kile kipengele cha JUMATANO YA MARUDIO KIMERUDI TENA MIKIKIMIKIKI ILIKUWA MINGI MNO. Haya karibuni na panapo majaliwa tutaonana tena:-) MWANAMKE: JE, BADO UNA HISIA ZA KUMPENDA MPENZI MLIYEACHANA...?
Tuesday, July 30, 2013
BUSTANI:- BUSTANI YANGU IMEINGILIWA NA VIWAVI/BUU WANAKULA FIGIRI YANGU:-)
Kutunza bustani ni kazi kidogo leo nimeamka asubuhi hii na kwenda kuangalia bustani yangu nakutana na wadudu wanakula figiri yangu nimechukia mno tena mna na nimengóa yote na sasa nataka ushauri wenu kwa yeyote anajua jinsi ya kuwaua buu/viwavi maana sijakata tamaa nataka kujaribu tena kupanda figiri nyingine.
Mboga yaa maboga inastawi sa tena vibaya mno yaani mpaka raha hapo nimechuma jana hivyo.....Mchicha nao inatia nanga unapendaza..nitauchuma kesho si mnajua akiba haiozi karibuni tu hapa kutakuwa na baridi kiasi kwamba hata kuchimba shima ni shughuli....
....Sasa hapa ndipo nilipoudhika kwa kweli angalia figiri yangu ilivyoliwa. Nimejaribu kila njia kuwatoa viwavi/buu hawa lakini nimeshindwa. Je kuna anayejua dawa ya kuwatoa hawa wadudu/buu?...kaka Bennet upo nisaidie...nimeudhika sana sana kiasi kwamba-----
Nimengoa figiri yote lakini nipo mbioni kupanda nyingine tena leo hii nitaatika...
Monday, July 29, 2013
JUMATATU YA LEO TUANZE KIHIVI ...ELIMU/KITABU.....
Mwaka huu nilipokuwa nyumbani sikukosa kwenda duka la vitabu Peramiho kununua vitabu na kitabu mojawapo ni hiki ukionacho pichani WANGONI....VITA, HADITHI, METHALI NA VITENDAWILI....Kwa kweli nakipenda sana kwani najifunza mengi.
Sunday, July 28, 2013
JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA WIMBO HUU..JICHO
AU TU NGOJA TUENDELEE NA HUU PIA
JUMAPIULI IWE NJEMA KWA WOTE NA YENYE AMANI NA UPENDO. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. KAPULYA
Saturday, July 27, 2013
JUMAMOSI YA LEO NA UJUMBE/MSEMO HUU!!
Mtu hujifunza kitu/vitu kidogo kidogo, lakini husahau kila siku.
JUMAMOSI NJEMA NDUNDU ZANGU NA UPENDO UTAWALE DAIMA.
JUMAMOSI NJEMA NDUNDU ZANGU NA UPENDO UTAWALE DAIMA.
Friday, July 26, 2013
UTAMADUNI:- LEO TWENDE MPAKA DODOMA NA MZIKI HUU WA ASILI NA HUKWE ZAWOSE NA KIJANA WAKE MSAFIRI ZAWOSE..EBU WASIKILIZE JINSI SAUTI ZAO ZINAVYOFANANA...
NA HAPA NI MSAFIRI ZAWOSE...AKIIMBA MSIMAMO AFRIKA
TUSISAHA UTAMADUNI WETU MAANA HII NDIYO ASILI YETU.....NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA.
Wednesday, July 24, 2013
MAPISHI:- LEO MLO NILIOANDAA NI HUU ANGALIA HAPA CHINI !!!!
Hapa ni mishikaki ya kidali cha kuku ambayo imeandaliwa kwa kuwekwa kwenye mafuta kidogo,soya kidogo, kitunguu saumu,tangawizi na limau. Na baada ya hapo ikatundikwa kama mishkaki kama muonavyo tayari kwa mchomo....
Na hapa ni sahani zitakazotumika kwa vile tutakuwa nje basi vilibebwa vingine pia kwenye sinia hilo. ambavyo ni nyanya, tikiti maji, njegere mbichi kutoka bustanini na zeituni za rangi mbili kijani na nyeusi.
Mishkaki imeweka kwenye moto tayari kwa kuchomwa na dada Kapulya ...bahati mbaya haonekani kwenye picha kwani anakimbia ndani na nje kuangalia wali....
Baada ya dakika kumi mishkaki inaonekana hivi nimechoma dakika tano kila upande..tayari kuliwa ..KARIBUNI TUJUMUIKE....
Na hii ni sahani ya Kapulya mshkaki mmoja, tikiti maji na nyanya pembeni, njegere, wali, na kitamu zaidi MCHICHI KUTOKA BUSTANI YANGU....MMMMMHHH. Hakika kulima raha..si mnaona eeeeh ..KARIBUNI ..ILA NIMEUKOSA UGALI..NITAANDAA KESHO NA MBOGA MABOGA:-)..HAYA MUWA NA JIONI/USIKU AU LABDA MCHANA AU ASUBUHI NJEMA. KAPULYA/KADALA.
Na hapa ni sahani zitakazotumika kwa vile tutakuwa nje basi vilibebwa vingine pia kwenye sinia hilo. ambavyo ni nyanya, tikiti maji, njegere mbichi kutoka bustanini na zeituni za rangi mbili kijani na nyeusi.
Mishkaki imeweka kwenye moto tayari kwa kuchomwa na dada Kapulya ...bahati mbaya haonekani kwenye picha kwani anakimbia ndani na nje kuangalia wali....
Baada ya dakika kumi mishkaki inaonekana hivi nimechoma dakika tano kila upande..tayari kuliwa ..KARIBUNI TUJUMUIKE....
Na hii ni sahani ya Kapulya mshkaki mmoja, tikiti maji na nyanya pembeni, njegere, wali, na kitamu zaidi MCHICHI KUTOKA BUSTANI YANGU....MMMMMHHH. Hakika kulima raha..si mnaona eeeeh ..KARIBUNI ..ILA NIMEUKOSA UGALI..NITAANDAA KESHO NA MBOGA MABOGA:-)..HAYA MUWA NA JIONI/USIKU AU LABDA MCHANA AU ASUBUHI NJEMA. KAPULYA/KADALA.
HITORIA YETU:- HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAPO ZAMANI TANGANYIKA AMBAYO SASA NI TANZANIA....
Ocean Road Hospital Dar-es -Sallam enzi ya wajerumani
Yakobo Lumwe, ambaye pia aliitwa Yakobo Ng'ombe, alikuwa ni Mchungaji (Padri) wa kwanza mwenyeji wa kanisa la kiprotestanti pwani ya kaskazini mwa Tanganyika. Alitumika ndani na katika mzunguko wa maeneo ya Tanga mjini, sehemu ambayo sasa ni ya Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri katika Tanzania. [1] Maisha yake na kazi ni mfano wa kusifu jinsi gani wakristo wananchi walivyojishughulisha katika kueneza Injili na kujenga kanisa pamoja na wageni wamissionari.Kanzu ndio lilikuwa vazi la Padri hadi leo hii kote duniani! Tusisahau historia zetu ...MUWE NA SIKU NJEMA!!
Tuesday, July 23, 2013
SWALI LILILONISUMBUA SIKU YA LEO...!!!!
Nimeamka asubuhi hii na nimemshukuru Mungu kwa kunilinda. Nikaona ngoja ninyooshe viungo:- Yaani nikaende nje kama kawaida yangu kukimbia, nimekimbia, nimekimbia mara nikakutana na mkimbaji mwingine naye kawaza kama mimi anakimbia. Sasa hapa kitu kilichonipa swali ni kwamba mdada huyu alikuwa akikimbia na mbwa wake ambaye amemfunga kamba shingoni. Swali likanijia huyu dada ana uhakika kama huyu mbwa/kambwa anataka kukimbia? Maana niliona kama mbwa mwenyewe hata hakufurahia. Nikataka kusimama na kumuuliza.....lakini nikaacha. Muda wote nilipokuwa nakimbia swali lilizidi kunisumbua hivi kweli yule mbwa alipenda kukimbia? Na pia nikazidi kuwaza....Nikaona niwape na wenzangu haka kakisa....TUSITENGANE TUWA TUNAKUMBUKANA. PAMOJA DAIMA SIKU NJEMA. KAPULYA!!
Monday, July 22, 2013
TUANZA JUMATATU HII KWA KUSIKILIZA NYIMBO HIZI MBILI AMBAZO ZINA UJUMBE UNAFANANA KIDOGO!!!!
Au tuendelee kusikiliza na huu ambao unaitwa HUJAREJEA BY CHIEF BEKA
JUMATATU NJEMA NA KILA LA KHERI..........NA KAPULYA LIKIZO IMEISHA NA SASA MZIGO KAMA KAWAIDA:-(
Saturday, July 20, 2013
SALAMU ZA JUMAMOSI HII KUTOKA KWA NANGONYANI!!!!!
Acheni niwape hai, sina shaka mpo hai, nami pia nipo hai, ndiyo maana nawapeni hai, kwa kuwa sote tupo hai tupeane hai, hai, hai hadi Wilayani. Ilikwa hivi tu kwa JUMAMOSI HII.MNAPENDWA WOTE JUMAMOSI NJEMA.
Thursday, July 18, 2013
KILIMO CHA BUSTANI NA MAUA CHA DADA YASINTA...KARIBUNI !!!!!
Habari zenu..kuna wengi wameniuuliza vipi kuhusu bustani pia mapishi nipi na bustani ipi ila pilikapilika ni nyingi na hizi likizo lakini leo nimeona sio mbaya nichukue muda na kuwaonyesha maendeleo ya bustani yangu...Karibuni
Nyanya zimeanza kukomaa karibu nitakula
Kushoto ni mchicha na kulia ni figiri mnaona ilivyokua
Njegere zimeanza kuchanua
Viazi mviringo(matosani) navyo vimwanza kuchanua
Mdada huyu ni mpenzi wa maua pia mawe hapa mnaona maua yako yanavyoendelea.Kwa kuwa mtundu nikajaribu kupandikiza pilipili pia maana pitiku bila pilipili mmmmhh na matokeo ni haya
Sikuchoka nikajaribu kupandikiza dodoki Nanasi na tangawizi---Dodoki kwenye hicho chombo cha bluu, nanasi chombo cha blauni na tangawizi chombo cheupe. Kwa msingi kwa kweli unaweza kupanda kila kitu na kuvuna. Haya nawatakieni Alhamisi njema na karibuni kula mazao.
Wednesday, July 17, 2013
NIMEUPENDA HUU WIMBO NA LEO NILIKUWA NAWAZA HIVI NA BAHATI NIMEKUTANA NA WIMBO HUU UKIPATA MUDA EBU SIKILIZA ASEMAVYO MUIMBAJI...MANENO MANENO....
Kila siku ninapoamka ninapoinza siku mpya ninamshukuru Mola kwa kunilinda nafasi nyingine nikapewa labda nikijituma kwa siku wataniletea ......haya endelea kusikiliza ujumbe wake..JUMATANO NJEMA SANA.
Tuesday, July 16, 2013
JUMANNE YA LEO TUANGALIE KATON HII...EBU SOMA MWENYEWE.....
USHOGA NI HATARI
Leo na katuni hii tuache umbea jamani hakikisha kwanza hilo jambo ndo ufanye tuacha tabia ya kugombanisha ndoa za watu. Nawatakieni wote mtakaopita hapa JUMANNE NJEMA SANA. NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA.
Monday, July 15, 2013
KWA NINI WANAUME WANASHINDWA KULING'AMUA HILI?
Kuna wakati niliwahi kueleza juu ya wanaume
kudhani kuwa kuwanunulia wake au wapenzi wao kila kitu kwa maana ya nyumba
nzuri, magari ya kifahari na mavazi ya thamani, inatosha kupeleka ujumbe kwa mke
au mpenzi wake kuwa anapendwa. Nilieleza kwa kirefu sana juu ya dhana hiyo jinsi
isivyo sahihi na niliweka bayana kuwa, wanawake ni viumbe wanaohitaji
kusikilizwa kuliko kitu kingine, bila shaka mlio wengi mnakumbuka makala
hiyo.
Kwa asili wanaume wanapenda sana kuwasikia wake au wapenzi wao
wakikiri kuwa wanawapenda na kufurahia tabia zao nzuri wema walio nao, vipaji
walivyo navyo na sifa nyingine lukuki. Wanaume wanapopewa sifa za aina hii na
wake au wapenzi wao hufurahia na kupata nguvu na kuona kwamba wana thamani kubwa
mbele ya wake au wapenzi wao, kinyume na hivyo wanaume hukerwa na kutowajali
wake zao.
Pamoja na kuoneshwa upendo lakini hata hivyo hiyo haitoshi
kuwafanya wanaume wawapende na kuwajali wake au wapenzi wao. Kuna wakati
mwanaume anakuwa na kazi nyingi sana na anatumia muda mwingi kwenye kujisomea au
kuangalia Luninga, hata pale mke au mpenzi wake anaponyesha kwamba anahitaji
kuwa naye kwa muda fulani. Kuna wakati pia mwanaume anajali zaidi kazi zake
kuliko mambo mengine ambayo mkewe anayataka na kuyaona ya maana.
Naamini
wengi mtakuwa ni mashahidi wa kauli hizi, “Yaani niache kazi zangu nikae
kukusikiliza wewe na upuuzi wako, subiri nikipata muda tutaongea mambo hayo”
kauli hizi ni sumu kali sana katika uhusiano, na huchangia kwa kiasi kikubwa
ndoa na mahusiano ya wapenzi wengi kuporomoka.
Ni kweli kuwa kuna wakati
mwanaume anaweza kuwa bize na shughuli zake,lakini pale mke au mpenzi wake
anapohitaji ukaribu na yeye ni wajibu wake kuonesha kujali.
Kama mwanamke
anahitaji kufanya jambo fulani ambalo inabidi mwanaume amsaidie, lakini
inapotokea mwanaume kuonyesha kwamba hajali sana juu ya jambo hilo bila kujali
kama yuko bize au hayuko bize, mwanamke huhisi kutothaminiwa na hiyo humuumiza
sana kihisia. Lakini kama mwanaume ataonesha kujali hisia za mkewe na
kumsikiliza kwa makini hata kama hatatoa ushirikiano hiyo tu inatosha
kumridhisha mke au mpenzi kuhisi kuwa anapendwa na anasikilizwa.
Lakini
utakuta wanaume wengi hawajali utashi wa kihisia wa wake zao na huamini kwamba
wanawake wanachohitaji ni kupewa fedha au mali na kuhakikishiwa maisha ya
kifahari basi.
Ukweli ni kwamba wanawake wanahitaji sana kusikilizwa hisia
zao na kupewa nafasi pekee na mume au mpenzi wake pale anapohitaji nafasi hiyo
ya kusikilizwa. Kumuonesha mwanamke kwamba hana thamani na hana nafasi ya
kusikilizwa na badala yake kazi na kusoma, au kuangalia luninga kukaonekana ndio
kuna thamani kuliko yeye ni kosa kubwa.
Ni jambo la msingi sana kwa
wanaume kulifahamu hili kwa ustawi wa ndoa au mahusiano yao na wake au wapenzi
wao, kwani wanawake wanahitaji nafasi kutoka kwa wanaume au wapenzi wao zaidi ya
kitu kingine, maana hayo mengine yatakuja kujazia tu
Saturday, July 13, 2013
UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO TOKA KWA KAPULYA NI HUU....
Ukimya wa rafiki yako unauma kuliko hata kueleza maadui zako/wako.
JUMAMOSI NJEMA!
JUMAMOSI NJEMA!
Wednesday, July 10, 2013
BAADA YA MASAA MATANO NA HUU NDIO MWANEKANO MPYA WA KAPULYA!!!
Hapa ni kichwa kizima, picha imepigwa kwa juu kuonyesha mwonekano wote...masaa matano nimekaa bila kuinuka na matokeo ndio haya..
Na hapa ni kwa mbele...mnaona kapulya alivyochoka si mchezo lakini nimefurahi nimeweza kusukwa maana zile nilisuka mwezi februari:-)..Dada Natalie kutoka Kongo ni mwepesi ajabu...Sijui hizi nitakaa nazo muda gani:-)
Na hapa ni kwa mbele...mnaona kapulya alivyochoka si mchezo lakini nimefurahi nimeweza kusukwa maana zile nilisuka mwezi februari:-)..Dada Natalie kutoka Kongo ni mwepesi ajabu...Sijui hizi nitakaa nazo muda gani:-)
Haya nawatakieni jioni njema ..Panapo majaliwa tutaonana tena...Kapulya ndani ya poziiii:-)
PICHA ZA WIKI:- KAPULYA NA NYWELE ZAKE!!
Hapa ni ijumaa wakati nasaka msusi...na ghafla jumamosi akanipa taarifa atanisuka kwa hiyo kazi sasa ni kufumua hizo nywele za kimasai...kazi ikaanza jumamosi..
..na jumatatu mzigo umekwisha sasa kazi kuchana eeeh bwana wewe si unaona hapa na afro yangu..leo jumatano ndo naenda kusuka ...nikirudi nitawaonyesha vipi imekuwa...Haya basi baadae:-)Tuesday, July 9, 2013
MATUNDA NA BEI YAKE..KAAAZI KWELIKWELI......
Jana nikawa na hamu kweli ya papai nikaenda dukani kuangalia bei mamaaa weeewewee kama muonavyo hapa 22kr ni sawa na 5000Tsh na kapapai ndo kama ngumi yangu...nikaanza kukumbuka mapapai yangu Ruhuwiko kwangu..nikaondoka na sikununua papai. Maisha haya kaaaaazi kwelikweli..
Monday, July 8, 2013
TUANZE JUMATATU HII KIHIVI...HISTORIA NA MAKUMBUSHO...
Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilikuwa kwenye kasafari kidogo kutafiti historia ya nchi kwa mfano kame hii na sikuishia hapa niliendelea na nikapata kuona haya pia ......
Hapa ni makumbusho ya redio ..si wote tunakumbuka zamani redio ilikuwa ni kitu muhimu sana kulikuwa hakuna njia nyingine kupata habari zaidi ya redio labda na magazeti...Hapa uliweza kutuma telegram na kudhalika ..
Na halafu nikashuhudia jinsi mdada huyu alivyoweza kutumia mikono yake kwa kazi hii ya kutengeneza gilasi kwa njia ya kupuliza. Hakika Mungu amempa kila kiumbe uwezo/kipaji chake. sikuishia hapa ...
...nikaendelea na halafu nikapata kuona hifadhi ya ndege. Kwa muda wa wiki moja nimepata kuona mambo yote haya na nimeona si vibaya kama nikiwajuza na wenzangu. Maana elimu kugawana. Jumatatu njema kwa wote.
Hapa ni makumbusho ya redio ..si wote tunakumbuka zamani redio ilikuwa ni kitu muhimu sana kulikuwa hakuna njia nyingine kupata habari zaidi ya redio labda na magazeti...Hapa uliweza kutuma telegram na kudhalika ..
Na halafu nikashuhudia jinsi mdada huyu alivyoweza kutumia mikono yake kwa kazi hii ya kutengeneza gilasi kwa njia ya kupuliza. Hakika Mungu amempa kila kiumbe uwezo/kipaji chake. sikuishia hapa ...
...nikaendelea na halafu nikapata kuona hifadhi ya ndege. Kwa muda wa wiki moja nimepata kuona mambo yote haya na nimeona si vibaya kama nikiwajuza na wenzangu. Maana elimu kugawana. Jumatatu njema kwa wote.
Sunday, July 7, 2013
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE DOMINIKA HII YA 14 YA MWAKA C
Simba huyu anatisha kweli utafanya nini ukikutana naye njiani?. Lakini kuna adui mwingine mbaya na anayetisha zaidi kuliko simba, Ndiyo maaana mtume petro anatuonya akisema " Nuwe macho; kesheni. Maana adui yenu, ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo". NAWATAKIENI WOTE MTAKAIPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA,.......KAPILYA
Saturday, July 6, 2013
UNAMKUMBUKA MZEE WA UTAMBUZI KAKA SHABAN KALUSE? BAADA YA KIMYA KIREFU KARUDI KWA KASI KUBWAAA ..KARIBU KAKA!!!
Habari zenu ndugu zangu....Nimerudi jana jioni baada ya wiki moja kuwa kwenye kasafari kidogo...Nimerudi kuja kuvuna mboga zangu, kuangalia mazingira nk. Baada ya kutembeatembea katika vibaraza na kuona kama kuna kipya au? Nimekutana na mzee wa UTAMBUZI baada ya kimya kirefu amerudi kwa kasi. Ukipata kaupenyo mtembelee HAPA ufaidi mambo. KAKA KARIBU SANA TENA KATIKA ULIMWENGU HUU WA KUBLOG. PANAPO MAJARIWA TUTAONANA KESHO DOMINIKA....Ngoja niendelee na usafi wa mazingira na kupalilia mboga zangu.
Friday, July 5, 2013
NIPO NJIANI NARUDI NA MARA NIMEKUMBUKA NA KUTAMANI MIHOGO NA KACHUMBALI UWE MLO WANGU WA MCHANA HUU!!
Mmm mihogo kachumbali mlo mtamu sana mate yanachuruzika...je nawe umetamani? Ijumaa njema ndugu zangu
Wednesday, July 3, 2013
NAWATAKIENI JIONI NJEMA KWA UJUMBEE UFUATAO!!
Unajua ya kwamba katika maisha kuna changamoto. Kama vile kuweza kugundua wewe ni nani..
Na pia kitu kingine kizuri ni kuwa na furaha na kile ambacho umekipata/ulichonacho
Nawatakieni wote jioni njema sana. Kapulya/Kadala au dada mkuu:-)
Na pia kitu kingine kizuri ni kuwa na furaha na kile ambacho umekipata/ulichonacho
Nawatakieni wote jioni njema sana. Kapulya/Kadala au dada mkuu:-)
Tuesday, July 2, 2013
VARBERG SWEDEN:-MCHANA WA LEO NIMETEMBELEA JENGO LENYE HISTORIA LAITWA FÄSTNING/FORT
Nimependa ujenzi huu jumba hili lilianza kujengwa 1300 na lilijengwa kwa ajili kwa ajili ya kulinda mji wa Varberg na nchi ya Sweden wakati vita na maadi wabaya
Monday, July 1, 2013
TUANZA MWEZI HUU MPYA NA JUMATATU HII NA SWALI HILI:-TABIA YA KUWAACHIA WAZAZI WATOTO MPAKA LINI?
BIBI NA WAJUKUU WAKE
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kuhusu hii tabia ambayo, bado inazidi kukua tu katika jamii zetu. Hasa inapokuja kwa sisi wadada/wanawake. Hii tabia ya kuwaacha watoto kwa wazazi, hivi hii haijalishi ya kwamba wazazi wamekwisha fanya kazi yao yaani kuku/kututunza sisi na sasa ni wewe/sisi inabidi pale inapowezekana tuwatunze wao?
Utakuta wazazi wanawatunza wajukuu na hapo hapo wanakuwa na majukumu mengine na ulemuda wa kupumzika unakuwa haupo. Halafu utakuta wanaweke wengine wameolewa, na kabla yake amezaa na yule/hao watoto anawaacha kwa wazazi je Huyo mume wake hawapendi watoto hao? Afadhali anemwacha mtoto kwa ajili ya kwenda shule.
Je? huu kweli ni uungwana...???
Subscribe to:
Posts (Atom)