Na Daniel Mbega, Songea
MVUA zilikuwa zikimtendea haki Josephat Komba, mkulima katika kijiji cha Ndilima Litembo wilayani Songea, wakati pepo za kusi zilipovuma vyema na hivyo shamba lake la mpunga kupata maji ya kutosha yaliyompa mavuno mengi. Lakini hana uhakika kama atapata bahati kama hiyo msimu ujao.
“Zamani, hatukuwa na mashaka kuhusu hali ya hewa,” anasema Komba, akiwa shambani kwake kilometa kadhaa kutoka Songea mjini. “Lakini hivi sasa, tatizo ni kubwa mno.”
Komba anaitazama Milima Matogoro kwa masikitiko, na kujiuliza kama mabadiliko hayo ya hali ya hewa yameletwa na Mungu au wanadamu.
“Tumesikia mara kadhaa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, lakini nikwambie ukweli, miaka ya nyuma milima hii unayoiona hapa ndiyo ilikuwa mkombozi wetu. Tuliitegemea sana kwa ajili ya kuleta mvua, sasa hatujui kama ni laana ya Mungu au ni binadamu ndio tunaosababisha majanga haya,” anasema.
Komba anasema, zamani walikuwa wakipanda kwa wakati na mvua zilinyesha katika kipindi kile kile. “Lakini tangu walipoanza kufyeka miti kwenye milima hii, kila kitu kimebadilika. Nadhani wameikasirisha miungu.”
Misimu kadhaa iliyopita, mvua zikaanza kuadimika. Mara kadhaa mpunga wake ulikomaa bila unyevu; karibu theluthi ya mimea yake ilikauka kwa ukame na hata Mto Ruvuma ambao amekuwa akiutegemea umekuwa hauna maji ya kutosha hata nyakati za masika.
Mabadiliko hayo ya ajabu ya hali ya hewa ndiyo ambayo wanasayansi wa mazingira wanaamini kuwa ni madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati mwingine kunaweza kuwa na ukame, lakini msimu mwingine mvua zinaweza kuwa nyingi kiasi cha kuleta mafuriko hivyo kushindwa kulima.
Komba analalamika kwamba, uchomaji wa moto kwenye msitu wa milima hiyo ni sababu nyingine inayoondoa hali ya asili ya milima hiyo ya Matogoro na hivyo kuleta wasiwasi mkubwa kwamba mito mikuu kama Ruvuma, Luhira na Luwegu itatoweka katika miaka michache ijayo.
Sehemu kubwa ya msitu wa Milima ya Matogoro imebakia vipara kutokana na uvunaji wa miti ya kigeni (exotic trees) kama Misindano (Pines) na Mikaratusi (Eucalyptus) ambayo wataalamu wa hifadhi ya vyanzo vya maji wanasema inayonya maji mengi.
Mhandisi Jaffari Yahaya wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Manispaa ya Songea (SOUWASA) anasema kwamba kuwepo kwa ukosefu wa maji wakati wa kiangazi katika Manispaa ya Songea kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya miti ambayo ipo katika misitu ya milima Matogoro ambayo hunyonya maji kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha mwaka
Soma zaidi hapa
8 comments:
Ujue Watu huwa tunajisahaulisha sana kuwa Miti ni muhimu sana kwenye jamii yetu...ukame unapotokea ndo tunaanza kusikitikia miti tuliyokata
Ni kweli na wengi husahau kabisa kwamba ukikata miti basi panda mwingine ili kusiwe na uhaba...tatizo hili ni tatizo kweli. na hii ya kuchoma moto ndiyo sababu kubwa ya ardhi kukosa rutuba hata katika mashamba si vema kuchoma moto.....
Mimi nimefurahishwa na majina tu. Mwandishi anaitwa MBEGA, halafu Bwana KOMBA anatoka kijiji cha li-TEMBO.
Hapo nimekosa akina MBAWALA na KIFARU.
Watani zangu ninawapenda sana!
Ha ha haaaaaa! Mtani umenichekesha kweli haya ni vizuri kama umefurahi..ila ningependa kweli kujua jina lako::LOL
Yasinta,
Umeanza tena!
mmmhhh! hapa kuna utata basi tuendelee na mada ya leo tu...:-)
Afadhali. Ukisema na dada yangu (Mija wa Sayi) msalimie sana!
Kata mti;panda miti!!
Post a Comment