Friday, November 30, 2012

TUNAKUMBUKA VIFAA HIVI VYA KUKOBOLEA NAFAKA ZETU TANGU HAPO KALE MPAKA SASA?!!!

Hapo kale kupata ugali uwe wa ulezi, mtama,mahindi au muhogo hiki ndo kilikuwa kinu cha kusagia ili kupata unga. Kama nakumbuka vizuri juzi tu nimeona huko India bado wanatumia kusagia mchele ili kupata unga wa mchele........
 
 Na baadae kikagundulika kinu kwa kukobolea nafaka na pia kupata unga kama vile wa muhogo nk.--
..na baadaye baadaye tukapata mashine ...na mikono ikawa inapumzika kidogo. Sijui  wenzangu mie binafsi nilikuwa mzembe sana hasa kukoboa mahindi. ...je? kuna kifaa kingine zaidi ya hapa unafiri?

4 comments:

ray njau said...

Hakika kila zama na waja wake!!

Yasinta Ngonyani said...

Nakwambia kaka Ray..maana duh! mikono imepata shida kweli kukoboa mahindi au fikiria kusaga hapo kwenye jiwe hadi familia ipate lishe..sijui walikuwa wanakula ugali wa mahindi hapo kale? au ndo mtama, ulenzi na uwele? najiuliza kwa sauti tu hapa....

mumyhery said...

Mama. Erick hao wanao twanga wamekumbusha kisamvu. Lol!!!

Steven Bulamu said...

Mmmmh? labda machine za kisasa ila sisi kwetu wakati nipo mdogo nilishuudia watu wakizaga ulezi kwenye jiwe, ata kalanga-