Kwa hiyo mkiona sionekani hapa basi nipo nje naongea na maua yangu. maua haya leo nimeyapatia kulikuwa na jua kwa hiyo mchana yanachanua ikifika jiona/jua lizamapo nayo hufifia. Jina sijui ...nitatafuta nikijua nitawajuza....
Na haya hapa nilipanda mwaka jana mwezi wa kumi na sasa yapo hivi ni yanaitwa(Tulpaner) mmmhh itabidi nijifunze kwa kiswahili...Bustani ya mboga bado sijaanza kwani bado ni baridi kweny udongo....Mija, Rachel, Edna Simon, Kaka S, aahh! na wengine wote nitawajuza itakapokaribia si mnakumbuka huwa kuna ushirika wa kulima/chama na baada ya kulima kupiga UGIMBI au mmesahau?...:-)...
.Halafu mwenzenu nina UDHAIFU SANA WA MAWE kuna mawe mengine ni kutoka TZ na sehemu mbalimbali niendako:-) JIONI NJEMA SANA JAMANI NGOJA MIE NIENDELEE kuongea NA MAUA YANGU......pia MAWE.....
10 comments:
Hongera ... naona summer ndo imeanza na msimu wa maua ndo huo na yanapendeza haswa na hasa kama yana rangi nzuri na za kuvutia. Mchana wote unaweza kutamani ushinde nje au kwenye upenu wa nyumba ukiyaangalia jinsi yanavyovutia macho.
Mtu na mazingira, sijaona mboga mboga, wapi mchicha? LOL!
Ahsante mutani wangu! unafikiri siku kama hizi huwa nahamia huko nje na kuyaangalia na kuongea nayo..LOL Bustani ya mboga mbona nimesema bado kuna ubaridi labda katikati au mwishi wa mwezi huu ni vyo mchicha, figili, mboga maboga(pitiku) nk.nawe unakaribishwa kuja kusaidia kulima:-)
Yasinta,
Figili chungu sana ... usije ukajaribu kunipikia, maana zilinishinda. Au inawezekana aliyenipikia hakuwa mjuzi na inawezekana upikaji wa wangoni ni tofauti na upikaji wa wahehe.
Andaa ugimbi wa kutosha nitakuja kusaidia kulima. Bila ugimbi siwezi kushiriki kilimo!
Haya dada huo wakati na ufike,nimeshaandaa ''JEMBE'' na nipo tayari hata ukitaka matuta ya viazi mimi pouaa tuu, Sijui wenzangu wameona kuna kazi wamekimbia ehehehehehhehh!!!!!!!!Siwaambie dada watanitia Makonnthiii mwenzio.
Yasinta si ungefungua Garden Gallery yako jamani..
Tafadhali usilipuuze wazo langu..na pia Gallery ikianza kulipa usin'sahau.....lol!!
Haya mambo ya unayaweza kabisa usiishie hapo ulipo ndugu yangu..
Nilikuwa nasema haya mambo ya ubunifu wa kupamba mazingira unayaweza..
Da Yasinta,wakati wewe unatunza bustani yako ya maua kuna wale ambao hawana hata mlo mmoja.Naamini kabisa mtu akishiba basi anaweza hata kuangalia bustani yani lakini mtu mwenye njaa hawezi.
Amani.
Nami naamini kabisa mtu akishiba anaweza kuanza kuperuzi mablogu, mtu mwenye njaa hawezi @Bobo Ashante Nyahbingi..
Amani daima kaka..
Da´Rachel! wala usikonde nitakuambia unajua kutakuwa na ulanzi pia hapo ndo kilimo kitanoga kweli..LOL
Mija dadangu! hivi una uwezo wa kusoma mawazo ya watu/mtu? Hilo ndilo dhumuni langu.
Kaka Nyahbingi...Wakati mwingine ukifikiria kila kitu basi hutaweza kufanya kitu chochote kile. Na nimekuelewa wazo lako.
Amani kwa wote!!
Naaaaaaaaaaam;ndiyoooooooooooo!!!!
Mandhari nzuri iilibuniwa na mtunza bustani mahiri na makini katika tasnia ya watu na mazingira yao.
Asante sana na kamwe usilegeze mikono yako.
-----------------------------------
Na Yehova Mungu akamchukua mtu na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza._Mwanzo 2:15
-------------------------------
Post a Comment