Thursday, May 31, 2012

SIJUI TUNAKOKWENDA NI WAPI? AU NI SHETANI ANATAWALA?

Najua wengi mtajiuliza mbona alisema AMEFUNGA MWEZI HUU WA TANO kama ilivyo hapo chini. Lakini baada ya pitapita nimeshindwa kuvumilia na habari hizi zimenisikitisha sana na ndio nikaona niziweka tu nazo kwani ni moja ya habari muhimu katika maisha yetu wanadamu.

 Mama mzazi wa Mtoto aliye nyongwa Mtotot wake kwa kumuvunjwa shingo akiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati mtoto akifanyiwa uchunguzi
Dakitari wa hospilata ya Mkoa Ruvuma Dakitari Mchirika akiuangalia mwili wa mtoto/malaika huyu.
Masikini mtoto mdogo mwenye umuri wa miaka mitatu akiwa amelala chumba cha kuhifadhia maiti baada ya mama yake mzazi akishirikiana na hawara yake ambao wana tuhumiwa kumua mtoto huyo ili asiwabuguzi wawapo kitandani. Na baada ya mauaji hayo waliahidi kuoana.  Hebu angalia watu walivyo hawana huruma akina mama, akina baba, wazee wetu utamaduni wa Mwafirika Mmeuweka wapi ? CHANZO CHA HABARI ni HAPA.  Halafu soma na hii  HAPA . INASIKITISHA SANA KWA KWELI....

ELIMU HAINA MWISHO:-USAID helping Maasai Women gain Literacy & Numeracy skills for self empowerment


Mwezi wa tano ndo huu unakatika leo..nami nimeona tuumaliza kiaina hii. Karibuni


USAID is helping Maasai women in Tanzania gain literacy and numeracy skills so that they can obtain land rights, start businesses, and become involved in local government.
By 2011, more than 2,000 women had completed the program. Their new communication skills allow them to conduct business activities more easily and empower them to assert their rights.
For the first time in their lives, these women are earning incomes independently through small enterprises and farming. One graduate of the program says, "It has helped me to mobilize other women because the program saw potential in us."
Video below by Ashiembi Productions. Produced by Megan Johnson/USAID - USAIDAfrica, published on May 24, 2012

Wednesday, May 30, 2012

TUMALIZIE SIKU HII HUKO WILAYA MPYA YA NYASA KWA MLO HUU!!!

Ndugu msomaji wa mtandao huu umesikia kuwa hivi sasa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kaanzisha wilaya mpya ya Nyasa sasa ufikapo wilaya hiyo chakula kikuu ni ugali wa Mhogo na Samaki kama unavyo ona hapo juu samaki alioko juu ya ugali anaitwa Mbufu
picha na maelezo hapa.
------------------------------------------------------------------------------------------------------Baada ya kusoma hapoa yaani jioni hii nimetamani kweli mlo huu. Huu ndio mlo ulionifanya niwe na afya hii niliyonayo leo. Mbufu ni samaki mtamu sana mwaka 2007 nilipokuwa Mbambab bay nilimla ila mwaka jana nilipokuwa Matema beach nilimkosa. Nikaona nisitamani tu ngoja niichukue picha hii ili iwe karibu nami. 
JIONI NJEMA KWA WOTE...





UNATAKA KUMUACHA MKE MKOROFI? FANYA HIVI.........!


Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEIKUTA HII KWA KAKA YANGU WA HIARI KALUSE Hebu soma na halafu tujadili kwa pamoja.KARIBU...



Kuna wanaume ambao wametokea kuoa wanawake ambao wana tabia mbaya . ninaposema kuwa na tabia mbaya sina maana ya mwanamke kuwa Malaya, maana hiyo ni fasili rahisi ya tabia mbaya kwa watu walio wengi. Ninaposema tabia mbaya nina maana kwenda kinyume na matarajio ya mume na pengine hata kwenda kinyume na matarajio ya jamii. Mwanamke ambaye ana tabia kama ghubu, mdomo mdomo (mkosoaji), mtapanyaji wa mali, mpenda makuu na tabia nyingine za aina hiyo, ni mwanamke ambaye kwa kiasi kikubwa anaweza kumsababishia mume matatizo ya kimwili na kisaikolojia. Mwanamke wa aina hii anaweza hata kuathiri makuzi ya watoto na kuathiri uhusiano na mume na watu wengine waliyo karibu yake. Kama mwanamke wa aina hii ameolewa na mume mweledi ndoa inaweza isiyumbe sana, lakini hii ina mipaka na kiwango chake.

Kuna wakati matatizo haya huweza kufika mbali zaidi kiasi kwamba huanza kumwathiri mume. Mwanaume ambaye huchukua kila uamuzi unaohusu maisha yake kwa hadhari kubwa, anaweza kuendelea kuishi na mke huyu. Lakini mara nyingi kuendelea kuishi na mke huyu kuna maana ya matatizo zaidi kuliko ufumbuzi. Bila shaka mmeshawahi kusikia wanaume ambao wanalalamika kuhusu tabia mbaya za wake zao (hata hapa JF wapo wengi sana), lakini huku wakiendelea bado kuwa na wake hao. Ukiacha sababu ya kugawana mali, wanaume wengi huwa wanafikiria mambo mengi ambayo huwazuia kuchukua uamuzi wa kuachana na wake hao.

Nimeona itakuwa vizuri kuwaambia wanaume hawa kwamba, kama ndoa zao zimefikia mahali ambapo zinataka kuwatia kichaa, wakiwa na uhakika kwamba wake zao ndio wenye matatizo na sio wao, (hili inabidi waliangalie kwa makini) inabidi wafanye uamuzi kwa kujiangalia wao na watoto wao zaidi kuliko watu au vitu vingine. Baadhi ya mambo ya kuangalia ni haya:

1. Kuathirika kwao: wajiulize wanaumia kiasi gani kimwili na kisaikolojia kwa kuendelea kuishi kwao na wanwake hawa. Kama ni ghubu na kukosolewa, kunawaathiri kiasi gani,? Na kama ni utumiaji mbaya wa mali unawaathiri kwa kiasi gani? Kama athari za tabia mbaya alizo nazo mwanamke zinafaa kudharauliwa na mume anaweza kuzidharau ni vyema akafanya hivyo, na kuendelea na maisha. Na kama akiona kuzidharau tabia hizo itakuwa na maana ya angamio kwake na pengine mbaya zaidi kwa watoto, inabidi hiyo iwe ni sababu ya msingi kuachana na mke huyo.

2. Ndugu watasemaje: wanaume wengi hukwamia hapo. Kama wake zao wanaelewana vizuri na baadhi ya ndugu, au hata wazazi wao, wanaume hushindwa kutoa maamuzi wa kuwaacha kwa hofu ya kulaumiwa na kushangawa. Wakati mwingine mume huyu anaelewena sana na watu wa upande wa pili, yaani ndugu wa mke na hasa wazazi na pengine wote. Hiki nacho ni kikwazo kikbwa sana, kwani mume hufikiria jinsi atakavyoonekana kwa watu hawa, pale atakapoamua kuchukua uamuzi wa kumuacha mkewe.

3. Sifa moja nzuri: pamoja na kuwa na matatizo, kila binadamu anaweza kuwa na upande mzuri. Kama mwanamke huyu ana sifa fulani ambayo ni nzuri sana, tuseme ni mpishi hodari sana na mkarinu kwa wageni , au labda ni mwaminifu sana katika ndoa, mwanaume anaweza kukwama kutoa uamuzi kwa kudhani au kujidanganya kwamba huenda anaweza asipate mwanamke mwingine mwenye sifa kama hizo. Huku ni kujidanganya kwa sababu kila sifa aliyo nayo binadamu fulani, ya kitabia, ipo kwa binadamu mwingine hata kama siyo wengi.

Ukweli ni kwamba mwanaume anaweza kushindwa kumpa talaka mkewe ambaye anakaribia kumuuwa kwa matatizo yake kwa sababu ambazo mtu mwingine anaweza kuzishangaa. Lakini jambo la msingi kwa mwanaume kama huyu ni kujaribu kupima kwa makini, je hizo sababu zinazomfanya asite kuachana na mkewe huyu zina nguvu au maana kuliko maisha yake, hasa mwili na akili yake?.
Angalizo: Sishauri watu kuachana, lakini nashauri watu kujua kwamba ndoa zenye mashaka makubwa ni hatari kwa afya na maisha yao. 
TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA..JUMATANO NJEMA.

Tuesday, May 29, 2012

BUSTANI YANGU INAVYOONEKANA KWA SASA..AU JANA JUMATATU!!!

 Hapa ni kaeneo ambako huwa nalima bustani  za mbogamboga za aina mbalimbali. Na jana Jumanne ya 28/5-12 ndio nimepanda . nimepanda Corrot, maharagwe, mchicha, maboga, figiri, vitunguu, nyanya, nk. Kutokana na hali ya hewa kuwa si nzuri sana mwaka huu inasemekana nimechelewa kidogo....Ila baada ya wiki chacha nategemea mimea itakuwa imeanza kuota...au kuwa kama ...


...katika bustani hii hapa . Majibu tutayapanda karibuni. Hii ndiyo moja ya shuguli nilizozifanya jana. PAMOJA DAIMA SANA!!!

Monday, May 28, 2012

JE? LAKINI ULIPENDA NINI AWALI?

Hili ni jambo muhimu sana, Tunapomwona mtu kwa mara yakwanza akatuvutia, tunaweza tusijue ni kwa nini ametuvutia, lakini kama tutakuwa wadadisi, tunaweza kubaini kwamba, tumevutiwa na sura, miguu, macho, nywele, mavazai au kingine.  Inaweza kuwa  ni kwa sababu ya kipaji chake, uwezo, umaarufu na vitu vya aina hiyo.
Tunashauriwa kujiuliza kitu au jambo ambalo limetufanya tumpende mtu fulani. Je?, tumevutiwa kwa mguu wake, kwa jicho lake, elimu yake, kipaji chake au kitu kingine tunachokifahamu?

Kama ni kwa kitu tunachokifahamu, tunatakiwa kujiuliza kama kitu hicho ni cha muda au cha kudumu. Kama ni cha muda, kama ilivyo kwa wengi, inabidi tujifunze jambo jipya. Inabidi tujifunze kutafuta kitu cha kudumu ambacho tutakipenda kwa  wapenzi wetu.  Kwa nini?
Kwa sababu, vile vyote vilivyo nje, ambavyo tulivipenda kwa sababu tumeviona,  havidumu sana, ukiwemo mwili kwa ujumla. kwa hali hiyo kama tulimpenda mtu kwa sababu ya mguu, jicho, tabia, fedha, umaarufu. Hivi vyote kuna siku vitachuja au kwisha au kubadilika, na hapo utakuwa ndiyo mwisho wa upendo wetu kwa watu hao.

Lakini kwasababu tulijifunga nao kwa ndoa, tunabaki tukiwa na hasira za kujifunga na watu ambao hatukujua kwamba, hatukuwa tukiwapenda. Tutakorofishana mahali ambapo tulipaswa kufurahi, tutakorofishana mahali ambapo tulipaswa kupendana zaidi.
Kwa sehemu kubwa, unakuta tangu awali tulikuwa hatujapendana. Tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza tulitamaniana tu. Tulitamani sifa za muda mfupi, ambazo hatimaye hufutika.

Ni kweli kwamba, kule tunakoita kupendana ambako hutokea tunapokuwa ndani ya ndoa, huanza kwa sisi kukutana kwanza, halafu kwa kila mmoja kuwajibika kwa upande wake, kupendana hutokea. Kupenda kumo ndani mwetu, ni jukumu letu kujua hilo na kukutoa huko kupenda ili kumudu kufurahia maisha na wengine.
Chanzo:- kitabu cha MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA na MUNGA TEHENAN.
MWANZO MWEMA WA JUMA.

Sunday, May 27, 2012

LEO NI SIKU YA AKIMNA MAMA (MORS DAG)


Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mama yetu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mama yetu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka.( kwa niaba ya mama)

Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mama yangu. NAWAPENDA AKINA MAMA WOTE DUNIANI.NA TUTAFIKA TU.

Saturday, May 26, 2012

JUMAMOSI HII TUANGALIA JINSI NDOA NDOANA INAVYOKUWA....!!!!


Mmmmhh hapa kaaaaazi kwelikweli!!! NATUMAINI JUMAMOSI YAKO ITAKUWA NJEMA...

Friday, May 25, 2012

HUU NI UJUMBE WA IJUMAA YA LEO!!

NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA..PIA WOTE MNAPENDWA!! KAPULYA!!

Thursday, May 24, 2012

JE? UMEKISIKIA KILIO CHA UPUNGUFU WA MADAWATI NCHINI TANZANIA?


Elimu ndiyo msingi wa maisha na kila mwenye elimu ni mwenye hazina na daraja la kumfikisha kwenye mji wa kufikirika wenye jina la maisha na mafanikio.
Mazingira rafiki ndiyo nyenzo muhimu kwa yeyote anayepewa elimu  kwa malengo ya manufaa ya sasa na  wakati ujao.
Miundombinu  katika shule za  msing nchini Tanzania  haikidhi mahitaji halisi na ile ya zamani inazidi kuchakaa.
Kilio cha upungufu wa madawati katika shule za msingi sasa ni wimbo kutoka kaskazini kwenda kusini na magharibi kwenda mashariki.
Madarasa yaliyopo ni machache na baadhi yake hayakujengwa katika kiwango na hadhi husika.
Nchi imejaa misitu na miti yenye miti ya mbao lakini bado kilio cha upungufu wa madawati kinazidi kulitawala anga la Tanzania.
Hakuna sababu yakuendelea kulia na jambo kuu hapa ni jamii kukusanya mawazo pamoja na  kusema sasa inatosha.
Taasisi  za kijamii zina wajibu wa kukusanya nguvu za pamoja na kubuni mpango wenye tija katika hii changamoto ya kitaifa chini ya uratibu wa SIDO na VETA.

Wednesday, May 23, 2012

KAZI YA UALIMU SI LELEMAMA NI NGUMU!!

Kwa vile ni JUMATANO YA MARUDIO NIMEONA SI VIBAYA TUKIANGALIA NA HII!!
Picha/katuni:- http://hapakwetu.blogspot.se/

BWANA MATATA HAJUI KUSOMA+KUMBUKUMBU


Mada hii nilishawahi kuiweka hapa kibarazani, lakini jana katika pitapita nimekukta picha kwa prof. Matondo nikakumbuka  kitabu cha bwana Matata na nimeona si mbaya kama tukijadili tena kwa pamoja . NA UKIZINGATIA LEO NI KILE KIPENGELE CHA JUMATANO YA MARUDIO YA MAMBO MBALIMBALI..Haya soma haabari yenyewendiyo hii

Kwanza naanza na kusema NAMSHUKURU  babangu kwa kutunza kitabu hiki leo nimefurahi sananwaeza kuwasomea hata wanangu. Nadhani hata wenzangu mtafurahi pia kukumbuka hadithi hii:-
Bwana Matata yupo mjini, anauliza uliza njia ya hospital. Kuna kibao hapo njiani, lakini haui kusoma kibao.Bwana Matata anaona aibu kuuliza njia tena, anaona aibu kwa sababu hajui kusoma. Sasa anafuata njia ya bomani
Bwana Matata amechoka sana. Amechoka na safari, pia amechoka kuuliza uliza njia. Amelala kwenye kibao, kibao kinasema HATARI. Lakini Bwana Matata hajui kusoma, tena amechoka mno. Amelala njiani kwenye kibao

Bwana Polisi anapita, anamwona Bwana Matata amelala kwenye kibao. Bwana polisi anamwita, mzee vipi? Kwa nini unalala hapa? Huoni kibao? Lakini Bwana matata amechoka sana amelele kama gogo. Polisi amawita tena, kwa nini unalala hapa kama gogo? Kuna hatari hapa. Lakini bwana matata hana habari ya hatari hajui kusoma.

Bwana Matata akaamka, akasimama na kumwambia polisi, nataka kwenda hospitali. Mtoto wangu yupo hospitali ni mgonjwa sana, lakini nimepotea njia. Bwana polisi akasema, umepotea njia? Fuata hii Bwana Matata akafuata njia ile. Kinachoendelea naadhani mnajua 
JUMATANO NJEMA........

Tuesday, May 22, 2012

TUIMALIZE SIKU/JIONI HII NA MWIMBO HUU:- MWANAMKE HAPIGWI!!


Binafsi leo nipo napumzika, ila ndo nini vijishughuli kibao.  Na wakati najipumzisha na hivyo vishughuli nikaona nisikilize kidogo mziki.Katika kusikiliza nikafika hapa, hakika nakuambia mpaka nimelia...NIMEGUSWA  sana  kuona/kusikia  hii. Mara nyingi inakuwa kweli kabisa ...kazi kwelikweli. JIONI NJEMA MUNGU AKIPENDA TUTAONANA KESHO.

SIKU YA GULIO KATERERO!!





Hiki ndiyo kitabu nilichokiota nakisoma!
 Wakipanga bidhaa!

Leo nimeamka na kukumbuka nimeota ndoto kuwa nipo darasa la nne na tupo darasani twasoma sura hii ya 11 SIKU YA GULIO KATERERO.Sura hii ipo hivi:-
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Gulio ni soko la siku moja moja. Katika kijiji cha Katerero, Wilayani Bukoba siku hiyo ni Jumanne. Wakulima hukusanyika kuuza mazao yao, na watu wengi huenda kuyanunua.
Watoto wa katerero hushirikiana na wazazi wao katika kazi za nyumbani. Kila Jumanne wakati wa likizo, Kiiza na wazazi wake huchukua mazao na kupeleka gulioni. Siku moja Kiiza, mama yake na shangazi yake walikwenda gulioni. Kiiza alichukua kikapu cha maharagwe na mama yake alichukua mkungu wa ndizi. Shangazi yake Kiiza alichukua tangawizi na kabichi. Kiiza alifunga kikapi kwenye baiskeli akawa anafuatana nao. Njiani walikutana na watu waliokuwa wanakwenda gulioni. Wengine walikuwa na mayai na kuku, na wengine walichukua nguo na mikeka. Walipofika gulioni walikuta watu wengi sana. Pale gulioni kulikuwa na vitu vingi vilivyoletwa kuuzwa.

Kiiza, mama yake na shangazi yake wakatafuta mahali pazuri pa kukaa, halafu wakapanga vitu vyao waviuze. Kiiza alipanga mafungu ya maharagwe; tangawizi na kabichi. Mama yake alitandaza majani ya mgomba na akauweka mkungu juu yake. Mara akaja kijana mmoja akauliza, "Mama, mkungu huu bei gani?" Mamake Kiiza akajibu, "Shilingi nane na thumuni." Yule kijana akaomba apunguziwe. Akasema, "nitakupa shilingi sita." Yule mama akakataa. Wakabishana bei mapaka yule mama akakubali kumwuzia kijana kwa shilingi saba. Kiiza aliwasikiliza mama na kijana.

Alipoondoka yule kijana, mama akamwambia Kiiza, "Nenda nyumbani ukaulete ule mkungu mwingine nilioukata jana jioni." Kiiza alichukua baiskeli akakimbia nyumbani na kurudi na mkungu. Mara tu alipofika gulioni alikutana na watu waliotaka kununua ndizi. Akawaambia, "ikiwa mnataka nipeni shilingi nane na nitawauzia." kwa vile mkungu ulikuwa na ndizi nzuri wale wanunuzi waliuchukua bila kusita kwa bei waliyoambiwa. Kiiza alipofika gulioni mama akamwuliza, "mkungu uko wapi? Tena basi umechelewa." Kiiza akamjibu mama, "Ule mkungu nimeuuza." Mama yake akamwuliza, "Fedha ziko wapi?" Kiiza akzichukua zile shilingi nane akampa mama. Mama yake alipoelezwa juu ya uuzaji huo alifurahi sana. Alimshukuru mwanae kwa kitendo hicho.

Kiiza, mama yake na shangazi yake wakaendelea kuuza maharagwe, tangawizi na kabichi. Kwa kuwa hawakuwa na mizani, walitumia mkono kupimia maharagwe na tangawizi. Waliuza kopo moja la maharagwe kwa senti hamsini na kopo la tangawizi kwa shilingi moja. Waliuza vitu vyao vyote mpaka vikamalizika.
Wakati huu, Kiiza alianza kuona njaa. Mama yake akamnunulia karanga na maandazi. Kisha wote watatu wakaenda hoteli kunywa chai. Walipokuwa hotelini, Kiiza alimkumbusha mama yake kumnunulia ndara: Mama yake akamwambia, "Tukisha kunywa chai nitakununulia. Tena umenikumbusha kumnunulia baba yako kitasa na kitana cha mti." Walipotoka hotelini waliona kuwa mahali walipokuwa pamepangwa vitu vingine. Kitu kilichomvutia zaidi Kiiza ni embe kubwa. Alimwuliza mama, "Embe hizi hutoka wapi"? Mama akamjibu, "Embe hizi hutoka Tabora." Kiiza alizimezea mate akamwomba mama amnunulie moja aionje. Baada ya kula moja alitaka ya pili, lakini mama alimwambia, "Twende kwanza tukanunue vitu vingine.

Kiiza, mamake na shangazi wakaondoka kwenda kununua vitu  hivyo. Mwisho mamake akanunua mafuta ya kupikia. Wakati huo mvua za rasharasha zilianza. Mama yake Kiiza shangazi yake na majirani wote wakapanda basi kurudi nyumbani. Gulio likavunjik. Mvua ilipokatika Kiiza akapanda baiskeli yake na kurudi nyumbani.
Walipofika nyumbani, Kiiza alimweleza baba yake mambo yote aliyoyaona sokoni. Alimweleza pia habari ya mvua iliyonyesha na kulifanya gulio livunjike. Baba yake akamwambia kwamba wazee wamekwisha amua kujenga soko zuri la mawe litakaloezekwa kwa bati, Watashirikiana  kukusanya mawe na kuanza kujenga mara tu masika yatakapomalizika.
------------------------------------------------------------------------------------------------------
Na mara nikashtuka na ule ukurasa ukawa umeisha ...halafu la ajabu pia nimeota ndoto hii siku ya JUMANNE!!!


Monday, May 21, 2012

BAADA YA MAPUMZIKO NIMEONA TUANZA JUMATATU HII KIHIVI!!!

Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu  twnajua/twakumbuka hapa ni wapi. Labda tu niuliza Je? unajua hapa ni wapi?...Nawatakieni mwanzo wa juma hili uwe mwema.

Sunday, May 20, 2012

JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA KWA WOTE

Kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, 
ndivyo mlivyo katika mkono wangu Yer 18:6.
Ujuzi hauzeeki:- Mafundi hao hutudhihirishia kwa ubora na unadhifu wa kazi yao. Tuige mfano wao tufanyapo kazi zetu. Hata zikiwa za kawaida.

Saturday, May 19, 2012

JUMAMOSI HII NIMEKUMBUKA MATETEREKA/MADABA HAKIKA ZILIPENDWA

Nimerudi nyuma na kufikiri sana na kila nikiangalia picha hii hapo ndio nionapo kweli watu tumetoka mbali Mwaka 1992 Wilima (Matetere) Madaba.
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA SANA...BINAFSI NAENDA KULIMA KABUSTANI KANGU .

Friday, May 18, 2012

The story of a blind girl:- LIFE IS A GIFT!!


There was a blind girl who hated herself because she was blind.
She hated everyone, except her loving boyfriend. He was always there for her.
She told her boyfriend, 'If I could only see the world, I will marry you.'

One day, someone donated a pair of eyes to her. When the bandages came off, she was able to see everything, including her boyfriend.

He asked her,'Now that you can see the world, will you marry me?'
The girl looked at her boyfriend and saw that he was blind. The sight of his closed eyelids shocked her. She hadn't expected that. The thought of looking at them the rest of her life led her to refuse to marry him.

Her boyfriend left her in tears and days later wrote a note to her saying: 'Take good care of your eyes, my dear, for before they were yours, they were mine.'

This is how the human brain often works when our status changes.
Only a very few remember what life was like before, and who was always by their side in the most painful situations.
Life Is a Gift

Today before you say an unkind word -
Think of someone who can't speak.

Before you complain about the taste of your food - Think of someone who has nothing to eat.

Before you complain about your husband or wife - Think of someone who's crying out to GOD for a companion.

Today before you complain about life -
Think of someone who went too early to heaven.

Before you complain about your children -
Think of someone who desires children but they're barren.

Before you argue about your dirty house someone didn't clean or sweep -
Think of the people who are living in the streets.

Before whining about the distance you drive
Think of someone who walks the same distance with their feet.

And when you are tired and complain about your job -
Think of the unemployed, the disabled, and those who wish they had your job.

But before you think of pointing the finger or condemning another -
Remember that not one of us is without sin and we all answer to one MAKER.

And when depressing thoughts seem to get you down -
Put a smile on your face and thank GOD you're alive and still around.
God Bless You.
SOURCE: PASTOR CARLOS KIRIMBAI FACEBOOK STATUS
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa blog ya Maisha na Mafanikioa toka nyumbani Tanzania. Ni habari ya kufunza binafsi nimejifunza mambo mengi na nimeona niwashirikishe na wanzangu pia.

HUU NI UJUMBE WANGU WA IJUMAA YA LEO!!!

Unajua kwamba:- Kuna uwezekano ya kwamba umekuwa katika miujiza mingi, ambayo huaminika kuna nguvu nzuri ndani yake....IJUMAA NJEMA WANDUGU!!!

Thursday, May 17, 2012

SWALI HILI LIMENISUMBUA SANA MUDA MREFU:- KWANINI WAIMBAJI WENGI WA AFRIKA MASHARIKI WAIMBAPO HUCHANGANYA LUGHA?...


Wimbo huu nimeusikiliza mara kadha pia waimbaji wengine wengi tu kuwataja wote itachukua muda. Hivi waingiziapo maneno ya kiingereza ndi wimbo unakuwa mtamu zaidi au? Kwanini kama huyu dada  Amani asiseme tu NAKUTAMANI MPENZI WANGU, badala ya hiyo I MISSING MY BABY?  Je? lugha yetu ya KISWAHILI haiimbiki?. Naomba msaada wenu/ tujadili kwa pamoja jamani...lugha yetu itapotea!!!!!

Wednesday, May 16, 2012

Wanafunzi wanasomea vibanda vya nyasi!!

Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUTEMBELEE WILAYANI NAMTUMBO.ELIMU NIMEIPATA HABARI HII  Albano Midelo Haya KARIBUNI. 



 Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi
 SelousWilayani Namtumbo wakiwa darasani.

WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.
Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi 296 wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi.
.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.
Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .
Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.
Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu .
“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’,alisema.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa Wilayani
Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga,Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini,Kidagulo,Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’,alisisitiza.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi .
“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’,alisisitiza.

TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO KWA JINGINE LA ZAMANI!!

Tuesday, May 15, 2012

NIMELIPENDA HILI VAZI NA NALITAKA...

...Si mnajua kijani...naipenda mno rangi hii . Yaani hapa Dada Jennifer Lopez duh! amemechisha kweli, ametoka chicha...

HAPA NI BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA SEHEMU MBALIMBALI TANZANIA!!!

1.Alipo mtu mwenye dosari si vema kuzungumza habari hizo (Kibena)
Maana ya methali hii ni kwamba mtu mwenye dosari huwa na wasiwasi kila mara dosari yake igusapo, na huwa mkali kiasi cha kushangaza wazungumzaji. Kama dosari hiyo ni kilema huweza kuwafikiria vibaya wasemaji. Hutumika katika kuwaonya watu kuwa iwapo wanafahamu kwamba mtu mmoja kati yao ana dosari wajihadhari kugusia hiyo wakati wa mazungumzo yao.

2. Mzigo kichwani mwa mwenzio waweza kuwa wako (Kiiraqw)
Kila mtu ana matatizo yake na kuyatatua kwa kushirikiana na wenziwe. Kuna watu wenggine wanaokataa kutoa msaada wakidhani wanajitosheleza wenyewe. Methali hii inafundisha umuhimu wa ndugu na ushirikiano katika maisha nayo hutumika wakati inapotakiwa kuonyeshwa fundisho hilo.
PAMOJA DAIMA!!!!



Monday, May 14, 2012

NIMEONA TUENDELEE NA JUMATATU HII NA KAMUSI....


Pale lugha inapokuwa ngumu basi mwokozi wangu ni hizi KAMUSI . Naweza nikasema haya ndio maisha yangu maana utakuta mara nyingine kuna neno na nashindwa kujua maana lakini ukiwa na hizi kamusi mambo poa kabisa. Umewahi kuisoma hii KAMUSI YA KISWAHILI? Kama hujasoma isome utaona utamu wake:-)

JUMATATU HII AU WIKI HII TUANZE NA:- DONGI DONGI EMBE!!!

Leo nimeona tuelekee Mbamba bay kula embe. Je mpo nami au? Yaani hapa nimetamani kweli hizi embe  ....Haya nawatakieni mwanzo wa juma mwema na  DONGI DONGI JE UNAKUMBUKA MCHEZO HUU UJIPATA KITU BASI NDIYO NDONGI DONGI!!!!

Sunday, May 13, 2012

JUMAPILI NJEMA NA TUSALI SALA YA BABA YETU!!

SALA KUU

Baba yetu uliye Mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako ufike,
Utakalo lifanyike , duniani kama Mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
Utusemehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika vishawishi, lakini utuokoe maovuni.(Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina
HII SALA IMEBEBA MAOMBI YOTE, LIKIWEMO LA KUSAMEHEWA DHAMBI NA KUOMBA RIZIKI.
UKISALI  HII , HUNA HAJA YA KUSALI VINGINE VYOVYOTE.
FANYA HIVYO KILA SIKU, KILA UPATAPO MUDA.
Basi ngoja dada Rose Muhando aikamilishe jumapili hii ni wimbo huu UTAMU WA YESU!!

JUMAPILI NJEMA SANA KWA WOTE NA WOTE MNAPENDWA!!


Saturday, May 12, 2012

RUDI NYUMBANI AFRIKA/TUSISAHAU TULIKOTOKA!!



Mmmhh nimepata hamu kweli kweli hapa ya kula vyakula hivi  mpaka naanza kufikiria kuwa ...naacha  bwana  labda ntasema siku nyingine. Je? nawe umepata hamu kidogo? ngoja Baba gaston amalizi na RUDI NYUMBANI AFRIKA!!!!
JUMAMOZI NJEMA. NYUMBANI NI NYUMBANI TUSISAHAU TULIKOTOKA.!!!!

Friday, May 11, 2012

HUU NI UCHAGUZI WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII IWE PICHA YA MWISHO WA JUMA!!

DUH1 NIMECHOKA KWELI!!
Ndiyo! Mara nyingi wengi tunachoka sana ufikapo mwisho wa juma. Picha inatoka http://simon-kitururu.blogspot.se/. Haya  jioni njema binafsi bado nabeba maboxi:-)

UJUMBE WA IJUMAA YA LEO NI:-

Mtu ambaye hajitendei wema mwenyewe, basi huyu hawezi kuwatendea wengine wema!!
NAWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA UWE MWEMA!!

Thursday, May 10, 2012

JELA -NA HUSSEIN MACHOZI

Nimeupenda wimbo huu wa Hussein Machozi na hasa ujumbe wake kuhusu jela. Ukipata muda hebu jaribu kuusikiliza.


Maisha haya jamani kaaazi kwelikweli...Bora nirudi jela.....!!!

TUSISAHAU METHALI ZETU/BAADHI NI IMANI ZA USHIRIKINA (SUPERSTITIONS)!!

1.Kuku wakionekana kama wananongónezana basi patafika wageni ghafla.
2. Kuweka mikono kichwani bure tu, kunaleta kifo cha mzee wake mtu.
3. mtu akiinuka akaona nguo imeganda matakoni basi inaonyesha kuwa mtu huyo ana tabia ya kusema uwongo.
4. Mwanamke hali ndizi pacha(hasa mwenye mimba) kwa kuchelea kuzaa watoto pacha..
5. Ukiona mwasho juu ya kiganja cha mkono wa kilia utapokea fedha.
6. Kiganja cha mkono wa kushoto kikikuwasha ni alama ya kutumia fedha.
7. Ukijikwaa mguu wa kulia pana heri inakungoja huko uendako.
8. Ukijikwaa mguu wa kushoto utafikwa na maafa huko uendako.
UKIWA NA METHELI NAWE UNAWEZA KUONGEZEA NA NDIYO KUJIFUNZA MENGI!!!

Wednesday, May 9, 2012

JIONI NJEMA NA :-WANAWAKE WA SHOKA/ WANAWAKE NA VILEMBA ("WRAPS")

 Dada Mija wa http://damija.blogspot.se.
 Mama Ana Tibaijuka.
Na Winnie Mandela, aliyekuwa mke wa Mstaafu Rais Nelson Mandela.
JIONI NJEMA!!!

Tuwe na shukrani. Tusikate tamaa kabla hatujaona yote


Ni kile chetu cha KIPENGELE CHA JUMATANI YA MARUDIO..NA LEO KATIKA PITA PITA NIMEKUTANA NA HII. BINAFSI NIMEIPENDA MNO SI KWINGINE NILIKOIKUTA BALI NI KWA MZEE WA CHANGAMOTO. KARIBUNI.

------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nakumbuka mwaka 2000 nilikuwa nikihudhuria mazoezi ya mgongo pale Muhimbili baada ya ajali ya Dec 1999. Siku moja niliamini kuwa katika maumivu makali saana. Na nilikuwa nikisubiri zamu yangu kwenda kuonwa na Daktari (pale taasisi ya mifupa) kabla ya kurejea mazoezini na nikiwa nimekaa nikaona wenzangu wakiongea na nilidhani hawakuwa katika maumivu kama niliyokuwa nayo. Nilihisi kuwa mwenye maumivu kuliko wote. Baada ya dk kama 30 kupita, ikaongezeka sauti ya kaka mwingine aliyekuwa akiongea kwenye simu kwa sauti ambayo haikuonesha kuwa anaumia. Mawazoni mwangu nikawaza tena kuwa "hawajui niko katika maumivu kiasi gani". Niliponyanyua uso, nikamuona kaka aliyesimama pembeni yangu ambaye alionekana kuharibiwa vibaya mguu wake ajalini. Nilishangaa kuwa ndiye aliyekuwa akiongea vile. Nilijihisi kupona na nilimpisha akae mahali nilipokuwa nimekaa. NIKAJIFUNZA.
Katika maisha ya kila mmoja kuna maanguko meeengi ambayo yanapotokea huwa tunajiona kama ndio tumefika mwisho wa maisha. Tunafikiria "kwanini" na pengine kuwaza kama "kuna anayepitia haya?" Hatujui kuwa wapo walio katika mataabiko zaidi ya tuliyopo.
Jana usiku nilienda kumtembelea mtoto mchanga wa rafiki yangu ambaye anaumwa saana. Na nikiwa katika hospitali hiyo ya watoto niliona watoto weeengi walio katika hali za kuendeshewa maisha yao kwa mashine. Nikasikitika. Nina mpenzi makubwa saana na watoto kwa hiyo hali hiyo ilichukua sehemu kubwa ya furaha ya asili ndani mwangu. Nilijiuliza maswali mengi saaana kuhusu hali ile na kunifanya kurejesha taswira za maisha yangu tangu pale nilipoweza kukumbuka. Kisha nikarejea katika ukweli kuwa na mimi nilikuwa mtoto kama wao na niliweza kuvuka umri walionao. Niliona nyuso za wazazi wakiwa na matumaini ilhali wana uoga mwingi na ilinifanya kumuomba Mungu juu ya watoto hao. Niliporejea nyumbani ilinichukua muda kurejea katika hali ya kawaida. Na bado naendelea kuwaza na kujiuliza kama NILISTAHILI KUWA NAKATA TAMAA NIPATAPO MAKWAZO / MAJARIBU? Najiuliza kama TUNA HAJA YA KUONA KAMA MUNGU HAYUKO UPANDE WETU KWA KUWA HATUNA UHAKIKA WA KUWA NA AKIBA YA KUTOSHA MPAKA WAKATI WA MALIPO YAJAYO, AMA KWA KUWA TUNAHISI TUTASHINDWA MTIHANI DARASANI AMA KWA KUWA HATUWEZI KUNUNUA TUNACHOPENDA KUWA NACHO AMA KWA KUWA TUMEPOTEZA KAZI.
Nikiwaangalia watoto wale, nilihisi kama wangepewa uchaguzi wa kuendelea kuwa pale walipo, ama wakue na wakutane na yale yatukatishayo tamaa, sina shaka wangekubali kukua na kupambana na tupambanayo sasa.
Nimezidi kugundua na kujifunza kuwa kila kitokeacho kina sababu na naamini Mungu ana kila sababu ya kutuweka mahala fulani, wakati fulani, tukutane na fulani na tujifunze kitu fulani. Safari yangu ya jana imenifungua macho ya ki-Imani na kunifanya kuuangalia uhai wangu kwa "vipindi" vifupifupi ambavyo nimejaribu kufikiri mengi niliyoepushwa katika vipindi hivyo. Maradhi na mapungufu ya kabla na baada ya kuzaliwa, ajali na hatari mbalimbali na nimeona kuwa wengi wetu (nikiwemo) tunaishi kama vile kila siku ILIAHIDIWA KWETU. Si kweli
Ni kwa kutojua namna tulindwavyo ama namna namna tulivyoepushwa ma vyanzo vingi vya kifo, tunashindwa kumshukuru Mungu kwa uwepo wetu licha ya yale tupambanayo nayo.
Tunastahili kumshukuru Mungu kwa maisha yetu, kisha kumuomba aendelee kutuonesha yaliyo mapenzi yake.
Hivi niandikavyo nakaribia kuelekea hospitali kuona hatua za mwisho za madaktari kuokoa maisha ya binti wa rafiki yangu huyo (hajatimiza hata mwezi mmoja) kabla hawajazima mashine zimsaidiazo kuishi sasa ambazo zimepangwa kuanza kuzimwa takriban masaa mawili kamili yajayo.
KATIKA KILA GUMU TUPITIALO, TUSHUKURU MUNGU NA TUSIKATE TAMAA KABLA HATUJAONA YOTE KWANI KUNA WEEENGI WANAOTAMANI KAMA WANGEKUWA TULIPO SISI PAMOJA NA MATATIZO YETU. Hawawezi na pengine hawatafika tulipo kwani hawana muda wa kuishi.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA NA RUDIO JINGINE..KILA LA KHERI!! MAISHA NA MAFANIKIO/KAPULYA

Tuesday, May 8, 2012

TUMEPUMZIKA SONGEA KIDOGO INATOSHA! SASA NAONA TUENDELEE NA SAFARI YETU !TUNAELEKEA KULE ALIKOZALIWA KAPULYA!!!

 Sio kwingine tena ni hapa:- katika  pichani ni moja ya fukwe bora katika ziwa Nyasa eneo la Lundo. Na ndio alikozaliwa mdada huyu. Ni sehemu nzuri sana kwa kutalii ukitembelea maeneo haya siku moja usikose kutembelea na hapa.
Pomonda jiwe la ajabu lililopo ziwa nyasa.
Hili ni jiwe la Pomonda, moja ya vivutio adimu vya utalii ziwa Nyasa ..Kuna mambo mengi katika nchi yetu ambaye ni mazuri na ya kuvutia ebuliangalia jiwe hili  halafu angalia huo ufukwe hapo juu. Mweee mpaka raha kweli. 

UNAPOJIKUTA UNATAMANI NYUMBANI BASI SI VIBAYA KUANGALIA PICHA ZA NYUMBANI:-SONGEA YETU!!

 Kwa wale wote waliofika Songea Mjini mnajua hapa ni wapi. Au niseme tu hapa ni Songea mjini
Na hapa ni soko kuu la Songea.
Picha hizi zimenikumbusha sana Songea nimepatwa na HAMU ya kuwa Songea hakika nyumbani ni nyumbani. Picha ni picha lakini ni kumbukumbu moja nzuri sana. KARIBUNI SONGEA!! 

Monday, May 7, 2012

KISA CHA WANYASA NA SUTI!!!


Habari za jioni jamani!
Baada ya kuweka hiyo picha ya suti leo, nimetumiwa hiki kisa cha suti cha wanyasa na msomaji pia kaka yangu wa hiari Che Jiah. Nimecheka kweli nikaona si vizuri kucheka peke yangu. Nimeona niweke hapa ili tuvunje mbavu pamoja.Tusinyimane uhondo ..Haya karibuni
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
HAPO ZAMANI WANYASA WALIKUWA HAWAPENDI KUVAA SUTI LAKINI KILA SIKU WALIKUWA WANAMWONA RAIS WAO ENZI HIZO KAMUZU BANDA YEYE ALIPENDA SANA KUVAA SURUALI YAANI KAPTULA YEUPE NA SHATI JEUPE. SIKU MOJA ALIVAA SUTI, SIKU  ALIPOTEMBELEWA NA MALKIA WA UINGEREZA. ENZI HIZO BASI NAE ALIVAA SUTI AKAPENDEZA SANA. HIVYO TOKA SIKU HIYO WANYASA WALIKUWA TAYARI KUVAA SHATI LAZIMA TAI NA SUTI. IKIBIDI HATA KAMA SUTI IMECHANIKA, LAIZIMA ATINGE TAI TUU. NA MPAKA LEO UKIENDA MALAWI HUU NDIYO MVAO WAO
KWAHERI!
CHE JIAH.

TUIANZE JUMATATU HII KIHIVI:- KAPULYA AKIWA NDANI YA SUTI KWA MARA YA KWANZAKATIKA MAISHA YAKE!!!

Vipi mbona umenuna mama au hupendi ?
Ah! wewe nawe haya ngoja basi nitabasamu kidogo:-)
Kama wasemavyo watu MTU UNAISHI MARA MOJA basi jana jioni nikaona kwanini nisijaribu kuvaa suti na kuina naonekana vipi ndani ya suti.  Hakika ilikuwa kichekesho kwelikweli kama uonavyo katika picha ilikuwa mara ya kwanza na mara ya mwisho...Au? HAYA JUMATATU NJEMA JAMANI.

Sunday, May 6, 2012

JUMAPILI :- LEO TUANGALIA NENO UZINZI!!

Uzinzi ni kinyume cha mpango wa Mungu kuhusu mapendo ya kibinadamu na ndoa. Kwa sababu hiyo, Uzinzi ulikatazwa kabisa katika Taifa la mungu. Kutoka 20:14,17 inaeleza amri ya Mungu
Usizini;
Usitamani mke wa mwenzako.
JUMAPILI NJEMA KWA KILA ATAKAYEPITA HAPA:-)

Saturday, May 5, 2012

HUU NDIO MLO WANGU WA JIONI HII YA LEO KARIBUNI!!!....

..NI kuku TANDORI kwa chips (viazi) pia kachumbali kwa mbaliiiii. Msiwe na wasiwasi kuna zaidi kwa hiyo anayejisikia kuja KARIBU SANA:-) JIONI NJEMA YA JUMAMOSI YA LEO!!!

JINSI YA KUTENGENEZA CHAPATI..


Kuna msomaji wa Maisha na Mafanikio aliniomba kujua jinsi ya kutengeza "recipe" ya chapati . Maana kila yeye anapojaribu huwa haziwi kama atakavyo yaani laini. Ndugu msomaji naokuomba jaribu kufanya kama hapa kwenye hii video. Mie nimejaribu na nimefaulu tena leo asubuhi ndo ulikuwa mlo wangu kwa chai. NAKUTAKIE KILA LA KHERI NAJUA UTAWEZA NA UTAFURAHIA. JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE ....

LEO IMETIMIA MIAKA MITANO TANGU HAYATI MUNGA TEHENAN AFARIKI DUNIA!!

Tutakukumbuka daima kwa kazi zakoambazo wengi wamepata manufaa kuanzia vitabu vyako binafsi nimevisoma viwili ambavyo ni MAISHA NA MAFANIKIO NA MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA NA BILA KUSAHAUGAZETI LA JITAMBUE

SAYANSI YAKIRI BINADAMU HAFI, HUBADILIKA.


Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho.
Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona.

Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine.

Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu.
Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.

Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.
Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.

Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa.
Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili.

Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo.

Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika.
Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi.

Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo.

Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Habari hii nimeipata katika gazeti la Jitambue la huko nyumbani Tanzania, ambalo siku hizi halichapishwi tena baada mmiliki wake Munga Tehenan kufariki dunia. Na leo ni miaka mitano tangu Munga auache mwili wake. Nimeona tumuenzi kwa njia hii. SISI TUNAKUPENDA LAKINI MUNGU ANAKUPENDA ZAIDI TUTAKUKUMBUKA DAIMA. UATAREHE MAHALI PEMA DAIMA AMINA.

Friday, May 4, 2012

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA PICHA YA WIKI :- JE? HUU NI UBUNIFU AU?

Nimetumiwa picha hii na msomaji wa Maisha na Mafanikio kwanza nikashikwa na butwaa, na pili nikajiuliza ni ubunifu? Na tatu nikajiuliza kukosa mtu wa kumtunza mtoto au chekechea? Nawaachia mwenzangu tusaidiana kujadili hapa...Duh! ila sidhali kama mtoto huyo anapata raha hapo.....MCHANA MWEMA MAJEMANI!!!

IJUMAA YA LEO TUANGALIE:- MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!

Hata kama mtu ni mwerevu, huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda mrefu. Siku moja utagunduliwa, kwa sababu "siku za mwizi ni arobaini" au "habari za uwongo zina ncha saba"
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NA MWISHO MWEMA WA WIKI!!!!

Thursday, May 3, 2012

MTU NA MAZINGIRA:- MAMBO AMBAYO NIYAPENDAYO KATIKA MSIMU HUU NI BUSTANI YA MAUA NA BUSTANI YA MBOGAMBOGA!!!

 Kwa hiyo mkiona sionekani hapa basi nipo nje naongea na maua yangu. maua haya leo nimeyapatia kulikuwa na jua kwa hiyo mchana yanachanua ikifika jiona/jua lizamapo nayo hufifia. Jina sijui ...nitatafuta nikijua nitawajuza....
 Hapa napo hili ua rangi zake nazipenda sana ila nalo jina sijui kwa kiswahili ila kiswidi ni (RÖDVIVA/GULLVIVA)
Na haya hapa nilipanda mwaka jana mwezi wa kumi na sasa yapo hivi ni yanaitwa(Tulpaner) mmmhh itabidi nijifunze kwa kiswahili...Bustani ya mboga bado sijaanza kwani bado ni baridi kweny udongo....Mija, Rachel, Edna Simon, Kaka S, aahh! na wengine wote nitawajuza itakapokaribia si mnakumbuka  huwa kuna ushirika wa kulima/chama  na baada ya kulima kupiga UGIMBI au mmesahau?...:-)...
.Halafu mwenzenu nina UDHAIFU SANA WA MAWE kuna mawe mengine ni kutoka TZ na sehemu mbalimbali niendako:-) JIONI NJEMA SANA JAMANI NGOJA MIE NIENDELEE kuongea NA MAUA YANGU......pia MAWE.....

EBU ANGALIA HAPA KAAAZI KWELIKWELI MAISHA HAYA JAMANI!!!


Habari/simulizi kama hii niliwahi kusikia wakati ule naishi Madaba/Matetereka kuwa akina mama walikuwa wakienda kilabuni walikuwa wakiwanywesha watoto pia. Kisa walikuwa wanataka watoto wasiwasumbue, maana wakipata pombe basi wanalala...duh! kweli tembeo uone!!! NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA INGAWA KWANGU YAMEIBUKA MASWALI KIBAO KICHWANI BAADA YA KUONA HII HABARI. !!!

IMETOKEA TU KWAMBA NAPENDA SANA MAMBO YA ASILI KAMA UTAMADUNI HUU!!


 Katika ukuaji wangu nimekuwa nikipenda sana kuva urembo uliotengenezwa kiasili  NAPENDA MNO juzi juzi tu tamaduni yangu ya mkononi imekatika nimelia kweli :-(....

....ni hapa chini kulia ila hicho kidani/cha shingoni bado ninacho...ila nitajitahidi kutengeneza au kutafuta mpya:-)

Wednesday, May 2, 2012

KISWAHILI CHETU NA MATUMIZI YA HERUFI!!!!

NIMEIPENDA HII NIMEONA TUENDELE NA HII JUMATANO  YA MARUDIO KIHIVI.....KARIBUNI!!!!

Usahihi ni: Hapauzwi. Utatapeliwa.
Lipo tatizo kubwa kwa baadhi ya watu wa makabila fulani nchini Tanzania kuhusiana na matumizi ya herufi, 'R' na 'L' au 'H' na 'U' katika matamshi na hata kwenye maandishi. Pia, wapo wale ambao hushindwa kutofautisha kati ya herufi 'S' na 'Z' au 'P' na 'B' ama 'V' na 'F' na 'DH' na 'Z' na kadhalika.

Ingawaje kwa maneno mengine huwa si rahisi kupoteza maana kusudiwa, makosa hayo bado huweza kuleta maana tofauti kabisa na iliyokusudiwa, hasa kwa mgeni au mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili.

Kwa mfano, neno 'ukiri' ni tofauti na neno 'ukili' au 'karamu' na 'kalamu'. Vile vile 'kazi' ni tofauti na 'kasi' kama ilivyo 'vuma' ikawa tofauti na 'fuma'. Kadhalika, 'barua' ni tofauti na 'parua' ama 'dhana' na 'zana'.

Matumizi yasiyo sahihi ya maneno hayo humlazimisha msomaji kujua maudhui ya habari kwanza ili kuweza kupata maana kusudiwa. Hii si vyema kwa wageni wanaojifunza lugha tunayojisifia kwayo kuwa ni asili yetu.
Chanzo toka wavuti.
OH! NIMEKUMBUKA  PIA BAADHI YA MAJINA YA MIJI KAMA VILI LILONDO WENGI WANASEMA RIRONDO, PIA RUHUWIKO  WENGI WANASEMA LUHUWIKO NK.

DUNIA HAINA SIRI......MNAIKUMBUKA HII?

Kama kawaida ni kipengele chetu cha JUMATANO YA MARUDIO YA MATUKIO MBALIMBALI  na leo katika kuperuzi nimekutana na hii. na nilipeperuzi ni hapa



Panapo majaliwa tukutane tena JUMATANO IJAYO na MARUDIO MENGINE/JINGINE...MUWE NA WAKATI MZURI WOTE!!!

Tuesday, May 1, 2012

BADO NIPO! NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JUMATATU YANGU MDADA MIMI!!!


 HAPA NI JANA JUMATATU KATIKA KANYUMBA KADOGO KA JOTO(SUMMER HOUSE)
Maji yanaonekana swali lakini baridi kivumbi kwa hiyo......
....nilishindwa kuogelea wala. Jumatatu iliisha vizuri namshukuru Mungu na natumaini nanyi pia mlikuwa na Jumatatu njema.PAMOJA DAIMA NA WOTE MNAPENDWA SANA.