Wednesday, November 30, 2011

SWALI LILILONIKERA KWA MIAKA MINGI!!!

Nimeshindwa kuvumilia mwenzenu, kwani hili jambo/swali limekuwa likinikera miaka sasa.

Ni hivi:- Hivi kwanini mwanamke mjane anweza kuishi peke yake mudamrefu au hata milele bila kuolewa tena na mwanamume mwingine? Maana ukiangalia asilimia kubwa ya wanaume wajane huwa hawaishi muda mrefu peke yao huwaa wanaoa tena.

Nina mfano mmoja, bibi yangu mzaa mama:- Babu alifariki mwaka 1980 na bibi amekuwa mjane mpaka Mwenyezi Mungu alipomchukua 2005. Na mafano mwingine nilionao ni baba mmoja nimfamuye mkewe alifariki 2004 na yeye 2006 tayari alipata mwanamke mwingine na kufunfa naye ndoa 2008.
Je?Hapa ndo kusema wanawake wanawapenda zaidi waume zao/wana uchungu zaidi kuliko wanaume?
NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA SWALA HILI JAMANI... KAPULYA WENU!!!!!

14 comments:

Rachel Siwa said...

Baba yangu kafariki 1994 mpaka Leo mama yangu hajaolewa!

labda wamama wanapenda kupumzika na kuangalia watoto/wajukuu zao vyema wanahisi wakileta NJEMBA nyingine haitakuwa na mapenzi mema kwa familia kwani yupo zaidi kwa MKEWE.

Na wababa labda kuhutaji msaada wa mabo ya ndoa na kusaidiwa kazi za nyumbani kama kupika,kuchota maji na kupenda kulelewa zaidi.
NIMEJARIBU WAPEDWA!!!!!!

Koero Mkundi said...

Da Yasinta hiyo ilikuwa zamani, siku hizi hatulazi damu........ Kwanza wewe mwenyewe ushasema hapo Bibi na sio Binti........LOL

Koero Mkundi said...

Samahani nuimevamia bila kusema hodiiiii..........

Jamani mie ni mgeni hapa nipokeeni, nimewaletea mabumunda........LOL

Najua kuna watu watasema "Karibu mwana mpotevu" Mnikome, akha! mie sio mpotevu nilikuwa uani nakosha vyombo..............LOL

Koero Mkundi said...

Da Yasinta "UYIMWIKI?"

Yasinta Ngonyani said...

Rachel uliyoyasema inawezekana ni kweli ya kwamba akina baba wanahitaji kupata msaada wa kuteka maji, kupika, usafi wa nyumba nk nk. Lakini je haiwezekani kuchukua msaidizi au watoto hawawezi kumsaidia babao?..ni wazo tu

Kaero! kweli ni muda sasa ulikuwa hujaonekana hivyo vyombo vilikuwa kiasi gani?
Ndiyo nimesema bibi yangu ni zamani lakini hata sasa kuna wanawake wanakuwa wajane mbona?
KOERO NENE NINYIMUKA MBENA WANGU:-) KARIBU SANA TENA SANA .

Simon Kitururu said...

Wanawake na wanaume ni tofauti KILIBIDO - na ndume kumbuka ni ndume tu liwezalo kuzaa mpaka uzeeni kuliko ilivyo kwa wanawake ambao ukiacha miaka fulani - mnogeo wa michezo ya chakula cha usiku KIHAMU ipandapo kunatofauti nk.


Na moja ya kisababishacho kuna waaminio sio sahihi kwa mwanaume kuoa mke walinganao miaka ni kutokana na tofauti hizo hata za KILIBIDO /staili za kuzeeka.

Mfumo wa maisha unachangia pia. Kwa mfano mwanamume afanyiwaye kila jambo la nyumbani BONGO anaweza kufa haraka akifiwa na mke au akajikuta kaoa haraka wakati Mwanamume wa KIFINI FInlanda ajifanyiaye yake anaweza wala asifikirie kuoa tokea ujanani na hata akioa akifiwa kuoa wala isiwe ni kitu kimsumbuacho kichwa.

Pia kijamii hasa Afrika kuoa kwa mwanaume hata kuwe ni kwa wake wengi sio bigi DILI ukilinganisha na kuolewa kwa MWANAMKE hasa MZEE. Na ndio maana kuna MDADAZ ziringazo umri ukianza kupitiliza wawezakuta zadaka yoyote tu yule kwenye mazingira yale ambayo MDADA MZEE kuna kijicho fulani hupewa akidaka kidume uzeeni.


Ni kamtazamo tu haka!
Na kumbuka swali gumu hili na jibu kirahisi laweza kuwa halipapasi kona zote likijibiwa kifupi!

Baraka Chibiriti said...

Hili swala ni zito sana; hata mimi huwa najiuliza sana....mimi nafikiri wamama huwa wanapenda sana, hata kama mwenzake katangulia mbele za haki, wanakuwa bado wana mawazo na yeye, sasa ukimwambia aolewe na mwingine inakuwa ishu. Siku moja nilikuwa naongea na Bibi mmoja Kijijini kwangu, kuna mzee mmoja alikuwa akimfuatilia sana/akimtaka...lakini yeye hataki, nikamwuliza huyo Bibi kwasababu gani hamtaki wakati mme wake tayari kashatangulia mbele za haki? na yeye bibi huyu yupo free tu! nilimwuliza au humpendi huyu Jamaa/mzee. Bibi alinijibu; sio kwamba simpendi...bali hata kama mme wangu kafariki lakini bado nampenda sana, na umri huu siwezi kumpenda mwingine. Bibi yule aliongea kwa hisia kubwa sana...kweli niliona bado anampenda mmewe hata kama alikuwa amefariki muda mrefu uliopita. Mimi huwa nafikiri kuwa akina mama wana hisia kali sana katika mambo haya, kushinda sisi wanaume, mwanaume husahau mapema...tena hapo usiombe atokee kimwana kijana anamtaka....anasahau kila kitu na kujivinjali na kimwana kijana....waswahili wanasema - mwanaume hazeeki....kazi kweli kweli!!!!

Anonymous said...

Nina rafiki yangu Mswed, yeye aliniambia alifiwa na mume wake aliyempenda sanasana wakati wa ujana. Hakutaka kuolewa tena na mume mwingine kwani hakupata wakumlinganisha na yule wa mwanzoni. Kazeeka hana mtoto na adai tangia hapo haja.....!!Kweli wanawake tunajua kupenda kwa dhati, ila wababa mmmh!

sam mbogo said...

Hapa ukweli ni kwamba,kwa mwanamke inategemea na umri,na jinsi mwenyewe anavyo taka.mara nyingi kama mwanamke kafiliwa na mumewe na hajavuka miaka hamsini,uwezekano wa kuolewa ni mkubwa kama akiamuwa,na wala hakuna tatizo lolote la kisaikolojia hapo.kumbuka mwana mke wa kitanzania hutafutwa/hutongozwa,hivyo kama hakuna mtu wa kumtokea, na umri pia umeenda bila kusahau na mazingira yaliyo mzunguka anaweza asiolewe.kwa wanaume ikopale huwezi kuuliza niwachache sana wasio taka kuowa, nahii nikutokana na hulka yetu ya kwamba ukitaka unapata labda tu umtakaye asiridhike nawewe,kwa mwanaume kama hakuna matatizo ya afya ,nk niwepesi sana kupata mtu wa kumtunza. kaka s.

Goodman Manyanya Phiri said...

@Simon

Na amini umemsaidia sana huyo dada yetu Kapulya kupata ufumbuzi wa swali lake.

Bila mapana na marefu wacha nami niongezee na hili.

Mwanamke ni shupavu kuliko mwanamume katika masuala ya kujilinda. Na hiyo inatokana na HORMONE nyingi kwa, hasa zile za kuzaa, alienazo mwamke!

Anonymous said...

Mimi ni mjane lakini Yasinta sifikirii kabisa kama kuna mtu mwingine zaidi ya Mungu aliye juu anaweza kuziba pengo la mume wa ujana wangu hata kama maisha yetu hayakuwa mazuri kama kweli uliishi na mwenzio kwa kumpenda na kumheshimu wazo la kuolewa halipo kwanza kuanzisha penzi jipya jamani ni kazi ni lazima kutakuwa na kasoro hapo siku njema!

ray njau said...

18 Na Yehova Mungu akaendelea kusema: “Si vema huyo mwanamume aendelee kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi, awe kikamilisho chake.” 19 Yehova Mungu alikuwa akifanya kutoka katika udongo kila mnyama wa mwituni na kila kiumbe kinachoruka cha mbinguni, naye akaanza kumletea huyo mtu ili aone atawaitaje kila mmoja wao; na jina ambalo huyo mtu aliita kila nafsi hai, kila mmoja, hilo likawa jina lake. 20 Basi huyo mtu alikuwa akiita majina wanyama wote wa kufugwa na viumbe vinavyoruka vya mbinguni na kila mnyama wa mwituni, lakini kwa ajili ya huyo mwanamume hakupatikana msaidizi wa kuwa kikamilisho chake. 21 Kwa hiyo Yehova Mungu akamletea huyo mwanamume usingizi mzito, na alipokuwa akilala, akachukua ubavu wake mmoja na kisha akafunika nyama mahali pake. 22 Na Yehova Mungu akaufanya ubavu ambao alikuwa ameuchukua kutoka kwa mwanamume kuwa mwanamke na kumleta kwa huyo mwanamume.

23 Ndipo huyo mwanamume akasema:
“Mwishowe huyu ni mfupa wa mifupa yangu
Na nyama ya nyama yangu.
Huyu ataitwa Mwanamke,
Kwa sababu huyu alitolewa katika mwanamume.”

24 Hiyo ndiyo sababu mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake nao watakuwa mwili mmoja. 25 Na wote wawili walikuwa uchi, huyo mwanamume na mke wake, lakini hawakuona haya.
YaliyomoSuraInayotanguliaInayofuata
-Mwanzo 2:18-24

emu-three said...

Yamkini zipo nyingi,. kwani wanawake wao wanakuja kuolewa, ni wachache sana wanaoweza kwenda kutafuta mume kuwa unioe....kwahiyo unapofiwa kama mwanamke, utasubiri kuwa huenda atapatikana mwingine, aje anioe, lakini anahitajika kujenga ushawishi...ushawishi wa kukufanya ukubali, kama sipotokea basi ...
Lakini kuna ambao, hawataki tena kuolewa, anatafuta nini tena...hiyo ni hoja mojawapo, na pia `libido'kama alivyosema mkuu, huwezi kulinganisha kati ya mume na mke, mume ni kubwa zaidi...pia hioo ni hoja mojawapo.
Sizani kwamba, kuna mtu kakatazwa kuoewa au kuoa baada ya mmojawapo kufa,

ISSACK CHE JIAH said...

HAYA MIMI LEO NACHANGIA MADA HII
Dada leo mimi nilikuwa nasubiri nione watu wamechangiaje kwani mimi nina baba yangu mama alifariki tangu mwaka 2001 ila kwakweli kuna mmoja alidakia kuwa kwanini asikae bila kuoa kwani nae ana weza kuhudumiwa na wajukuu au watoto wake .SASA mimi nawajulisheni kuwa kwakweli hawa watu wanategemea na muda gani matatatizo yalipowakuta ,mimi baba yetu wakati mama anafariki wote walikuwa wastaafu nikisema hivyo nadhani mtanielewa si kwamba walikuwa wanfanya kazi ya kuajiriwa la, ila ni kuwa tayari mama na baba walikuwa na wajukuu jumla 32 na vitukuu 15 na sisi tupo 9 na kila mmoja ametuacha tupo na familia yake kaoa au kaolewa, hivyo nadhani kwa hapo baba yangu si kuwa alikuwa hana matamanio la kwakweli hapa nipo nae tangu mwaka huu uanze lakini haishi kuniambia anahitaji kurudi kwake sasa ukimuliza unaenda kufanya nini anakueleza kuwa yeye anakazi zake kule kwao ukiangalia ni kazi gani hujuwi, na yeye haoni ,hebu fikiria lakini anakueleza ana kazi zake ,yeye kwakweli mpaka leo hajaoa ila haishi kuwaambia wajukuu zake nipeni kitenge niende nacho kule kijijini ,wakimwuliza wewe kwani unavaa kitenge anawaambia kuna mtu ananichotea maji kule, na kazi kubwa ya watu kama wale kule shamba ni kuwa yeye kwavile ndo analetewa misaada toka sehemu mbalimbali basi anao uwezo wa kuwabadilisha wale wajane wote pale kijijini kila anapomuhitaji ooo hapo burudaniii, wana mtumiaaaa, ujuwe nao wajane wengi hawapendi ile kujidhalilisha kuolewa wanachojivunia ndich hicho kuwa wale wasio na wake basi mechi ni kati ya timu hizo mbili kwa hilo mchezo unakuwa droo wewe utajuwa hawa hawahitaji looo? hapana michezo yao huwezi kuijuwa muda wake ni mpaka ukae nao na kule mashambani wao wanaweza malizana juu kwa juu .ukisema kuwa ati watalelewa na wajukuu hiyo sahau hakuan mjukuu anaweza kumlea bibi au babu hapana na tabu hasa akibaki baba, kwakweli mimi nasema bora abaki mama maana anaweza kujimudu kikazi na hii ndo utakuta kama watu wengine waliochangia kuwa wale wengine wasio na aibu basi wanaamua kuoa mimi nazungumzia kwa wanaume wengi ni wavivu,kilichozaliwa kwa baba yangu kwanza aliku mtemi nikisema mtemi baba alikuwa mkorofi hivyo hamna hata mtu alithubutu kukaa nae mpaka watoto wake mwenyewe walikataa mwisho wake mzee wangu alipatwa matatizo ya macho mpaka muda huu naongea ila hakuna kitu kilicho lala ndiyo maana aishi kuniambia nimrudishe kule alikotoka ili mambo yake akayamalize nadhani yeye pale kijijini ndo dj maana hakuna wazee wengi naye alikuwa handsame wa pale kijijini miaka hiyo ,kwakweli wadau waacheni wazee waliomaliza kazi zao waendelee kula raha zao ila msiwajaji ati kwanini wanaoa hii inategemea na umri na muda Kama nguvu ipo au kama meno iko mwache avunje MIFUPA
ASANTENI SAMAANI KWA MCHANGO MREFU
CHE JIAH