Thursday, May 20, 2010

Ujumbe/kichekesho au sijui kucheza na lugha

Mmasai kaingia hotelini akaagiza chai na mkate. Alipomaliza kunywa akataka ankara (bill) yake. Alipopewa akakuta imeandikwa, Chai shilingi 300 na mkate shiling 200 jumla ikawa shilingi 500. Mmasai akalipa shiling 200, alipoambiwa hela haitoshi, akajibu...ero mimi nalipa mukate na mukate italipa shai. Kwa sababu mimi nakula mukate na mukate nakunywa shai. Akiwa na maana kwamba alikuwa akichovyo mkate kwenye chai na kula kwa hiyo hakunywa chai bali mkate ndio uliokunywa chai......Hii nimetumiwa na rafiki nimecheka sana nikaona tucheke pamoja

11 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

umeifanya siku yangu iwe murua kwa sana tu :-)

Fadhy Mtanga said...

Ha ha haaaaaa!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

JE wewe unachovya au unachovywa?

kuna aina nyingi tu. ulimi na midomo, na south to south

kwangu sio kichekesho ni fumboo

Koero Mkundi said...

Ha ha ha ha ha haaaaaaaaa!!!
Eti mukate italipa shai.....

Bennet said...

MMASAI soda nausa bei gani
MUUZAJI mia tano
MMASAI fungua
MUUZAJI tayari
MMASAI (akitoa hela) sasa pima ya 200
MUUZAJI @#%*&)(????

BLACKMANNEN said...

Dada Yasinta yuko wazi kwa kile kilichomchekesha. Sasa wewe ndugu yangu "kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa" unataka kutuelekza wapi? South to South, una maana kule "bondeni?" "Kwa Madiba?". Angalia usije ukawa unatupeleka taratibu Kagera kwenye shule ya "Katerero", walikochapwa mboko walimu wa kike na Mkuu wa Mkoa.

This Is Black=Blackmannen

SN said...

hahahahaha, hii kali sana! tena ukifikiria sura za hawa ndugu zetu jinsi walivyo siriaazz kwenye mambo ya malipo, lzm ucheke zaidi.

nilidhani visa vya wamasai vimeisha...

Jacob Malihoja said...

Hiyo kali nimeipenda! unataka kucheka tena? ngoja nikupe na hii:

Kuna mama mmoja mlokole aliyekuwa akiishi peke yake .. siku moja alirudi usiku sana amechelewa kwenye mambo ya maombi. Alipofika nyumbani baada ya kujiandaa kulala..kabla ya kulala aliamua kusali kama ilivyo kawaida yake.. aliomba mambo mengi.. ikiwemo kuwaombea wezi, vibaka na majambazi... alisema .. Eee Mungu ondoa hasira za wanadamu..uwaokoe wezi,majambazi, wakabaji na vibaka kutoka katika mikono ya hasira za wananchi.wasiuawe. wananchi wasiwauwe kwa hasira... aliendelea kuangusha sala zake..kuwaombea majambazi na vibaka...

Mara ghafla waliibuka jamaa kutoka uvunguni mwa kitanda chake na maficho mengine na kumwambia .. Asante sana mama..tunakushukuru kwa kutuombea tusiuawe.. sisi tunaondoka na vitu vyako hivyo tunaviacha... mama wa watu alibaki ameduwaa! akamshukuru Mungu.

chib said...

:-)

Unknown said...

MMASAI: Dakitari nasani mimi inaumwa
DAKTARI: Fungua mdomo nikuwekee hiki kipima joto...
(Baada ya dakika mbili Daktari akakitoa kile kipima joto na kukitikisa kabla ya kusoma matokeo..)
MMASAI: Memesa, memesa, memesa.. nafikiria ni nyu modeli ( akiwa na maana kwamba daktari alipoweka ile themometa mdomoni kwake alikuwa anajaribu kuimeza lakini akashindwa na kudhani hiyo dawa ni nyu modeli kwani haimezeki!!

Yasinta Ngonyani said...

kakamrope umenichekesha yaani sina mbavu maana hiyo sikuwahi kuisikia.