Wednesday, January 6, 2010

MAISHA YA MUME,MKE NA WATOTO:- MASWALI YA LEO!!

Hivi ni kwa nini watu wawili wanaopendana wakifunga ndoa wanabadili majina yao ya ukoo au mke anabadili jina lake la ukoo na kuitwa jina la ukoo la mume wake?

Na kwa nini watoto huitwa jina la ukoo wa baba sio la mama?

Nimesoma post ya Kamala ya 7/12-09 yenye kichwa cha habari "Ndoa":- Kwa nini kuzaa watoto?

Amesema watoto sio wa baba wala wa mama. Swali langu ni hivi:- je? kwa nini kwanini baba na mama wachanapo watoto wanabaki kwa baba? Je ni kwasababu wanaitwa jina lake la ukoo au ni kwanini? Nitafurahi kama nikipata majibu kwani nimekuwa nikijiuliza sana na nimeona ni vema mnisaidie.

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

Mambo ya Patriarchy na Matriarchy hayo, nasikia huko India ni mfumo jike tupu, baba hana nafasi kabisa katika familia.

Nahisi na Liberia itafuatia..lol!!

Koero Mkundi said...

Labda tumuulize Kamala, maana kaoa juzi, Je akipata watoto watatumia jila la Lutatinisibwa au la ukoo wa mkewe, bahati mbaya hajatujuza ukoo wa mkewe....LOL

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Da Mija: hivi usukumani si mtoto aweza kuwa na majina ya kwa mjomba na kwa baba?

kwa wazanaki nadhani ni hivo japo mambo yako msobemsobe ambapo kijana aweza kurithi mke wa mjomba akakandamija kuendeleza uzao wa mjomba...:-(

mnadhani kuna umuhimu wa kubadili hiyo trend?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koero, dhana ya majina ya ukoo sijui. natarajia kuwa baba ndiyo. lakini mimi sina neno sana kuhusu majina, sidhani kama mimi namiliki jina lolote kwani yoote nilichaguliwa na kupewa. hata ukoo sikuuchagua, ni bahati mbaya tu.

wife ameishapendekeza majina ya watoto atakaowazaa,mimi sina noma ila sharti jina liwe la kihaya/kinyambo analolijua maana yake na iwe nzuri au la kiswahili. sio la kwenye bible wala koran labda liwe Yesu Kristo

jina la ukoo mimi sijui. kwetu waliniletea za kuleta na mimi nikalegeza kamba ya ukristo, nikabadili jina la mwisho likawa la kwanza na la biblia likabakia alama tu, kwa hiyo naitwa Kamala J Lutatinisibwa

Simon Kitururu said...

Hili swala linategemea tu MILA nad esturi za watu hasa ukifikiria MILA na DESTURI huletwa na baadhi ya maswala yazungukayo jamii ambayo huzaa U- Patriarchy na U-Matrirchy kama alivyosema Da MIJA tukiacha mengine.

Lakini nimekutana na watu wengi tu kutoke TAnzania , Ethiopia, mpaka PERU ambao huchukua jina la ukoo kutoka kwa MAMA. Na kwa rafiki zangu kadhaa Waperu moja ya kasheshe katika kuolewa ilikuwa ni jinsi ya kumgeuza Mume awe na jina la mke.


Kwa kifupi zaidi katika jamii ya sasa JIBU la swali lako Da Yasinta ni Tamaduni, MILA na Desturi zilivyozoeleka na sio jinsi ziletavyo maana ndio kisababishacho kikufikirishacho.

Na jamii ikielewa na kuona JAMBO TOFAUTI NI poa ndio kizaliwacho ni kama uwasikiao akina John WAYNE, Elton JOHN, Nicolas CAGE , au mtoto wa Jon Voight ajulikanaye kama Angelina JOLIE na wengine wengi magharibi kisa tu kupenda jina tofauti kwa mvuto wake waliachana na majina ya UKOO au yote kabisa waliyokuwanayo utotoni.

Kwa mfano huo hapo juu na maana UTAMADUNI , mila na DESTURI za jamii zikikubali jambo usishangae Jina langu lisiwe na UJITA wala UPARE na nikasajili jina langu kuwa ni CHAPATI pepsi kidogo BIn MAHARAGE.

mwandani said...

Haya ni mambo tu ya tamaduni - sie kwetu kulikuwa hakuna surname mpaka hivi karibuni ndio tumeanza mambo ya surname. Kila mtu ana jina lake toka kwa babu au bibi fulani na jina jingine ni la lahaja tu. Ndio maana wakati wa kusalimiana kwetu yanachukua muda mrefu sana kwani mtu lazima aulize jina, apate kujua somo yako alikuwa nani, na wewe ni mtoto wa nani, mama yako katokea wapi, na baba yako ndio yupi...

Huu ugomvi wa majina, katika utamaduni wetu sisi wengine kabla bado mtoto hajazaliwa kuna bibi au babu anakuwa keshatoa jina automatically, na kama umeoa kwenye tamaduni nyingine kazi inakuwa kubwa sana kumfafanulia mkeo. Tena wazee wanasikitika sana ukimnyima jina somoo wao. Suluhisho linakuwa gumu sana hapo.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote kwa kunisaidia na swali hili kidogo nimepata mwanga. Kwa mfano mimi mwenyewe baba na mama yangu wote walikuwa na jina la pili Ngonyani. Kwa hiyo ilikuwa rahisi kwa mama. Fikiria kubadili jina la ukoo na kuitwa jina la ajabu kabisa ambalo hujalizoea duh! mie nimekataa nitaitwa Ngonyani mpaka Mungu ataponiita na hata huku nitaendelea kuitwa Ngonyani. Ahsanteni