Monday, December 14, 2009

Haya ni baadhi ya matatizo ya kuchaguliwa mchumba

Kuna mwanadada mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wasomi sana. Amemaliza chuo hapa mlimani. Wakati alipokuwa chuoni alibahatika kupata mchumba ambaye walikubaliana kuoana. Na walikuwa katika maelewano mazuri katika uchumba wao,

Baada ya uchumba wao huo kuendelea, aliamua kumpeleka kwa wazazi wake na kuwafahamisha kuwa mimi nimepata mtu ambaye naona atanifaa katika maisha yangu. Baada ya kuwafahamisha ishu hiyo, mama wa dada huyo alikubaliana na wazo lake la kutaka kuolewa na huyo mchumba wake lakina upande wa baba yake kulikuwa na shaka. Huyo binti alikuwa karibu sana na baba yake na aligundua kuwa baba yake hataki kukubaliana na wazo lake. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mvulana yule kuondoka, binti alimfuata baba na kuzungumza naye na akasema kwa jinsi nilivyomuona huyo mvulana hakufai. Binti akamwambia si vizuri kumhukumu mtu kwa kumwangalia tu. Mimi nimekuwa naye kwa muda mrefu namfahamu vizuri sina shaka naye. Baba yake bado hakukubaliana na hilo lakini upande wa mama yake hakukuwa na shida.

Uchumba uliendelea na yule mvulana akasema inaonesha baba yako hataki kabisa, lakini nitaumia sana endapo kama bado ataendelea na msimamo wake huo. Ni mtu ambaye nimekuzoea, tumeheshimiana sana. Yule binti akamwambia kila kitu kinawezekana na itawezekana tu.

Siku moja yule binti akiwa katika mizunguko yake ya hapa na pale akiwa mjini, alikutana na kaka mmoja akiwa katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa na mwonekano mzuri sana, lakini cha kushangaza yule kaka baada ya kumwona binti huyu aliduwaa. Baada ya kuduwa kwa kipindi aliamua kumfuata binti na kumsalimia na kumwuuliza kila kitu, na baadaye walianza kuwasiliana mawasiliano ya kawaida kabisa lakini mwanajeshi huyo alikuwa na mawazo tofauti, na ndipo siku moja akamweleza kuwa angetamani siku moja awe mke wake. Yule binti akamwambia hapana, mimi tayari nina mtu wangu na tunaheshimiana sana, akamwambia sawa. Kwa ni watu marafiki alimrudisha mpaka kwao, kumbe lengo lake yule kijana ni kutaka kujua binti anaishi wapi.
Na ndipo siku hiyo yule kijana aliamua kwenda peke yake nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kukutana na baba yake (Baba wa binti). Na ndipo alipozungumza ukweli wa kile alichokiona na lengo lake ni lipi. Na mzee aliweza kumdadisi kijana na kumweleza kila kitu. Kwa wakati huo yule binti pamoja na mama yake walikuwa hawapo na binti aliporudi akamweleza akaelezwa na baba yake kuwa kuna kijana mmoja alikuja yuko hivi na hivi akanieleza kila kitu, nadhani huyo ndiye atakayekufaa. Binti akamwambia hapana, wewe ndiye umemuona na mimi itabidi nimuone. Baadaye yule mjeshi akaja wakazungumza.

Baadaya ya mazunguzo marefu ya hapa na pale yule kijana mjeshi aliamua kuondoka, na kwa kuwa binti hakutaka kukorofishana na baba yake aliamua kukubaliana na mawazo yake na baadaye wakamwita tena kijana huyo mjeshi. Baadaye taratibu zote za kuoana na mjeshi huyo zikafanyika, kisha binti huyo alienda kwa mchumba wake wa kwanza na kumweleza yote yaliyotokea na kumrudishia pete ya uchumba waliyovishana hapo awali. Kijana huyo alisikitika sana kwa uamuzi aliouchukua lakini hakuwa na jinsi aliamua kufuata shinikizo la baba yake. Hatimaye baadaye yule binti aliolewa na mwanajeshi na ndoa ilifungwa kanisani.

Baada ya tu ndoa kinachotokea sasa hivi ni kwamba kosa kidogo tu anaambulia kipigo ambacho hajawahi kukipata, kiasi kwamba inampelekea kumkumbuka yule wa kwanza ambaye walikuwa wakiongea naye kwa utaratibu kabisa.

Ndipo baadaye binti (ambaye sasa ni mke wa mwanajeshi) akamtafuta yule mchumba wake wa kwanza na kumweleza kila kinachotokea. Lakini kijana huyo alijaribu kumweleza namna ya kufanya ili waendelee kuishi vizuiri na mme wake na kuzidi kumwombea ili waishi vizuri.

Kwa wakati huu kijana huyo bado hajaoa na anamweleza binti huyo kuwa itachukuwa muda mrefu kwa sababu kwanza itabidi nikusahau wewe pili nikae chini nitulie tatu nijianze upya hivyo itachukuwa muda sana.

Kikubwa zaidi ni kuwa binti huyo amekubali kuolewa na mwanajeshi kwa shinikizo la baba yake, lakini kinachoendelea ni kwamba kosa dogo tu anaambuliwa kipigo kisicho cha kawaida na kinachomuuma zaidi huyo dada ni kuwa siku walipotoka OUT walienda sehemu ile ile ambayo walikuwa wakienda na mvulana yule wa kwanza na hivyo kuumia zaidi.

Sasa dada huyu anaomba mawazo, ushauri na maoni afanyaje?
Makala hii inataoka Jamii Forum. Nimeona si mbaya kama tutaweza kujadili kwa pamoja hapa kibarazani.

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuchaguliwa mchumba? hiyo kali

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

avumilie tu si aliamua 'kuolewa na babake?'...lol

aende FAJI aonane na akina Kaluse ;>)

Halil Mnzava said...

Kuchaguliwa mchumba siku zote hatima yake ni maisha kama haya.Tatizo ni kwamba maji yameshamwagika......

Yasinta Ngonyani said...

Kamala hii ipo na nimeshuhudia mwenyewe. Ila ni mila za kizamani sana na nilidhani zimepotea lakini naona bado zinaendelea. Kali haswa.

Chacha:-)

Hali Mnzava! Ni kweli lakini kitu kimoaja wanasahanu ni kwamba nani ataishi na yule mchumba maisha yote je ni baba/wazazi au binti?