Tuesday, January 27, 2009

KISWAHILI NI LUGHA YA WATU GANI?

Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi kiswahili ni lugha ya watu gani? Kwani sasa naona watu/nchi nyingi sana wanaongea kiswahili. Na pia nimesikia ya kwamba inasemekana ya kwamba imependekezwa kiswahili kiongewe Afrika nzima.


Swali:- Wenzangu mnafikiri itasaidia nini? Na kwa nini Afrika nzima waongee kiswahili? Wakati kiswahili ni lugha yetu ya TAIFA?.

4 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Kiswahili ni kibantu. hata kama waafrika wote watazungumza lakini kiswahili kia asili yake. TAFUTA

Anonymous said...

kwani english si ni lugha ya taifa ya england lakini kinaongelewa dunia nzima,na kiswahili kina haki ya kuongelewa dunia na si africa tu.

na kitabakia kuwa asili yake na kuzaliwa kwake ni tanzania tu.

ni hayo tu toka kwangu.

Ansbert Ngurumo said...

Kiswahili ni lugha ya kimataifa, kimeshavuka mpaka wa kuitwa lugha ya kundi fulani. Hadi sasa mamia ya mamilioni ya binadamu duniani wanazungumza Kiswahili. Vyuo vikuu zaidi ya 100 maarufu duniani vinafundisha Kiswahili. Ni lugha rasmi (mojawapo) ya lugha za kazi za Umoja wa Afrika - ikiwa pekee yenye mzizi ya Afrika. Umesoma mhadahara wangu kuhusu kublogu kwa Kiswahili? Niliutoa mwaka juzi katika Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini wakati wa kongamano lijulikanalo kama Digital Citizen Indaba, liendeshwalo sambamba na lile la Highway Afrika.

Yasinta Ngonyani said...

karibu kijiweni hapa kaka Ansbert na asante kwa jibu.