Friday, February 15, 2013
IJUMAA..TUSISAHAU TULIKOTOKA...UTAMADUNI WETU!!!
Kwa kawaida huwa napenda kusikiliza mziki ambao sielewi wanasema nini kwangu haina shida..kwa mfano hapa sijui wanasema nini ila nimependa sana na hapa nipo hoi ...najua hata wewe utapenda haya twende pamoja ....IJUMAA NA MWISHO WA WIKI UWE MWEMA KWA WOTE!!!!
Thursday, February 14, 2013
NINATISHIWA UHAI WANGU...EVARIST CHAHALI
Evarist Chahali
JUMAMOSI Februari 2 mwaka huu itabaki katika kumbukumbu zangu kwa muda mrefu, pengine katika uhai wangu wote.Majira ya saa 3 asubuhi nilikurupushwa usingizini na kelele za mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu. Wakati ninajiandaa kwenda kufungua mlango, nikasikia sauti yenye dharura ikisema, “bwana Chahali, polisi hapa, tafadhali fungua mlango.”
Nilichanganyikiwa kwani tangu nifike nchi hii zaidi ya miaka 10 iliyopita sijawahi kufanya kosa lolote au kukwaruzana na vyombo vya dola/sheria. Baada ya kufungua mlango, askari waliovalia kiraia walijitambulisha na kuonyesha vitambulisho vyao. Pia walinisihi kuwa nisiwe na hofu ya kudhani kwamba nimefanya kosa lolote.
Kwa kifupi, walinieleza kuwa wamepewa ujumbe kutoka moja ya taasisi za intelijensia za hapa kuwa kuna tishio la uhakika dhidi ya maisha yangu. Hata hivyo, walieleza kuwa kwa vile wao walipewa tu ujumbe huo na kutakiwa kuuwasilisha kwangu, hawakuwa na maelezo ya ziada. Walisisitiza kuwa nichukue tahadhari muhimu na kunipa maelekezo ya mawasiliano ya dharura.
Kwa vile nilikurupushwa usingizini, awali taarifa hiyo ilionekana kama ndoto iliyokuwa inaendelea hata baada ya kutoka usingizini. Ilinichukua takriban saa tatu kuzinduka kutoka katika mshituko huo, na kutambua uzito wa taarifa niliyopewa na polisi hao.
Nikaamua kwenda kituo kimoja cha polisi kupata ufafanuzi zaidi. Mara baada ya kujitambulisha, mazingira ya namna suala hilo lilivyokuwa likishughulikiwa kituoni hapo lilinipa picha kuwa jambo hilo lina uzito. Kwa kifupi, baada ya kitambo nilipewa ufafanuzi ambao haukutofautiana na maelezo niliyopewa awali na polisi walionitembelea katika makazi yangu.
Kikubwa ni kuwa taarifa hiyo ilionyesha kuwa tishio hilo dhidi ya maisha yangu linatokea huko nyumbani. Swali linaloendelea kunisumbua kichwa ni KWA NINI iwe hivyo.
Wakati si vigumu kwangu kuhisi wahusika wa mpango huo wa kijahili, napata shida kuelewa kwanini wahusika hao watumie fedha za walipakodi kuandaa operesheni ya kutaka kunidhuru ilhali ninaamini kwa asilimia 100 kuwa mimi si tishio kwa usalama wa Taifa letu.
Ndiyo, baadhi ya ninayoandika kwenye makala zangu na tweets zangu huko kwenye mtandao wa kijamii wa twitter yanaweza kuwachukiza baadhi ya watu, lakini kwa hakika kuchukizwa huko si sababu ya kutaka kunidhuru.
Hadi wakati ninaandika makala hii nimekuwa nikiishi kwa tahadhari kubwa. Faraja kubwa kwangu inatokana na sababu tatu za msingi. Kwanza, kwa vile nilizaliwa na kukulia katika familia inayomtanguliza Mungu katika kila jambo, nina imani kubwa kuwa mamlaka pekee kuhusu uhai wangu (yaani kuwa hai au kufa) ni Mungu pekee. Hakuna mwanadamu anayeweza kupora jukumu hilo la Mungu na kufanikiwa kufupisha uhai wa yeyote.
Pili, nina imani kubwa na taasisi za usalama za hapa Uingereza. Kimsingi, wenzetu hawa wanathamini sana usalama na uhai wa binadamu pasi kujali mhusika ni mzaliwa wa hapa au ni ‘mgeni’ kama mimi. Ushauri na sapoti ninayoendelea kupata inanipa matumaini makubwa kuwa nipo kwenye ‘mikono salama.’
Lakini tatu ni ukweli kwamba takriban miaka mitano sasa nimekuwa nikiishi na uelewa kwamba kuna baadhi ya watu huko nyumbani wanaoniona kama kimelea cha maradhi hatari ambacho kikiachwa bila kudhibitiwa kitazua balaa.
Kwa sababu hiyo, tangu wakati huo nimekuwa nikiishi kwa tahadhari japo si kubwa kama hii ninayolazimika kuichukua sasa. Lakini ili uweze kuchukua tahadhari ni lazima uwe na mbinu na ujuzi wa kuchukua tahadhari husika. Kwa bahati nzuri, watu hao wanafahamu fika kuwa nina ujuzi wa kutosha na kuelewa na kumudu fika mbinu za kuishi kwa tahadhari.
Hata hivyo, kumudu mbinu ni suala moja na kuishi kwa kutumia mbinu hizo ni kitu kingine. Si jambo la kupendeza hata kidogo kuishi ukiwa na uelewa kuwa siku moja, mahala fulani unaweza kukumbana na madhara fulani. Lakini kadri unavyolazimika kuishi kwa namna hiyo inakuwa kama sehemu muhimu ya maisha yako, na ndivyo ilivyo kwangu.zaidi soma hapa
Happy Valentines Day/Upendo Daima kwa siku ya wapendanao /Alla Hjärtans Dag
VALENTINES DAY.!!!!
Leo ni Valentineday/siku ya wapendanao/alla hjärtans dag. Sio kama siku zote watu
hawapendani HAPANA bali ni kuhamasisha watu wazidi kupendana . Kwangu mimi ina
maana kubwa kwani nimekuwa mwanaharakati bora wa Upendo kwa jamii haijalishi
nimefika kiwango gani . Nashukuru hata kama sijafika robo. Nakuomba nawe shiriki
kutangaza Upendo Duniani. Upendo ulimwenguni kote! na Heri ya siku ya wapendanao kwa wanablog wooooooooooooote! HAPPY VALENTINES DAY.!!!!
Wednesday, February 13, 2013
UJUMBE WA MCHANA/JIONI YA LEO KUTOKA KWA KAPULYA....
Mapendo/upendo hauonyeshwi/hauonekani kwa macho isipokuwa kwa moyo/kutoka moyoni.Kwa roho yote.
KILA LA KHERI, UPENDO DAIMA!!!
KILA LA KHERI, UPENDO DAIMA!!!
CARDIOLOGY CLINIC AT AGA KHAN
Monday - Friday, 2:00pm - 4:30pm and FREE consultations on Wednesdays and Thursdays.
For Booking / more information call: +255 22 2115151-53 ext 4702.
Tuesday, February 12, 2013
PAPA BENEDICT WA 16 ATANGAZA KUJIUZULU FEB 28 MWAKA HUU 2013!!!
Baba Mtakatifu ameelezea kwamba matatizo
ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu
Jana jioni nilipatwa na mshituko niliposikia katika habari, uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.
Wanawake wenye sura hii hawawezi kumuuwa nyoka akafa….!
Sura hiyo hapo ni ya mwanamke. Bila shaka umeshwahi kukutana na sura kama hii katika maisha yako. Kama hujawahi kukutana nayo huenda kuna siku utakutana nayo. Jaribu kuzingatia mdomo, meno, macho na paji la uso. Zingatia baadaye, sura nzima kwa ujumla.
Mwanamke mwenye sura kama hii ana tabia zifuatazo:
Ni mwanamke mcheshi na anayependa kujichakesha. ni mwanamke ambaye ana uwezo na ufahamu mkubwa kiakili. Anajua sana kujiuliza maswali kabla hajafanya jambo lolote kuhusiana na namna anavyohusiana na watu wengine. Ni mwanamke mvumilivu na mwenye subira kubwa kwa wengine, hasa wanaomhusu.
Nikisema ni mvumilivu na mwenye subira, nina maana kwamba, anapokerwa na mpenzi, ndugu au rafiki, huchukua muda kufanya uamuzi, hakurupuki tu. Hujiuliza maswali ya hekima kabla hajafanya jambo. Lakini ni mwanamke ambaye hawezi kuuwa nyoka akafa. Ina maana kwamba, akitendewa ubaya leo, ataendelea kuukumbuka kwa muda mrefu sana. Hatalipa kisasi, lakini itakuwa ngumu kwake kusahau.
Mwanamke mwenye sura kama hiyo, hakawii kubadilika. Anaweza kuonekana amekata tamaa kabisa katika jambo au mambo fulani, lakini akitiwa nguvu kidogo anabadilika kabisa na kujipa nguvu ya kuweza na akaweza hasa. Mwanamke mwenye sura hii ana juhudi ya kujenga maisha yake kwa kiwango chenye kushangaza. Anapoamua kufanya hivyo, hufanya kweli na hana mzaha na kile anachofanya.
Ni rahisi kwa mwanamke mwenye sura hii kuvunjwa nguvu, lakini sifa moja kubwa kwake itakuwa ni ile hali ya kujiambia kwamba, ana maisha yake. Lakini kuna bahati mbaya kwamba, wanawake wenye sura kama hii, huwa wanaingia kwenye uhusiano wenye mashaka kirahisi. Wanatokea kupenda kama vipofu na kushikwa kirahisi na wanaume ambao wameingia nao katika uhusiano. Huwa wanasaidia sana kama wamempenda mtu na kusaidia huku hufikia hatua ya utumwa na siyo upendo.Wenye sura hii wanavyoonekana sivyo wanavyojibu kwenye ombi la tendo la ndoa. Wanaweza kuonekana kama wako tayari kushiriki tendo la ndoa kwa kuonesha dalili zote muhimu, lakini majibu yakaja tofauti kabisa, hadi mwanaume akashangaa.
Hii inatokana na ucheshi wao, kuwa huru katika kujadili mambo na kuchelea kuwakera wengine. Kwa hali hiyo, huwa wanajenga uadui na wanaume au watu wengine ambao hushindwa kuwaelewa. Uzuri wao mwingine ni kujiamini, kusimama kama wao. Kama nilivyosema, mara nyingi hujihesabu kama wao na sio kama watu wengine. Mara nyingi sana ni watu wasiojali sana wengine wanasema kitu gani juu yao.
Chanzo:- Utambuzi na kujitambua.

Monday, February 11, 2013
JUMATATU HII TUANZA HIVI:-DHULUMA KWA WATOTO YATIMA...
Je huu kweli ni uungwana... tutafakari pamoja..kila la kheri!!
Sunday, February 10, 2013
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU:- LEO NA UJUMBE HUU!!!!
Elimu ni ufunguo wa maisha. Tuwaelimishe watoto wetu tangu wangali wadogo ili tuwajengee maisha bora. Wapate kupendwa na kila mmoja wetu na pia Mungu.
UNAJUA UKIAMBIWA KRISTU NAWE UTAJIBU NINI?.............YEYOTE ATAKAYEPITA HAPA LEO AWE NA JUMAPILI NJEMA SANA.
UNAJUA UKIAMBIWA KRISTU NAWE UTAJIBU NINI?.............YEYOTE ATAKAYEPITA HAPA LEO AWE NA JUMAPILI NJEMA SANA.
Friday, February 8, 2013
MWANADADA NA MIKANDA YAKE..MWANAMTINDO WA WIKI!!
Hapa alianza na mkanda wa kipepeo mwaka 1992 hakika zilipendwa haswaaaaaa.................
.....................akaona ngoja ajaribu na mkanda wa kitaifa si mbaya au??? 2011
,,,,na leo 2013 yupo na mkanda mwingine, inaonekana anapenda sana mikanda huyo dada...ni kweli:-)
nawatakieni IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA WIKI UWE MWENYE FURAHA NA UPENDO KWENU PAMOJA NA MAJIRANI ZENU. TUPO PAMOJA.

Thursday, February 7, 2013
ULIJUA KWAMBA SABABU YA KUWAITA JINA "WAZUNGU" LILITOKANA NA-----
Kuna mzungu aliniuliza maana ya neno mzungu. Nikamwambia haihusiani kabisa na rangi bali inatokana na wale weupe wa kwanza waliofika Afrika na hawakujua wanakwenda wapi, hivyo walikuwa wanazunguka ovyo! Kuna stori nilisimuliwa nikiwa mdogo, kuna kundi la wazungu walifika kijijini. Walikaribishwa vizuri na Chifu wakaondoka. Baada ya wiki mbili wazungu hao hao wakarudi pale kijijini. Chikfu kauliza, "Jamani, hao si ndo tuliwaaga majuzi!" Mzungu kashangaa hakufika popote bali anatembea katika mduara!
Imenukuliwa kutoka kwa Da’Chemi kwenye blogu yake - “SwahiliTime”.
Imenukuliwa kutoka kwa Da’Chemi kwenye blogu yake - “SwahiliTime”.
Tuesday, February 5, 2013
KWA WALE WANYWAJI WA KAHAWA SASA KUNA YA KIKOMBE KIMOJA KIMOJA...MAANA KILA MARA NAONGELEA KUHUSU CHAI KWA VILE MIMI NI MPENZI WA CHAI...
KAHAWA KUTOKA TANZANIA TANICA CAFE NA AFRICAFE KWA KIKOMBE KIMOJA
Hata hivyo sikuweza kuacha bila kusema kuhusu chai....kwa kikombe kimoja kimoja pia. Haya karibuni mchagua ni ipi ikufaayo..mimi nachagua chai:-)
Monday, February 4, 2013
MKE MWEMA NI UTULIVU NA NEEMA.......
KATIKA PITAPITA MTANDAONA NIMEKUTANA NA SHAIRI HILI NIMELIPENDA NI TAMU NA NIKAONA NISIWE MCHOYO NIWEKE HAPA...KARIBUNI
--------------------------------------------------------------------------------------------------
1.Mke mwema utulivu, hili halina Ubishi
Anakutoa machovu, ya kazini kama moshi
Hana chembe ya uvivu, kila kitu hash hashi
Mke mwema utulivu, ndio raha ya dunia.
2. Ni raha juu raha, nyumbani ukibakia
Wala hamna karaha, bashasha hunawiria
Huna haja ya kuhaha, baridi roho hukaa
Mke mwema utulivu, ndio raha ya dunia
3. Kidogo kwake chatosha, hakuna kudangadanga
Na hakuna mshawasha, hata upande wa kanga
Mahaba hunawirisha, japo kibaba cha unga
Mke mwema ni neema, ndio raha ya dunia
4. Na munapoambizana, hukaa na kusikia
Hafanyi hata kuguna, ishara ya kuchukia
Nyuso zina ng'ara sana, na watu huulizana
Mke mwema ni neema, ni fahari ya dunia
5. Na mume awa hakongi, majirani hushangaa
Kwa nini jamaa dingi, a shine na kung'aa
Siri chini ya mtungi, hataki hata umbea
Mke mwema ni neema, ndio pepo ya dunia
6. Na hapendi vijishoga, mara huku mara kule
Na hana muda wa soga, kila siku yuko mbele
Hapendi kuigaiga, kila kitu kwa sumile
Mke mwema rah a sana, kila mtu alijua
7. Na hata kwenye kibanda, mutaishi kwa murua
Na japo kupanda punda, msimamo hushikia
Hakuna kupinda pinda, na nyuma kufikiria
Mke mwema ni neema, mola akikujalia
8. Utulivu huwa moyo, si mali wala magari
Wangapi waliyonayo, kukicha haweshi shari
Asubuhi wenda myayo, usiku kucha ngangari
Mke mwema ni neema, Muume akiwa nayo
9. Tabia haifundishwi, mtu hujengeka nayo
Na mtu hababishwi, hiyo huwa mwenendoyo
Ni vibaya havipishwi, nafsi huwa na choyo
Mke mwema ni neema, kiumbe ukiwa nayo
10. Kukicha yananawiri, miaka nenda ishapita
Wala husikii kwiri, hutembea na kunyata
Shamsham bila shari, wajukuu washapata
Maisha huwa matamu, mke mwema kuwa nae.
11. Na ukipata mkorofi, atakutoa kipara
Kukicha hwishi makofi, na hakuna masikhara
Hugombana na mawifi, ajae humcharara
Mke mwema ni neema, na ni raha ya dunia.

SARESARE MAUA ASIYEJUA KUCHAGUA KABILA YAKE...au???
Unaweza kushona shati pia kama kaka Kitururu alivyofanya si unaona kapendeza mwenyewe......
.....na halafu kama kawaida unaweza kushona gauna kama uonavyo hapa safi kabisa
aise na hapa pia unaona gauni..kitenge kimoja ila tofauti hasa rangi zake kinapendeza kwa kweli ....Jumatatu njema jamani.

Sunday, February 3, 2013
NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA NA IWE YA UTULIVU...
Kucheka hakuna majira, chenye majira ni kulimo. Msemo huu hutufundisha kuwa, mtu anaweza kucheka wakati wowote anapoona kuwa pana haja ya kucheka. Lakini, kilimo kina majira yake.Tusiwe wavivu, tufanye kazi. Mungu atatusaidia. JUMAPILI NJEMA SANA NDUGU ZANGU WAPENDWA.
Friday, February 1, 2013
IJUMAA YA LEO NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WAFANYAKAZI WENZANGU KWA YOTE MEMA NA HASA SIKU HII JINSI WALIVYOIFANYA KUWA SIKU YA FURAHA KWANGU!!!
Leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafanya kazi wenzangu kwa kuikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwa keki ila haipo kwenye piacha na pia haya maua...ingawa ilikuwa tarehe 5/1.tarehe hii nilikuwa nyumbani TZ.Kwa hiyo ilikuwa ilikuwa mshtuko kwangu kidogo maaana siku zilikuwa zimepita. Ni furaha ilioje kuona kuwa kuna watu wanakuthamini, wanakujali na wanakupenda kihivyo. Ahsanteni sana na mwenyezi Mungu awajalia upendo zaidi..
Na hapa ndio wao wafafanyakazi wenzangu isipokuwa katika picha anakosekama mmoja...hawa ni kama familia yangu ya pili..ahsanteni sana.....
Thursday, January 31, 2013
Neno La Leo: Mwaka Ni Kama Noti Ya Elfu Kumi Ya Bongo, Ukiichenji, Inapukutika!
Ndugu zangu,
Leo ni mwisho wa mwezi wa mwaka mpya. Na mwaka ulivyo ni kama noti ya shilingi elfu kumi ya Bongo. Ukiichenji tu, utashangaa inavyopukutika!Ukae sasa ukijua, kuwa kesho ndio Februari Mosi. Hivyo, mwaka mpya wa 2013, kama ilivyo kwa noti elfu kumi, ndio tutakuwa tumeuchenji. Subiri sasa uone siku, wiki na miezi inavyopukitika. Fumba na kufumbua utasikia tumeshaingia Juni tunaelekea Bajeti ya Serikali ya Julai, na ukitoka hapo utafikiri mwaka unateremsha milima ya Kitonga.
Inatukumbusha nini?
Umuhimu wa kupanga mambo yetu. Inahusu muda na matumizi ya muda. Na mwanadamu usipokuwa makini na muda, itakuwa sawa na kisa kile cha mzazi aliyeulizwa na wanawe; " Mbona nguo za Krismasi hatujanunuliwa?"
Mzazi akawajibu wanawe; " Jamani, Krismasi ya mwaka huu imekuja ghafla sana!"
Kana kwamba hakujua, kuwa kwenye kalenda ya mwaka tarehe ya Krismasi imeshawekwa, Desemba 25!
Ndio, Afrika mvua hainyeshi ghafla, huwa kuna dalili zake. Na katika maisha, mambo mengi hayaji ghafla, bali hutukuta tukiwa hatujajiandaa. Jiandae na mwaka unaoanza kupukutika kuanzia kesho, kama noti ya shilingi elfu kumi. Kila la kheri.
Nimetumiwa na kaka Maggid Mjengwa.
POLENI KWA MSIBA DADA MIJA NA WANANDUGU WOTE!!
Mwenzetu mwanablogu Mija Shija juzi amefiwa na mjomba wake mpendwa mzee Moses Tito Kachima (pichani juu)katika hospital ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge Dar es salaam.Kwa habari zaidi mtembelee Mija Shija. Poleni sana, tuko pamoja.
Wednesday, January 30, 2013
LEO TUANGALIA HADITHI: MWENDO WA KINYONGA!!!
Hapo mwanzo, yasemekana kuwa Kinyonga alikuwa na mwendo wa haraka na hata kukimbia kwa kasi kama wanyama wengine. Hakuwa na mwendo wa kusuasua kama tumwonavyo siku hizi. Je, ni kitu gani kilichomfanya Kinyonga awe hivi alivyo?
Siku moja, lilipogwa la mgambo la kuwataka wanyama wote wakusanyike pamoja ili kuwe na mashindano ya kukimbia, wapate kujua ni mnyama gani hodari wa kuchanganya miguu kushinda wengine. Taratibu zilifanyika ili kuweka mambo yote sawa. Siku ya siku ilipowadia, mashindano ya kukimbia yakaanza: Msimamizi wa mashindano alianza kuhesabu: Moja, mbili, tatu! Loo, vumbi likaanza kutimka kutokana na kishindo cha mbio za wanyama wale. Kwa vile mbio zilikuwa za kasi sana, baadhi ya wanyama walioweka vitu mfukono mwao, vikaanza kudondoka, kimoja baada ya kingine. Kinyonga kutokana na ukali wa macho yake, akaviona vitu hivyo. Kadiri mbio zilivyozidi kupamba moto, na ndivyo vitu viliendelea kudondoka. Hatimaye, Kinyonga akashindwa kujizuia. Vitu vile vilimtinga sana. Akabadili uelekeo. Akawapisha wanyama wengine na kujifanya kama vile anakwenda kujisaidia. Kumbe, anarudi nyumba na kuanza kuokota vitu vilivyodondoshwa na wanyama wenzake. Kwa kuwa vitu vile vilikuwa vingi na vilidondoka ovyo ovyo bila mapangilio wowote, Kinyonga alianza kwenda polepole, kwa maringo na makini, ili aweze kuokota vizuri vitu vyote kisiachwe hata kitu kimoja. Alifanya hivyo sio kwa ajili ya kuwarejeshea wale waliopoteza, la hasha, bali kuweka kibindoni, ili vimfae mwenyewe maishani.
"Tamaa mbele, mauti nyuma." Sasa basi, kutokana na tamaa hiyo, alikiona cha mtema kuni. Jamaa tangu siku ile, hadi leo hii, hakuweza tena kutembea haraka wala kukimbia. Akawa "amejitaiti" mwenyewe. Halafu, akawa anabadilika badilika rangi kufuatana na mazingira ya sehemu anayokuwepo ili asije akaonwa na wenye mali zao. Vile vile, anazungusha zungusha macho huku na huko kana alivyofanya siku ili "alipookota" vitu vilinyodondoshwa na wanyama wenzake.
Na Kat.V.A. Ndunguru kutoka gazeti la Mlezi.
Je hadithi hii wewe msomaji inakufundisha nini?

Tuesday, January 29, 2013
MILO AMBAYO NINGEPENDA SIKU YA LEO NILE NI HII HAPA...!!!
Chai ya rangi na ndizi mzuzu za kuchemsha
Mlo kama huu kwangu ni mali sana kuliko chai ya maziwa kwa mikate. Vyakula vyetu kama viazi, mihogo, magimbi na ndizi hakika jamani tuendelee kula kwanza unakula unashiba na halafu vina faida. Karibuni....na mchana...mmmmmhhh
Mchana, Nimekaa hapa naota mlo huu ugali, samaki, chuzi, mbogamboga na kachumbali kidogo bila kusahau pilipili... ila duh naona niishie kula kwa macho tu....au ...na jioni sijui itakuwaje ..hii ndiyo mara nyingi akina mama huwa tunawaza ili familia ipate chakula..tuna kazi kweli kweli......
Monday, January 28, 2013
KWANGU MIMI ILIKUWA NI KAMA NDOTO....!
Jana wakati nipo kazini nilipata nafasi kidogo na kupita hapa kwenye kibaraza cha kaka yangu mzee wa Utambuzi. Nikakutana na kisa hiki hapa kwa kweli kilinigusa sana kiasi kwamba nimeona niweke hapa na wengine msome...haya karibuni.......
...............................................................................................................................................
Hadi leo naona kama ndoto.............!
(Picha haihusiani na habari hii.)
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 wakati huo nikiwa nafanya kazi kwa mtu binafsi, Muasia mmoja. Nakumbuka katika mojawapo ya majukumu yangu, nililazimika kwenda Nairobi nchini Kenya. Nilikwenda huko kikazi na nililazimika kukaa kwa mwezi mmoja. Nilipomaliza kazi ile, niliamua kukaa kama siku tatu zaidi ili kujionea hali ya Kenya ilivyo. Nilizunguka jijini Nairobi na kwenda maeneo ya karibu kama vile Thika, Kinangop na miji mingine iliyo karibu na jiji hilo maarufu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Siku moja wakati natoka kwenye matembezi yangu nje ya jiji hilo la Nairobi, nilikutana na mtu mmoja. Huyu bwana alikuwa anaonekana kuchoka sana, ama kwa kuumwa au kwa njaa. Nilikaa naye kiti kimoja kwenye Matatu, yaani daladala za Kenya. Huyu bwana alikuwa ananitazama mara kwa mara na kujitahidi kutaka kama kutabasamu, ingawa hakumudu sana.

Niliingiwa na huruma na kulazimika kumuuliza kama alikuwa yu mzima wa afya. Alisema anaumwa na hana hata senti tano ya kulipia matibabu yake. Nilimuuliza kama anao ndugu. Alisema hana na familia yake iko mashambani, ambapo haina kitu kabisa. “Nina watoto watatu mmoja amemaliza shule hana kazi na wawili wanasoma, lakini ni kwa mashaka sana, kwani mara nyingi hurudishwa nyumbani kutokana na kukosekana ada.” Aliniambia.
Ilibidi nimchukue yule bwana hadi hospitalini ambapo alichukuliwa vipimo. Aliambiwa arudi kesho yake kuchukua majibu yake. Tuliagana tukutane pale hospitalini kesho yake. Kwa kweli hakuamini kwamba, nilimfikisha hospitalini na kumlipia matibabu. Hakuweza hata kushukuru na nilielewa ni kwa sababu gani. Mshangao ulikuwa ni mkubwa sana kwa upande wake.
Kesho yake alipata majibu yake ambayo yalionyesha kwamba alikuwa na maji kwenye pafu moja pamoja na kifua kikuu. Ilibidi aandikiwe dawa. Hakuwa na fedha kabisa. Ilibidi nitoe fedha zote za matibabu yake. Ilikuwa kama silimia 20 ya pesa zote nilizozipata pale Nairobi kama posho. Lakini hiyo haikunisumbua. Nilikuwa najisikia vizuri kuona angeweza kupona.
Ilibidi niombe ruhusa ya siku saba zaidi ili nikae Nairobi kukagua hali ya yule jamaa. Wakati huo huo nilimwambia kwamba, kama anaweza kumwita mkewe akae naye pale mjini wakati anatibiwa ingekuwa vizuri. Nilimwambia ningemsaidia pesa kidogo za kumwezesha mkewe kukaa naye angalau kwa siku kadhaa. Alikubali na kumwita mkewe. Mkewe alipofika hakuamini kwamba niliweza kumsaidia mumewe vile. Yule mama alilia sana na aliniombea sana kwa kikwao, yaani Kikikuyu kwa majina ya mizimu yote. Nilijisikia furaha kwa namna mke wa jamaa alivyojisikia vizuri kuona mumewe amepata matibabu.
Niliondoka Nairobi siku ya tatu tangu mkewe kuja. Niliwaachia hela kiasi cha shilingi 14,000 za Kenya, ambazo nilimwambia yule mama zingemsaidia kufanyia shughuli yoyote ambayo ageona inafaa. Niliondoka bila hata kuwaachia anuani yangu wala simu yangu. Labda wao walitegemea ningewapa anuani yangu, lakini sikufanya hivyo. Mimi sikuona sababu ya kuwapa kwani, niliwasaidia kama binadamu ambao wanahitaji msaada wangu, siyo ili wanijue au tuwe marafiki.
Hivyo ndivyo nilivyo hata leo. Sijisifu kwa sababu sioni kuwa ni sifa, bali naona kila binadamu angetakiwa kuwa hivyo, ila basi tunazuiwa na choyo ya kufundishwa. Sikuwahi kusoma kuhusu masuala ya kusaidia na kupata furaha wala kumsikia mtu. Tabia hii nilitoka nayo kwetu, niliitoa kwa baba yangu ambaye, alikuwa mtu wa kusaidia sana bila kujali malipo. Hilo nalijua.
Mambo yangu yalienda vizuri hadi mwaka 1994. Mwaka huo nilipoteza kibarua change na hata shughuli zangu zikawa zimepoteza umaarufu kutokana na mabadiliko ya teknolojia. Ilibidi nianze kuhangaika. Kufikia mwaka 1996, nilikuwa hoi bin taabani kiuchumi. Watoto wangu watatu wakawa hawaendi tena shule, hakuna ada. Tulishindwa kulipa kodi ya nyumba, ambapo ilibidi tufukuzwe na kwenda kuishi kwa ndugu wa mke wangu. Huyu naye hatukukaa hata mwezi masimango yakaanza. Siwezi kumlaumu, kwani kusaidia siyo jambo rahisi, ingawa naamini ndipo mahali furaha ya binadamu ilipo.
Tulilazimika kuhama na kwenda kuishi Mtoni Kijichi. Huko hatukuwa tumepanga. Jamaa yangu mmoja alikuwa anajenga kule na alikuwa anataka mlinzi, ambapo nilimwambia ningefanya kazi hiyo. Hivyo tukawa tunaishi kwenye kibanda cha mtumishi. Lakini tulihisi nafuu. Hata hivyo watoto wote walisimama shule, kwani hata nauli ya kuwapa ili waende shule ilikuwa ni vigumu.
Sunday, January 27, 2013
UJUMBE WA JUMAPILI HII YA NNE YA MWAKA 2013 NI KAMA IFUATAVYO!!
Unapotafakari mema ya Mungu ya leo:-
WASAMEHE WALIOKUKOSEA,
WAKUMBUKE WALIOKUSAHAU na UILINDE AMANI YA MOYO ISIPOTEE.
Kwani utakuwa na furaha daima!!!
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!
WASAMEHE WALIOKUKOSEA,
WAKUMBUKE WALIOKUSAHAU na UILINDE AMANI YA MOYO ISIPOTEE.
Kwani utakuwa na furaha daima!!!
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!
Friday, January 25, 2013
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA KWA WIMBO HUU:- MOYO WA SUBIRA NA LINEX!!!!
IJUMAA NJEMA JAMANI ...TUWE NA MOYO WA SUBIRA HATA KAMA TUMEUMIA/UMIZWA....KAPULYA
Thursday, January 24, 2013
HABARI YA KUSIKITISHA SONGEA:- MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA SONGEA BOYS AJINYONGA
MWANAFUNZI wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea mkoani Ruvuma amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwenye mti uliopo kandokando ya njia kwenye eneo la milima ya matogoro ya hifadhi ya msitu ya taifa nje kidogo ya manispaa ya Songea.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi alisema kuwa tukio hilo lilitokea januari 21 mwaka huu majira ya 12.30 asubuhi huko katika eneo la milima ya matogoro
Kaimu kamanda Chiposi alimtaja mwanafunzi huyo aliyekutwa amekufa baada ya kujinyonga kuwa ni Ahabu Richard Ng’ondya (21) wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea ambapo alidai kuwa siku hiyo ya tukio watoto wawili ambao walikuwa wakipita njianimajira ya saa za asubuhi ghafla waliona kama kuna mtu ananing’inia kwenye mti mrefu ambao upo kandokando ya njia hiyo.
Watoto hao baada ya kuona hali hiyo walikimbia na kukutana na mtu aliyejulikana kwa jina la Osward Kahongo walimwonyesha tukio hilo ambaye nae pia aliwasiliana na polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari.
Alisema baada ya polisi kufanya uchunguzi ulibaini kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Songea ambaye anadaiwa aliondoka kwenye eneo la shule katika mazingira ya kutoroka siku chache kabla ya kutokea tukio hilo.
Alibainisha zaidi kuwa upelelezi wa awali wa polisi umebaini kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mwanafunzi huyo ni kwamba alikuwa amefukuzwa shule na uongozi wa shule baada ya kutofanya mitihani ya majaribio hivyo uongozi wa shule ulimtaka arudi nyumbani kwao Matamba Uwanji wilaya ya Makete mkoani Njombe ili akamlete mzazi wake.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kuambiwa hivyo mwanafunzi huyo alitoeka kwenye eneo la shule na kwenda kusikojulikana hadi hapo alipokutwa akiwa amekufa kwa kujinyonga, hata hivyo alieleza kuwa mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Matamba Uwanji nyumbani kwa wazazi wake kwa ajili ya mazishi
CHANZO:- Songea yetu.
LEO:- TUSISAHAU VITENDAWILI VYETU/ JE UNAVIKUMBUKA HIVI?
1. Chini chakula, juu chakula, katikati kuni. Nini hicho
2. Nimefika ugenini, ameniamkia mtoto. Mtoto huyu ni nani?
3. Mtu anabadilika badilika
4. Watoto wawili wanapigana kila wakati. Watoto gani hao?
5. Ndege wangu ametagia kwenye miiba. Ndege gani huyyo?
6. Shamba langu nimelima kubwa, nimepanda mbegu zangu tatu: Mbegu hizo ni nini?
7. Mgeni yupo ndani nyumbani, hasemi, mimi simwogopi
8. Nje kukavu, ndani maji. Nini hicho?
9. Nyumba yangu ina nguzo mbili, kama zinaanguka siwezi kuzisimamisha.
10. Nimekata tete, nimevuka mto mkubwa. Tete hili ni nini?
11. Natoka kwa mama, naenda kufa.
12. Ugonjwa wa watu wote ni nini?
NAWATAKIENI KILA LA KHERI KWA KILA JAMBO...!!!!!!!

Subscribe to:
Posts (Atom)