Monday, February 26, 2018
Friday, February 23, 2018
BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA KUMI LEO!!
Mmmmhh! Miaka KUMI leo imefika kama mchezo!!!!
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka kumi (10) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!......Halafu la kufurahisha siku niliyoanza kublog ilikuwa ni JUMAMOSI na leo ni IJUMAA... HAYA IJUMAA IWE NJEMA SANA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE.
Thursday, February 22, 2018
NIMEKUMBUKA KWETU KIJIJINI LUNDO ....
Kwetu kijijini Lundo hata mawese yapo. Tulikuwa tukiyale kama yalivyo:-) Lakini pia hukamuliwa mafuta ni mafuta mazuri sana kwa kupikia vyakula
Tuesday, February 20, 2018
Monday, February 19, 2018
MUNGU AKIAMUA KUFANYA JAMBO ANAFANYA ANAFANYA KWA UKUBWA MPKA WANADAMU WATABAKI WANAULIZANA
Mwanzo mwema wa juma ndungu zangu na uwe mwanzo wa amani na furaha!
Sunday, February 18, 2018
Saturday, February 17, 2018
NAPENDA KUWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA NGAWA HALI YANGU NI DHAIFU KIDOGO!
Ni jumamosi nyingine tena na kapulya leo kapataikana na tumafua kidogo lakini kwa maombi yenu naamini nitakuwa mzima kabla juu halijazama:-) Nawatakieni JUMAMOSI YENYE AMANI NA FURAHA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA.
Thursday, February 15, 2018
TAULO ZA KIKE!...........
NIMEKUTANA NA HII MADA IMENIGUSA SANA EBU KUWA SAMBAMBA NAMI....
LEO nimekumbuka moja kati ya matukio yaliyopata kuniumiza sana hapo zamani. Nakumbuka nilikuwa darasa la sita, Shule ya Mazoezi Mwenge, mkoani Tabora.
Siku hiyo, nikiwa nimeketi dawati la mbele kabisa darasani, lilizuka kama zogo maeneo ya katikati ya darasa; wanafunzi wakawa wamesimama; wengine wakicheka, wengine wakionekana kufadhaika. Kusogea eneo la tukio, nikamwona binti mmoja (jina ninalihifadhi) akiwa ameketi juu ya dawati ilhali wenziye wakiwa wima wamemzunguka.
Nikiwa sijatanabahi juu ya kilichotokea, baadhi ya wasichana wakamwinua mwenzao, kisha wakamfunga sweta kiunoni ili limsitiri sehemu ya nyuma. Aliposimama, ndipo nikaona kilichotokea. Damu ilienea kwenye sketi yake huku nyingine ikibaki kwenye dawati. Wenziye kadhaa wakaungana naye kumsindikiza nje ili kumpa nguvu. Lakini mambo ya kitoto, bila kujua hofu na fadhaa vilivyomuathiri kisaikolojia mwenzetu, baadhi (hususan wavulana) wakawa wakishangilia na kumcheka.
Siku kadhaa zilipita bila msichana yule kurudi shuleni. Baadaye tulikuja kujulishwa kuwa, aligoma kurudi kwa aibu na fadhaa. Alipoteza kabisa hali ya kujiamini, akawa anawataka wazazi wake wamuhamishe shule.
Kimsingi, wanapokuwa katika hali kama hii, watoto wa kike hudhalilika na kufadhaika mno. Na hata wanapowahi kujitambua, bado wanakosa namna bora, yenye heshima na staha katika kujistiri. Inafikia pahala, mtoto wa kike anashindwa kusaidia kazi nyumba na anakosa kwenda shuleni kwa kushindwa kumudu gharama za taulo za kike (pedi) ili kudhibiti hali hiyo na kuwa huru. Kama taifa tunashiriki kumfelisha mtoto wa kike kwa kujua ama kutokujua.
Leo ninapoikumbuka kadhia hiyo, niliyoishuhudia nikiwa mdogo shuleni, nabaki nikistaajabu kusikia ati kuna wanaojiita viongozi, halafu wanazuia na kukwamisha hoja ya kuitaka serikali itoe ruzuku ili wanafunzi wa kike wagawiwe taulo hizo bure mashuleni au walau kwa bei ya chini. Leo hii, imefikia mahala huko vijijini, kwa uhaba wa taulo za kike, mtu akibahatika kuipata anatamani aivae hata mwezi mzima bila kuivua.
Mmnfyuuuuuuuuu
Maundu Mwingizi (MwanaBalagha),
Dar es Salaam.
Wednesday, February 14, 2018
LEO NI SIKU YA WAPENDANAO!
Blog ya Maisha na Mafanikio yapenda kusema ya kwamba yawapenda sana wote ambao mpo bega kwa bega nasi. Nawawote siku hii ya wapendanao iwe yenye furaha na amani pia upendo
Monday, February 12, 2018
Friday, February 9, 2018
TUMALIZE WIKI/JUMA NA PICHA HII...MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWENU WOTE MTAKAOPITA HAPA
KILOSA VIJIJINI
HII PICHA UMENIGUSA SANA. TAFADHALI JAMANI NDUGU ZANGU HAWA WATOTO WANAHITAJI DARAJA
Thursday, February 8, 2018
Wednesday, February 7, 2018
SAFARI HII NILIPOFIKA SONGEA/RUHUWIKO NILIKUTANA NA KITU HIKI
RUHUWIKO HUNT CLUB
Ndugu zanguni ufikapo/ukitembelea Songea usikosa kupitia hii sehemu ni sehemu nzuri kupumzika na kupata chakula kid
CHIPS NA SAMAKI
Monday, February 5, 2018
SIMULIZI; TUSISAHAU TULIPOTOKA
*** Kisa hiki kimenigusa sana na nampenda sana Mama yangu hata kama ameshatangulia mbele za Mungu, hakuna kama mama.....haya ndugu yangu hebu twende sambamba nami**** KARIBU
Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.
Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini.
Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki na yeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.
Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.
Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona mama yake kwani alikuja bila taarifa.
Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.
Binti alimdanganya mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.
Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwa kuwa alikwisha muona mwanae roho yake imetulia kwani hakwenda kukaa pale alikwenda tu kumuona.
Binti alimuacha mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.
Walimkuta mama yake akiwa nje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama asijitambulishe, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.
Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.
Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.
Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yake alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumona akaingia kwenye gari na kuondoka.
*****
Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nje wakati yeye anatoka na gari.
Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa manane lakini mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwaajili yake.
Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia mama yake. Alimtafuta yule kaka ambaye alimleta mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.
Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda polisi na kuanza kumtafuta mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye ya pili ilipita bila kumuona mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.
Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge rafiki yake alisema.
“Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule bibi ambaye tulimkuta kwao jana?”
“Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.
“Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bondaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.
Na mimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale bibi wa watu mpaka polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi bibi wa watu amesha fariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”
Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.
Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.
Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.
Kila siku ilikua akilia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, sasa hivi amefukuzwa kazi. Kahama nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.
Thursday, February 1, 2018
USIMUHUKUMU MTU YEYOTE ...MAANA HUYAJUI MAISHA YAKE
```Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.
Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.
Baada ya kumuona tu, baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”
Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwa kuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!
Hivi ingekuwaje kama mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.
Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu”
“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.
Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa ana furaha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.
Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:
“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwa hiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”
HEKIMA:
1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI
KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.
2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO.```
Nimeitoa mtandaoni nimeiweka hapa kibarazani kwa vile imeniguse sana na pia iwe fundisho kwa wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)