Baada ya kupata chai/kahawa kidogo tukawa tunaongea kuhusu makabila yetu kwa vile mimi nilikuwa nafanya utafiti wa neno MAMA kwa makabila yetu mbalimbali na kwa vile yeye ni MHAYA basi akanisaidia...:-) Ebu niona basi kama umeandika ipasavyo....
...na hapa amechukua karatasi niliyoandika kuangalia kama nimeandika inavyotakiwa......
Hapa kwa pamoja dada Meraby na mimi Mama Maisha na Mafanikio kwa pamoja tunapia orodha ya neno mama kwa makabila mbalimbali:-
Ilikuwa ni siku ya furaha sana katika Kaya yetu. Tuliongea mambo mengi sana hasa kuhusu vyakula na hasa ndizi/matoke....
Monday, February 29, 2016
Sunday, February 28, 2016
NI JUMAPILI YA TATU YA KWARESMA:- UJUMBE... MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO....
Mungu akikuacha katika hali fulani:-
Basi mshukuru wala usilalamike. Kwani yeye ndiye akujuaye zaidi. Pia usidhani kama maisha yamekamilika kwa mtu yeyote.
Kuna mwenye nyumba lakini hana gari, kuna mwenye gari lakini hana watoto, kuna mwenye watoto lakini hana pesa, kuna mwenye pesa lakini hana afya, kuna mwenye afya lakini hana kazi na kuna mwenye vyote lakini hana AMANI wala FURAHA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO. Nami naanza kwa kusema AHSANTE MUNGU KWA KILA JAMBO.
Basi mshukuru wala usilalamike. Kwani yeye ndiye akujuaye zaidi. Pia usidhani kama maisha yamekamilika kwa mtu yeyote.
Kuna mwenye nyumba lakini hana gari, kuna mwenye gari lakini hana watoto, kuna mwenye watoto lakini hana pesa, kuna mwenye pesa lakini hana afya, kuna mwenye afya lakini hana kazi na kuna mwenye vyote lakini hana AMANI wala FURAHA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO. Nami naanza kwa kusema AHSANTE MUNGU KWA KILA JAMBO.
Friday, February 26, 2016
MAPISHI:- HATA SISI TUNAWEZA.....! NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA ...
Nimevitamanije hivi VITUMBUA... haya tulage kwa macho....maana mwenzenu hapa tayari nimekaa na kikombe changu cha chai ....:-(
Thursday, February 25, 2016
LEO TUANGALIA BAADHI YA MAKABILA NCHINI MWETU YASEMAVYO/ITAVYO MAMA...
UTAFITI WANGU KAPULYA:-
Nitaanza na Kabila langu nililozaliwa nalo:-)
1. Kingoni - MAWU
2. Kimanda - MAU/MAWU
3. Kinyasa - AMAWO
4. Kibena - YUVA
5. Kihehe - YUVA
6. Kikinga - UJUVA
7. Kimpoto - AMAU
8. Kinyamwezi - MAYU
9. Kimatengo - AMABO
10. Kinyakyusa - JUUBA
11. Kigogo - YAYAA
12. Kikurya -BHABHA/MAYO
13. Kisukuma - MAAYO
14. Knyiramba - MAU
15. Kifipa - IMAMA/NYIMA
16. Kipare - MCHEKU
17. Kihaya - MAWE/MAE
18. Kisambaa - MNAA/MMAA
19. Kimburu - AYII
20. Kburange- YAYI
21. Kizigua - MAME
22. Kichagga - MAI/MAE
23. Kimasai - YEYO
24. Kipogoro - MAWU
25. Kijita - MAI
26. Kingorema - YAYA
27. Kikisi - MAWHU/MABHU
HUU NI TAFITI WANGU KAPULYA WENU, PIA MAKABILA MENGINE YALIKUWA KICHWANI MWANGU kama kuna yeyote anatambua zaidi TAFADHALI usisite kuandika hapa ili tuweze kujifunza kwa pamoja...ntafurahi kama kutajitokeza kbila jingine...KAPULYA
Nitaanza na Kabila langu nililozaliwa nalo:-)
1. Kingoni - MAWU
2. Kimanda - MAU/MAWU
3. Kinyasa - AMAWO
4. Kibena - YUVA
5. Kihehe - YUVA
6. Kikinga - UJUVA
7. Kimpoto - AMAU
8. Kinyamwezi - MAYU
9. Kimatengo - AMABO
10. Kinyakyusa - JUUBA
11. Kigogo - YAYAA
12. Kikurya -BHABHA/MAYO
13. Kisukuma - MAAYO
14. Knyiramba - MAU
15. Kifipa - IMAMA/NYIMA
16. Kipare - MCHEKU
17. Kihaya - MAWE/MAE
18. Kisambaa - MNAA/MMAA
19. Kimburu - AYII
20. Kburange- YAYI
21. Kizigua - MAME
22. Kichagga - MAI/MAE
23. Kimasai - YEYO
24. Kipogoro - MAWU
25. Kijita - MAI
26. Kingorema - YAYA
27. Kikisi - MAWHU/MABHU
HUU NI TAFITI WANGU KAPULYA WENU, PIA MAKABILA MENGINE YALIKUWA KICHWANI MWANGU kama kuna yeyote anatambua zaidi TAFADHALI usisite kuandika hapa ili tuweze kujifunza kwa pamoja...ntafurahi kama kutajitokeza kbila jingine...KAPULYA
Tuesday, February 23, 2016
BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA NANE /8 LEO :-
MAISHA NA MAFANIKIO INATIMIZA MIAKA NANE LEO NA KWA HIYO WOTE MNAKARIBISHWA NA KIFUNGUA KINYWA KWANZA AMBACHO NI NDIZI ZA KUCHEMSHA KWA CHAI! KARIBUNI TUJUMUIKE.
HAPA NIPO NJOMBE
Mmmmhh! Miaka NANE leo imefika kama mchezo!!!!
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka Nane (8) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!.......... HAYA JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE
Sunday, February 21, 2016
LEO NI KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA BINTI YETU CAMILLA ANATIMIZA MIAKA 18 HONGERA SANA BINTI TEYU....
Mwaka 1998 tarehe 21/2 alizaliwa binti huyu. Ni siku ambayo familia hii haitaweza kusahau. Twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Na twazidi kumwomba amwongoze binti yetu Camilla katika kila akifanyacho ili kiwe vema. Pia twamshukuru Mungu kwa kutuongoza sisi wazazi/walezi katika malezi ya binti Camilla. TWAKUTAKIA SIKU YAKO IWE NJEMA SANA. HONGERA Binti, dada, rafiki, mjukuu nk.
Nyumbani Ruhuwiko 2015...naenda kwa babu kuomba mboga (mandondo) maharage si mnaona eti nimechukua na bakuli yangu kabisa/Poti:-)
Keki nayo haikukosa katika kumbukumbu hii ya leo ya miaka 18....Duh mama sasa najiona ule uzee/utu uzima unazidi kupiga hodi. Haya karibuni tujumuike kumpongeza binti Camilla!!
Saturday, February 20, 2016
UKAGUZI WA SHAMBA 2014 - 2015 ...KAMA MCHEZO LEO TWALA NDIZI, MANANASI NA MATUNDA MENGINE
Kapulya/Mama Maisha na Mafanikio akipita katika moja ya shamba kwa ukaguzi 2014-2015..nyumbani Songea-Ruhuwiko. Hizo ni kazi za mikono yetu mwenyewe!
Hapa nahisi anasema ...EEEhhh wewe acha tu hizi ndizi inabidi kuzitenganisha ili tupate mazao mazuri. NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA KILA LA KHERI NA KWARESMA IWE TULIVU NA YENYE MAOMBI.Friday, February 19, 2016
WANA HATIA GANI? IKUMBUKWE SISI WOTE NI WATOTO WA BABA MMOJA
ALBINA HAWANA HATIA NA SI TOFAUTI NA MIMI NA WEWE NAO WANASTAHILI FURAHA KAMA WEWE, YULE NA MIMI...NAWATAKIENI MWANZO WA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA MWEMA!! IJUMAA NJEMA
Thursday, February 18, 2016
BADO TUENDELEE NA WILAYA YA NYASA HAMU HAIJAISHIA ..BIO CAMP HII IPO KATIKA KIJIJI CHA NDEGERE KARIBUNI SANA...!
Mwenzenu bado nipo Nyasa kwangu...na hapa ni sehemu ya jengo la mapumziko katika ufukwe wa ziwa Nyasa kwenye kijiji cha NDENGERE. Sehemu hiyo ni maarufu kwa jina la BIO CAMP.
Wednesday, February 17, 2016
WOSIA WA BABA KWA BINTI YAKE
Aliyoyasema baba siku moja kabla bintie hajafunga ndoa....
Binti yangu, kuanzia kesho hutakuwa ukiitwa tena jina langu. Utakuwa na furaha kuolewa na mwanaume uliyempenda. Usinikumbuke sana mimi kwasababu nimeshatimiza majukumu yangu. Sasa ni wakati wa kutimiza majukumu yako.
Kuanzia utoto wako, nimekulea vema kwa neema za Mungu. Ila kabla hujasema mbele ya kasisi kuwa unakubali kuolewa ningependa nikueleze kuhusu kuishi na mwanaume na maisha ya ndoa kiujumla.
Unakumbuka ulivyokua umekaribia kufanya mtihani wako wa mwisho wa kidato cha sita? Unakumbuka Ulikuja kwangu na nikakupa Tsh laki moja kwa ajili ya maandalizi ya mtihani? Sawa, ingawa nilikupa mimi, lakini ukweli ni kwamba pesa ile ilikuwa sio yangu.
Najua siku zote ulikua ukijua kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikikulipia ada. Ukweli ni kwamba mimi nilikuwa nimefirisika sina mbele wala nyuma...lakini mama yako alinipa pesa zake. Angeweza kukupa wewe moja kwa moja ila aliamua kunipa mimi kwanza.
Hii inamaanisha nini mwanangu, muunge mkono/msaidie mume wako! Muda mwingine atakuwa kama amechanganyikiwa kutokana na ugumu wa maisha, madeni na vinginevyo ingawa ataonekana yuko sawa ila akilini mwake anayo hofu na majonzi makuu...atahisi hutaweza kumthamini tena kwa vile mambo yamemuendea kombo. Huo ndio muda utakao kubidi kuwa nae bega kwa bega ukimfariji.
Mwanangu njia sahihi ya kumuonesha mume wako kua unampenda ni kumuheshimu, najua inaweza tokea ukabishana nae, ukakwaruzana nae ila mwisho wa siku mwache ajue kuwa heshima yako kwake iko pale pale.
Mwanangu, unakumbuka siku ile nilipomkalipia vibaya sana mama yako? Alifanya nini? Alibaki kimya kabisa. Unakumbuka pia siku ile mama yako alivyonijia juu? Nilifanya nini? Nilibaki kimya kabisa! Binti yangu jifunze kuwa kimya muda mwingine pale mume wako atakapokuwa na hasira. Mmoja kati yenu atakapokuwa na hasira na gadhabu nyingi mmoja lazima atulie kimya. Kama wote mtaanza kupandishiana hasira tatizo hapo ndio huibuka. Na matatizo ya ndoa ndio huanzia hapo.
Mwanangu, kitu cha kwanza kujua kuhusu mume wako ni chakula anachokipenda. Kama anapenda vyakula vya aina nyingi weka katika akili yako. Usiache mpaka aombe chakula siku zote muandalie.
Kuna siku mama yako alinidaka nikiwa nimemshika mwanamke mwingine mkono, hakuwa mchepuko wangu ila ni rafiki yangu niliyepotezana nae kitambo. Mama yako aliponiona hakuanzisha ugomvi na yule mwanamke. Aliondoka kimya kimya.
Nilikuwa na hofu kuu kurudi nyumbani, ningemwambia nini anielewe? Lakini niliporudi nyumbani hakunisema chochote. Aliniandalia chakula mezani kama kawaida. Ila nafsini nilijiona kama nina hatia. Nikaanza kumuomba msamaha.
Kuanzia siku ile sikukaa kumtazama mwanamke wa pembeni mara mbili. Nani anajua? Je kama mama yako angegombana na mimi siku ile, labda ningeondoka nyumbani nakuangukia katika mikono ya mwanamke yeyote tu barabarani akanipoze. Muda mwingine ukimya huleta ufumbuzi mkubwa kuliko ugomvi.
Sahau kuhusu riwaya za mapenzi ulizosoma ulipokuwa shuleni. Unakumbuka filamu za kihindi na za kimarekani? Unakumbuka filamu za kitanzania na Kinaijeria? Unakumbuka tamthiliya za kifilipino? Nyimbo za westlife unazikumbuka? Sahau kabisa hayo mambo mwanangu! Usitegemee vitu ulivyokua ukiviona huko vitakuwepo katika ndoa yako. Maisha halisi ni tofauti na hadithi za kufikirika.
Kitu cha mwisho nachotaka nikuambie... Unakumbuka jinsi ulivyozaliwa? Sijawahi kukwambia! Baada ya ndoa yetu mimi na mama yako mambo yalikuwa magumu. Na mama yako ilimlazimu afanye kazi mbili kusaidia familia. Nami pia nilikuwa nikifanya hivyo.
Tuesday, February 16, 2016
MCHANA WA LEO NIMETAMANI NA KUKUMBUKA MLO HUU WA UGALI WA MHOGO NA MLENDA
Baada ya kukumbuka Lundo kwangu nimejikuta ninatamani na ugali huu wa muhogo na mlenda mweeh yaani utamu wake hauna maelezo kwa mtu asiye wahi kula. Hakika vyakula vya asili vina utamu Wake. Na hasa ukizingatia UGALI WA MUHOGO.... Kwa hiyo basi tulage kwa macho:-(
Monday, February 15, 2016
WIKI HII TUANZE NA KUTEMBELEA ALIKOZALIWA KAPULYA WENU KIJIJI CHA LUNDO/ WILAYA YA NYASA
Hapa ni kilimo cha maksai katika kijiji cha Lundo Wilaya ya Nyasa
Na hapa ni Beach ya BioCamp-Kijiji cha Ndengere Wilaya hiyo hiyo ya Nyasa... yaani nimefurahi, furahi mno kupata tena taaswira ya vijiji hivi Ndengere, Lundo, nk...ni sehemu zangu nilizokulia yaani nimekumbuka mengi sana hasa mlo wa samaki na ugali wa mhugo:-) hapa ndipo nilikotoka...Sunday, February 14, 2016
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SIKU HII YA WAPENDANAO KWANGU. ..KIJANA WETU ALIKUWA NA MECHI NA TIMU YAKE IMESHINDA
Hapo wapo katika mstari tayari kupokea dhahabu ya ushindi
Tayari wamepokea...nilichelewa naona kijana wetu anatoka....
Tayari wamepokea...nilichelewa naona kijana wetu anatoka....
Saturday, February 13, 2016
NAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA IKIFUATANA NA UJUMBE HUU...!
Muwe na JUMAMOSI njema sana na upatapo wasaa mkumbuke ambaye hujamkumbuka kwa muda. Ukizingatia kesho ni SIKU YA WAPENDANAO. JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI...KAPULYA WENU!
Friday, February 12, 2016
MUNGU WANGU...!WATU WANAKIMBIA TOKA NDANI YA PANTONI KUWAHI KATIAKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU....
Picha hii inaonyesha jinsi watu wanavyokimbia toka ndani ya Pantoni kuwahi katika shughuli zao za kila siku jambo ambalo ni hatari katka maisha Yao. Wandugu ni vyema tukajali maisha yetu maana ndiyo yenye thamani zaidi kuliko kazi tunazokimbilia. Kazi utapata nyingine lakini maisha yatapotea milele. MUNGU IBARIKI TANZANIA PIA WABARIKI WATU WAKE! TUNAKUOMBE WIKI HII IISHE SALAMA.
Thursday, February 11, 2016
SONGEA: MPUNGA WATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE!
Pombe inayotokana na mpunga ikiandaliwa kwa kuchemshwa
Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, unasababisha mpunga kutengeneza pombe ya kienyeji.
Pombe hiyo ijulikana kama pombe ya mpunga, inachangwanya kwa mapumba laini ya mpunga, kwa kuyaloweka kwa siku tatu, pia wanachanganya na uji wa ulezi uliolowe kwa kwa siku tatu.
Baada ya kuchanganya inalowekwa kwa siku mbili, siku ya tatu wanaweka unga wa mchele na kuipika katika pipa kubwa kwa masaa matatu, inakuwa imeiva tayari kwa kunywa. Lita moja Tsh. 400, ubovu wa barabara na kukosa soko la zao la mchele unaolima kwa wingi ndio unasababisha mchele huo tutengeneze pombe ya mpunga kwa kujipatia kipato
“Mazao mengi tunalima lakini hakuna barabara ya uhakika kusafirisha mazao mpaka soko kuu la mazao SODECO Songea, unaweka mpunga ndani mpaka unaliwa na wadudu na kuharibika, ukiwa na mpunga inakubidi utengeneze pombe ya mpunga ili usiharibike,” Alisema Emanuel Komba.
Wanakijiji wa Ifinga wanalima mazao ya chakula na biashara lakini wanakwama kufikisha katika soko la mazao SODECO kwa ubovu wa barabara, mazao hayo kama mtama, ufuta, tangawizi, ndizi, ulezi, uwele, mpunga, maharage na miwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Beatrice Msomisi, alikili kuwepo kwa ubovu wa barabara katika kijiji hicho, alisema sio Ifinga tu Vijiji vingi vya Wilaya ya Songea barabara zake ni bovu sana.
Kipindi cha Masika barabara mbalimbali za vijijini hazipitiki kiurahisi kwa sababu ya ubovu, sio mazao tu kuletwa sokoni, hata mgonjwa na kufikisha madawa kwenye Zahanati mbalimbali ni tatizo kubwa.
“Bajeti ninayopewa katika barabara ni ndogo sana napewa Tsh. Milioni 600 kwa mwaka, za kukarabati barabara mbalimbali za vijijini na mjini, pesa ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya ubovu wa barabara hizo na ukubwa wake,” alisema Msomisi.
Milioni 600 tunayopewa kwa ajili ya kukarabati barabara ni ndogo sana ukilinganisha na ubovu wa barabara zenyewe, pesa hiyo ukikarabati barabara kwa kiwango kizuri ikiwa inapitika kipindi cha masika na jua kali unakarabati barabara moja tu. Umbali wakutoka kijijini kwa kutumia gari ni masaa 2 na nusu kwa pikipiki ni masaa 3 hadi 4.
Aidha aliiomba Wizara husika kuwaongezea pesa katika ukarabati wa barabara mbalimbali za Wilaya hiyo, kwa sababu ziko katika hali mbaya sana na kipindi kama cha masika hazipitiki kabisa na kunakuwa hakuna mawasiliano kati ya Vijiji na Wilaya.
Kutoka Ifinga mpaka kufika makao makuu ya Wilaya ya Songea ni kilometa 219, na kilometa 48 ni barabara ya vumbi, Wilaya ya Songea ina ukubwa wa kilometa za mraba 16,000 idadi ya watu kwa sensa ya mwaka huu ni 170,000.
Imeandikwa na Mariam Mkumbaru January 3rd, 2013.
Ahsante kwa makala hii labda niingezee kidogo hapa ni kwamba kijiji hicho pia ni hulima machungwa au walikuwa wanalima machungwa na wwalikuwa wakibadilishana machungwa kwa chumvi kama mtu alikwenda huko na chumvi yake. Nasema hivi kwa vile kuna mtu ambaye yupo karibu sana nami alishafanya hivyo. Walifurahi sana kupata chumvi na yote inatokana na kutokuwa na usafiri/barabara nzuri.
Tuesday, February 9, 2016
NIMEUPENDA UBUNIFU HUU TOFAA KUWA RAMANI YA DUNIA, MAUA KUWA NDEGE NA KANGA KUWA MWAMVULI.....EBU TAZAMA....
Hapa ni tofaa limechongwa hadi kuwatufe la ramani ya dunia.
Na maua nayo yamepangwa vizuri na kutoa picha ya ndege au sijui jogoo. Hii nimeipenda kwa sababu ni ubunifu mzuri kwa kuanza ujasiriamali, maana hili ni pambo tosha kwa nyumba........Hapa sasa ni ubunifu wa mwamvuli wa KANGA..ni ubunifu mzuri hasa kwa nchi za jua kali. Na kama kwa mvua sijui itakuwaje.....KANGA ZINA MATUMIZI MENGI SANA NI UBUNIFU WETU TU.....
Monday, February 8, 2016
JUMATATU HII YA LEO TUANZIA HUKU KUSINI KWA NDUGU ZETU WANGONI..EBU WASIKILIZE....NIPELEYI MWANA WANGU NIPAGATE...
Ni jumatatu nyingine na tupo na ndugu zetu wangoni na huu wimbo NIPELEYI MWANA WANGU NIPAGATE wakimaanisha NIPE MTOTO WANGU NIPAGATE....Yaani hapa nipo hoi kabisa jongeeni tucheze pamoja:-)
Friday, February 5, 2016
CHAGUA LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA WIKI...
Ama kweli haya ndio maisha yetu wengi wetu...tutafika kweli? Najiuliza itabidi ninunue gari mpya kila kukicha kwa mtindo huu...kaaaazi kwelikweliii! mizigo michache ndio msingo harakahara haina baraka !
Thursday, February 4, 2016
SARE SARE MAUA....CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO MWANAMITINDO NDANI YA DASHIKI
Mmmhh! Gauni hili la Dashiki nimelipenda sana lakini.....
.....hili nalo nimelipenda zaidi na ndio likawa chagua langu:-) Hata hivyo natamani yote yangekuwa yangu...Wednesday, February 3, 2016
UJUMBE WA LEO:- MPENDE AKUPENDAYE!
Usimpoteza umpendaye kwa ajili ya unaye mtamani, kwani unaye mtamani anamuwaza ampendaye.... TUDUMISHE UPENDO DAIMA!
Tuesday, February 2, 2016
TUPENDANE, TUSAIDIANE MAANA SISI SOTE NI NDUGU....
Watoto wengi wanatamani kuishi maisha ya furaha na upendo ebu tazama wanavyoishi watoto hawa katika mazingira magumu tuishi kwa kufikiriana kusaidiana. Ebu chukua dakika chache kusikiliza ujumbe wa wimbo huu wa Ben Paul na halafu linganisha na picha hii ya hawa watoto.
TULICHO NACHO TUGAWANE TUACHE UBAHILI SISI SOTE NI NDUGU NA BABA YETU NI MMOJA. UPENDO DAIMA!
Monday, February 1, 2016
NI MWEZI MPYA: NA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUANZA HUU MWEZI KIHIVI:- TUANGALIE MISEMO NA METHALI TOKA TANZANIA NA MAANA YAKE....!
1. Anayetembea huokota, anayekaa huvimba tumbo (Kikerewe)
Maana ya methali hii ni kwamba riziki hupatikana kwa kutafutwa siyo kwa kukaa tu na kusubiri. Methali hii hutumika kwa wale wasiojishughulisha na kwa wale wanaojishughulisha na kufanikiwa kwa kudhihirisha ukweli wa juhudi yao
2. Atembea na moto mgongoni (Kibena)
Maana ya methali hii ni kwamba kama wewe si mkarimu, basi ujitegemee mwenyewe kwa kila kitu popote pale utakapokwenda. Methali hii hutumika kama fundisho kwamba hakuna mtu anayeweza kutenda kila jambo bila msaada wa wenzake Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
3. Penye majani makavu mabichi hayawaki (Kizigua na kinguu)
Maana yake nikuwa penye wazee ni heshima kwa watoto au vijana kuwaachia wazee wakate mashauri; ikiwa vijana watakata shauri mbele ya wazee ni utovu wa adabu. Hutumika kuwaonya watoto wawe na heshima mbele ya wazee hasa katika kusema.
4. Siku hufanana laini hazilingani (Kiha)
Maana ya methali hii ni kuwa kila mtu anayo bahati yake, leo wewe kwsho mwingine. Methali hii hutumika wakati wa kufariji mtu aliyepatwa na maafa.
5. Kichwa cha msitu (Kipare)
Maana yeke, kichwani mwa mtu kuna siri nyingi kama ulivyo msitu mkubwa. Methali hii hutumika wakati wa kuwambia watu kuwa hata kama ukifanya nini, huwezi kuzifahamu siri za mtu. Ni yeye peke yake anayeweza kuzifahamu siri zake mwenyewe. Huweza pia kutumika kwa kuwaonya watu wasiwadharau wengine wanapokuwa kimua kwani huenda wanafikiri mengi kichwani mwao.
6. Kushindwa na kufa ni mapacha (Kimasai)
Ushujaa huheshimiwa sana katika jamii kwa sababu unadumisha ulinzi wa nchi. Ushujaa na ujasiri vikipunguka maadui wa kila aina na dhiki kadha wa kadha husumbua jamii. Mashujaa wakishindwa basi jamii hufadhaika kwani mipango yake yote huvurugika. Methali hii hutumika kama onyo na pia kwa kukaza ujasiri.
7. Leo ni ugali wa kumpigia mbwa kiko cha mkono (Kisukuma)
Maana yake ni kwamba leo tunakula nyama. Mara nyingi Wasukuma hawapendi kumchinja ng`ombe bila sababu maalum. Kwa hivi hutumia mboga za majani kama kitoweo, wapatapo nyama hugawana mikononi wakati wa kula kwa hiyo hutumia kiko cha mkono kumfunza mbwa anayekaribia. Hutumika wakati mtu anapotunukiwa kitu kizuri.
8. Maneno mengi huvunja nyumba (Kichaga)
Maneno mengi nyumbani huvuruga unyumba kwa sababu mwisho wa maneno hayo ni ugomvi uletao mafarakano. Methali hii inatumika kama onyo kwa jamaa, ikiwa kumbusha kwamba maneno mengi ndio chanzo cha kugombana na kukosana.
Naona kwa leo inatosha lakini kama nawe unayo Misemo/methali usisite kuongezea...elimu ni kugawana...TUPO PAMOJA
Maana ya methali hii ni kwamba riziki hupatikana kwa kutafutwa siyo kwa kukaa tu na kusubiri. Methali hii hutumika kwa wale wasiojishughulisha na kwa wale wanaojishughulisha na kufanikiwa kwa kudhihirisha ukweli wa juhudi yao
2. Atembea na moto mgongoni (Kibena)
Maana ya methali hii ni kwamba kama wewe si mkarimu, basi ujitegemee mwenyewe kwa kila kitu popote pale utakapokwenda. Methali hii hutumika kama fundisho kwamba hakuna mtu anayeweza kutenda kila jambo bila msaada wa wenzake Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
3. Penye majani makavu mabichi hayawaki (Kizigua na kinguu)
Maana yake nikuwa penye wazee ni heshima kwa watoto au vijana kuwaachia wazee wakate mashauri; ikiwa vijana watakata shauri mbele ya wazee ni utovu wa adabu. Hutumika kuwaonya watoto wawe na heshima mbele ya wazee hasa katika kusema.
4. Siku hufanana laini hazilingani (Kiha)
Maana ya methali hii ni kuwa kila mtu anayo bahati yake, leo wewe kwsho mwingine. Methali hii hutumika wakati wa kufariji mtu aliyepatwa na maafa.
5. Kichwa cha msitu (Kipare)
Maana yeke, kichwani mwa mtu kuna siri nyingi kama ulivyo msitu mkubwa. Methali hii hutumika wakati wa kuwambia watu kuwa hata kama ukifanya nini, huwezi kuzifahamu siri za mtu. Ni yeye peke yake anayeweza kuzifahamu siri zake mwenyewe. Huweza pia kutumika kwa kuwaonya watu wasiwadharau wengine wanapokuwa kimua kwani huenda wanafikiri mengi kichwani mwao.
6. Kushindwa na kufa ni mapacha (Kimasai)
Ushujaa huheshimiwa sana katika jamii kwa sababu unadumisha ulinzi wa nchi. Ushujaa na ujasiri vikipunguka maadui wa kila aina na dhiki kadha wa kadha husumbua jamii. Mashujaa wakishindwa basi jamii hufadhaika kwani mipango yake yote huvurugika. Methali hii hutumika kama onyo na pia kwa kukaza ujasiri.
7. Leo ni ugali wa kumpigia mbwa kiko cha mkono (Kisukuma)
Maana yake ni kwamba leo tunakula nyama. Mara nyingi Wasukuma hawapendi kumchinja ng`ombe bila sababu maalum. Kwa hivi hutumia mboga za majani kama kitoweo, wapatapo nyama hugawana mikononi wakati wa kula kwa hiyo hutumia kiko cha mkono kumfunza mbwa anayekaribia. Hutumika wakati mtu anapotunukiwa kitu kizuri.
8. Maneno mengi huvunja nyumba (Kichaga)
Maneno mengi nyumbani huvuruga unyumba kwa sababu mwisho wa maneno hayo ni ugomvi uletao mafarakano. Methali hii inatumika kama onyo kwa jamaa, ikiwa kumbusha kwamba maneno mengi ndio chanzo cha kugombana na kukosana.
Naona kwa leo inatosha lakini kama nawe unayo Misemo/methali usisite kuongezea...elimu ni kugawana...TUPO PAMOJA
Subscribe to:
Posts (Atom)