Thursday, January 29, 2015

TUSISAHAU METHELI ZETU:

1. Njaa ni adui, hata mchawi yaua.
2. Haki ya nyani kuona fahari kwa mkia wake
3. Heri yao wazee kujifunga kwa mshipi tumboni.
4. Yu mcheshi machoni moyoni kuna mengine.
5. Binadamu ujikaze, Mungu atakusaidia.
6. Ee mtoto utakutana na watu katili.
7. Yakiteguka mapaja choo hutoka ovyo.
8. Mtoto wa simba sharti naye awe simba.
9. Yu ndugu machoni
10. Fuata maji yanakokwenda.
Methali hizi nimezipata katika kitabu cha SIASA HAPO KALE  ni methali katika hadithi za kingoni. Ambazo zimetafsiriwa kwa kiswahili. Na kwa kingoni nimeweka kwenye blog ya vangoni.blogspot.com.

Tuesday, January 27, 2015

JINSI KAPULYA ALIVYOINASA TASWIRA YA LILONDO....AKINA MAMA WAJASILIAMALI....

Hapa ni Lilondo, huwezi kupita hapa bila kusimama ni kijiji chenye ndizi nyingi sana kama unavyoona akina mama wajasiliamali wanavyochangamka wakati  basi la Super Feo  liliposimama. Kwa hiyo upitapo Lilondo usikose kusimama kununu ndizi... maana kuan kila aina uwezo wako tu..karanga pia. PAMOJA DAIMA!!

Monday, January 26, 2015

TUANZA JUMATATU/WIKI HII NA MSEMO HUU!!!

Kama binadamu, huwezi kamwe kuona aibu kwa kutokubali kosa.  Kwa maneno mengine hii inaweza ikasemwa ya kwamba mtu ana akili leo kuliko jana.
NI MATUMAINI YANGU WIKI IMEANZA VIZURI KWA WOTE!  MWANZO MWEMA WA WIKI.

Saturday, January 24, 2015

JUMAMOSI NJEMA...NIPO NA KAKA ZANGU KATIKA UPANDAJI WA MITI RUHUWIKO/SONGEA 2015 JANUARI

Nipo na kaka zangu tunapanda miti, huu mti niliosimama nao karibu niliupanda mwaka 2013 na sasa umenipita urefu kazi kwelikweli. Kata miti na pia panda miti  kwani ndio uhai.  Huu ndio ujumbe wangu wa leo!JUMAMOSI NA  MWISHO WA JUMA MWEMA!! KAPULYA.

Thursday, January 22, 2015

HOSPITAL YA MBEYA YATEULIWA KUPIMA EBOLA!!


Mbeya. Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), imeteuliwa rasmi kuwa na maabara maalumu ya kuwapima watu watakaohisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa ebola.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Mpoki Ulisubisya alisema hayo jana jioni alipozungumza mambo mbalimbali kuhusu changamoto zinazoikabili hospitali yake.
"Ni kweli Serikali imeiteua maabara yetu ya hospitali kuwa maabara maalumu ya kupima virusi vya ebola nchini na kwa sasa maandalizi yote yanakamilishwa na tutaanza kazi mwishoni mwa mwezi huu au mapema Februari’’ alisema.
Kwa kipindi cha miaka mitano sasa, Maabara ya Hospitali ya Rufaa Mbeya ni maabara ambayo imethibitishwa kimataifa kwa ubora na kwamba vipimo vikitolewa kwenye maabara hiyo vinakubalika hata nchi za Marekani na Uingereza.
Akizungumzia uboreshaji wa utendaji kazi amesema wafanyakazi kupitia kwa viongozi wao kwa sasa wameimarisha utendaji kazi.
Kuhusu chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali hiyo, Ulisubisya amesema Serikali imempata mtu atakayejenga jengo kubwa la kuhifadhi maiti na kuliboresha ili kuendeshwa kwa ubia katika hali ya usafi na kisasa zaidi.
‘’Bila shaka unakumbuka , mfanyakazi wa chumba cha maiti aliwahi kumweleza Waziri kwamba ukifariki dunia ukiwa Mbeya maiti yako italazwa chini. Sasa Serikali imeamua kuchukua hatua ili kuboresha nyumba hizo ingawa wahusika watatakiwa kutoa mchango kidogo’’alisema.
Mapema mwaka jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid wakati huo akiwa Naibu Waziri alitembelea hospitali hiyo ambapo mfanyakazi wa Chumba cha maiti, Vuruga P Vuruga alimweleza kiongozi huyo kwamba maiti zinalazwa mbili mbili kwenye chumba chenye uwezo wa kuhifadhi watu sita.

Vuruga amesema kutokana na kasi ya kufa, hivi sasa maiti zinalazwa chini na kwamba hata Naibu Waziri angefariki akiwa Mbeya ajue maiti yake ingelazwa chini.
CHANZO: MWANANCHI

Tuesday, January 20, 2015

NA ZANZIBA PIA TULIFIKA!!

 PAJE BY KITE ZANZIBAR
Kama kawaida ukifika Zanzibar ni vigumu kuacha kwenda kusuhudia jinsi ndugu zetu walivyoteswa kama watumwa.

Monday, January 19, 2015

KUMBIKUMBI NA DAGAA NYASA ZILIKUWEPO PIA

 KUMBIKUMBI
DAGAA NYASA 
Ilikuwa raha sana kula vyakula hivi kwa kweli ulikuwa wakati mzuri sana 

Sunday, January 18, 2015

JUMAPILI HII YA TATU NAONA WIMBO HUU :- NAMSHUKURU MUNGU UNAFAA.


Nami nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Ahsante Mungu-

Wednesday, January 14, 2015

HII NI KAZI YA MIKONO YETU WENYEWE....UTAKULA ULICHOPANDA.....NYUMBANI SONGEA/RUHUWIKO!!!!

 Tumekuta ndizi tulizopanda zimekomaa na tumezila  hapa ni baadhi tu.....
 ...tuliendelea na mihogo pia nanasi/mananasi.. kazi ya mikono ya kapulya------hatukuishgia hapo
 ....tukayala na maembe maana huu mti upo ndani ya eneo letu yaani tunaumiliki:-)......
----bado tukaendelea na matunda ya  ambayo pia ni kazi ya mikono yetu.."passion"....tutaendelea na picha zaidi...zinakuja:-)

Tuesday, January 13, 2015

TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO

Ni muda mrefu sijafungua barua pepe yangu, kwa vile nilikuwa safarini. Nimefungua nimekuta  hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio, nimeona si vibaya kugawana elimu....karibu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.
Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.
Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”
Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!
Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.
Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu:“Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu” Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu.
“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.
Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.
Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”
HEKIMA:1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.
2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO.

Monday, January 12, 2015

HODI..HODIII....NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU NIMESAFIRI SALAMA NA NIMERUDI TENA SALAMA

KAPULYA KIZIZINI PERAMIHO 2/1/2015
Nachukua nafasi hii kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda katika safari yetu na pia sasa tumerudi salama tena. Pia ahsanteni kwa  sala zenu. Nilikuwa natamani kula nyama ya ngómbe nikaona ngoja nitembelea kizizini  Peramiho kwa wale wanaotokea Songea wanajua ni wapi. Na wewe usiyejua ni njia ya kwenda Peramiho upande wa kushoto kama unatokea Songea.
TUPO PAMOJA ....

Monday, January 5, 2015

KAPULYA ANATIMIZA MIAKA LEO... NI TAREHE NILIYOZALIWA LEO:-)

Leo ni tarehe/siku ambayo familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa na furaha kumpati binti yao ambaye alizaliwa siku hii ya leo. Na leo ameongoza mwaka tena na kuzidi kuzeeka. Lakini hata hivyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...KAPULYA Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama .

Thursday, January 1, 2015

SALAMU KUTOKA SONGEA/RUHUWIKO ...KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2015!!!

MDADA YUPO KATIKA MAOMBI 
Habari zenu jamani!!
Leo ni siku ya kuusheherekea mwaka mpya 2015. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2015 UWE WENYE MAFANIKIO. NAMSHURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA YOTE.. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!  HERI SANA YA MWAKA MPYA 2015!!!