Marafiki wapendwa!Wacha mwaka mpya huu ulete mafanikio, amani, mwanga na furaha ndani ya maisha.....
Nakuombea wewe na familia yako furaha na mafanikio. KATIKA MWAKA MPYA 2012.
KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2012. KAPULYA!!!
Kabla mwaka 2011 haujaisha/haujafikia tamati nimeona picha hii iwe ya kufungia mwaka kwa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO. Pia nachukua nafasi hii kusema mawili matatu kuwa mwaka huu umekuwa na matukio mengi mazuri na mabaya lakini hata hivyo sina budi kusema NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa yote. IJUMAA NJEMA!!!
Akimsimulia rafiki yaka Laila, walipokutana mjini Arusha
Hapa ni baadhi ya wakazi wa spenco Vingunguti wakiwa wamekusanyika kusubiri boti iwaokoe.
Habari zenu jamani!!
Wiki iliyopita niliweka hapa picha ya upupu na baadhi ya wasomaji walisema kwamba ni chakula kitamu sana ingawa unawasha. Lakini nijuavyo mimi picha hii hapa juu ndio huliwa kule kwetu tunaita MANGATUNGU. Chakula hiki inabidi upike kwa makini sana. Kwanza unachemsha kisha unamenya. Na hapo kazi inaanza unachemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi. Sababu ni kwamba inasemekana kuna sumu ndio maana maji ya mwanzo huwa meusi sana . Kwa lugha ya kiingereza huitwa "velvet beans au cowitch beans"...pia inasemekana:- Mangatungu ni dawa kama viagra, ni kahawa, na ni dawa ya kutibu magonjwa ya nerves kama vile Parkinson disease. Kwa habari zaidi soma http://en.wikipedia.org/wiki/Mucuna_pruriens#Uses
Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho. Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona. Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine. Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu. Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo. Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma. Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri. Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali. Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata. Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi. Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule. Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya. Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa. Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo. Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja. Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine. Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko. Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa. Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu. Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miili tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki. Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani. Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa. Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili. Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo. Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika. Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi. Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo. Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Kama kubaka ni hali ya mwanaume au mwanamke kulazimisha kufanya tendo la ndoa bila hiyari ya mwingine, basi wanawake wengi sana walioko kwenye ndoa hubakwa na waume zao kila siku.
Picha ya Babu Blezi Chibiriti, akiwa na mwanae wa mwisho mpendwa wake Fabiani Chibiriti
Nimelipenda swali hili: "Jamaa aliniuliza hivi; Bro hebu nijibu swali hili....au waulize hata wana blog wenzio wa kiume; Ni kweli supu ya pweza huchajisha?
Kaka Mrope pole sana kwa msiba wa mama yetu mzazi kwani naamini mama yako ni mama yetu.Katika pita pita zangu nimekutana na habari hii ya kusikitisha.
Tarehe 26/11/1989 ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya Ngonyani kupata binti mwingine ambaye ni Asifiwe. Ni hisia za ajabu sana mwaka huu bila kumpigia simu na kumtakia HERI kwa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo. Na hii ni sababu kubwa nikaona wiki nzima iwe yake kwa vile imekuwa wiki ya matukio matatu kwa mpigo. Kweli Mwenyezi Mungu ndiye muweza ebu jaribu kuangalia Asifiwe alizaliwa 26/11/1989 siku ya jumapili ,na leo na jumamosi 26/11/2011 ange/ametimiza miaka 22 halafu sasa siku aliyozikwa ni 26/3/2011 siku ya jumamosi tena…HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MDOGO WETU,DADA YETU,MAMA MDOGO WETU, SHEMEJI YETU, PIA RAFIKI YETU. NA USTAREHE KWA AMANI, TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
UA HILI NIMETUMIWA NA KAKA ISSACK CHE JIAH AMBAYE PIA NI MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO. AHSANTE SANA.
Ni mwaka mmoja na siku 24 tangu ilipobandikwa MAKALA HII YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUFANIKISHA UPAUSAJI WA Dada Mdogo Asifiwe Ngonyani. Leo hii NAMSHUKURU MUNGU kwa maisha na mapumziko ya Dada Asifiwe, ambaye aliaga dunia Machi 23 na kuzikwa Machi 26.Dada wa Asifiwe, ni Da Yasinta Ngonyani. Sio bloga mwenzangu tu, bali ndiye anayewasiliana na familia yangu kuliko bloga yeyote. Twawasiliana kwenye chat, kwenye simu na hata skype ambapo huwa tunaongea mara kwa mara.Mara nyingi tumezungumza kuhusu Asifiwe.
Na kila mara alikuwa akitujulisha maendeleo yake. Na kwa kila wakati ambao afya ya Da Asifiwe ilikuwa ikihitaji msaada wa uangalizi wa watabibu, Da Yasinta alikuwa mnyonge. Na nakumbuka siku ambayo alisema hakuweza kuweka bandiko kwenye blogu yake kwa kuwa hakuwa na furaha. Baadae tukawasiliana kuwa ameweza kuongea na Asifiwe na alikuwa na furaha kusika maendeleo yake ni mema.Lakini juma hili, taarifa zimefika kuwa ASIFIWE HATUNAYE. Binafsi niliumia sana. Nilikuwa sijapata kuonana na Asifiwe, lakini mazungumzo juu yake kutoka kwa Dadake na Da Koero yalinifanya kuwa karibu naye kwa namna ya pekee.Lakini kwa wote hawa (Yasinta na Koero), nililogundua ni namna ambavyo FURAHA ZAO ZILIATHIRIWA NA HALI YA ASIFIWE. Kwa maongezi nao, niligundua juu ya maisha yake ambayo ndicho kilikuwa kivutio kikubwa kwa ndugu zangu hawa ambacho ni TABIA. Da Yasinta hakuwa tu akimzungumzia Asifiwe kama ndugu yake ambaye ni wao wawili pekee wa kike katika familia, lakini alikuwa akimzungumzia kama RAFIKI.NA HILI NDILO NILILOJIFUNZA NA NINALOJIFUNA.Ninapomuwaza ASIFIWE, nikimuwaza Dada Yasinta na dugu, jamaa na marafiki wakimlilia, naona AKISI YA MAISHA YA ASIFIWE. Naona jambo ambalo sisi sote twatakiwa kujifunza kutoka kwa Asifiwe, kisha kuona maisha yetu na ya wali walio kwetu yakibadilika.KILIO cha kumlilia Asifiwe ni ishara nyingine kuwa alipendwa, na licha ya kuwa ni KAZI YA MUNGU kumpumzisha baada ya kuyagusa maisha yetu kwa namna alivyoyagusa, bado tungependa kuendelea kuwa naye.Nakumbuka Juni mosi mwaka 2009, NILIBANDIKA MAKALA HAYA KUHUSU KILIO CHANGU KWA MJOMBA WANGU, ambaye nililia kwa kuwa nilimlilia, na katika makala hiyo, niliandika kuhusu kilio cangu kwa mjomba kuwa "nililia kwa kuwa kwa tafsiri yangu, kulia ni kutokubali kuwa wakati wa mjomba kupumzika ulikuwa umefika na hakika alistahili kupumzika baada ya kutenda mema mengi tena kwa mapambano ya hali ya juu. Mjomba alikuwa mtu mwema kwangu na kwa wengi..." Mtu wa kwanza kutoa maoni kwenye bandiko hilo (kama ilivyo kwa mabandiko mengi kwenye blogu nyingi) ni Dada yangu Yasinta ambaye alisema "Mzee wa Changamoto pole sana tena sana. Nalia pamoja nawe kwani nakuelewa kabisa. Na nakushauri lia sana kwani kulia ni moja ya kutoa uchungu wako. Natumanini Mjomba wako yupo nawe kila siku amini. Astarehe kwa amani."Leo hii nami namkumbuka Asifiwe, na licha ya kuwa NAMLILIA, bado nakumbuka kuwa ALISTAHILI KUPUMZIKA na kuwa aligusa maisha ya waliohusiana na kuishi naye na yetu tuliomfahamu kupitia ndugu na marafiki.Lililo kubwa kwetu tuliobaki, ni kuishi maisha sahihi na maisha yaliyo mema. Kama ambavyo aliishi ASIFIWE NGONYANI....Na ndio maana (kama kisemavyo kichwa cha post) namuona "ASIFIWE NGONYANI kama Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu"Chris Rice anasema....COME THOU FOUNT