Wednesday, July 30, 2014

WANAWAKE 280 PERAMIHO/LUNDUSI WAJITOKEZA KUPIMA KWA HIARI!!!

 

Baada ya kusoma habari hii sikuweza kuacha kuisambaza LUNDUSI ni nyumbani  mnajua. Mtu kwao ni furaha kuona wanawake wanajitokeza kwa hiari kwa zoezi hili. Habari yenyewe ndiyo hii hapa chini, karibuni
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
WANAWAKE 280 katika kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma wanahitaji huduma ya kupimwa kwa hiari virusi vya ukimwi ili kutambua afya zao.
Wanawake hao wametoa ombi la kutaka kupimwa virusi vya UKIMWI kwa hiari baada ya kupata elimu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yaliyoendeshwa na shirika la maendeleo ya wanawake Ruvuma RUWODA.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki moja katika vitongoji vya Ringa,Lundusi,Dodoma na Kiburungi vilivyopo katika kijiji cha Lundusi chenye wakazi zaidi ya 2500 ambapo wananchi hao wameweza kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na Radbord Ngonyani ambaye ni mratibu wa shirika la RUWODA.
Kulingana na mratibu huyo wa RUWODA, mada ambazo zimefundishwa katika mafunzo hayo ambayo yalishirikisha jumla ya watu 350 ni pamoja kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCI),ongezeko la vituo vya huduma na wajibu wa jamii katika kuzuia maambukizi.
Mada nyingine ni lishe kwa mtoto aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI toka kwa mama kwenda mtoto,,uwezekano wa mama mjamzito wa kumwambukiza mtoto,namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na uwezo wa mama mjamzito kuzuia maambukizi kwenda kwa mtoto.
Ngonyani amezitaja mada nyingine ambazo zimefundishwa kuwa ni athari za kuishi na virusi vya UKIMWI,mahitaji ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI,wajibu wa jamii katika kuzuia virusi vya UKIMWI na UKIMWI,uaminifu katika mahusiano ya mapenzi na mkakati wa kuhamasisha umuhimu elimu na faida ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mratibu huyo wa RUWODA amefurahishwa na wanawake wa kijiji cha Lundusi kuamua kwa hiari kutaka kupimwa virusi vya UKIMWI ambapo ameahidi kuwasiliana na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea ili kutoa wataalamu wa upimaji waweze kwenda katika kijiji hicho kuwapima wanawake wanaotaka kupima kwa hiari.
“Wananchi waliojitokeza kutaka kupimwa kwa hiari watasaidia serikali kupata takwimu sahihi za maambukizi ya virusi vya UKIMWI na namna ya kuwasaidia watakaobainika kuathirika,tatizo la ,maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado kubwa katika wilaya ya Songea’’,alisema.
Sera ya afya Tanzania ya mwaka 2007 inatamka wazi Serikali inafanya juhudi kubwa kukabiliana na janga la UKIMWI. Hata hivyo, kutokuwepo mwitikio sahihi wa kukabiliana na janga la UKIMWI miongoni mwa wananchi, kunaendelea kuathiri juhudi za kukabiliana na janga hili.
Kulingana na sera hiyo, hali hiyo, inaendelea kuathiri nguvu kazi, kuongeza vifo, yatima, umaskini na gharama za matibabu pamoja na kuathiri ustawi, uchumi na usalama wa taifa.
Kudhibiti maambukizi na ya Virusi vya UKIMWI nchini na kutoa matunzo na tiba ya kupunguza makali ya UKIMWI.Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kukabiliana na janga la UKIMWI katika nyanja zote zikiwemo, kinga, huduma za tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya na majumbani, ili kupunguza athari zinazosababishwa na VVU/UKIMWI.
Kulingana na takwimu za UKIMWI kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Mkoa wa Njombe, Mbeya Iringa na Ruvuma ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.

Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.
Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Kwa mujibu wa takwimu hizo mkoa wa Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzani maambukizi ya Ukimwi yanapungua kwa kasi ndogo.

Hata hivyo shirika la Afya Ulimwenguni WHO limetoa takwimu zinazoonyesha kuwa maambukizi mapya yamepungua kwa asilimia 50 katika nchi 13 za kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1999 inakadiriwa kuwa watu wazima na watoto milioni 33.6 walikuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI na watu milioni 16.3 walikuwa tayari wamefariki dunia katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.
Pamoja na takwimu za shirika la afya duniani kutoa matumaini makubwa kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado nchi za Afrika mashariki zinawajibika kuongeza jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI hasa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pamoja kutoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Tuesday, July 29, 2014

MTU UNAISHI MARA MOJA TU DUNIANI HAPA KWA HIYO UNAPASWA KUJIPA RAHA PALE UPATAPO WASAA NA WALE/YULE UMPENDAYE!!

 Wakati mwingine mtu unapaswa kupumzika kupika ..kwa hiyo mimi na kijana wangu tulitoka nje na hiki chakula nilikula mimi au tusema tuliagiza tofauti na tukawa tunaonja  kipi ni kitamu zaidi
Kama muonavyo nikawa naonja cha kijana"Pizza" huwa sipendi sana  ila nilionja kwa vile naye alionja changu ambacho ni mshikaki  wa nyama ngómbe, viazi na bonge la saladi  bila kusahau cha kuteremshia mimi maji na kijana cocacola. Hapo sijui ni utamu au pozi??? Siku njema

Monday, July 28, 2014

USIWE MWEPESI WA KUHUKUMU MTU KWA KUTAZAMA UMBO LA NJE KABLA HUJAJUA NINI ANATAKA KUFANYA

Katika pitapita zangu kama kawaida nikakutana na hii baada ya kusoma nikaona si mbaya kama nikiiweka hapa maana tusinyimane Elimu na mafunzo katika maisha. Nimeikuta BIDII FORUM....Haya karibu uungane nami kuisoma.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba. Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa...hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo... Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake.. Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake. Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho... Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana. Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!! Lahaula... watu wote wakastaajabu.. mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!! Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!! Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high table na kusema "baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya.." Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema "Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa.. ..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza.." Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late.. MORAL OF THE STORY..! Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana.. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida... kuna vingi vya thamani ndani yako. Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!! JE WEWE UMEJIFUNZA NINI KWENYE STORI HII?

Sunday, July 27, 2014

TUIMALIZIE WIKI HII NA MREMBO HUYU...MWANAMKE WA SHOKA DADA MKUU MSAIDIZI WANGU

 Kanga zina matumizi mengi na hasa ukimpata anayeweza kutumia kama dada yetu hapa. Binafsi nimependwazwa sana na alivyopendeza
Hapa pia safi sana. Picha kwa idhini ya da´Mija...mwanamke wa shoka. JUMAPILI IWE NJEMA SANA KWA WOTE.

Friday, July 25, 2014

MSIONE KUADIMIKA NIPO...PIA NIPO LIKIZO MUDA AMBAO NI MZURI KUWA NA FAMILIA...ILA NIPO!!!!

 Samahani kuadimika  ila nipo  kiaina ....
 ..Nipo likizo na nilikuwa nimejificha hapa na kublog ilikuwa ni kaziii kwelikweli. Nilikuwa na wakati mzuri sana na familia pia baadhi ya marafiki.  katika picha hapo unaona kitu fulani ni wanetu  wapo ziwani kuvua samaki...baada ya muda wakarudi na samaki...
...Na ndo ikawa kazi yangu kumtoa samaki magamba. Kwa vile nimekulia samaki hakuwa kazi kubwa na ngungu kwangu.:-)

Sunday, July 20, 2014

EBU LEO TUANGALIA VITU VYA MSINGI VYA KUTINGATIA KATIKA MAISHA YAKO!!

Katika pitapita kutoa salamu hapa na pele nikakutana na hii  nimeipenda sana na nikaona niiweke na hapa  Maisha na Mafanikio. Nimeipata baada ya kupita hapa. Haya karibuni!!
1. Kuwa karibu na wazazi wako na familia yako pia.
2. Kuwa makini na kila kitu katika maisha yako.
3. Kuwa na kiu ya kuipenda afya yako, kufanya kazi kwa bidii, kula na kuvaaa vyema.
4. Usijihusishe na mambo yasiyo na faida katika maisha yako.
5. Jali thamani yako machoni mwa watu hata kama unapitia katika nyakati ngumu maishani mwako.
6. Usiuabudu umbea.
7. Kuwa makini na marafiki unaowachagua kuwa nao maishani.
8. Usicheze na muda kwa kuamini kesho ipo.
9. Kuwa halisi wakati wa kupanga plan zako na hakikisha kila mara unazipitia kuona kama uko sahihi.
10. Kuwa mwerevu kwa kuishi vyema na jamii inayokuzunguka.
11. Andaa mipango inayoendana na wakati uliopo.
12. Maliza kazi zako kwa muda muafaka.
13. Usilale kwa kuchelewa ukijitetea kuwa unamalizia kazi, panga muda wako kwa kufanya kila jambo kwa wakati wake.
14. Hakikisha unatatua kwa busara, hekima na uvumilivu mkubwa kila tatizo linalokukabili katika maisha yako.
15. Usiwe mtu wa lawama kila mara kwa wakuzungukao.
16. Jitahidi kuwa mtu wa kuyakubali makosa yako na sio kumrushia mwenzako.
17. Heshimu kila anayekuzunguka pamoja na changamoto zao.

Imeletwa kwenu na Fred Kihwele.

Saturday, July 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELE...

 Ni mboga ya maboga na mahindi, ila hasa mboga maboga. Hii imekubali sana na nimeanza kula lakini mchicha na figiri mwaka huu vimekataa kabisa. Hata sijui kwa nini...
 Na hapa ni viazi mviringo na mahidi ...Mahindi nilijaribu tu  yanakaribia kuchanua ila sijui kama nitavuna muhindi. Ila viazi karibu nitavuna kwani sasa vinachanua kwa hiyo mwezi ujao tutakula.
Mwaka huu tutakula na ZABIBU  kama mnavyoona hapa:-)
JUMAMOSI NJEMA BINAFSI NIPO LIKIZO KWA HIVYO MKIONA SIPATIKANI  MJUE  MAJUKUMU. ILA SITAPOTEA SANA MAANA SISI NI NDUGU LAZIMA KUTAKIANA HALI.

Friday, July 18, 2014

UJUMBE WA LEO !!!

Ni kwamba katika maisha ipo hivi: Pale unapowafurahisha  wengine, ndipo furaha yako inazidi kuongezeka. Kwa hiyo pale upatapo nafasi jaribu kumfurahisha labda rafiki, au wale walio karibu nawe.
PAMOJA DAIMA!!!

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA UKIPATA WASAA SIKILIZA KIPANDE HIKI....




Au tu labda tusikiliza na hii pia

MUNGU IBARIJKI AFRIKA YETU..PAMOJA DAIMA . IJUMAA NJEMA

Wednesday, July 16, 2014

WIKI ILIYOPITA JUMATANO YA TAREHE TISA NILIPATA NAFASI KUWA NA WAFANYA KAZI WENZANGU KAMA NILIVYOWAAMBIA....NA HAPA NI BAADHI YA PICHA NYINGINE NA BARO ZAIDI

Nadhani mnakumbuka hapa . Basi leo mfanyakazi mwenzangu naye kumbe alipiga picha . karibu....

 
 Sijui kwa nini napunga mkono hapa. ni mwenyewe Kapulya na Dada AnnSofi
 Kapulya/Yasinta
 AnnSofi na rafiki yangu mpendwa Marlene
Hapa ni Dada Pernilla na Marlene ..meza nayo ilichafuka kiduchu.
NAWATAKIENI JIONI/SIKU/ASUBUHI AU MCHANA NJEMA/MWEMA

Tuesday, July 15, 2014

LEO NINGEPENDA SANA KULA MLO HUU..NDIZI

Nimetamani sana mlo huu...ndizi ila basi tu. Ila si siku nyingi bado nitapika mlo huu na kuula...hasa nikiendaMatetereka nitakula mpaka kushindwa....SIKU NJEMA KWA WOTE!!!

Monday, July 14, 2014

TUANZE JUMATATU HII NA TANGAZO:- CITE SUMMER CONFERENCE 2014

HABARI HII NIMETUMIWA NA DADA RACHEL NAMI NIMEONA SI MBAYA KAMA NIKIIWEKA HAPA  SIKU HII YA LEO.  MWANZO MWEMA WA JUMA.

Sunday, July 13, 2014

TUANZE JUMAPILI HII NA KIKOMBE CHA CHAI...NINYIME VITU VYOTE LAKINI SIO CHAI!!!

You´re Just my Cup of Tea,
Our Love Warms my Heart.
Najua wote mnajua mie ni mpenzi sana wa chai tena ile isiyo na sukari(Chingambu) :-).
BASI NIWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA SANA. UPENDO NA AMANI ITAWALE KATIKA NYUMBA ZETU.

Thursday, July 10, 2014

PALE MNAPOPATA NAFASI YA MARAFIKI/WAFANYAKAZI KUKUTANA NA KUPATA MLO PAMOJA...JANA JUMATANO

 Hapa ni jana tulipata muda wa kukutana na kwenda kupata moja barifdi na chakula kidogo...hapa picha haionyeshi vizuri kulikuwa na jua sana na nilimwomba muhudumu atufotoa kutumia simu...:-)
 Hapa ni chakula nilichokula mimi ni mshikaki wa kondoo na wali wa binzali ...nyanya na majani matatu tu wabahili wa mboga hao....
Na hapa ni chakula alichokula rafiki mmjoa /Elizabeth ni saladi ya kamba yeye hali nyama...ilikuwa tu baadhi ya vyakula  vya wengine sikupiga picha.
KILA LA KHERI

Wednesday, July 9, 2014

LEO TUANGALIE BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA TANZANIA

1. Mtoto wa kwale hapotezi njia yake (Kibena)
2.  Mtoto wa nyoka hukua na sumu yake (Kisambaa)
3. Mtoza ushuru sokoni huvumilia (Kichaga)
4. Mtu hodari husifiwa na watu (Kizigua na kinguu)
5. Mtu si sikio (Kiiraqw)
6. Muwa mmoja haujazi mtungi (Kipare)
7. mvua ya vuli imeanza (Kinyakyusa)
8. Mwanamke ni kambalemamba huamshwa na mkuki  (Kikerewe)
9. Ukiona mishale nyanyo ziko nyuma (Kimasai)
10. Kucheka hakuna majira, chenya majira ni kilimo (Kiha)
11. Tumbo la nguruwe halipasuliwi mbele ya watoto (Kisukuma)
12. Wazee walimtoa nyoka katika pua ya mwene (Kifipa)
KAMA NAWE UNA CHA NYONGEA KARIBU SANA SI MNAJUA  TUPO PAMOJA.....JUMATANO NJEMA SANA KWA WOTE..PANAPO MAJALIWA .  KAPULYA

Tuesday, July 8, 2014

USAFIRI WA BAISKELI NI MZURI NA WA HARAKA PIA NI MZURI KWA KUTUNZA MAZINGIRA...NAWE WATUMIA BAISKELI KAMA KAPULYA?!!!

 Baiskeli yangu imeharibika na imenilazimu kununua mpya
......na hapa ndiyo baiskeli yangu mpya ambayo ina gia 7 . Kama wote tujuavyo baiskeli ni usafiri wa haraka na bila foleni,.....Bahati mbaya hakukuwa na mtu kupiga picha pamoja nami:-)

Sunday, July 6, 2014

JUMAPILI YA LEO NIMEMKUMBUKA SANA MJOMBA WANGU JOHN BOSCO.......JUMAPILI NJEMA

Hapa ilikuwa mwaka 2007 nilipokwenda kumsalimia mjomba wangu ni yeye katikati na huyo mwingine ni kakangu mdogo yaani wa mwisho na bila kusahau huyo mdada ni Kapulya...:-) Hapo ni Lundo/nyasa....JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

Friday, July 4, 2014

NIMETAMANI NYUMBANI RUHUWIKO LEO

HAPA NDIPO KWETU RUHUWIKO ...NA LEO NIMEKUMBUKA MNO KUNYUMBA/NYUMBANI. NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA PIA MWANZO MWEMA WA JUMA...KAPULYA WENU:-)

Thursday, July 3, 2014

BADO TUNA MWENDO MREFU......

Nimeyatamani hayo maembe mno...ila zaidi ni kwamba hawa watoto ilibidi wawe darasani lakini wapo barabarani kutafuta maisha. Hapo ni barabara ya Tunduru Namtumbo…kijiji baada ya Namwinyu!.....picha kwa idhini ya kaka Chacha. Basi niwatakieni siku njema wote najua tupo wengi tunaotamani haya maembe:-)

Wednesday, July 2, 2014

PALE INAPOTOKEA KUPEANA HABARI KUNAPOKOSEKANA NA PALE PANAPOKUWEPO KUPEANA HABARI KWA WANANDOA....

MAISHA YA NDOA YA YOSEFU NA PAULINA...
Walikuwa katika hali ya uchumba kwa mwaka mzima sasa. Kwa muda wa miezi sita walikuwa wakionana karibu kila siku. Lakini baada ya hapa, Yosefu aliondoka kwenda kutafuta kazi nzuri. Mwanzoni alimwandikia barua Paulina mara kwa mara. Lakini muda kidogo, barua zilianza kupungua na zile alizopata Paulina hazikuwa na maneno ambayo alitazamia yawemo. Yusefu aliongelea machache sana kuhusu maisha ya mjini, na alisema kidogo tu kuhusu kazi yake mpya na rafiki zake wa huko.
Paulina alianza kupatwa na wasiwasi, kwa kweli wasiwasi mwingi. Lakini hakumwambia Yosefu. Mwanzoni alikuwa anamwandikia juu ya yale mambo aliyopenda na Yosefu ni mzima na angelikuja kumwona hivi karibuni. Lakini mara aliacha kutaja mambo haya. Aliongea tu juu ya mambo ya kijijini na matukio yaliyotukia hivi karubuni katika parokia yao. Zaidi kuhusu mwenyewe hakusema tena.
Kadri miezi ilivyopita ndivyo moyo wake ulivyozidi kujawa na uchungu na bumbuwazi. Angewezaje kuzungumza juu ya mambo yake binfsi kama Yosefu alikuwa hatilii maanani mambo haya? Bada ya miezi sita Yosefu alirudi nyumbani kwa likizo la majuma matatu. Alishangazwa na hata kushtuka kuona jinsi Paulina alivyokuwa hamjali.






























Wazo na swali kutoka kwa Kapulya wenu:- "Na ndio maana kupeana habari ni muhimu kwani mwenzio hawezi kujua wewe unawaza nini na wewe huwezi kujua wenzio anawaza nini.
Na sasa hata  Yosefu anausikitikia mwenendo wa Paulina. Je? watafanya nini?...unfikiri ikiwa wataongelea waziwazi juu ya tatizo lao mapenzi yao yaweza kufufuka?  "  Halafu leo ni tarehe ambayo nilifunga pingu za maisha na baba watoto:-)

CHANZO :- KITABU NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA

Tuesday, July 1, 2014

BUSTANI YETU MWAKA HUU INASUA SUA ..ILA HAYA NDIYO MAENDELEO YAKE.....

 Hapa ni mboga ya maboga tena ni zile mbegu nyeusi kutoka njombe nilipewa na mama yangu wa hiari mama Mgaya.
 Na  hapa ni viazi mviringo na mahindi ..ila mmmhhh haya mahindi sijui kama nitakula....
 Kwa vile ni Kapulya nikaona ngoja nijaribu na parachichi na huu ndio mti wa parachichi ila na hapa nina wasiwasi kama nitakula....
Mnazi pia unapatikana ... MNAZI MMOJA:-)
KILA LA KHERI PANAPO MAJARIWA TUTAONANA....KAPULYA A.KA DADA MKUU.