Tuesday, November 29, 2016

JUMANNE HII YA MWISHO WA MWEZI HUU TUBAKI TU KIDOGO HAPA NYASA-MBAMBA BAY-LIULI

 MWONEKANO WA ZIWA NYASA
 WAVUVI KATIKA ZIWA NYSA
NA HAPA NI POMONNDA ROCK  KATIKA KIJIJI CHA LIULI HAPA HAPA NYASA. 

Monday, November 28, 2016

MLO KAMILI WA KWETU NYASA ...NA NDIYO MLO AUPENDAO KAPULYA WENU...!

Kwa vile Nyasa ni maalufu sana kwa kilimo cha MIHOGO:- Basi hapa ni ugali wa mhugo, maharage, samaki na dagaa.  NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMA!

Friday, November 25, 2016

BADO TUPO MKOANI RUVUMA ...NGOMA YA ASILI YA NDUGU ZETU WAMATENGO


Ni ngoma ya uzinduzi wa harusi.... AU SI TUENDELEE TU KUCHEZA NA HII....


MUWE NA SIKU NJEMA. NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA.

Tuesday, November 22, 2016

LEO TUTEMBEE KWETU SONGEA:- TUSISAHAU YALIYOTOKEA WAKATI WA VITA YA MAJIMAJI


Hii hapa ni nyumba ya jiwe  ya SONGEA MBANO ambayo ipo Chandamali katika mlima wa Msamala Songea kwetu.

Monday, November 21, 2016


Leo nimetumiwa huu ujumbe na RAFIKI nami nikaona ni ujumbe mzuri nisiwe mchoyo nikaona niuweka hapa kibarazani kwetu...ukipata wasaa basi soma...

Bwana mmoja maskini sana aliishi na mkewe. Mkewe alikuwa na nywele ndefu za kuvutia. Siku moja mkewe akamwambia bwana huyu akamnununulie chanuo la nywele zake ili azichane zirefuke na kunawili vizuri. Bwana huyu alijibu hana pesa kabisa hata ya kutengenezea saa yake iliyokuwa imevunjika. Mwanamke huyu hakuendelea tena kusisitiza ombi lake. Kesho ilipofika bwana yule akiwa anarejea nyumbani alipitia dukani akaiuza ile saa yake na kununua chanuo kwa ajili ya mke wake. Alipofika nyumbani akiwa na lengo la kumshangaza mkewe  akastaajabu kumkuta mkewe kanyoa. Mke naye kumbe alizinyoa nywele zake na kuziuza kisha akamnunulia mumewe saa mpya. Wote walikuwa na furaha  ya kupendana na kujitoa kwa mwenzie wakajikuta wanalia kwa furaha.
UJUMBE:- KUMBUKA KUPENDA SIO KITU  ILA KITU NI KUPENDA . ILA KUPENDANA NI ZAIDI YA KITU. MPENDE AKUPENDAYE!

Friday, November 18, 2016

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA HILI....PICHA YA WIKI!

Kwa wale wanaopenda ulabu ...hivi ndivyo pombe aina ya komoni inavyoanza kutengenezwa....msije mkasema tusubiri mpaka lini.......kuna
n
Hapa ni ulanzi...ni pombe ya kienyeji na ya asili...IJUMAA NJEMA KWA WOTE.

Wednesday, November 16, 2016

Tuesday, November 15, 2016

MAVAZI: VALI LILILOSHONWA KWA KITENGE...TWAPASA KUJIVUNA!

Waafrika/watania tuna haki ya kujivunia vazi la KITENGE NA KANGA ambalo linaweza kubuniwa kwa mitindo mingi sana ya mavazi ebu angalia hili vazi...NIMELIPENDA SANA ningejua wapi ameshona ningeagiza. Kama kunayejua TAFADHALI ANIJUZE.

Monday, November 14, 2016

TUANZE WIKI HII NA KUTEMBELEA HUKO IRINGA KUANGALIA MICHORO YA ASILI...KUMBUKUMBU

Kwenye hili jiwe tunaona michoro ambayo hapo kale ilichorwa kwa ustadi mkuu ni michoro kama ile ya Kondoa.
Hapa ni jiwe Igereka lambalo lipo katika mtaa wa Kihesa Kilolo katika Manispaa ya Iringa Nkoani Iringa. Ukiwa maeneo ya Iringa usikose kutembele...FAHARI YA TANZANIA... JUMATATU NJEMA!

Friday, November 11, 2016

IJUMAA NA MWISHO MWEMA WA JUMA NA NDUGU ZETU WAGOGO...


MUWE NA MWISHO MWEMA WA JUMA .
UJUMBE: Afya sio kula vizuri tu. Afya pia ni kuhusu jinsi ya kufikiri na kusema.

Thursday, November 10, 2016

MICHEZO:NETIBOLI NI MCHEZO NILIOKUWA NIKIUPENDA SANA

Ukitaka mpira ni lazima uutafuta mie nafasi yangu ilikuwa kama huyo mwenye sketi nyeusi...kwa hiyo hapa mchezo mzima upo mikanoni mwako... 
 Kwa hiyo hapa mzuiaji inabidi afanya kazi sana ila kwa hapa naona itakuwa kazi rahisi kwa vile ni mrefu...Netiboli ni mchezo mzuri, kwana kwa afya na pia kwa mazoezi ....na mwisho inabidi uwe mwepesi kukimbikia:-)  Ila mmmhhhh siku hizi  kukimbia ....

Wednesday, November 9, 2016

KUMBUKUMBU:- UNAVIKUMBUKA VITU/VIFAA HIVI?

Kwangu sio vigeni kabisa ndivyo vilivyonipa maarifa yote na pia bado namiliki mpaka hivyi nisemavyo...Nimewahi  kusikia minongòno ya kwamba, hasa mwanaume akimiliki vifaa kama hivi siku hizi basi ajua mke atakimbia.....Swali kwani ni vifaa au mume ndiyo tuwapendao au wanatusingizia tu..Wanawake wenzangu mpo nami?...Eti binti/mwanamke akikuta vifaa hivi kwa manaume, penzi linakufa muda  huo huo....KWELI?

Tuesday, November 8, 2016

KARIBUNI TUJUMUIKE KATIKA MLO HUU WA UHAKIKA

UGALI WA ULEZI, MBOGA MAJANI NA SAMAKI
Hii picha imenikmbusha mbali sana huu ulaji kwa kushirikiana/kuchangia sahani moja na sio kila mtu na sahani yake...Hivi kwa nini hii tamaduni inakufa?

Sunday, November 6, 2016

JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU KATIKA KRISTU.....


Kwaya Mt.Maria goreth chuo kikuu cha ushirika wimbo wa Dela dela. Wimbo huu kwa kawaida imeibwa na wangoni na kuchezwa katika ngoma ya lizombe lakini kumbe hata kwa maombi yawezekana nimeFURAHI SANA.

Friday, November 4, 2016

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA MWISHO MWEMA WA JUMA HII YA KWANZA YA MWEZI WA KUMI NA MOJA ...

:-) EMBE nimetumiwa hizi na rafiki nia yake kubwa ni kunitamanisha na kweli nimetamani  maana hapa nilipo mate yanachuruzika tu....MWISHO MWEMA WA JUMA!

Thursday, November 3, 2016

ILI MRADI VIIVE:- MCHAGUA JIKO SI MPISHI!!!!

 Hii nadhani wengi wetu tumepitia na bado tunaendelea kutumia hasa uwapo sehemu  kama vile mstuni kwa matembezi. Vyombo kama hivi ni muhimu sana kuwa navyo vipo vingi sana SIDO tena ni imara zaidi kuliko plastiki....
Hapa ni ubunifu wa kisasa ambao hata sijawahi kufikiria ...ila najiuliza kama yawezekana kupika mchele hapo au maji ya chai tu?
Au tu upo katika kuchimba labda shimo huku ukichoma taka labda na ghafla njaa inapiga hodi,,, je Ungejaribu?

Wednesday, November 2, 2016

JE WAKULIMA WA VIJININI WANATHAMINIWA?

Tanzania Iringa:- Ndugu zanguni! katika picha tunamwona bibi kikongwe akiwa na mzigo mkubwa wa kuni huku katika mkono wake wa kulia uliopata kufanya mamia ya shughuli ukiwa umeshika jembe, ni dhahiri kuwa bibi huyu ni mtu anayejali kazi zinazompatia riziki yake kwa kuwa dhana ya jembe ni kilimo na kuni ni chakula lakini serikali inawapa nguvu gani akina bibi kama hawa ili kuboresha kilimo chao mfano nyenzo za kilimo au mikopo.

wakulima wengi maeneo ya vijijini hulalamika kuwa serikali haiwapi msaada na matokeo yake wakulima hao hujikuta wakifanya kilimo duni, kila mwaka huwa hivyo tu. Je? mwaka mpya ujao (2017) inaweza kuwa ndo fursa ya serikali kuwainua wakulima.?