Monday, January 30, 2017

JIKONI LEO...KUOKA MIKATE

 Hii ni kazi ya mikono yangu...huwa napenda kuoka mikate mwenyewe kwa hiyo leo nimeoka ...hapa imekwisha umuka....
.....baada ya dakika 12 kwenye oveni tayari ....karibu  wale wapenzi wa mikate mimi napendaga magimbi bwana:-)

Friday, January 27, 2017

KUMBUKUMBU...JINSI YA KUPATA POMBE YA ULANZI

Kuhusi Ulanzi:- Kwanza nakumbuka nilipokuwa msichana mdogo bibi na babu yangu walikuwa na "vitindi" miti ya ulanzi mingi sana na walikuwa wakiuza sana ulazi ...na baada ya miaka nikawa naishi Madaba-Matetereka kule nako kulikuwa na ulazi mwingi sana ...ila bahati mbaya au nzuri sijui utamu wa ulanzi...sijawahi kuonja:-)...NAWAPENDA WAOTE NA NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA HILI...USIBUGUE SANA ULAZNI:-).....KAPULYA

Thursday, January 26, 2017

MBUZI WA AJABU MPAKA JUU YA MTI...

Binafsi sijawahi kuona  mbuzi wakipanda juu ya mti...yaani wamenipita hadi mie:-) kaaaazi kwelikweli

Tuesday, January 24, 2017

Monday, January 23, 2017

ZILIPENDWA..UNAKUMBUKA HIVI?

FANTA SIO FANTA TU  BALI HAZIKUWA ZIKICHAKACHULIWA
Nakumbuka sana haya makopo vilikuwa na ubora sana hivi vitu, siku hizi duh! kaaazi kwelikweli...sijui  wenzangu mnasemaje?

Thursday, January 19, 2017

SWALI LA LEO: SISI BINADAMU NI KITU GANI HASA?

Tunajitahidi sana katika kuvaa vizuri, kula vizuri, kujenga nyumba bora, kendesha magari makubwa na kufanya mengine ambayo yanaweza kuipa raha miili yetu na kutupatia  umaarufu ikibidi. Moja ya sababu za kufanya kwetu hivyo, ni ile imani yetu kwamba sisi ni miili yetu. Lakini ajabu ni kwamba, pamoja na kufanya hivyo, bado tunajikuta haturidhiki. Wengi hatujui kwamba, kutoridhika kwetu huko ni taarifa kwamba sisi ni kitu kingine, siyo miili hii tuliyonayo. Je, tumeshawahi kujiuliza sisi ni akina nani hasa? Kama bado, tumepata nafasi ya kujiuliza sasa na bila shaka tutapata jibu litakaloturidhisha.
Chanzo:- kitabu cha MAISHA NA MAFANIKIO

Wednesday, January 18, 2017

PALE NDUGUZO NA MARAFIKI WANAPOKUTAMANISHA CHAKULA /VYAKULA UVIPENDAVYO:-)

Ugali wa ulezi  kwa kuku(mawondo ni kingoni) paja na mchuzi. utadhani mlima Kilimanjaro ukiisha huo itabidi kupumzika haswaaa
 Kuna mdogo wangu anajua sana mimi ni mpenzi sana wa ugali  kanitumia hii ili nitamani na kweli nimetamana...ugali na dagaa ...
....na mwingine kunitamanisha hiii wali, kuku na mboga mboga ...:-) watu wachokozi sana kwa kweli

Tuesday, January 17, 2017

USIHANGAIKE, FANYA MAMBO YAKO KWA UBORA NA USHUKURU KWA KILA HATUA KISHA SAHAU MENGINEYO

Tupo wengi sana tunaofikiri hivi:-Ya kwamba kuna mambo mengi sana tunapitia katika maisha yetu ya kila siku mengine mazuri, na mengine mabaya na wakati mwingine tunakutana na watu wazuri ambao wana tufurahisha lakini wakati huohuo yawezekana ukakutana na mtu ambaye akakuumiza sana moyo wako iwe ni kazini, nyumbani au katika mahusiano.
Jambo la muhimu ni kujua namna ya kukabiliana na changamoto zote nzuri na mbaya, kwani ukiweka moyoni yale yanayo kuumiza huwezi kusonga mbele, ila ukiamua kusahau nakufanya juhudi katika maendeleo yako, basi utafanikiwa hata  wahenga walisema  " SAHAU YALIYOPITA UGANGE YAJAYO".
PANAPO MAJALIWA NDUGU ZANGUNI!

Sunday, January 15, 2017

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE...AMANI NA FURAHA ZITAWALA KATIKA NYUMBA ZETU!

Zipo furaha nyingi duniani, watu wanafurahia kufaulu mitihani, kupata ajira, mtoto, kuoa na kuolewa, kuwa na mali nyingi na mambo mengi kadha wa kadha. Lakini hebu tuone furaha iliyo kuu kuliko zote, "Ndipo wale sabini  waliporudi kwa furaha wakisema hata pepo wanatutii, YESU akawambia msifurahi kwa vile pepo wanawatii BALI FURAHINI KWA SABABU MAJINA YENU YAMEANDIKWA MBINGUNI. Kumbe furaha kuu ni jina lako kuwa limeandikwa katika kitabu cha uzima. Luka 10:17-20".  JUMAPILI NJEMA.

Friday, January 13, 2017

TANZANIA TUNA NGOMA NYINGI SANA ZA ASILI...UNAKUMBUKA NGOMA HII YA MHAMBO?

Nakumbuka wakati nikiwa nikisoma shule ya msingi tulikuwa tukicheza ngoma zote za asili MUHAMBO ílikuwa mojawapo. na mwalimu wa ngoma hii namkumbka sana, aliitwa mwalimu Ndumbalo "Moyoumo" ...yaaani nimekumbuka sana ....pia nimetamani kwa hiyo nimecheza cheza hapa....PANAPO MAJALIWA NA NITAKULETEENI NGOMA NYINGINE YA ASILI:-) MWISHO WA JUMA UWE MWEMA NA MWENYE FURAHA NA AMANI...Kapulya

Thursday, January 12, 2017

HADITHI:- DALILI YA MVUA NI MAWINGU

Hii ni hadithi kuhusu kijana mmoja, aliyechagua msichana wa kumwoa, na kuzaa naye watoto, na kwa kali hiyo kuukuza ukoo wake. Lakini kabla ya mipango ya mwisho ya harusi na baba mkwe wake, aliamua awajaribu wakwe zake kwa mtihani mdogo.

Asubuhi moja, akaomba ruhusu kwa wake zake aende kijijini kwao akachukue vifaa vyake vya kulimia, na angeshukuru kama shemeji yake, dada wa atayekuwa mkewe atafuatana naye. "Umekuja hapa, kumtafuta mke utakayeishi naye, karibu tutakuwa ndugu, kwa hiyo shemeji yako akikubali, sisi hatuna kuzuizi," wakwe walimjibu.

Hivyo Kijana na shemeji yake wakaondoka, na walipofika kijijini kwake, badala ya kuchukua vifaa vya kilimo, akachukua mkuki, pamoja na shemeji yake, wakaenda kuwinda. Kijana akauwa mnyama mkubwa, wakaanza safari ya kurudi kijijini kwa wakwe zake. Shemeji yake akawa amebeba kitoweo huku kijana amebeba mkiku wake.

Njiani akamwambia shemeji yake, kuwa kuleta kitoweo nyumbani, ni njia mojawapo ya kuhakikisha uhodari na uwezo wa kuwatunza wakwe na familia yake. Wakapokewa kwa shangwe, kijana naye akapongezwa kwa uhodari wake.

Usiku huo huo, akawaeleza wakwe zake kwamba alitaka ajaribu tena jwenda kuwinda na vile vile akaomba ruhusu ya kufuatana na shemeji yake.
"Sasa tuko kama ndugu, sisi tunataka tukusaidie kwa kila njia tutavyoweza!" Baba mkwe akamwambia.

Hivyo, siku iliyofuata, wakaondoka tena na haikuchukua muda, kijana kwa uhodari wake, akauwa mnyama wapili. Mara hii mnyama aliyemwua alikuwa mkubwa na mzito kiasi kwamba, wote wawili walishindwa kumbeba. Uamuzi ukawa kwamba yule kijana, arudi kijijini kwenda kuomba msaada, na shemeji yake abakie kuchunga kitoweo. Kijana alipoondoka, yule msichana akapanda juu ya mti, kuhofia wanyama wakali, akisubiri msaada ufike.

Kijana alipofika kijijini akajitupa kwa kilio chini ya miguu ya mkewe wa mtarajiwa. Akisema kama amefanya kosa kubwa sana.
Badala ya kutupa mkuki kumchoma myama, sababu ya giza alimchoma dada yake ambaye sasa amemwacha amekufa porini.
Familia nzima wakajiwa na chuki na wakaanza kumtukana maneno mbali mbali, kusikia kisa hicho. Wakaanza kumpiga vile vile: " unawezaje kusema wewe ni mwindaji hodari, kutaka kutunza familia ikiwa umefanya upumbavu kama huu?" Walimpiga sana mpaka kidogo azirai. wakagundua kwamba wakiendelea kumpiga wanaweza kumuua na wasiweze kupata maiti ya msichana wao. Maana ni yule kijana peke yake alifahamu maiti ilipo. Wakamwamuru yule kijana ambaye alikuwa hai kwa mapigo, aongozane nao akawaonyeshe maiti ya msichana wao ilipo.

Walipofika, walistaajabu sana kumwona msichana wao akiteremka toka juu ya mti. Akishangaa na kuwauliza kwa nini yule kijana alikuwa katika hali mbaya hiyo huku ametapakaa damu. Familia nzima  ilishindwa kusema cho chote kuhusu kitendo hicho kwa kuona aibu, Kwa maovu waliyomfanyia. Wakamwomba msamaha yule kijana. Wakasaidiana kumchukua yule mnyama na kumkata vipande. Wakavibeba hivyo vipande na kurudi kijijini. Walipofika tu, yule kijana akafungasha mizigo yake na kabla hajaondoka, akawaambia kuwa hataoa msichana kutoka kwenye familia ya watu wasiokuwa na huruma na wakorofi.  Hivyo akafunga safari na kuondoka.

Haukupita muda, kwenye kijiji kingine alichohamia, akapata mchumba mwingine. Vile vile akawajaribu wakwe zake kama alivyofanya awali na mchumba wake wa kwanza. Safari hii mambo yakawa tofauti! Wakwe zake wapya, walishtuka na madhara yaliyotokea, akasamehewa kwa ajali iliyotokea na wakamwomba yule kijana akawaonyeshe sehemuu ambapo ajali ilitokea, ili wachukue maiti na kuja  kuzika ipasavyo. Walipofika sehemu ya ajali ilipotokea wakamkuta shemeji yake, yaani msichana wao mzima kabisa amesimama kando ya mnyama aliyeuawa na mkwe wao.

Ikabidi yule kijana aeleze mkasa toka mwanzo mpaka mwisho, akatoa sababu za kufanya kitendo hicho. Na kamaliza kusema kwamba, sasa amepata mke aliyekuwa  akimtafuta ambaye tabia yake pamoja na familia yake, ni ya watu adili. Akamuoa mchumba wake, wakaishi kwa muda kabla ya kuhamia kijijini kwa yule kijana na kuishi maisha yao yote
CHANZO:-  HADITHI NA VISA KUTOKA TANZANIA

Wednesday, January 11, 2017

UJUMBE MZURI KUTOKA KWA MAMA TERESA...

Kama unataka kubadilisha dunia hii nenda nyumbani na uipende famIlia yako. UJUMBE: Mama Teresa

Sunday, January 8, 2017

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE ....KUSIFU NI KUZURI

NAWATAKIENI WOTE MTAOPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA... KAPULYA

Thursday, January 5, 2017

LEO NI SIKU/TAREHE YANGU YA KUZALIWA

Leo ni tarehe/siku ambayo familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa na furaha kumpatabinti yao ambaye alizaliwa siku hii ya leo. Na leo ameongeza mwaka tena na kuzidi kuzeeka. Lakini hata hivyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI  wengine wote  wanaotimiza miaka leo pia mwezi huu wa januari. SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...KAPULYA Nachukua nafasi hii  kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama .

Wednesday, January 4, 2017

UJUMBE WA WIKI KUTOKA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO

ANAYEKUTHAMINI MPE THAMANI YAKE HATA KAMA MASKINI BASI JALI UTU WAKE.
AU TU TUSISAHU HILI PIA
WATU WENGI  WANAHITAJI UPENDO ZAIDI  KULIKO WANAVYOSTAHILI.

NAWATAKIENI KILA LA KHERI. UPENDO DAIMA.

Sunday, January 1, 2017

KHERI KWAMWAKA MPYA 2017

NACHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURUNI WOTE KWA MWAKA ULIOPITA 2016 KWA KUWA NAMI MAANA BILA NINYI  NISINGEKUWA HAPA NILIPOFIKA. NATUMIINI TUTAENDELEA KUCHIRIKIANA TENA MWAKA HUU 2017.