Sunday, January 31, 2010

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA KWA SALA HII

Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.
Na pia nakuomba:Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE JAMANI NA PIA NI JUMAPILI YA TANO NA YA MWISHO YA MWEZI HUU!!!!!!!!JANUARI

Friday, January 29, 2010

Napenda kuwatakia mwema wa juma hili pia ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa kwanza!!

Kunywa lakini kumbuka pombe si maji (na kumbuka kama utaendesha usinywe ugimbi mwingi)

Wazee na vijana wa kijiji cha kibaa wakicheza bao kama sehemu ya kupoteza muda baada ya kumaliza kazi.
Au ngoja tumsikilize Dada Saida Karoli ili wenye kuselebuka

Muwe na wakati mzuri wote

Thursday, January 28, 2010

HATUA MUHIMU KATIKA MAKUZI YA MTOTO

Katika udadisi wangu nikawa nimepitia blog ya http://kaluse.blogspot.com/ na kukuta makala hii na nikashidwa kuiacha kwa vile najua wote katika hizi blog lengo letu ni moja kuelimisha jamii.

Hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, kwa nini watu wengine ni walevi? Wengine waongeaji sana? Wengine wakimya sana? Wengine waongo sana? Wengine wana tamaa ya ngono kupita kiasi na kadhalika? Lakini pengine una maswali mengi ya namna hii ambayo yanaonyesha jinsi wanadamu wanavyotofautiana.

Kuna hatua 5 muhimu ambazo mtoto lazima afanye mambo ambayo yanastahili kufanyika katika hatua husika. Na iwapo hayatafanyika, hali hizo huhifadhiwa katika mawazo yake ya kina na hivyo kumsababishia matatizo makubwa ukubwani.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

Hatua ya kwanza – oral stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili. Katika hatua hii ya kwanza, furaha na raha ya mtoto huwa imejificha mdomoni. Utakuta mtoto kila wakati anafurahia kunyonya maziwa ya mama yake, vidole au midoli. Mtoto anatakiwa atumie mdomo wake mpaka ile hamu yake yote iishe. Kama ni kunyonya basi aendelee kufanya hivyo mpaka pale utakapofika wakati mzuri wa kumwachisha ziwa. Kumnyanyasa mtoto wakati ananyonya au kumfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana ikiwa ni pamoja na kumwachisha ziwa mapema, husababisha hamu yake ya kuutumia mdomo ibaki na hivyo kuhifadhiwa kwenye mawazo yake ya kina. Anapokuwa mtu mkubwa hulipa kisasi bila kujua kwa kuutumia mdomo kwa kadri anavyoweza. Hivyo anapokuwa mtu mkubwa anaweza akawa muongo sana, mlevi kupindukia, mvuta sigara sana, muongeaji sana, au mmbeya sana. Kama kuna watu unawafahamu wenye tabia hizi, jaribu kupeleleza kama walinyonyeshwa bila kunyanyaswa au kama hamu yao ya kunyonya iliisha.

Hatua ya pili – anal stage: Hatua hii humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Matumizi ya mdomo huwa yamekwisha na raha huhamia sehemu za haja. Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia au jinsi ya kutumia choo. Kinyume na hivyo ni kumfanya mtoto awe na tabia ya kujifanyisha na hivyo kuwa na hali mbaya ukubwani. Mtoto aliyenyimwa huduma hii akiwa katika hatua hiyo hubakiwa na deni, anapokuwa mkubwa anaweza kupata matatizo ya kiakili. Watoto waliokosa huduma hiyo wanapokuwa wakubwa, mara nyingi huwa mashoga, na wengine huwa waoga kufanya mapenzi, lakini mbaya zaidi ni kukosa kabisa hamu ya mapenzi, wengine huwa wazembe na huwa na tabia fulani fulani ambazo zinahitaji msaada mkubwa wa wengine.

Hatua ya tatu – phallic stage: Hatua hii huwahusu watoto wenye umri wa miaka minne. Ni katika hatua hii ambapo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hivyo kuwa karibu na mama yake au baba yake. Mtoto wa kiume hupenda kulala na mama yake na mtoto wa kike pia huwa hivyo hivyo hupenda kulala na baba yake (interest of opposite sex). Mtoto wa kiume humchukia baba yake bila kujua na kumuonea wivu mama yake na kuona kama anamfaidi baba yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake, pia mtoto wa kike humchukia baba yake na kumuonea wivu baba yake na kuona kama anamfaidi mama yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake. Watoto waliokosa kuwa karibu na wazazi wao wa jinsia tofauti katika hatua hii, wengi hupata matatizo, lakini hulipiza kisasi kwa sababu hawakuwa karibu na jinsia tofauti wanapohitaji kufanya hivyo. Usishangae kumkuta binti akiwa kwenye kundi la wavulana au mvulana akiwa kwenye kundi la wasichana.

Hatua ya nne – latency stage: Hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita, minane na wakati mwigine mpaka miaka 12, ambapo mtoto macho yake yote huwa katika michezo ya kawaida na kwenda shule. Hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika hatua hii kati ya jinsia ya kike na ya kiume.

Hatua ya tano - genital stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13. katika kipindi hiki vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo. Katika hatua hii ndipo mtu hukabiliwa na vitu vingi katika maisha yake yote. Huanza kujishuhulisha na kutafuta maisha yake mwenyewe na ndipo hatua nyingine zote huanza kujirudia tena kama hazikufanywa vizuri katika umri huo. Raha ya mwanadamu yoyote katika kipindi hiki huwa ni mapenzi, lakini hutofautiana kiwango cha kupenda au kutamani kutokana na jinsi alivyolelewa katika hatua nne za mwanzo. Nakuomba sana kila unapokutana na watu waongo, wambeya, wakimya, wapenda ngono kupita kiasi n.k. waulize maisha yao ya utotoni.

Wednesday, January 27, 2010

WATOTO WENYE VIPAJI MAALUM

Je unawezaje kuwagundua?

Watoto wenye akili za ziada au wenye vipaji vya ajabu ni watotot ambao, wamejaaliwa kuwa na IQ {Intelligence Quotient} kubwa kuliko kawaida. IQ ni kifaa maalumu kinachotumiaka kupima akili za binadamu.

Kwa kawaida, watoto wa ain hii wanakuwa na uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi na hisabati, pia ni wabunifu na wajanja wa kufikiri haraka haraka na kupata majibu kwa njia za ajabu mno.

Ni watoto wenye uwezo mkubwa sana katika uongozi au wanweza kuwa na vipaji tofauti tofauti kama vile muziki, uigizaji na michezo mbalimbali.

Hata hivyo, tunawezaje kuwatambua watoto wa aina hii?

Kwanza watoto wenye vipaji maalumu , mara nyingi huanza kujibainisha wakiwa na umri wa kuanzia miaka miwili au umri wa miaka wa kuanza masomo ya awali. Wakati mwingine watoto wa aina hiiwhawajibainishi hadi wanapomaliza elimu ya msingi na hii inatokana zaidi na sababu za kibaiolojia .

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za kumtambua mtoto mwenye akili za ziada.
* Huanza kuongea mapema kwa kutengeneza sentensi kwa ufasaha ukilinganisha na watoto wa umri wake.
* Wanakuwa na uwezo wa kupanga vitu kwa mpangilio sahihi kwa kufuata rangi au aina ya vitu.
* Wanakuwa wajuaji wa hesabu kwa kupenda kuhesabu vitu na hata kukokotoa hesabu.
* Wamejaaliwa kuwa na maono au wanweza kusoma hisia za mtu mwingine, kwa mfano mtoto wa aina hii anweza kumwona mama yake anahangaika ktafuta kitu na yeye akajua anatafuta nini na hata kujua mahali kilipo na hivyo kukifuata na kumletea mama yake, pia wanakuwa na uwezo wa kusoma mawazo ya wazazi wao au hata watu wa karibu wanaowazunguka
* Wanavutiwa sana na sanaa au muziki mapema mno na hata kupenda kuchezea vyombo vya muziki kama viko karibu nao.
* Wanakuwa na moyo wa upendo na hurumawakiwa bado ni wadogo wa umri ukilinganisha na watoto wengine wa umri wao
* Wanakuwa na tabia ya kujitegemea zaidi badala ya kuomba msaada kwa kila kitu, kwa kawaida huwa wanjiamini sana, hivyo ni aghalabu sana kuomba msaada kabisa. Huwa wanaamini katika wao.

Dalili za kuwatambua watoto wa aina hii ziko nyingi sana kulingana na mazingira yaliyowazunguka watoto hao.

Je watoto wa aina hii wanasaidiwaje ili kukuza vipaji vyao?
Watoto wa aina hii wanhitaji mapenzi sawa na watoto wengine kwani wazazi wengine huwa wanashindwa kuwaelewa watoto wa aina hii na hivyo kuwapuuza, kitu mabcho ni hatari sana kwa maendseleo yao. Wazazi wanatakiwa kufahamu kuwa, licha ya watoto hawa kuwa na akili za ziada, pia bado ni watoto kama watoto wengine.

Ila inashauriwa, wazazi kuwatengenezea watoto wa aina hii mazingira mazuri ya kuendeleza vipaji vyao, kwa kuwanunulia vifaa mbalimbali vya kuchezea, kulingana na matakwa ya vipaji vyao. Ikiwezekana kuwatengea vyumba vyao ambavyo watavitumia kufanya mambo yao bila bughuza, pia inashsuriwa kuwa ni vyema kuwasikiliza na kuwatimizia mahitaji yao.

Huko mashuleni nako inashauriwa kuwaandalia vipindi maalum vitakavyoamsha hisia zao, bila kusahau kuwachanganya na wanafunzi wenzao wenye akili za kawaida.

Tuesday, January 26, 2010

Kukatwa mshahara wakati ukiwa mgonjwa!!!!

Wiki iliyopita nilikuwa mgonjwa na kabla sijapona sawasawa nilikwenda kazini tena. Na wakati naumwa kulikuwa na baadhi ya marafiki kutoka nyumbani TZ, walikuwa wananitaka hali kila siku pia marafiki wengine waliojua kuwa naumwa.

Nachotaka kusema hapo ni kwamba:


Hapa Sweden kuna sheria ya kwamba ukiwa unaumwa ile siku ya kwanza ukishatoa ripoti kazini kuwa ni mgonjwa unakatwa mshahara wote wa siku ile. Siku ya pili 80% na siku ya tatu hivyo hivyo na kuendelea inategemea kama bado unaendelea kuwa mgonjwa. Kama unapata laki tatu kkwa mwezi siku ya kwanza wanakata elfu kumi na siku ya ifuatato elfu nane. Kama nilivyosema hapo juu kama utaendelea kuugua utakatwa kila siku elfu nane.


Hii ndiyo sababu nilikwanda kazini bila kupona sawasawa.

Monday, January 25, 2010

Wazungu bora kuliko waafrika!?

Makala hii nimeikuta Jamii Forum nimeipenda na nimeona niiweka hapa kwangu ili tusaidiane kwa mapana swala hili.


Baba yangu mzungu, mchanganyiko Irish/dutch
Mama yangu msambaa lakini nilishangaa jana kukuta hii post kule JIACHIE.
JE NI KWELI KUWA WANAUME WAKIBONGO HAWANA MPANGO? Sunday, January, 17, 2010
Salama jamani huko?? Kuna huyu dada mmoja wakiTanzania, yeye baada yakuolewa na mzungu anaona kuwa manamume wakibongo hawana mpango. Hebu soma hii blog yake.... Ni kweli wajomba zangu wakiswahili ni wayeyushaji?

Im not a great writer, that is evident. Sijui kupangilia sentensi zangu…..so bear with me Sasa leo nataka tuweka wazi swala zima la wasichana wa kitanzania kuolewa au kuwa na maboyfriend wa kizungu.

Mimi binafsi nime-notice kwamba wasichana wengi wa kitanzania wamekuwa wakiona kwamba kuwa na boyfriend ama mume ambae ni mzungu is actually an achievement in life. Na wengi wamekuwa hawataki kabisa hata kuwa na ma-boyfriend ambao ni waa-africa especially watanzania.

Na kuna wasichana ambao nawajua ambao wako kwenye relationships na mwanaume wa kitanzania lakini anaeleza wazi wazi kwamba anatamani apate mwanaume wa kizungu. Mdau wewe unanaoje swala hili? Je hawa wasichana ni kwamba they are shallow and stupid? Or are they very smart???

Really kabla huja-judge na kutuma comment za kuwatukana lifikirie hili swala vizuri… Mimi personally naona kuna 2 sides to this issue.kuna wale ambao watanaka kuwa na wazungu na hawataki ku-date watanzania wenzao kwasababu za kijinga na zisizo na msingi, 1st side…

Kwa mfano kuna wengi facebook unaona mtu akipata boyfriend wa kizungu basi anamwaga picha zake na mzungu facebook, sasa hizo comments za marafiki nayeye mwenye mchumba ndio zinazotuharibia wengine wote..nashindwa kuelewa kabisa ni kwanini mtu akiweka picha yake na mzungu facebook basi kila mtu anamwandiki comment ‘UKO JUU’, ‘UMEOPOA MAMA UKO JUU’ , ‘KWELI MUNGU MKUBWA’ , ‘RISKI ZIMEFUNGUKA MWAKA HUU’, KWELI MUNGU AMEKUKUMBUKA’ , comment kama hizi na zingine za disini hii zinanisikitisha mno…jamani hivi kweli kuwa na mwanaume mwenye ngozi nyeupe ni kitu cha maana kiasi hiki? alafu hivi kweli tumejishusha utu wetu kiasi cha kwamba tunafurahia in public? Kwanini msiweke comment kama ‘u look happy’ ,’hongera kwa kupata mchumba and so forth’ …kuwa na mzungu sidhani kama inamaanisha uko juu or whatever. (kama moja ya comment nilizoandika hapo zipo kwenye picha yako ,please usijisikie vibaya, niliitumia tu kama mfano ili kuwapa wasomaji wangu picha kamili,its really not about you) hivi kweli hawa wazungu wenyewe wangekuwa wanajua kusoma Kiswahili humo facebook ingekuwaje??

Wanawake wenzangu wa kitanzania, tuache kujiabisha na hili swala zima la mzungu mzungu mzungu, especially kwenye facebook, mtu akikuwekea comment ya kishamba kama hizo hapo juu usiishadadie sana, ikiwezekana i-delete akuwekee comment ya maana, … Kama wewe ni mwanamke ambae kupata mzungu is an achievement basi , I am sorry to say ,you are without a doubt a loser,

Wazungu wanamatizo mengi tu, na hata ukiangalia the highest divorce rates in the world zipo western countries na sio kwetu.

na kwa wale wenzetu wanaodhani wazungu wote wanapesa na kwamba atakuhonga basi unajidanganya kabisa, mzungu sio muhongaji , kama unataka kuhongwa bora mapedeshee ya kibongo litakununulia hata gari baada ya kukujua kwa siku chache tu.hahahahha…. Wazungu wanachukua muda wao kumsoma mtu na tabia zake, na kama kuna chochote atakachokufanyia ni baada ya muda mrefu na kwamba umeshakuwa mke wake au labda anahisi utaishia kuwa mke wake.

Na pia ndugu zetu wa kibongo wanaweza kuishi na mwanamke asie na income yoyote, na asiejishughulisha la lolote, asilimia kubwa ya wazungu hawawezi kabisa hii tabia. So kabla hujarukia na kugeza watu, angalia usije kuchanika msamba…lol….

2nd side… Kuna wale wasichana wa kibongo wanaotaka kuolewa na wazungu for the right reasons. Hao ndio ninaowalewa mimi…

Ukweli lazma tuuseme leo… Asilimia kubwa ya wanaume wa kibongo ni miyeyusho mitupu , tuseme labda 80%....sasa wewe utakuwa na bahati gani mpaka upate mmoja wa hiyo 20% ambao ni wastaarabu. Ukweli ni kwamba, nikiangalia rafiki zangu walioolewa na wanaume watanzania na walioolewa na wanaume wazungu, walioolewa na wazungu, are way more content in their marriages, ofcourse kuna exception za rafiki zangu wachache waliiolewa na wabongo na wana-enjoy ndoa zao na ndoa zao haziwapi homa kila siku…

Mie nafikiri,wanawake wengi wa kitanzania wameamua kuwa na wazungu kwasabu wanatafuta pumziko la roho…ukweli ni kwamba wanaume wengi wa kitanzania wanasumbua mno tena kupita kiasi.

Mwanaume wa kitanzania amelelewa akiona baba yake ana wake wawili na nyumba ndogo kama tatu, je unadhani yeye atakuja kuwa mume wa aina gani???? Mwanaume wa kitanzania anajiona ni mwanaume kamili zaidi kama anawanawake wengi, na kitu ambacho yupo proud nacho kiasi ya kwamba anaweza kukaa na rafiki zake bar akaadisia jinsi gani anawanawake wengi na wenzio wakamuona ‘YUKO JUU’….

Mwanaume wa kizungu, hajakulia kwenye mazingira haya and automatically ipo kichwani mwake kwamba anatakiwa kuwa faithfull kwa mke wake na kumtreat as an equal.hata ikitoea akawa macho juu akapata kidosho nje, atajificha, hutojua lolote na ni jambo la aibu sana kwake kiasi cha kwamba hawezi kuongelea hadharani. Umeona tofauti hapo?

Huwa nasikitika sana, nikienda disco, unaona kabisa janamme lina mke na watoto, lipo disco na totos nyingine na anajua unamjua mke wake na labda utamueleza lakini haogopi kabisa, Hivi kweli hapo unaweza kumlaumu mtoto wa kitanzania akianza kutafuta mzungu??? Anakuwa ni kwamba ameamua hataki kuumizwa roho yake wala akili yake ana anataka kuishi maisha yake in peace.

Sio kwamba wazungu hawacheat au na wao sio washenzi wakati mwingine, tofauti ni kwamba hiki sio kitu cha kawaida kwao na hata akiwa mshenzi basi huu ni samaki mmoja mmbovu,inabidi tu awekwe kwenye kapu la pekee…lol…

Mwanaume wa kitanzania, kama hajatembea na rafiki zako,au mtu ambae unamjua basi haoni raha kabisa,

And whats worse, wanaume wa kitanzania haachi mke wake hata siku moja, atamtesa mke wake miaka kibao lakini hamuachi..yani mmbongo atakufanyia vituko weeeee mpaka utaondoka mwenyewe utarudi kwenu, but mzungu akipata mtu nje, atakuja kukwambia on your face, i don’t love you anymore,I love somebody else. Ofcourse inauma sana but atleast utakuwa umeachwa with respect, lakini kaka zetu atamake sure amekutoa all your dignity, kakuabisha mji mzima, amekutoa confidence yote ndio anakuacha…lol…

Na wasichana wengine wameniambia pia wanachukia tabia za kaka zetu za kufanya nao ngono alafu wanakaa bar na kuanza kuhadithia rafiki zao, Yule demu yuko hivi yuko vile, huu mji ni mdogo sana, unaingia sehemu unadhani umevaa nguo kumbe watu wanakujua ulivyo ukiwa uchi…

Basi siku hizi utawasikia wanaume wa kitanzania wanatukana hawa wanawake wetu wanatamaa sana, sijui wanawafatia nini wazungu,kila mtu mzungu,kila mtu mzungu. Kaka zetu you are the best, lakini badilisheni tabia zenu….

Kuwa na wanawake wengi sio haki yako.sana sana ni kujitafutia magonjwa na kumpelekea mkeo asie na hatia.

Tunawapenda sana, lakini anzeni kutu-treat with respect ,love and humanity. Ni hayo tu wadau kwa leo ambayo nimeweza kuyaelewa ndani yah ii issue nzima ya wanawake wa kitanzania na wazungu…….
wewe una yapi mdau?

Sunday, January 24, 2010

SALA YA LEO NI KUWAOMBEA WATU WOTE DUNIANI!!!

Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Je? unajua hapa chini ni lugha gani??? zawadi nono itatolewa.

Yethi Maria ogcwele igrasiya, iNkosi inawe, ubusisiwe wena esifazaneni, ibusisiwe nenzalo yesisu sakho uJesu. Maria ocwebileyo, Nina kaNkulunkulu, mawusikhulekele thina zoni, kalokhu nasesikhathini sokufa kwethu. Amen.


Var hälsad Maria, full av nåd.
Herren är med dig.
Välsignad är du bland kvinnor
och välsignad är din livsfrukt Jesus.
Heliga Maria, Guds Moder,
be för oss syndare
nu och i vår dödsstund.
Amen

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI HII YA NNE IWE NJEMA KWA WOTE!!!!

Friday, January 22, 2010

MZIKI NI MOJA YA MAISHA YETU LEO NGOJA TUMSIKILIZE DADA HUYO SOPHIA GEORGE!!



Mwaka ulikuwa 1992 kulikuwa na sherehe, katika ukumbi wa sherehe Wilima sec.school. EEhhh!! bwana we wacha watu wajimwage kwa mziki wa dada huyu. Kwa hiyo leo nimekumbumbuka sana Wilima-Matetereka na hasa siku ile. Ebu sikilizeni nawatakieni usikilizaji mwema na pia ikibidi uchezaji mwema. Muwe na wakati mzuri wa mwisho wa juma hili. Nataka kusema tuanza mwisho wa juma na muziki. TUTAONANA WAKATI MWINGINE!!!

Thursday, January 21, 2010

SWALI:- NI VYAKULA GANI KATIKA KABILA LAKO AMBAVYO UKILA UNAONEKANA WEWE NI MASKINI WA KUTUPWA?

Kila kabila lina mila na desturi zake kuhusu vyakula. Kuna vyakula akina mama na watoto hawatakiwi kula kutokana na mila hizo. kwetu Ruhuwiko,Litumbandyosi, Kingoli ukila MANGATUNGU(aina ya upupu)au ukila ugali wa BUNDURA(mihogo ya kuvundika) ukila ....unaonekana wewe ni maskini sana. Pia nimeishi kule Ubenani na wao walikuwa wanakula sana MAKANDE(ng´nde)na kuna makabila waliona kuwa wao ni maskini sana. Katika utafiti nimegundua/nimekikuta kitu kama hicho Usukumani, kwa wasukuma wa sehemu za Maswa mpaka Mwagala njia ya kulelekea Meatu ambapo mtu akionekana anakula ugali wa MTAMA anaonekana amechacha ile mbaya!

Je? hali ikoje kwa makabila yenu? Je? wasukuma (najua wamegawanyika; wa Bariadi, Malya, kahama, mwanza, tabora nk) wote wana mila hizi?

Tuesday, January 19, 2010

PIACHA YA LEO:- NAKUMBUKA ZAMANI NILIPOKUWA MDOGO!!!

Leo nimekumbuka nilipokuwa mdogo kwenda mstuni kuokota kuni, na hapo ujue ukirudi inabidi uende mtoni/kisimani kuchota maji. Wakati huo huo maharage yapo jikoni inabidi uchochee na kisha inabidi kutwanga mihogo. Ama kweli tumetoka mbali!!! Haya ndio maisha tuliopitia wengi huwa najiuliza sijui ni muda gani nilisoma?....!!

Sunday, January 17, 2010

MADA YA “SITARAJII KUWA MWANAHARAKATI” NAOMBA KUTOA HOJA

Makala yangu niliyoiweka hivi karibuni niliyoipa kichwa cha habari kisemacho Sitarajii kuwa mwanaharakati, imeleta changamoto kubwa sana kiasi kwamba nimeshindwa kuiacha ipite hivihivi. Kwa yule ambaye hakupata fursa ya kuisoma anaweza ku bofya hapa na kujikumbusha.

Nimesoma maoni ya wadau wote kwa umakini kabisa na pia nimefurahishwa sana na barua ya mdogo wangu Koero aliyoiweka hapo kibarazani kwake na kuipa kichwa cha habari kisemacho Dada Yasinta nimeishitukia janja yako, unaweza kubofya hapa kumsoma. Katika barua hiyo, pamoja na utani mwingi lakini kuna mambo ya msingi kabisa yaliyojitokeza ya kujadili kwa kina.

Nakumbuka nilipokuwa likizo nyumbani Songea mwaka juzi nilikutana na utitiri wa taasasi nyingi zisizo za kiserikali maarufu kama NGOs. Kila taasasi ilikuwa imelenga jamii fulani. Nilikuta NGOs, za Ukimwi, unyanyasaji wa wanawake na watoto, za wajane, za kidini, za kilimo, za afya, za walemavu, ilimradi kila eneo linaloonekana kama litavutia wafadhili limeguswa na hizi NGOS.

Binafsi sikushughulika sana kutaka kujua manufaa yanayopatikana kupitia hizi NGOs, kwa sababu ya labda ya majukumu niliyo nayo wakati nilipokuwa likizo.
Baada ya mtundiko wangu wa hiyo makala ya kukanusha kuwa na nia ya kuazisha NGOs, Mdogo wangu Koero na kaka Bwaya wakaja na hoja kuwa sio NGOs zote zilizo na malengo yaliyokusudiwa.

Kwamba NGOs nyingi zimeanzishwa kinafiki na wamiliki wake ni wasanii tu kwa ajili ya kutaka kutafuna fedha za wafadhili kwa mgongo wa kusaidia jamii fulani.
Hata hivyo kaka yangu Chacha Wambura na yeye akaja na hoja nyingine, kwanza hakupinga hoja iliyotolewa na Koero na Bwaya pamoja na wadau wengine, bali yeye alikwenda mbali zaidi akitaka mjadala huu ujadiliwe kwa mapana. Chacha Wambura anadai kuwa kuna wakati wafadhili wanatoa $ 5,000 kwa ajili ya mradi halafu wanatumia $15,000 kwa ajili ya kufanya Monitoring na evaluation.

Chacha hakuishia hapo akazidi kubainisha kuwa unaweza kusikia zimetolewa bilioni kadhaa za dola kama msaada katika mradi fulani lakini asilimia 85 ya msaada huo ni technical support ambapo wanaotoa hiyo technical support ni wao hao hao yaani wafadhili, kwa hiyo utaona kuwa kuna mlolongo wa unafiki kutoka kwa hao wafadhili mpaka wanaotumia yaani wenye hizo NGOs.
Kitu kingione kilichojitokeza ni wamiliki wa hizo NGOs, ambapo inasemekana wengi wao ni wastaafu, waliotoka serikalini au world bank, ambao wanajua namna ya kuandaa makabrasha na kupata hizo fedha za wafadhili.
Wengine wanaotajwa ni vijana walioshindwa kujiajiri kulingana na taaluma zao, na kutokana na kuonekana kuwa NGOs ni njia ya mkato katika kujitengenezea fedha za chap chap kutoka kwa wafadhili, vijana wengi wamekimbilia huko na ndio sababu ya kukuta kuna utitiri wa hizo NGOs lakini tija hazionekani

Jamani mimi ni muongoza mjadala tu hapa na nilichoandika ni mnyumbulisho wa kile kilichozungumzwa na wachangiaji kwenye mada kuu. Je wadau mnasemaje juu ya hizi hoja zilizojitokeza?
Nawasilisha
NA NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA TATU YA MWAKA 2010 IWE NJEMA KWA WOTE!!!

Saturday, January 16, 2010

LEO NI SIKU ALIYOZALIWA MTAKATIFU SIMON KITURURU!!

Napenda kukutakia kila la heri kwa siku hii maalum. Yaani ni tarehe ambayo ulifungua macho yako katika ulimwengu huu. Ila sina uhakika kama ilikuwa siku ya jumamosi pia. Nakuombea Mwenyezi Mungu akujalie afya njema wewe na familia yako. Na zaidi ya yote akujalie baraka zake kwa kadri ya mahitaji yako.

Friday, January 15, 2010

HILI LIMENITATIZA, NAOMBA MSAADA WENU

Habari zenu wanablogu na wasomaji wa blogu hii. Kama wengi waniitavyo Kapulya kutokana na maswali yangu niwaulizayo.

Ni juzi juzi tu nilikuwa naongea na rafiki mmoja wa nyumbani Tanzania. Akaniambia kuwa atakuwa off (hatafanya kazi kwa muda wa siku kadhaa) kwa vile alifanya kazi wakati wa sikukuu. Nikamuuliza kama zile siku za sikukuu alizofanya kazi hakulipwa? Akanijibu hakulipwa. Nilishangaa sana na nikaona kweli dunia ni ya ajabu kwani hapa Sweden mtu kama unafanya kazi siku za sikukuu mshahara unaongezeka yaani kama unapata 100kr kwa saa basi utapata 200kr kwa saa.

Na mimi nilikuwa nafikiri sheria hii ipo sehemu zote ulimwenguni. Swali langu ni hili je? hii sheria ya kutolipwa wakati wa sikukuu TZ tu na kama ipo je? ni kwa wafanyakazi gani? nina maana hata wafanyao kazi serikalini?

Thursday, January 14, 2010

Mitindo tofauti ya kuonyesha hasira

Ana hasira

Hebu fikiria kuhusu mwanao huyu. Wamekuja wageni nyumbani kwenu na unamwambia mwanao awaletee wageni kinywaji. Ukweli ni kwamba hakuna vinywaji huko kwenye jokofu. Badala ya kukuita pembeni na kukueleza hali halisi, mwanao huyo ambaye ni mkubwa kiumri, anakuelewa hapo hapo mbele ya wageni kwamba, hakuna vinywaji. Je, utafanyaje baada ya hatua hiyo?

Kwa sehemu kubwa, baada ya kukerwa kwa kwa namna hiyo, uwezekano ni kuchukua hatua moja kati ya hizi tatu zifuatazo. Hii ina maana kwamba, huwa tunaonyesha hasira zetu kwa njia kuu tatu. Kuna kukasirika, ambako hufuatwa na utulivu baada ya mkasirikaji kukagua na kufanya tathmini ya mazingira. Baada ya kutathmini huko, mkasirikaji huamua kuahirisha hasira zake hadi pale mazingira yatakaporuhusu. Kwenye huu mfano wetu, mkasirikaji atasubiri wageni waondoke ndipo amkaripie mwanaye.

Bila shaka hata wewe (kwa kutegemea malezi au kiwango chako cha hasira) umeshawahi kuahirisha hasira. Kama siyo wewe, umewahi kuona mtu akiahirisha hasira. Mara nyingi wanandoa wenye busara wanapokuwa kwenye hali ya hasira na akaingia mgeni huwa wanaahirisha hasira zao.

Kuna kukasirika ambako hakuangalii mazingira. Mtu huonyesha hasira zake popote na kufanya mambo ya ajabu mahali ambapo kamwe asingetarajiwa kufanya hivyo. Mtu kishakasirika anaropoka au kufanya mambo mengine yenye kufedhehesha sana. Hapa mkasirikaji hajali matokeo ya kauli na vitendo vyake vya hasira.

Kuna kukasirika ambako kila mtu anweza kubaini kwamba fulani amekasirika, lakini mtu huyo aliyekasirika hatoi kauli wala kutenda jambo lolote lenye kuonyesha kukasirika. Pamoja na ukweli kwamba, kuna kila dalili kuwa mtu amekasirika, hafanyi au kutoa lkauli yoyote yenyewe kuthibitisha kukasirika kwake. Hata kama atatoa kauli yoyote itakuwa tu ni ya kuonyesha kukereka bila kutoa maneno makali.


Kuna wale ambao wanapokasirika hulia sana, huvunja vifaa, hupiga ngumi ukutani au hupiga mateke hovyo. Ni kwa kufanya hivyo tu, ndipo hasira zao zinapopungua au kwisha. Lakini wapo ambao wanapokasirika hucheka sana, badala ya kununa au kulia. Wanapomaliza kucheka hununa ghafla na hapo hufanya chochote.

Ni wazi kila mmoja kati yetu anayo namna yake ya kuonyesha hasira, ingawa hata hivyo uonyeshaji huo hutegemea hali na mazingira tofauti. Je, ni nani aliyemuudhi mtu, wapi, kwa sababu ipi na mengine. Lakini bado ukweli unabaki palepale kwamba, mara nyingi namna ya mtu kuonyesha hasira yake huwa ni ileile bila kujali mazingira au hali.

Makala hii nimeichukua kutoka kwenye kitabu cha Maisha na Mafanikio kilichoandikwa na Hayati Munga Tehenan ambaye alikuwa ni Mwalimu mzuri wa maarifa ya Utambuzi akitoa elimu hiyo kupitia magazeti yake ya Jitambue, vitabu na semina zake nchini Tanzania kabla ya kufariki dunia

Tuesday, January 12, 2010

SITARAJII KUWA MWANAHARAKATI

Nimekuwa nikipokea email kutoka kwa baadhi ya wasomaji wa blog hii ya MAISHA wakinitaka nijiunge na Organization za kutetea haki za wanawake za huko nyumbani au nianzishe NGO yangu ya kutetea haki za wanawake na watoto. Ni email ambazo zimenitia moyo, kuona kuwa kumbe kile ninachoandika kinaigusa jamii, na huenda kuna wasomaji wengi hujifunza kupitia maandishi yangu hayo.

Watumaji wengi wa email hizo wamekuwa wakinipongeza kwa kuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake, lakini pamoja na kunipongeza pia wamenipa ushauri huo wa kunzisha NGO yangu au kujiunga na NGO za huko nyumbani ili kupigania haki za wanawake hapo nyumbani au hata ulimwenguni kote.

Bila shaka hata wewe unayesoma hapa huenda pia ulikuwa na wazo kama hilo la kunishauri nianzishe hicho kinachoitwa NGO, kwa kuona kuwa nimekuwa mwanaharakati kutokana na kuzungumzia sana habari za manyanyaso ya wanawake hapo nyumbani Tanzania.
Sitaki niwakatishe tamaa, lakini ni vyema nikaweka bayana kuwa lengo la kuandika makala za kutetea haki za wanawake sio kwamba ninayo dhamira ya kuanzisha NGO, sijawahi kuota na wala kuwaza kufanya kazi hiyo. Binafsi naamani kwamba, kuwa mwanaharakati haimaanishi kuwa na Organization. Kwamba huwezi kuwatetea wanawake na watoto isipokuwa mpaka uwe na NGO. Mimi siamini hivyo, bali naamini kuwa mtu yeyote, akiwa mahali popote kwa utashi wake anaweza kuwa mwanaharakati wa kutetea haki, ziwe ni za wanawake, watoto au hata jamii kwa ujumla, na sio lazima mtu huyo awe na Organization.

Naamini kuwa ile kuandika makala tu, iwe ni kupitia magazetini , ukurasa binafsi, yaani Blog au kuzungumza redioni au hata katika luninga inatosha kabisa kuwa mchango katika kuibadilisha jamii kimtazamo.
Nimelizungumza hili maana nadhani kuna baaadhi ya wasomaji wa blog hii wanadhani kuwa huenda ninavyoandika makala za kutetea haki za wanawake ni kamchakato kangu ka kuelekea kuanzisha Organization yangu nitakaporeja nchini.
Kusema kweli sina wazo hilo kwa sasa, bali nafurahia sana, kile ninachoandika na jinsi wasomaji wanavyotoa maoni yao huku kukiwa na tofauti za kimtazamo. Kusema kweli huwa najifunza mengi kupitia changamoto za wasomaji wa blog hii.

Labda ingekuwa ni vyema nikaweka bayana kuwa, mimi nimfuatiliaji wa habari za hapo nyumbani Tanzania, kupitia magazeti na mitandao tofauti tofauti, na hata ninapokuwa nyumbani Tanzani huwa nanunua vitabu na nasoma sana magazeti mengi ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watu wa rika tofauti na kada tofauti ili kupata uzoefu wao juu ya kile ninachokisoma kupitia vyombo vya habari vya nyumbani.

Mimi nimezaliwa kijijini huko Lundo Nyasa na nimekulia kijijini kabisa Kingoli au Litumbandyosi mkoani Ruvuma, nimekulia kijijini kabisa, nafahamu maisha halisi ya mwanamke wa kijijini, kuanzia kulima, kukata kuni, kupika, na shughuli ndogo ndogo zinazofanywa huko vijijini. Pia nafahamu juu ya ndoa za mapema kwa wa watoto kike na athari zake kwa kuwa nimezishuhudia, nimeona wanawake wanaonyanyaswa na waume zao, nimesikia habari za wanawake kubakwa, kwa hiyo ninapoandika habari yoyote juu ya madhila ya wanawake, ni kutokana na uzoefu wangu, maana ninajua ninachoandika.

Huku ughaibuni nilipo kuna visa na mikasa mingi sana, kuna mitandao mingi ya habari na vyanzo vya habari pia ni vingi, ninaweza kuandika habari za huku na zikavutia, kwani nimeshajaribu mara kadhaa, lakini kwanini niandike habari zao? Nimeona ni vyema nikiwa naandika habari za huko nyumbani kwa wingi ili jamii itambue kuwa japo niko huku ughaibuni lakini nayafahamu madhila yao, na niko tayari kuyakemea japo niko mbali.
Hata hivyo naomba nikiri kuwa nimevutiwa sana na wale wanaoniunga mkono kataka makala zangu. Nawashukuru sana na ninaomba msiache kunipa changamoto pale ambapo mtaona labda nimekosea au nimeteleza, kwani mimi sio mwanahabari bali ninapenda sana kuandika na ninafurahia kuandika yale yanayoigusa jamii kwani huo ndio mchangao wangu, pamoja na hayo sitaacha kale katabia kangu ka udadisi, yaani UKAPULYA, kwani huwa sioni haya kuuliza pale ninapokutana na jambo nisilolifahamu au lililonipitia kushoto.
Tuko pamoja
Mungu awabariki wote!!

Sunday, January 10, 2010

Aneth Mbilinyi: Mwanamke tajiri asiyejua kusoma wala kuandika

Aneth Mbilinyi
Asomesha watoto wake, na yeye aamua kuingia darasani
Habari hii nimeipata kutoka gazeti la Mwananchi. Na Tumaini Msowoya
Nimeipenda sana habari hii na nimeona ni vizuri niiweka hapa ili tujadali kwa pamoja.

UKITAKA kuwazungumzia wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, bila shaka hutaweza kuacha kumtaja Aneth Mbilinyi.
Mwanamke huyo ambaye ni msambazaji wa maji ya kunywa katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa, amejizolea sisa kutokana na uwezo wake wa kuendesha biashara kubwa.
Kuna msemo unaosema elimu ni ufunguo wa maisha, kwa mama huyu ni tofauti kidogo yeye hakupata elimu ya darasani lakini yeye anasema hajui kusoma wala kuandika, lakini amepata elimu ya maisha ambayo inamsaidia kuendesha shughuli zake za kila siku.
"Sijawahi kwenda shule hivyo kifupi sijui kusoma wala kuandika, lakini nina uwezo mkubwa wa kuendeleza biashara zangu. Mungu akipenda nitaanza darasa la kwanza wakati wowote,"anasema.
Anasema kabla ya kufikia mafanikio yake biashara, maisha yake yalikuwa magumu kwa sababu haikuwa rahisi kwake kupata ajira hakuwa na elimu ambayo ingemwezesha kufanya hivyo.
Aneth anasema ugumu wa maisha ulimpa changamoto hivyo akatafuta mtaji mdogo na kuanza bishara ya kukopesha vitenge ambayo aliiacha mapema kutokana na wengi kushindwa kumlipa madeni yake hivyo kuua mtaji.
Anasema baada ya kuachana na biashara hiyo alianza kusaga unga wa sembe ambapo alikuwa akiusafirisha jijini Dar es Salaam alikokuwa na wateja wengi.
Hata hivyo,biahsara ya sembe ilimshinda kwani nayo haikumpa mafanikio yoyote kitu kilichomkatisha tamaa na kuamua kuachana nayo.
Mwaka 2000 Aneth alianza kuuza maji ya kunywa ambayo alikuwa akiyafuata katika kijiji cha Kidamali kiwandani kisha kuyasambaza Iringa mjini.
"Uaminifu katika biashara ya maji uliwafanya wamiliki wa kiwanda kunipenda hivyo wakaniongezea mtaji na nikawa na uwezo wa kuyasambaza mkoa mzima, na hapo nikaanza kuona mafanikio makubwa," anasema.
Anasema kuna wakati alikuwa akipewa mzigo mkubwa wa maji unaozidi milioni 20 na kuusambaza bila hasara yoyote licha ya kuwa hawajahi kuhudhuria darasa lolote.
"Hakuna asiyejua kuhesabu hela, kamwe sijawahi kudhurumiwa kwa sababu nipo makini sana kwenye biashara zangu," anasema.
Anasema miezi sita baadaye alifanikiwa kununua gari aina ya Fuso ambalo lilimwezesha kusambaza maji kirahisi zaidi tofauti na awali alipokuwa akitumia magari ya kukodi au ya kiwanda hicho.
Kutokana na kuwa makini katika uendeshaji wa bishara zake biasharayake ilizidi kukua na akafanikiwa kushi mashas mazuri pamoja na kuwasomesha watoto wake katika shule nzuri ili wasiishi maisha ya kubahatisha kwa kukosa elimu.
"Nilijibana sana japo faida iliyokuwa ikipatikana kutokana na baishara yangu ilikuwa kubwa, malengo yalianza kutimia taratibu na mpaka sasa namshukuru Mungu kwani namimiliki mamilioni ya fedha bila kuingia darasani, anasema.
Baadaye alinunua malori mengine mawili aina ya scania kwa ajili ya kusiadia kusambazia bidhaa zake.
Mbali na mradi wa kuuza maji, Aneth anamiliki maduka ya vyombo na bidhaa nyingine huku akisema siri kubwa ya mafanikio yake ni Mungu na kujituma.
"Hakuna mafanikio yatakayokufuata mwanamke kama atakaa na kusubiri awezeshwe, lazima tukubali kufanya kazi kama watumwa ili siku moja tuishi maisha ya kifahari," anasema.
Anasema ingawa hajafikia malengo yake , lakini kwa hapo alipo anamshukuru Mungu kwani tayari amejenga nyumba za kisasa, gari kwa ajili ya usafiri na watoto wake wamesoma.
Bila elimu anawezaje?
"Nikubali nikatae, elimu ni kila kitu, napata shida kwenye kazi zangu kwani huwa nalazimika kukariri mambo kichwani ili nisikosee mahesabu, mfano mzuri ninapoenda benki," anasema.
Anasema kukariri namba na mambo mengine ya kibiashara vimekuwa vikimsaidia katika biashara zake.
Pamoja na mambo hayo, mwanamke huyo anasema amekuwa akishirikiana na mtoto wake wa kwanza ambaye amehitimu shahada ya Uchumi na bishara Chuo Kikuu cha Tumaini.
"Kwa sababu sikubahatika kusoma, wanangu nimejitahidi kuwasomesha hadi watakaposhindwa ili wasije kuishi maisha ya kubahatisha hasa wakati huu ambapo elimu inaonekana kuwa kila kitu," anasema.
Hata hivyo, anasema taasisi za fedha zinatakiwa kupunguza masharti ya mikopo ili kumwezesha mwanamke mjasiliamari kumudu kuchukua mikopo hiyo pamoja na kurejesha.
"Mara nyingi taasisi za fedha huhitaji mkopaji awe na mali isiyohamishika kama nyumba ama hati ya kiwanja, sharti hili ni gumu kwa wanawake walio wengi jambo ambalo huwakatisha tamaa wanawake kuchukua mikopo," anasema.
Anasema alifanikiwa katika biashara yake kwa sababu kiwanda kilimuamini na kuanza kumpa bidhaa kwa kumkopesha, lakini kama isingekuwa hivyo hali ingekuwa tofauti kutokana na ugumu wa mashari ya mikopo.
Anaongeza kuwa taasisi za fedha zina wajibu wa kutoa elimu kwa wanawake wajasiliamari ili kuwawezesha wanawake hao kutambua faida na hasara ya biashara zao.

NALIA:- NA JENNIFER MGENDI:- JUMAPILI NJEMA WOTE!!!

Saturday, January 9, 2010

HONGERA DADA AJUNA NA KAKA MATHEW SENGA- Mwanasosholojia kwa siku yenu ya kuzaliwa!!

Hongera mwanasosholojia

Hongera dada Ajuna :-Dada wa Musee wa Changamoto
Ni furaha kwa blog ya MAISHA kuwapongezeni kwa siku hii malumu kwani ni pia wote tumezaliwa mwezi mmoja na wiki moja. Hongereni sana, muwe na siku nzuri

Thursday, January 7, 2010

WANAWAKE NA SHERIA YA KUBAKWA


Nilipokuwa nyumbani Tanzania mwaka juzi, niliwahi kuzungumza na binti mmoja ambaye ni mhitimu wa sheria chuo kikuu. Katika mazungumzo yetu nilimuuliza juu ya tatizo la ubakaji hapo nchini kuwa sheria za nchi zinasemaje juu ya makosa ya aina hiyo?
Kama nilimnukuu vizuri, binti yule aliniambia kuwa sheria ya ubakaji ipo na inafanya kazi, kwa mujibu wa maelezo yake, alidai kuwa sheria hiyo inamlinda mwanamke kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mfano hata kama mwanamke aliridhia kufanya kitendo cha kujaamiana na mwanamume, na baada ya kitendo kile bila kujisafisha akaenda polisi na kuripoti kuwa amebakwa, na ikathibitika kupitia vipimo vya DNA kuwa (manii) shahawa zilizaokutwa katika uke wa mwanamke yule ni ya mwanaume mtuhumiwa, basi moja kwa moja mwanaume huyo atakuwa matatani.

Kwani kwa mujibu wa sheria inasema, kama mwanamke yule angekuwa ameridhika kuingiliwa na mwanaume mtuhumiwa basi asingekwenda kuripoti polisi. Nilimuuliza mbona makosa ya aina hiyo yapo sana hapa nchini na yanaandikwa sana katika vyombo vya Habari? Alinijibu kuwa tatizo ni ukosefu wa ushirikiano kati ya wanawake wanaobakwa na polisi kutokana na wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo kuona haya kwenda kuripoti, hususani wale walioolewa, huogopa kutoa taarifa katika vituo vya polisi ili kuepuka kuachika pindi waume zao wakifahamu. Polisi nao kwa upande wao, hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa waathirika wa vitendo hivyo kwani huwakejeli na kuwapuuza kwa madai kwamba waliyataka wenyewe.

Tulizungumza mambo mengi yanayofanana na hayo, na kusema ukweli yule binti alinifumbua macho kwa kiasi fulani, kwani kabla ya hapo sikuwa nikiyafahamu hayo.

Bila shaka wasomaji wa blog hii mtajiuliza kulikoni leo kuzungumzia jambo hili.
Ni kwamba nimekuwa ni mfuatiliaji sana wa habari za huko nyumbani na nimekuwa nikishangazwa sana na kuripotiwa kwa matukio ya watu kubakwa kwa kiasi cha kutisha, niliwahi kuweka habari moja ambayo niliichukua kutoka katika gazeti la Mwananchi juu ya waendesha pikipiki wa kule Songea maarufu kama yeboyebo jinsi wanavyowabaka wanawake pindi wanapowabeba kuwapeleka katika safari zao kwani usafiri huo hutumika kama taxi kule vijijini.
Ni jambo la kushangaza kuwa pamoja na kuwepo sheria hii lakini matukio ya aina hiyo yapo na hayakomeshwi.

Hata hivyo lipo jambo moja ambalo nilijiuliza. Hivi kama kubaka ni kitendo cha mwanaume kulazimisha kumuingilia mwanamke bila hiyari yake, je kwa wanandoa inakuwaje? Ikumbukwe kwamba sheria hiyo haikutenganisha kati ya wanandoa na wale wasio wanandoa, sheria imesema tu kwamba, kama mwanamke akiingiliwa na mwanaume bila matakwa yake akienda kuripoti katika vyombo vya sheria, basi mwanaume yuko matatani.
Kama sheria inamlinda mwanamke kwa kiasi hicho, basi wanawake wengi sana walioko katika ndoa hubakwa na waume zao karibu kila siku, kwani wakati mwingine wanawake walio katika ndoa hulazimika kukubali kufanya tendo la ndoa nje ya utashi wao. Mila na desturi zetu zimemnyima mwanamke uwezo wa kusema hapana pindi mwanaume akitaka, kwani neno “geuka huku” sio ombi ni amri ambayo inatakiwa kutekelezwa bila kupingwa. Bila shaka mtakubalina na mimi kuwa mila na desturi zetu zinatufundisha kuwa kuolewa kwa mwanamke ni kwenda kutumika kama chombo cha kumstarehesha mwanaume na kumzalia watoto, na ndio maana kama ikitokea mwanamke akiolewa halafu asipate mtoto, anayeangaliwa na kushutumiwa ni mwanamke na sio mwanaume kwani aliolewa ili amzalie mwanaume watoto ikiwa ni pamoja nakumstarehesha.
Hata kama mwanaume ndiye mwenye tatizo, bado jamii itamtetea. Niliwahi kusimuliwa kuwa yapo baadhi ya makabila hapo nchini mwanamke hulazimishwa kutoka nje ili amzalie mwanaume watoto ikiwa kama mwanaume amekosa uwezo wa kutia mimba, lengo ni kulinda heshima ya mwanaume, na jambo hilo hufanywa kwa siri sana.

Wanaume huamini kwamba wanazo haki zote kwa miili ya wake zao, lakini wake zao hawana haki hizo, na kutokana na mfumo huo dume wanawake nao wameaminishwa kuwa wenye mamlaka na miili yao ni waume zao.

Kwa kawaida wanawake huishi kihisia, hivyo inapotokea kuathiriwa kihisia na hamu ya kushiriki tendo la ndoa hupotea, hivyo wanaume wanapowambia, “geuka huku” hulazimika kufanya hivyo sio kwa mapenzi yao bali hutekeleza ili kuepusha shari vinginevyo itakuwa nongwa.

Hivi ni mara ngapi tumesikia kupitia vyombo vya habari kuwa mwanaume kamuua mkewe kwa kunyimwa unyumba? Ni mara nyingi tu, lakini binafsi sijawahi kusikia mwanamke kamuua mumewe kisa kanyimwa unyumba, sidhani!


Naamini kuwa kama wanawake walioolewa wataamua siku moja kuwashitaki waume zao kwa kubakwa kama sheria inavyoruhusu, basi magereza hapo nchini yatajaa mpaka pomoni, maaana hakuna atakayebaki, lakini, thubutuuu….nani ajaribu, jamii yote itamhukumu kuwa amekosa adabu kwa mumewe.

Wednesday, January 6, 2010

MAISHA YA MUME,MKE NA WATOTO:- MASWALI YA LEO!!

Hivi ni kwa nini watu wawili wanaopendana wakifunga ndoa wanabadili majina yao ya ukoo au mke anabadili jina lake la ukoo na kuitwa jina la ukoo la mume wake?

Na kwa nini watoto huitwa jina la ukoo wa baba sio la mama?

Nimesoma post ya Kamala ya 7/12-09 yenye kichwa cha habari "Ndoa":- Kwa nini kuzaa watoto?

Amesema watoto sio wa baba wala wa mama. Swali langu ni hivi:- je? kwa nini kwanini baba na mama wachanapo watoto wanabaki kwa baba? Je ni kwasababu wanaitwa jina lake la ukoo au ni kwanini? Nitafurahi kama nikipata majibu kwani nimekuwa nikijiuliza sana na nimeona ni vema mnisaidie.

Tuesday, January 5, 2010

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA




Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama mpaka kufika siku hii ya leo na kuongeza limwaka limoja zaidi. Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi.

Sunday, January 3, 2010

NILILAZIMIKA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Ni furaha isiyo kifani kutumiwa barua kama hii na ukizingatia ndio mwaka umeanza tu. Kwa vile napenda kugawana na wasomaji wengine wa blog hii na pia wanablog wenzangu nimeona niufikishe ujumbe huu:- Karibuni sana KUSOMA hapa.


Kwako dada Yasinta, ni matumaini yangu kuwa umzima wewe na familia yako huko uliko.
Dada mimi ni msomaji wa blog yako na nimejifunza mengi sana kupitia blog yako hii ya maisha, kwani mijadala unayoianzisha katika blog yako imekuwa ikileta changamoto na migongano ya mawazo kiasi kwamba nimekuwa nikijifunza mambo mengi kupitia mijadala hiyo.

Kusema kweli nimekuwa ni mfuatiliaji wa blog yako na kupitia blog yako hiyo ya MAISHA nimekuwa nikijifunza mambo mengi juu ya maisha na mafanikio pia.

Mimi ninao uzoefu wangu ambao ningependa uuweke katika blog yako ili wasomaji waweze kujifunza kupitia uzoefu wangu huu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 37 na nina mke na watoto watatu. Kikazi mimi ni mtumishi serikalini na mke wangu by Professional ni mpishi na pia anao ujuzi kidogo wa ushonaji. Mke wangu alikuwa na ndoto za kumiliki biashara ya Catering wakati namuoa kwa sababu aliwahi kufanya kazi kwa mtu mwenye biashara hiyo alipokuwa kwao Mbeya kabla sijamuoa na kuhamia naye Dar, hivyo alitengetengeneza picha kuwa biashara ya Catering ndio biashara pekee yenye faida kubwa.

Ni kweli kuwa biashara ya Catering ina faida kubwa lakini inategema na mtaji utakaoanzishia biashara hiyo. Kusema ukweli nilikuwa na dhamira ya kumuanzishia biashara hiyo ya Catering na nilianza mchakato wa kutekeleza azma yangu, lakini nikakutana na vikwazo vingi sana, kwani ili kuanzisha biashara hiyo ni lazima uwe na vifaa kama Serving Dishes, maturubai, viti na meza, vyombo vya kupikia, sahani, vifaa vya Mziki na MC. Kama ukimudu kuwa na vitu hivyo basi na faida yako itakuwa kubwa kwani shuguli utakazokuwa unapata zitakuwa ni kubwa na zenye kulipa faida kubwa. Kwa mfano hapa Dar shughuli kama harusi, Send Off, Kitchen Party, Misiba, na kumaliza misiba wengine huita kumaliza arobaini, Vipa imara achilia mbali semina ndogo ndogo za kidini na za NGO’s, zote hizo ni kazi ambazo zinategemea sana watu hawa wa Catering, lakini kutokana na mtaji wangu kuwa mdogo nikajikuta nikikwama kwa sababu nilikuta vifaa hivyo vinauzwa ghali kutokana na watu wengi kukimbilia biashara hiyo kwa kuwa inalipa.

Nilikata shauri kumfungulia biashara nyingine ili japo asikae bure bila kazi na pia kuokoa hizo pesa tusije tukazifuja bure. Kwa haraka, niliamua kuanzisha biashara ya ushonaji, pamoja na uuzaji wa vifaa vya ushonaji.

Awali nilipata upinzani mkubwa sana kwa mama watoto na hakupenda hilo wazo langu kabisa, nilipata wakati mgumu sana kumuelimisha mpaka akakubali lakini hakuwa na mwamko wa kuipenda kazi hiyo. Sikukata tamaa, niliendelea kumuelimisha huku nikiendelea kununua vifaa kama vyerehani vitatu na ya kudarizi kimoja pamoja na vifaa vya ushonaji vya kuweka dukani kwa ajili ya kuuza na vifaa vingine muhimu kama makabati nakadhalika na kulifungua duka hilo rasmi. Hata hivyo nilimuahidi kuwa ahadi yangu iko pale pale, nitamfungulia biashara yake ya Catering kama nilivyomuahidi wakati ukifika.

Hata hivyo mwanzoni hakuipenda biashara hiyo na nilikuwa kama vile namlazimisha kwenda dukani kufungua kila siku asubuhi, lakini sikukata tamaa.

MSHANGAO………..

Dada siku za karibuni biashara ikaanza kukua na wateja wakaanza kuja kwa wingi kununua bidhaa, na mtaji umeanza kukua sasa. Hivi karibuni katika mazungumzo yangu na yeye nikamwambia kuwa mpaka mwezi wa pili mwakani nitakuwa nimemfungulia biashara yake ya Catering kama nilivyoahidi, ili ndoto yake itimie, lakini kwa mshangao aliruka na kukataa kabisa kuwa hataki tena biashara ya Catering kwani ile biashara ya ushonaji ina faida na ameipenda sana.

Sikuamini masikio yangu. Unajua wakati nabishana naye kuhusu kuanzisha biashara ya ushonaji nilidhani yeye yuko sahihi kuwa hiyo biashara haifai, na ilikuwa nusura nikubaliane naye, ila kuna kitu huwa tunaita machale au mlango wa sita wa fahamu, ambao huwa nautumia katika kufanya maamuzi magumu.

Baada ya kutafakari sana niliamua kufungua hiyo biashara, na sasa nimepata jibu kuwa nilikuwa sahihi, maana ameuona ukweli kuwa wazo langu lilikuwa ni sahihi. Kuna msemo mmoja unasema kuwa mwanaume ni kichwa cha nyumba, ki ukweli sikuwa nauzingatia huo msemo kwa kuwa niliona ni dalili ya kujikweza na kuwadhalilisha wanawake, lakini nadhani hiyo dhana ina ukweli fulani.

Nimejifunza jambo moja, kuwa kuna wakati mwanaume analazimika kuwa dikteta ili kufikia maamuzi fulani magumu, hasa pale mke anapoonekana kupinga bila kutoa wazo mbadala au kutoa ushauri.

Sio kwamba wanawake hawawezi kutoa ushauri au wazo zuri, la hasha, ninachomaanisha hapa ni kwamba kuna wakati kunapohitajika maamuzi magumu, mume anatakiwa kupewa nafasi ili aamue. Ila inategemea tabia za mume huyo.

Inasemwa kuwa nyuma ya mafanikio ya mume kuna mke na nyuma ya anguko la mume kuna mke pia, lakini huwa najiuliza, je utamjuaje mke ambaye maamuzi yake yanakupeleka shimoni?

NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWAKA 2010 IWE YA FURAHA TELE!!

Saturday, January 2, 2010

MWAKA MPYA 2010!!!!!!!

Mwaka mpya huwa ni wakati wa malengo mapya na mwelekeo mpya. Kila binadamu ana malengo yake hapa duniani. Mimi nina malengo yangu na wewe pia una yako. Kila kukicha huwa tunajitahidi kuyatimiza. Tunapasua vichwa kujaribu kuyatimiza malengo yetu . Ndio maisha.

Bila shaka na wewe umeshaketi chini na kujiuliza swali hili:- ninataka kutimiza malengo gani mwaka huu? Je? ni kurudi shule kuongeza ujuzi? Je? ni kuoa au kuolewa? Je? ni kujitolea zaidi katika jamii yako? Je? ni kutunza na kulinda mazingira? Msururu wa malengo unaweza kuwa mkubwa. Kama kutimiza malengo fulani fulani ndio mkakati wako wa mwaka huu basi zingatia ushauri ufuatao:-

Weka malengo yanayotimizika au yenye uhalisia-Jiangalie ulipo, angalia vitndea kazi ulivyonavyo, tizama kwa makini ujuzi ulionao kisha yapime vizuri malengo yako.

Jiulize swali au mawswali:- Nitayatimizaje malengo yangu? ukishafanya hivyo jiwekee utaratibu wa jinsi ya kutimiza malengo yako. Wazungu wanasema weka vyema Action Plan yako.

Nenda utaratibu -Mwaka ndio kwanza umeanza, yakaribiribie malengo yako kwa mwendo wa taratibu. Usiwe na haraka wala pupa. Si unakumbuka kwamba mambo mazuri hayataki haraka?

Usiogope kurekebisha malengo-Kadri mwaka unavyoanza kusonga mbele, unaweza kugundua kwamba huenda kutimiza malengo fulani. Hiyo inawezekana kutokea kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kiafya au kibinafsi. Usihofu kurekebisha malengo yako.

Usiogope kushindwa-Yawezekana kabisa ukashindwa kutimiza malengo fulani fulani. Kwa sababu zaweza kuwa kama hizo nilizozitaja hapo juu, usiogope. Cha muhimu ni kujaribu na kujaribu na kujaribu. Jitahidi kadri unavyoweza, nina uhakika ukijaribu utafanikiwa kwa hiyo mwisho wa siku hadithi ya kushindwa wala haitokuwepo.

La muhimu ni kuomba msaada inapobidi yapo mambo mengine ambayo hutoweza kuyatekeleza peke yako. Hilo linapotokea, usiwe mgumu kuomba msaada.

Kwa mara nyingine tena nawatakieni wasomaji wa blogya MAISHA kila la kheri katika mwaka huu wa 2010