Tuesday, September 29, 2015

SALAMU ZA MAKABILA YETU TANZANIA

 


Wasomaji wapendwa wa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO, nimejaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini Tanzania. Kama tujuavyo ni kwamba kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini. Nami nimeamua kuangalia zaidi salaam, hasa za asubuhi, kutokana na utafiti wangu pia kwa msaada wa marafiki nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumika katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:

KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi
KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi
KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi
KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi
KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi
KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi
KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi
KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi
KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi
KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi
KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi
KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi
KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi
KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi
KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi
KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi
KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi
KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi
KIMATENGO: Ja kujumuka = Habari za asubuhi
KIKURYA:  Agha nyinkyo = Habari za asubuhi
KIPOGORO: Za mandawila = Habari za asubuhi
Hayo ni baadhi tu ya makabila machache katika mengi yaliyomo nchini kwetu, unaweza ongezea salaam za makabila unayofaham wewe ndugu yangu

Friday, September 25, 2015

TUMALIZE JUMA HILI KWA USEMI HUU.....!!!

Kila kitu/mtu kina/ana uzuri wake, lakini sio wote wanaouona usuri huo!
BASI NGOJA MIMI /KAPULYA WENU NIWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA JUMA HILI.

Wednesday, September 23, 2015

HEBU LEO TUANGALIE KICHEKESHO HIKI CHA MZARAMO V/S MCHAGA...KARIBU

Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: "unaumwa nini?"
MCHAGA: "Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa.."
MZARAMO: "sawa, toa laki kabisa.."
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; "Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu.."
MCHAGA akanywa akatema faster; "Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?"
MZARAMO: "Umepona karibu tena.."
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa.."
MZARAMO akamwambia "hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..'
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..'
MZARAMO: "nesi naomba kikopo no.27.."
MCHAGA: "ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?"
MZARAMO: "UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.
PANAPO MAJARIWA TUTAONANA TENA!

Monday, September 21, 2015

NIMEONA KUWA NA KIPENGELE KIPYA NACHO NI UTAMADUNI WA MTANZANIA/AFRIKA NA NIMEONA IWE JUMATATU NA KWA KUANZA NIMEONA TUANZA NA KUSIKILIZA NGOMA HII YA KUNYAKYUSA....KUTOKA MBEYA


Kama tunavyotambua Tanzania ni nchi yenye makabila mengi ni 121 kama sijakosea. Kwa hiyo kila kabila lina utamaduni na mila zake kuanzia kwenye chakula  hadi ngoma. Kwa hiyo leo nimeona tuwatembelee ndugu zetu Wanyakyusa na ngoma hii ya kuvutia.
TUONANE TENA JUMATATU IJAYO NA KABILA JINGINE!

Friday, September 18, 2015

KARIBUNI TUJUMUIKE CHAKULA CHA MCHANA HUU. .....

Ni wali, kebichi su wengine wanasema kabichi  na maharage tena ya kutoka Mbinga. Karibuni sana ndugu  zanguni. Na pia nichukue nafasi kuwatakieni mwisho mwema wa juma.

Monday, September 14, 2015

VYAKULA VYETU VYA ASILI-----

Ulijua ya kwamba chakula kinachopikwa kwenye chungu ni kitamu sana kuliko kupika kwenye sufuria? Basi ngoja niwatakieni JUMATATU NJEMA NA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!

Friday, September 11, 2015

TUMALIZE WIKI KWA USEMI HUU...

Kuna njia moja tu ya kuwa na furaha, nayo ni kuwaacha kuwa na wasiwasi juu ya jambo ambalo halipo juu ya uwezo wetu.
Panapo majaliwa tutaonana tena...wenu Kapulya

Wednesday, September 9, 2015

TASWIRA YA MLIMA KILIMANJARO

Mlima wetu Kilimanjaro

Labda tu tusikilize hapa ni vipi kupanda mlima Kilimanjaro

Tutaonana tena tupo pamoja!

Tuesday, September 8, 2015

PICHA YA WIKI:- KUWA MAKINI UNAPOFUNGUA GARI YAKO !!

Hapa kazi ipo fikiria huyo nyoka yupo pia ndani ya gari, au kwenye kiatu na pia hata chooni, Ndugu zangu tuwe makini  tusikurupuke tu tuchunguze kwanza....Hata kitandani uendapo kulala chunguza kwanza......Niwatakie kila la khri na panapo majaliwa tutaonana tena...Kapulya:-(

Sunday, September 6, 2015

NNAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TISA (9) KWA USEMI HUU

Ukisha muamini Mungu basi yatosha, ya walimwengu waachie wenyewe!!
BARAKA NA UPENDO WA BABA MUNGU MWENYEZI VWEE MIOYONI MWETU KILA WAKATI.

Friday, September 4, 2015

MATUNDA NI MUHIMU KWA AFYA ZETU!!

Nimeyatamani kweli machungwa...Niwaambie kitu nilipokuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza na pili. Shuleni kwetu Lundo kulikuwa na miti mingi sana ya matunda mbalimbali mojawapo machungwa...Basi nakuambieni baada ya shule unaaga nyumbani kwenda kuchota maji au kuokota kuni kumbe kula machungwa ya shule...shhhh.:-(.....Ila mmhhh ilikuwa ukikamatwa na mlinzi basi ni viboko tu ...Kaaazi kwelikweli:-) PAMOJA DAIIMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. Kapulya.

Thursday, September 3, 2015

SWALI NILILOULIZWA NA MSOMAJI /MFUATILIAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO:-

Swali lenyewe lipo hivi:- Hivi ni  kitu gani akina mama/wanawake kinawafanya wampende mtoto fulani zaidi kati ya watoto wao wa kawazaa?
Akaendelea:- Utamkuta mama ana watoto wanne, lakini anampenda mmoja zaidi ya wengine? Hii inakuwaje kwa upande wako? akanipa hili swali mimi......akaendelea nakuuliza kwa kuwa nadhani una watoto.....halafu akaendelea kusema ....Pia nadhani utakuwa umeshawahi kuisikia hii au inatokea.
Jibu langu lilikuwa kama ifuatavyo:- Binafsi kama mama nawapenda wanangu sawasawa na sijawahi kufikiria  KUWAPENDA  TOFAUTI.
Baadaye nikakumbuka kwanini niwashirikishe ninyi wasomaji/ ndugu zangu. Maana naamini palipo na wengi pana mengi
Hata hivo nami nikajiwa na swali:- Je?  Hiki kitu kipo? na kama kipo kwa akina mama/wanawake tu?  na sio akina baba/wanaume? Maana nao pia ni wazazi. NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA......Kapulya wenu!

Wednesday, September 2, 2015

UJUMBE WA WIKI HII KUTOKA KWA KAPULYA!

Msione nipo kimya nipo sema tu mambo ya afya hayapo sawa sanma na majukumu ni mengi basi kila kitu kimejichanganya...Ila tupo Pamoja.....Kapulya.