Saturday, October 31, 2009

MUZIKI NI MOJA YA STAREHE KATIKA MAISHA


JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE KUMBUKENI SIO UGIMBI/ULANZI MWINGI:-)!!!!!

Friday, October 30, 2009

WIKI ILIYOPITA TULIONA MAJINA TUWAITAYO WATOTO WETU:- NGOJA LEO TUANGALIA MAJINA YA UBINI(VIB0NGO) TULIYONAYO!!

Hivi haya majina ya ukoo/ubini(vibongo) alianza kupata nani wanadamu, wanyama au ndege?

Ninekuwa nikijiuliza hili swali na nimewauliza watu wengi hivi haya majina tuliyonayo nani alianza kupata/kuitwa? Yaani kwa mfano:-Ngonyani, Nguruwe, Nyati, Tembo, Komba, Mwaipopo, Sungura, Soko, Mapunda, nyoka, kunguru, Mbawala, Kifaru. Tujadili pamoja......

Thursday, October 29, 2009

KUPOTEA KWA SIKU CHACHE + JIBU KWA DA MIJA KUHUSU PICHA HII HAPA CHINI!!!!

Kwanza kabisa napenda kuwataka wote radhi kwa kupotea kwa siku hizi chache. Ila sasa nimerudi tena na TUPO PAMOJA.
Pili napenda kumjibu Da Mija swali lake "Yasinta ile picha yako pale juu kabisa katikati uliipiga lini? naizimia sana." Jibu ni hili Da mija nilipiga mwaka 1992 nikiwa Wilima Sec. huko Madaba-Matetereka. Natumaini nimejibu kama ulivyotegemea dadangu.

Dada Subi:- Kutangaza mabadiliko ya tovuti

Naomba nafasi katika blogu yako kuwataarifu wasomaji kuwa tovuti ya mpya ya wavuti.com imechukua nafasi ya iliyokuwa nukta77.com na nukta77.blogspot.comNaomba yeyote aliyekuwa ameweka linki ya nukta77 aihariri na kuweka wavuti.com
Karibuni sana kutembelea kwa taarifa za nafasi za masomo na kazi kwa burudani na bila kusahau habari na porojo!Asanteni.wavuti.com

Sunday, October 25, 2009

JUMAPILI NJEMA WANDUGU:- LEO NI DOMINIKA YA 30 YA MWAKA B!!!!!!

Kuwa na furaha sio kuwa na mali mengi. Isipokuwa ni kupenda/kupendwa na kuwa na tumaini/matumaini!!!

KRISTU..........TUMAINI LETU

Friday, October 23, 2009

BARUA KUTOKA SWEDEN: Hatujiamini, tutaendelea kutawaliwa na wazungu

Baada ya kuisoma barua hii nimeona si mbaya kama nikiiweka hapa ili wengi waisome na na tujadili kwa pamoja.

KUJIAMINI ni jambo la maana sana katika maisha ya kila siku ya mwanadamu. Kujiamini katika kila uamuzi unaofanya na kila kitu unachofanya ndio siri kuu ya mafanikio ya mwanadamu yeyote. Bila kujiamini, hakuna chochote utakachofanikiwa na kila siku utakuwa 'mtumwa' wa wengine.

Kujiamini ni muhimu na chachu ya maendeleo si katika maisha ya mtu binafsi tu, bali hata katika taasisi kama vile serikali, mashirika ya umma na mashirika binafsi. Ili taasisi au shirika lolote liendelee, ni lazima kuongozwa na wataalamu waliobobea na wenye kujiamini kwa maamuzi na matendo.

Sababu kubwa ya nchi yetu kuendelea kuwa masikini ni kuwa na viongozi wasiojiamini na kuendekeza utegemezi hasa kwa wazungu.

Viongozi wetu bado wanaamini kuwa wazungu wanajua kila kitu kinachohusiana na nchi kupiga hatua mbele kimaendeleo. Wanaamini kuwa wazungu ndio wenye kujua mbinu na mikakati ya kufuta umaskini katika nchi yetu. Hawaamini kama Watanzania wana uwezo wa kujiendeleza wenyewe bila kutegemea usaidizi wa watu wa nje.

Viongozi wetu wanadanganyika kirahisi wanapoona nchi nyingi za Ulaya na Marekani zimeendelea, hivyo wanadhani kuwa wazungu ndio 'mwarobaini' wa matatizo yetu, ndio maana wakati wote wanajidhalilisha wao wenyewe na sisi wananchi wao kwa ujumla kwa kuwapigia magoti wazungu kuwaomba 'watuendeleze.'Wanaamini kuwa wao pekee (wazungu) ndio wenye akili hapa duniani, na sisi ni kama ‘misukule’ tu!

Kila kukicha viongozi wetu na Afrika kwa ujumla wanapishana katika nchi za Ulaya na Marekani kwenda kuomba misaada, wanaamini kuwa bila misaada hawawezi kuendesha nchi zao, wamekuwa akina 'Matonya,' wanatembeza kibakuli. Sijui wameona nani au nchi gani duniani iliyoendelea kwa kutegemea cha kuomba.

Viongozi wetu wanawaheshimu na kuwanyenyekea watawala wa Ulaya na Marekani kuliko hata wananchi tuliowaweka madarakani, wanakubali kila wanaloambiwa na ‘mabwana wakubwa'hawa.

Kwa mfano, wakati ule walipoambiwa wayabinafsishe (wayauze) mashirika na makampuni yote ya umma kwa hoja eti serikali haiwezi kufanya kazi mbili, yaani kuongoza nchi na wakati huo huo kufanya biashara, walikubaliana na ushauri huo bila hata ya kuhoji au kuja kwa wananchi kutuuliza maoni yetu, wakaanza kuuza mali zetu moja baada ya nyingine, na walipomaliza kuuza hawakuja kutuambia wamepata kiasi gani cha fedha.

Lakini ukiwauliza leo kama tumeendelea baada ya kuuza mashirika na makampuni ya umma? Hawatakujibu kitu, watabaki wanakutolea macho tu ingawa jibu wanalo, lakini wanapata kigugumizi kulisema kwa sababu wanaona haya kwa kuwa walitapeliwa au waliingizwa mjini na wazungu.

Tazama, wakati huu wa tatizo la kiuchumi lililowakuta wazungu hawa hawa ambao tunawaamini kuwa ‘waganga’ wa matatizo yetu ya kiuchumi, wakati makampuni yao mengi yakifilisika, wanakimbilia hazina za serikali zao na kuchota mabilioni ya dola, pauni na euro za umma ili kuyaokoa, wanadai wanalinda nafasi za kazi kwa raia wao, sisi makampuni na mashirika yetu yalipotetereka, wakatuambia tuyabinafsishe (tuwauzie wao).

Tatizo letu kubwa ni kutojiamini. Na hili halipo kwa viongozi wetu tu, bali pia kwa wananchi wa kawaida. Wengi wetu tunaamini kuwa mzungu ni mweledi kuliko sisi, hatujui kuwa wazungu wengi ni mbumbumbu wa masuala mengi tu kuliko waswahili.

Ninachojaribu kusisitiza hapa ni Watanzania na Waafrika kwa ujumla kujitambua na kujiamini kuwa tunaweza kufanya mambo makubwa kuliko hata wazungu, katika kila nyanja ya maisha ya mwanadamu, iwe ni kiuchumi, kisayansi na hata kiteknolojia.

Ipo mifano hai ya nchi zilizokuwa taabani kiuchumi na kijamii kuliko hata sisi, lakini kwa kuwa walijitambua na kujiamini, walichukua hatua ambazo leo zinawafanya kuwa tishio dhidi ya wazungu waliotangulia kupata maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.

Nchi kama vile China na India ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine zinazoendelea. Wachina kwa sasa ndio tishio pekee dhidi ya Marekani kiuchumi, na wakati huu wa mparaganyiko wa uchumi katika Marekani na Ulaya, China imetwaa uongozi wa uchumi duniani na inalitumia kikamilifu tatizo hili kukwea katika kilele na kuipiku Marekani. Wachina pia hawako nyuma katika maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Mwasisi wa Taifa letu, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, alikuwa kiongozi pekee wa nchi hii aliyekuwa na nia na maono ya dhati ya kujinasua kutoka katika minyororo ya ukoloni wa wazungu.

Mwalimu alitaka Tanzania ijitegemee kwa kila kitu, ndio maana alianzisha siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambamo Watanzania tulishuhudia viwanda vya huduma mbalimbali vikijengwa nchi nzima.

Mtazamo wa mbali wa Mwalimu ulikuwa kuhakikisha kuwa ifike wakati Tanzania iwe na ‘viwanda-mama,’ yaani viwanda vya kuzalisha malighafi kwa ajili ya viwanda vingine, haya yalikuwa malengo thabiti ya kujitegemea.

Mwalimu alifanikiwa kwa sababu alikuwa kiongozi mwenye kujitambua na anayejiamini, na alitaka pia Watanzania wote wajitambue na kujiamini. Lakini kwa bahati mbaya waliompokea wawakuliona hilo.

Ndio maana miaka 24 imepita sasa tangu Mwalimu ang'atuke uongozi, lakini hakuna chochote walichoongeza, zaidi ya kuuza kila kitu tulichokuwa nacho na kujaribu kufisidi hata kile kidogo tulichobaki nacho.

Kwahiyo, kama kweli tunataka kuwa taifa huru na kukomesha ukoloni wa wazungu, hatuna budi kuchukua hatua sasa. Viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanapaswa kutuongoza katika jitihada hizo za kujikomboa, vinginevyo tutaendelea kutawaliwa na wazungu

Na George Maziku, Sundsvall, Sweden toka gazeti la mwananchi

Thursday, October 22, 2009

NIMEUTAMANI KWELI MLO HUU/NAKUMBUKA MBALI NYASA!!!!!


Yaani hapa roho inauma kweli , nakula kwa kuingalia picha hii, basi tu sijui mwenzangu nanyi hivyohivyo. Mbaya zaidi hapa unga siku hizi haupatikani Sijui nijaribu kupika ugali na unga gani? Ok karibuni basi tule msosi tayari.



NGOJA LEO TUANGALIE BAADHI YA METHALI ZETU KUANZIA A MPAKA Z

  1. A. Akili ni nywele, kila mtu ana zake.
    Asiyefunza na mamaye, hufunzwa na Ulimwengu.
  2. B. Baada ya dhiki, faraja.
    Bendera hufuata upepo.
  3. C. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
    Cheruru – Si ndo! Ndo! Ndo!.
  4. D. Damu nzito kuliko maji.
    Dawa ya moto ni moto.
  5. F. Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu hulingámua.
    Fimbo iliyo mkononi, ndiyo iuayo nyoka.
  6. G. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
    Gonga gogo usikilize mlio wake.
  7. H. Hapana siri ya watu wawili.
    Heri kujikwaa dole kuliko kujikwaa ulimi.
  8. I. Ikiwa hujui kufa tazama kaburi
    Iliyopita si ndwele, ganga ijayo.
  9. J. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
    Jungu kuu halikosi ukoko.
  10. K. Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana.
    Kinyozi hajinyoi na akijinyoa hujikata.
  11. L. Lisemwalo lipo:- Ikiwa halipo, lipo nyuma linakuja.
    Lisilokuwepo moyoni halipo machoni.
  12. M. Mcheka kilema hafi bila kumfika
    Mficha uchi hazai.
  13. N. Nnzi kufa juu ya kidonda si haramu.
    Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune.
  14. P. Penye uermbo ndipo penye urimbo.
    Penye mafundi hapakosi wanafunzi.
  15. R. Radhi ni bora kuliko mali.
  16. S. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utayokytana na mkweo.
    Sumu ya neno ni neno.
  17. T. Tamaa mbele, mauti nyuma.
    Tonga si tuwi.
  18. U. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyenona.
    Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
  19. V. Vikombe vikikaa pamoja havina budi kugongana.
    Vita vya panzi ni furaha ya kunguru.
  20. W. Wema hauozi.
    Werevu mwingi mbele kiza.
  21. Y. Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyomo na yajayo.
    Yote yangáayo usidhani ni adhabu.
  22. Z. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.

Wednesday, October 21, 2009

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA,MJOMBA,SHEMEJI NA RAFIKI PIA JAMAA YETU!!


Hapa ni Mikumi 2005!!
Imefika siku nyingine tena, ya kumpongeza kaka yangu mwingine siku yako ya kuzaliwa. Najionea fahari sana kuwa na kaka wengi. Huyu ni kakangu wa tano kuzaliwa na leo ametimiza miaka makumi matatu na kidogo!!!!!






HONGERA KAKA SELAFIM KWA SIKU HII MAALUMU KWAKO UWE NA WAKATI MZURI.

Tuesday, October 20, 2009

KWA NINI TUNAWAPA WATOTO WETU MAJINA KAMA HAYA????

Ni juzi tu nilikuwa naongea na rafiki mmoja kuhusu majina. Nimeona niandike machache na tujadili kwa pamoja:-

Majina yenyewe ni kama haya:- Matokeo, Maneno, Sikujua, Zawadi, Mashaka, Matatizo, Asante, Baraka, Wasiwasi, Sikudhani, Shida, Huzuni, Halimoja, Majuto, Bahati, Mapambano, Tuombe, Maombi, Tumaini, Masikitiko, Maua nk.
Na huku kwetu kusini yaani Songea (wangoni) wanawaita watoto majina kama haya wa kike Kachiki na wa kiume Kadoda. Maana ya majina haya angalia kwenye kamusi ya kingoni:-)

Monday, October 19, 2009

Salma: Kwa nini alifungiwa ndani kwa miaka 24?

Mlemavu wa viungo Salma Mkomwa

Mama yake asimulia kisa cha kupata ulemavu

SIMULIZI ya msichana Salma Mkomwa (26) wa Morogoro kufungiwa nyumbani kwao kwa miaka 24 bila kutoka ndani imewashtua wengi hasa baada ya kujitokeza kwenye vyombo vya habari kuomba msaada wa kumwezesha kujikwamua.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kisa cha kufungiwa kwa msichana huyo mlemavu kwa kipindi chote hicho. Wapo waliowashutumu wazazi wake na wengine wakidhani kwamba walistahili kupewa elimu juu ya malezi ya mtoto wao badala ya shutuma, alimradi kila mtu alisema lake.
Ili kujua kisa na mkasa, nilifunga safari hadi Kijiji cha Kichangani, Morogoro anakoishi msichana huyo kujua kulikoni? Nilikutana na kuzungumza kwa kina na mama yake, Mwanangavia Sewa.
Alijibu swali la kwa nini alimfungia binti yake kwa miaka 24... "Hatukuwa na uwezo wa kufanya chochote na wala hatukujua hata pa kuanzia baada ya Salma kuanza matatizo haya. Sababu kubwa ni kwamba hali ilikuwa ngumu."
Baada ya majibu hayo, mama huyo alianza kueleza mambo ambayo anadhani ndiyo chanzo cha binti yake huyo ambaye ni mtoto wa pili kati ya sita aliojaaliwa kupata ulemavu huo.
Akiwa na mimba ya miezi tisa, alifunga safari ya kutoka hapo Morogoro kwenda Handeni, Tanga kwa ajili ya kujifungua. Anakumbuka hiyo ilikuwa mwaka 1982.
Wiki moja kabla ya kumpata mtoto huyo, alikwenda shambani kuvuna ndizi, baada ya kupata mkungu wake, alijitwisha tayari kwa safari ya kurudi nyumbani. Akiwa njiani alidondoka.
"Kama unavojua mambo ya kijijini nilijifungua kwa mkunga sikujifungulia hosipitali lakini mwanangu Salma alikuwa mzima kabisa" anasema na kuendelea:
"Lakini wiki moja baada ya kujifungua mtoto akawa analia kupita kiasi kuna kulia kwa mtoto kawaida lakini yeye alizidi hadi kuwashtua watu nyumbani. Tukampeleka Zahanati ya Mzindu, Handeni walipompima wakasema mtoto hana tatizo lolote, wakatupa vidonge lakini hali ilibaki vilevile."
"Baada ya mwezi mmoja miguu ilianza kuvimba usawa wa magoti. Ikabidi nifunge safari kurudi Morogoro na kwenda Hospitali ya Mkoa.
Nilipomfikisha akapigwa x-ray sehemu za magoti ili kujua tatizo. Majibu yakaonyesha kuwa sehemu hizo zimeachana na damu haitembei.
"Madaktari wakasema nimechelewa hawezi kunyooshwa tena mifupa imekomaa. Wakati huo alikuwa na umri wa mwezi mmoja. Nadhani hii yote imetokana na kutojifungulia hospitali labda tatizo lingeweza kujulikana mapema."
Baada ya majibu hayo ilirudi nyumbani. Hali ya Salma iliendelea kuwa mbaya. Aliishia kupewa dawa za kutuliza maumivu na kupunguza uvimbe uliokuwapo miguuni.
Alipofikisha miaka mitano alipata nafuu. Uvimbe ulikoma hata kulialia kulipungua. Wakati wote huo mikono yake haikuwa na tatizo hata kidogo lakini siku zilivyozidi kusonga nayo ikawa inajikunja pamoja na miguu.
"Madaktari walishindwa jinsi ya kufanya na hatukuweza hata kununua gari la kumsaidia ndiyo maana ilibidi akae tu ndani kwa muda wote huo."
Habari kuhusu Salma zilijulikana baada ya Taasisi ya Faraja Trust Fund ambayo inashughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutembelea nyumbani kwao.
Hata hivyo, hawakuwa wamekwenda kwa ajili yake bali mdogo wake wa kiume ambaye amekataa kwenda shule akiwa darasa la tano.
"Ilikuwa kama ndoto na sitakuja kusahau siku ile ambayo alikuja mlezi kutoka Faraja ambaye alikuwa akishugulika na watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na wasiopenda shule akiwemo mdogo wangu ndipo akanikuta," anasema Salma.
"Siku alipokuja nilikuwa ndani. Aliniona lakini aliondoka bila kuniambia kitu chochote hadi mwaka 2006 alipokuja tena na mama Ligaya alinipiga picha na kuipeleka katika Kituo cha Faraja."
Alipelekwa katika kituo hicho na baada ya kufika huko, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Lucy Nkya kwa kushirikana na shirika hilo walimpokea na kumpatia baiskeli pamoja nyuzi sita kwa ajili ya kuanza kufuma kwa kuwa tayari alikuwa na ujuzi huo.
"Namshukuru Mungu picha hizo zilipokwenda huko zilipokewa na hatimaye nilipata baiskeli ambayo inanisaidia katika maisha yangu kwani siwezi kutembea bila ya baiskeli."
Katika kipindi alichokuwa ndani alikuwa akijifunza kushona kwa kutumia chelewa za ufagio kwani hakuwa na uwezo wa kununua sindano ya kufumia vitambaa.
"Ninaweza kufuma vifuko vya kuhifadhia simu na tai na namshukuru Mungu naviuza Sh2,000 na watu wananunua. Shirika (Faraja), lilinipeleka katika maonyesho ya Sabasaba na hapo watu mbalimbali walielewa nini ninachofanya. Niliuza bidhaa zangu na kupata Sh200,000 na kupata msingi wa kuuza mkaa."
Fedha zinazopatikana katika shughuli zake wakati mwingine humsaidia mama yake ambaye ni mfanyabiashara wa mbogamboga hasa anapokosa bidhaa.
Salma hawezi kutembea wala kutambaa na hiyo ni changamoto kubwa katika maisha yake kwani anapokosa mtu wa kumsogeza alipo hulazimika kubaki hapo alipo liwepo jua au mvua.
Anayo tamaa kubwa ya kupata elimu lakini anasema wazazi wake hawana uwezo wa kumpeleka shule. Anatamani angejitokeza msamaria mwema kumsaidia pengine hiyo ingekuwa sehemu ya kujikomboa kimaisha.
"Nitashukuru pia kama nitapata mahala pa kuishi kwani hapa mazingira ni magumu. Baba ana wake wawili wote wanakaa katika nyumba hii na ana watoto 14 ambao wanamtegemea baba huyo na nyumba hiyo hivyo."
"Naomba tu Mungu mama yangu asitangulie mbele za haki kwani nitapata shida lakini kama nina nyumba yangu kidogo afadhali nitaweza kujisitiri."
Mwanamke aliyemfichua msichana huyo ni Jalia Lupapulo ofisa wa kituo hicho cha faraja chenye makao yake Kihonda, Morogoro. Anaungana naye kuomba wasamaria wema wamsadia akisema hajawahi kusoma. Kituo hicho hivi sasa kipo katika mchakato wa kumtafutia mwalimu maalumu.
Baadhi ya wataalamu wa tiba ya mifupa wanasema kwamba tatizo Salma linaweza kutibika kwa kupunguza kiwango cha ulemavu alichonacho.
"Nikimuona naweza nikajua tatizo ni nini hata kama ana umri mkubwa anaweza akasaidiwa tatizo likapungua ama siyo kwisha kabisa," alisema daktari mmoja.
Na Mahija Mpera gazeti la mwananchi

Sunday, October 18, 2009

Saturday, October 17, 2009

JUMAMOSI NJEMA WOTE:- TUMSIKILIZE LAMECK dITTO NA WIMBO WIVU WA KUPENDA.

Mara nyingi mapenzi huambatana na wivu, ni kama mapacha. Nimeupenda msemo huu mapenzi bila wivu ni kama chai bila sukari (chai bila sukari wala kitafuno) Ili mapenzi yakolee, wivu lazima uwepo .

Friday, October 16, 2009

KUMUITA MKEO MAMA…AU MUMEO BABA KWELI….NI HAKI?


Ni kawaida sana kumsikia mke akimuita mume baba, au mume kumuita mke mama...jamani mbona yapo majina mengi ya kuitana kama vile mpenzi, kipenzi, habib, na mengine mengi. Na kama mna mtoto ndio rahisi zaidi yaani kumuita mama fulani au baba fulani. Ila si mama au baba. Mama anaheshima yake mambo yote unayoyafanya na mkeo kweli anastahili kuitwa mama??!...au unayoyafanya na mumeo unaweza muita mumeo baba???

Au hata majina ya ubatizo (ya kwanza) tuitane. Au kama kule kwetu kusini wanaitana vibongo yaani majina ya ukoo kama Na-Ngonyani, Na-Nyoni, Na-Komba nk. Na waBena/waHehe wao wanasema Sa au Se badala ya Na kwa hiyo itakuwa kwa wao. Sa-Mgaya, Sa-Mwageni, Sa-Mbilinyi kama kuna wabena na wahehe mnisaidie kama nimekosea. Na hiyo ya kuita Na na Sa ni kwa akina mama tu isije ukamwita mwanaume pia.

Pia sasa kuna mtindo wa kuwaita wazazi wetu babu na bibi yaani tunawita kama watoto wetu wanavyoita. Mara nyingi nimekuwa nawasikia watu wakisema ni bibi alipiga simu ukimuuliza bibi yako bado anaishi anasema hapana ni mama yangu lakini kwa vile watoto wanasema bibi /babu basi nami nasema hivyo. Na babu yako utamwitaje?
Naomba mnisaidie kufafanua hapo!!!!!!

TUSISAHAU UTAMADUNI WETU TINGATINGA (BATTIK) NI KAZI YA MIKONO YETU/NI UBUNIFU WETU

Hapa naona kazi zimezidi kidogo lakini tutafika tu.

Sisi ni wamoja tunatwanga

Na sisi pia tunatoka kuchota maji
Ni mapambo lakini pia yana maelezo yake kwa hiyo inakuwa raha katika nyumba kuwa na mapambo kama haya. NAPENDA KUWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA KWA PICHA/TINGATINGA/BATIKI HIZI.
UKITAKA KUJUA MENGI USISITE KUULIZA.


Thursday, October 15, 2009

LAITI KAMA NINGEKUFAHAMU KABLA.........HADITHI YA KUFIKIRIKA

Miaka mitano iliyopita nilikuwa natafuta mke wa kumuoa ambaye angekuwa na sifa nizitakazo. Nilikuwa natafuta msichana mzuri wa wastani maana sikutaka kuoa mke mzuri kupindukia asije niua bure kwa presha na jakamoyo. Nilikuwa natafuta binti atakanikubali kama nilivyo na mapungufu yangu na mimi niliahidi kumkubali na mapungufu yake ili mradi asiwe ni mwenye tamaa ya kupenda sana pesa na mfujaji.
Awe na staha na anayeweza kukabiliana na hali yoyote, niwe nacho, nisiwe nacho au kwa kifupi tupendane kwa shida na raha.

Pamoja na sifa nyingine ndogo ndogo, lakini muhimu ni upendo na amani vitawale nyumbani kwangu.
Hatimaye nilimpata Binti Yasinaty, na kukutana kwetu kulikuwa ni kama muujiza, nakumbuka siku hiyo nilipanda daladala nikielekea kazini na kwa bahati kiti nilichokalia kilikuwa ni cha mwisho upande wa dirishani. Wakati nakaa nikahisi kukalia kitu kigumu, nilipopapasa ilikuwa ni simu mpya kabisa tena ya bei mbaya kama sikosei wakati huo ilikuwa inauzwa shilingi laki nne kwa wakati huo, kumbuka kwamba hapa nazungumzia habari ya miaka mitano iliyopita.

Kwa bahati mbaya simu ile ilikuwa imezimwa, na nilipojaribu kuiwasha iliwaka na kuzima kuashiria kwamba betri yake iliisha chaji. Niliiweka mfukoni na kujiuliza kuwa ile simu ilikuwa ni ya nani, sikusikia mtu kulalamika kwamba amepoteza simu na niliogopa kuuliza maana nilichelea mtu kujitokeza na kusema kwamba ni yake ilihali sio yakwake.

Nilifika ofisini na kuanza kazi, baadae nilimuita katibu muhtasi wangu na kumwomba anisaidie kutafuta chaji ya ile simu kwa kuwauliza wafanyakazi pale ofisini, nilikuwa na shauku ya kumfahamu mwenye simu ile ili nimrudishie, kwani nilikuwa namuoana dhahiri akisikitika kwa kupotelewa na simu yake, kwa jinsi ilivyoonekana ilikuwa bado ilikuwa ni mpya kabisa na ilikuwa haijatumika zaidi ya wiki.

Katibu wangu muhtasi hakufanikiwa kuipata ile chaja ya ile simu. Niliweka ile simu kwenye droo ya ofisini kwangu ili jioni nikitoka nipitie nayo kariakoo ninunue chaja yake.
Ilipofika jioni alikuja mchumba wangu ambaye tulitofautiana wiki iliyopita na kuamua kutengana naye. Sikutaka kuonana naye na nilimwambia katibu wangu muhtasi amwambie kuwa niko bize na sitaki afike tena pale ofisini kwangu.

Ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini kitendo chake cha kukuta mwanaume mwingine chumbani kwake tena akiwa amelala kitandani kwake halafu anajidai kunidanganya kuwa eti ni binamu yake hakikunifurahisha kabisa. Nakumbuka nilisafiri kikazi kwenda Mbeya, na ilikuwa nikae kule kwa wiki moja, lakini ilitokea dharura huku Makao makuu Dar ikabidi nirudi baada ya siku mbili tu na nilipofika kwa kuwa ilikuwa ni usiku kama saa mbili niliamua kupitia kwa mchumba wangu ambaye alikuwa akiishi Mwengeili kupata chakula cha jioni kabla sijaenda kwangu Maeneo ya Sinza. Nilipofika nilimkuta akiwa nje akipika, lakini aliponiona alishtuka sana akabaki kinywa wazi, hakunipokea alibaki ameduwaa, nikahisi kuna jambo. Nilimsalimia alijibu kwa wasiwasi nilipotaka kuingia ndani, alinizuia, na huku akiongea kwa sauti yenye kutetemeka aliniambia eti ndani kuna binamu yake kaja na amejipumzisha kitandani kwake, nilishtuka. Niliiingia ndani moja kwa moja na kumkuta kijana amelala kitandani nilipomuhoji kuwa yeye ni nani na anafanya nini pale akaniambia kuwa yuko pale kwa girlfriend wake na alitaka kujua eti mimi ni nani..Sikutaka kuzua ugomvi, nilimwambia kuwa pale ni kwa dada yangu na nilifika kumsalimia, nilimuomba radhi kwa kuingia bila hodi, ila nilimshauri aharakishe kulipa mahari ili tujue kuwa dada yetu anaye mtu, ili wakati mwingine tubishe hodi, niliongea kwa utani, yule kijana alimsifia sana mchumba wangu kuwa ni mzuri hasa na anajua kupenda, alibwabwaja mambo mengi na upuuzi wao wanaofanya nikiwa sipo, niliongea naye kwa utani mwingi na kuaga na kuondoka, lakini moyoni roho ilikuwa ikiniuma kweli. Nilikuwa nampa yule binti karibu kila kitu alichohitaji, lakini kumbe hakuridhika bado akawa na mwanaume mwingine.

Nilitoka na nilimkuta kajiinamia pale nje, sikumuaga nikaondoka zangu. Nilipofika nyumbani nilimtumia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani nikimwambia kuwa kuanzia siku hiyo ilikuwa ni mwisho wa uhusiano wetu. Hakijibu na siku iliyofuata alipiga simu lakini sikupokea, alibadilisha namba na nilipopokea na kugundua kuwa ni yeye nilikata simu, baadae zilifuata ujumbe kadhaa wa simu yake ya kiganjani akitaka tuonane ili tuyamalize. Sikumjibu. Na ndio akaamua kuja ofisini.

Nilimpigia simu katibu muhtasi wangu na kumuamuru amwambie yule binti aondoke pale ofisini. Niliambiwa kuwa amekataa, nilimpigia simu dereva wangu na kumuuliza kama gari limeshatoka gereji, akanijibu kuwa gari litatoka baadae kidogo, nikamwambia akitoka gereji aende nalo nyumbani kisha kesho asubuhi anifuate. Gari langu liliharibika siku mbili zilizopita, hivyo nililazimika kupanda daladala au taxi kama nikiwa na dharura. Niliondoka pale ofisini nikimuacha akiongea na katibu wangu muhtasi na kuondoka zangu. Nilikodi taxi na wakati niko njiani nikakumbuka kuhusu ile simu, lakini niliisahau ofisini, kwa hiyo sikupitia kariakoo tena. Nilikwenda moja kwa moja hadi kwa rafiki yangu anayeishi maeneo ya kijitonyama na kupoteza muda huko hadi usiku ndio nikarudi nyumbani.

Siku iliyofuata dereva alinifuata na kunipeleka ofisini, nilipofika nilimpa ile simu na kumtuma akanitafutie chaja ya ile simu. Baadae alirudi akiwa na chaja ya simu ile na kunikabidhi. Niliichaji na ilipojaa niliiwasha ziliingia ujumbe kadhaa kutoka kwa watu waliokuwa wakimtafuta mwenye simu ile, nilipozisoma niligundua mwenye simu ile alikuwa anaitwa Yasinaty, nilikata shauri nimpigie mmoja wa watu waliokuwa wametuma ujumbe ambaye alionekana kuwa ni mama yake. Nilipompigia simu na kuuliza kama anamjua mwenye simu kwanza alitaka kujua mimi ni nani na kwa nini simu ya mwanaye ninayo mimi. Nilimsimulia kila kitu na nilimuomba ampe mwanae namba yangu ya simu na kumuomba amwambie awasiliane na mimi ili nimpe simu yake. Yule mama alifurahi sana na kunishukuru sana, kumbe ile simu Yasinaty alitumiwa na kaka yake aishie Ughaibuni.

Mchana nilipigiwa simu na Yasinaty na tuliongea mengi na alionekana ni binti mchangamfu kweli, alinimbia kuwa anafanya kazi kwenye Hoteli moja ya kitalii maarufu iliyoko katikati ya jiji, nilimuahidi kumpitia kazini kwake jioni nikitoka ofisini.
Nilimpitia jioni na kama alivyonielekeza kuwa yuko reception nilimkuta pale akimalizia kazi na aliniomba nimsubiri kweye kijimgahawa kilichopo pale ndani, kwa kuwa mimi sio mnywaji wa pombe niliagiza juisi ili kumsubiri. Baadae alinipitia pale nilipokaa na kunimbia kuwa anatoka hivyo tukutane nje kwani anakwenda kubadili sare za kazini. Alitoka na kunikuta nje nikimsubiri, alipanda kwenye gari na nilimuomba dereva wangu atupeleke Hoteli nyingine ya kitalii maarufu pale hapa jijini ili tupate kahawa na Yasinaty. Tulifika pale tuliagiza vinywaji. Nilitumia wasaa ule kumtazama vizuri Yasinaty, alikuwa ni binti mrembo sana, na mchangamfu hasa, naamini alistahili kufanya kazi reception.

Nilimkabidhi simu yake na yakafuata maongezi mengine ya kujuana na simulizi za hapa na pale. Huo ndio ukawa mwanzo wa kujuana na Yasinaty, ambaye baadae alikuja kuwa mke wangu mpenzi.

Laiti kama ningekufahamu kabla Yasinaty………………….

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa blog hii ya MAISHA ambaye anasheherekea ndoa yake kutimiza miaka mitano leo. Na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa.

MUZIKI NI MOJA YA MAISHA TUMSIKILIZE DADA NURU LEO



Maisha yetu wengine hawawezi kuishi bila kusikiliza mziki hata siku moja na wengine hawawezi kusikiliza redio hata siku moja na wengine kusoma vitabu na magazeti. Kila mtu anapata habari kwa namna ya pekee. Haya leo nimeona tumsikilize Mwanablog mwenzetu Da Nuru the lihgt.!!!!

Monday, October 12, 2009

WANANDOA NA KAULI HIZI: HATA VIKOMBE KABATINI HUGONGANA, ITAKUWA SIE?

Je unadhani au kuamini kwamba kuna ndoa ambazo wanandoa wake hawagombani kabisa? Kama unaamini hivyo, basi unajidanganya na labda unaishi katika dunia ya peke yako.

Ni jambo lenye ukweli wa kutosha kabisa kwamba wanandoa wote duniani hutokea kugombana, lakini kugombana huko hutokana na migongano au mizozo ya muda tu ambayo huweza kutatuliwa na pande mbili kama wakiamua kufanya hivyo.

Wewe unayesoma hapa, napenda kukuambia ukweli kwamba usiogope migogoro ya ndoa, kwani hicho ni kitu ambacho kamwe huwezi kukiepuka. Kuna msemo mmoja unatumika sana huko nyumbani usemao, " hata vikombe kabatini hugongana itakuwa wana ndoa?" Hii ina maana gani, ina maana kwamba haiwezekani watu kuishi pamoja halafu msiwe mnatofautiana, na kama ukiona hivyo, jua kwamba hiyo ndoa si salama kwani siku yoyote bomu litapasuka na madhara yake yatakuwa ni makubwa kuliko kawaida.

Kuna watu ambao hata kama wamekosewa na wenzi wao hunyamaza kimya na kumeza hasira zao, wengine huogopa kuwakabili wenzi wao na kuzungumzia jambo linalowakera kwa kuhofia kuonekana kama wana kasoro au ghubu. Jambo hili ni hatari sana.

Kumkabili mwenzi wako na kumwambia hisia zako kama amekukosea au amekwenda kinyume na matarajio yako ni jambao la maana sana katika kudumisha uhusiano. Lakini naomba nitahadharishe kwamba, ni vyema kufanya hivyo bila kumshusha, kubeza au kusimanga kwani hiyo sio dalili nzuri ya upendo.

Inashauriwa kwamba wanandoa au wapenzi wanapokwaruzana inabidi wajadili tofauti zao bila kusigishana, kila mmoja akitaka kuwa mshindi, hiyo haitasaidia kuimarisha ndoa bali itaongeza tatizo. Ni vyema upande unaohusika na tatizo, uwajibike na kuomba radhi kwa ustawi wa ndoa, huo ndio ukomavu.

Kutojadili mgogoro kwa wanandoa na kuupatia ufumbuzi wa tatizo huwafanya wandoa kuwa mbali kihisia, na athari zake ni kuwakuta wanandoa wakiwa wageni wa kila mmoja kwa mwenzake, yaani hakuna mawasiliano, kila mtu na lwake.

Jambo la msingi kwa wanandoa ni kujadili tofauti zao pindi linapojitokeza jambo linalomkera mmoja wa wanandoa, kwani hakuna jambo linaloweza kujitatua lenyewe bila kutatuliwa na wandoa husika. Kuacha jambo lolote bila kulitafutia suluhu ni sawa na kutega bomu, ambapo siku likilipuka madhara yake ni makubwa sana.

Unaweza kukuta mwanandoa anakereka na mambo madogo madogo ya mwenzi wake lakini hasemi, ingawa yanamkera kupita kiasi akitegemea huyo mwenzi wake atajua na kuacha, thubutu…..inapotokea siku yeye amekosa jambo dogo tu na huyo mwenzi wake akamsema, basi atatumia fursa hiyo kuanza kujibu mapigo kwa kueleza yale yanayomkera kutoka kwa mwenzi wake, na hapo itakuwa kila mtu anavutia kwake kama mwamba ngoma………na aamini nawaambia kuwa kamwe hawezi kupatikana mshindi katika jambo hilo, kwani mjadala huo unaweza kutoka nje ya mada kila mmoja akijitahidi kutafuta makosa ya mwenzi wake hata yale yaliyotokea wakati wa uchumba wenu ili mradi vurugu tupu.

Inatakiwa wanandoa wajadili kila jambo linalojitokeza hadi kulipatia suluhu, vinginevyo ni kuichimbia ndoa yenu kaburi la mapema. Wakati mwingine unaweza kukuta mwanamke analalamika juu ya kutoridhishwa kwake na matumizi ya mumewe, na hapo mume naye ataanza kukumbusha juu ya matumizi yasiyo ya lazima yaliyofanywa na mke huko nyuma. Mke naye hataridhika atakumbushia jambo lingine na lingine hadi hata mada iliyokuwa ikijadiliwa inasahaulika.

Jambo lingine ni kujumuisha mambo, matumizi ya maneno kama, mara nyingi, kila wakati au mara kwa mara si mazuri sana. Unaweza kukuta mtu mwenzi wake amekosea jambo halafu mwenzie anamwambia “Kila mara huwa unafanya hivi” au mara nyingi huwa unafanya hivyo…..Hii ni hatari kwa ustawi wa wanandoa, kwani kwa kujumuisha ni sawa na kumwambia mwenzi wako kuwa kila mara yeye ndiye mkosaji.

Kwa haya niliyoyaeleza hapa sina maana kwamba huu ndio muarobaini pekee wa kuimarisha mahusiano kwa wanandoa, bali ni moja ya mambo muhimu kati ya mengi ambayo yakizingatiwa na wanandoa wote basi ndoa yao itakuwa imara Tujadili pamoja………..

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA DA SUBI!!


Ni furaha kuwa na rafiki kama Da Subi na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe bibi kizee na wajukuu wengi uwe nao. Subi ni mtu mtukutu sana kwa hilo nakuheshimu na pia nakupenda sana .HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU!!!!!!

Sunday, October 11, 2009

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA NGOMA HII MAALUFU KWA KABILA LA WANGONI KUSINI WA TANZANIA KARIBUNI TUBURUDIKE!!

Kunyumba nga kunyumba hata ngati kudahi!!!!

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA UPENDO UTAWALE DAIMA MIOYONI MWETU!!

Saturday, October 10, 2009

URAIA WA NCHI MBILI

Kwa Pro. Mbele nimesoma kuhusu watu kuwa na uraia wa nchi mbili. Kwa hapa Sweden sheria ni kwamba ukisha ishi mika 5 unaruhusiwa kuwa raia wa nchi. Kwa mimi sioni umuhimu wa kuwa raia wa nchi nyingine kwa hiyo mimi bado ni raia wa nchi moja na nina passport ile ya kijani.

Watoto wetu ni raia wa Sweden tu. Huwa tunapata shida sana kuomba ruhusa (VIZA) kwenda TZ kwani kwa wao na baba yao wanaruhusiwa kuwa ndani ya nchi miezi mitatu tu. Lakini mimi sihitaji ruhusa.

Ila ningefurahi sana kama kungekuwa na hii sheria ya uraia wa nchi mbili hapo ndiyo ningechukua nafasi na kuwa raia wa nchi mbili. Ila sasa hapana, mimi ni mTanzania tu. Kwa undani zaidi soma blog ya Pro. Mbele URAIA WA NCHI MBILI

Friday, October 9, 2009

NAPENDA KUWATAKIA WOTE MWISHO WA JUMA NA MUSIKI HUU HAYA TUFURAHI PAMOJA



UJUMBE WA LEO:- UKITAKA KUJUA MENGI BASI ULIZA (FRÅGA OM DU VILL VETA MERA)

Thursday, October 8, 2009

MTOTO AJIFUNGUA MTOTO MWENZIE!!!!!

Mtoto huyo ana miaka kumi na ana mtoto
Dunia hii sasa ni hatari kweli. Mtu na akili zake kabisa anathubutu kumfanyia unyama mtoto wa mwenzie. Kiasi cha kumpa mimba na kuzaa mtoto mapema. Kabla ya wakati wake wa kuzaa haujafika. Inaonekana huku tunakoelekea sasa ni hatari tupu au ni kweli labda ni mwisho wa dunia.

Wednesday, October 7, 2009

MILA NA DESTURI HIZI KAAAZI KWELI KWELI!!

Ni miaka karibu 15 sasa inakaribia tangu nilipoingia hapa Sweden. Na ni miaka 6 imepita tangu niwe mwanafunzi yaani kukaa darasani na kubukua.

Kuna kitu nataka kuwasimulia ambacho nilikiona miaka sita iliyopita wakati nasoma. Katika darasa letu tulikuwa wanafunzi mchanganyiko, wenyeji na wahamiaji. Kwa hiyo siku hiyo kulikuwa na somo la mila na desturi. Ilikuwa tuangalie filamu inayoonyesha mambo ya hali halisi. Basi tukawa tunaangalia hiyo filamu ambayo ilikuwa inahusu maisha ya mwanadada mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake na alikuwa mtoto pekee katika familia ile.

Mwanadada huyu alikuwa hana maisha ya kawaida. Alikuwa mlevi na mvutaji yaani si sigara tu na madawa ya kulevya alikuwa anatumia. Sasa, kibaya zaidi alikuwa akiwaibia wazazi wake vito vya thamani, na kuuza ili kupata pesa na kwenda kununu hayo mahitaji yake na pengine aliiba pesa pia. Ila alikuwa mwema alikuwa akiwapa rafiki zake pia.


Kwa tabia hiyo ilifikia mahali wazazi walishindwa kumvumilia wakamtimua pale nyumbani na akawa hana sehemu ya kuisha. Akawa analala vibarazani bila hata hata ya kuwa na shuka ya kujifunika, chakula hana na anachovaa hakieleweki…...Siku zikapita.......

Maisha yakazidi kuwa magumu, siku moja akaamua kurudi kwa wazazi wake na kusema ameacha ile tabia. Wazazi wakawa shingo upande ila kwa vile uchungu wa mtoto wanaujua wazazi wakampokea. Siku zikapita lakini ghfla siku moja akabadilika na kuanza tena ila tabia. Kama tusemavyo ukionja asali ni ngumu kuacha. Akawa anaiba vito tena na kuuza ili kupata pesa za pombe na madawa ya kulevya.Wazazi walivumilia, lakini mwisho walishindwa na wakamfukuza tena. Akawa hana kwa kwenda isipokuwa kule mitaani kuungana na marafiki na kuendela kulala vibarazani kama awali.

Mnajua ni jambo ambalo mimi sijaelewa mpaka leo katika kutafakari kwangu. Kwasababu mimi naona hapa sweden kuna misaada mingi ya kuwasaidia watu wa aina hii na nilishangaa kwa nini naye asingetafutiwa msaada? Ukizingatia wazazi wake walikuwa na uwezo na pia alikuwa mtoto pekee wanamwacha na kuwa mlevi tu??

Cha kushangaza zaidi ni kwamba hazikupita siku nyingi wazazi wa mwanadada huyu walijitafutia mbwa. Wakamnunulia mbwa huyo vitu vizuri vya kuchezea, sehemu nzuri ya kulala na chakula kizuri pia alipata. Wakati binti yao yupo hatarini hana chakula, hana mavazi wala sehemu ya kulala.

Hapo ndipo nilipokuja amini sisi binadamu tupo tofauti sana katika kuthaminiana. Mbwa/wanyama wanathaminiwa kuliko binadamu tena mwanao? Kazi kwelikweli!! Ila siku ile nililia sana kwa vile niliguswa sana na nilifoka sana darasani. Mwalimu wangu akanituliza na kuniambia karibu Sweden, Habari ndio hii. Je? Wenzangu mngejisikiaje?

Tuesday, October 6, 2009

Nimekumbuka zamani wakati nasoma+ Ubunifu wa kutengeneza vihesabio!!!

Pia nimekumbuka mwimbo huu nilipikuwa darasa la kwanza na pili tulikuwa tukiimba kila siku:-

1. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kusoma huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuandika huko shuleni pamoja na mwalimu.

2. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuhesabu huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuchora huko shuleni pamoja na mwalimu.

3. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuimba huko shuleni pamoja na mwalimu.
Twaimba sote pamoja pamoja na mwalimu.

Monday, October 5, 2009

Kupanda kwa bei za nafaka Ruvuma...Haijawahi kutokea kama mwaka huu

Mnunuzi wa viazi mviringo akishangaa kupenda kwa bei ya vyakula katika soko la mazao la Sodeco mkoani Ruvuma

KUENDELEA kupanda kwa bei za vyakula, hususan nafaka mkoani Ruvuma kunaelezwa kwamba kunachangiwa na mfumuko wa bei, ushuru wa mazao ambao unatozwa na halmashauri za wilaya pamoja na mavuno madogo msimu huu baada ya wakulima wengi kuchangamkia mazao yasiyohitaji pembejeo kama mbolea. Wakulima wengi wanalima mazao mchanganyiko ya biashara kama ufuta, karanga, soya pamoja na jatrofa ingawa pia wanalima mahindi kidogo. Sababu kubwa ni kukwepa kununua mbolea ambazo wanasema ni ghali na hawana uwezo kuzinunua licha ya kuwa na nguvu za kuzalisha mahindi mengi.

Wafanyabiashara katika Soko la Mazao la Sodeco, Songea wanasema mahindi yamekuwa machache kutokana na ushuru mkubwa kwa wakulima hivyo kuwauzia wafanyabiashara kwa bei kubwa.
"Tunaiomba serikali itusaidie kupunguza ushuru katika halmashauri kwani kutoza ushuru mkubwa kwa wakulima na wafanyabiashara ndiko kunakochangia bei za mazao kupanda kila mara,"anasema mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo, Bakari Musa. "Kwetu kupanda huko kwa bei za vyakula ni dalili mbaya kwa maisha ya kila siku ya wananchi, hususan wale wenye kipato cha chini, kwa sababu kupanda kwa gharama hizo hakuendani na kuongezeka kwa ajira wala viwango vya mishahara inayotolewa katika sekta ya umma na binafsi nchini,"alisema.

Mfanyabiashara huyo anasema iwapo halmashauri zitaendelea kuwadai ushuru wa mazao wakati wanaposafirisha mazao kutoka kijijini na kutoka mjini kwenda mikoa mingine, nchini nao wataendelea kupandisha bei ya mazao ili wapate faida. Katibu wa Umoja wa Wanunuzi wa Mazao Mkoa wa Ruvuma (UWAMAVIRU), Thadeo Mwakaguo anasema ushuru umekuwa tatizo kubwa na faini zimekuwa kubwa kitu ambacho ni kero kwa wakulima.
Anasema doria ambazo zimewekwa na halmashauri ndizo zilizochangia kwa kiasi kikubwa masoko kukosa mazao na hivyo kusababisha kupanda kwa bei. "Haijawahi kutokea kupanda kwa bei za nafaka kama mwaka huu Ruvuma. Kilo moja ya mahindi iliyokuwa ikiuzwa kati ya Sh150 na 180 inafika hadi Sh 300 kitu ambacho ni hatari kwa wananchi," anasema Mwakaguo.

Anasema mavuno yamekuwa mabaya wengi wamevuna tofauti na matarajio yao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mvua zilikatika mapema na Februari kukawa na jua kali hivyo kusababisha baadhi ya mazao kunyauka na mengine kufa kabisa. Anasema kwa kawaida katika kipindi cha Mei na kundelea kunakuwa na ongezeko kubwa la mazao sokoni hapo kwani hupokea wastani wa tani 30 mpaka 40 kwa siku kutoka kwa wakulima vijijini lakini mwaka huu kuna uhaba mkubwa wa chakula kwani mazao yanayopelekwa ni kidogo.

Katibu huyo anasema uongozi wa wafanyabiashara umepanga kukutana na halmashauri ili kuzungumzia suala hilo la ushuru. Anasema mbali ya hali kuwa mbaya, halmashauri hiyo inataka kuongeza ushuru huo kutoka Sh 1,000 kwa gunia la kilo 100 hadi Sh1,500. Anaitaka serikali kuwa makini na kuwadhibiti mawakala wanaouza mbolea zilizokwisha muda wake kwani zimewasababishia wakulima hasara kubwa msimu uliopita. Mkuu wa Masoko ya Manispaa ya Songea, Salum Omera anashauri kuwa biashara ya mahindi ifanyike kwa uangalifu kuwaepusha wananchi dhidi ya balaa la njaa.

Anawataka wakulima wasipende kuuza mazao yote ya chakula bali wabakishe kwa ajili ya kusadia familia zao hasa wakati wa njaa. Anasema kumekuwa na mfumuko mkubwa wa bei katika nafaka. Gunia la kilo 100 la mahindi linauzwa Sh 35,000 na linaweza kupanda muda wowote kuanzia sasa, mchele kilo moja ni Sh 1,400 hadi 1,500, maharagwe gunia moja ni Sh 100,000 maeneo mengi ya hayana mazao ya kutosha.
Anasema kwa sasa halmashauri ina mpango wa kupanua masoko ya mazao ili kuwasaidia wananchi kupata huduma katika maeneo yote na pia kuimarisha miundombinu ya masoko hayo.
Hata hivyo anawalaumu wafanyabiashara wengi kwa kukwepa kulipa kodi.
Hata hivyo, anasema kwamba ofisi yake haitumii nguvu katika ukusanyaji wa mapato zaidi ya kutoa elimu.
Lakini Meneja wa Takwimu Mkoa wa Ruvuma, John Lyakurwa anasema kupanda kwa bei za vyakula mara kwa mara kumechangiwa na kupanda kwa bei za usafirishaji wa mafuta. Anasema bidhaa zikiwa chache wafanyabiashara wanapandisha bei tofauti na wakati wa mavuno. Lakini anasema cha kushangaza mwaka huu hata wakati wa msimu wa mavuno, bado hali ni mbaya, bei zimeendelea kupanda kila mwezi. "Pamoja na kuwa sasa hivi ni msimu wa mavuno bado vyakula na baadhi ya vitu vimeendelea kupanda, kwa mfano, mchele ulitakiwa kuuzwa kilo moja Sh 800 lakini unauzwa Sh 1,400 mpaka 1,500,"anasema Lyakurwa. Anasema uwezekano wa bidhaa hizo kuendelea kupanda kutokana na gharama za usafirishaji, ushuru ni mkubwa na kumsababishia mzigo mkubwa mlaji wa kawaida ambaye ni mwananchi.
"Tunataraji kufanya tathmini ya upungufu wa chakula ili kujua kilichosababisha kupanda kwa bei ya vyakula na hatua zitakazochukuliwa ili kuzuia kupanda holela kwa bei za vyakula na bidhaa mbalimbali za viwandani. Mkazi wa Songea, Julian Haule anasema kuwa bei za vyakula zimeendelea kuwa juu hali inayoashiria kupungua kwa bidhaa hiyo vijijini. Anaamini kwamba sababu kubwa ni upungufu wa mvua za vuli.
Anasema serikali inapaswa kuwa makini dhidi ya wafanyabiashara wajanja ambao wanatumia mwanya huo kupandisha vyakula kiholela kwa madai kuwa inachangiwa na usafirishaji kupanda pamoja na kukosekana kwa mazao ya kutosha msimu huu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
"Wafanyabiashara wanatuumiza sana tumekuwa tukilazimika kununua bidhaa na chakula kwa bei wanayopanga wao kwani hata kama mwananchi mmoja akigoma, wengine ambao wana uwezo watanunua hivyo kutufanya sisi tunaotegemea mishahara ambayo ni ya kipato cha chini kuishi maisha ya tabu. Tunaiomba serikali itusaidie kudhibiti mfumuko wa bei ya vyakula hali ni mbaya hasa huku mikoani," anasema Haule.



Habari hii imeandikwa na Joyce Joliga wa Songea katika gazeti la mwananchi

Sunday, October 4, 2009

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA MDOGO DISMAS

Ni siku nyingine, tarehe nyingine na kaka mwingine anatimiza miaka leo na sisi wote hapa Hammarö. Pamoja na marafiki pia jamaa tunapenda kukutakia HONGERA nyingi kwa siku hii.
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA,MJOMBA, SHEMEJI PIA RAFIKI DISMAS.

Saturday, October 3, 2009

MUHIMU: CHUNGUZA KWA MAKINI KWANZA!!

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.

Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.
Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi (authentic) na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.
Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja (mtanashati) alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.
Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!
Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).
Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja. Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia (hearing aid). Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa, Guess what!
Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!
Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!
Chanzo: The Hill Of Wealth

Friday, October 2, 2009

HATIMAYE MZEE WA LUNDUNYASA, AANZISHA BLOGU NYINGINE

Mzee wa samaki au mzee wa kuvua samaki hatimaye kaanzisha blog Mpya. Hii ni kwa mujibu wake baada ya tafakuri yamuda mrefu. Karibuni alikuwa kipitia hudma za wordpress lakinihakufanikiwa kuanzisha blog hapo, badala yake ameamua kuendelea kutumia huduma za blogger.

Blog yake hiyo mpya inaitwa http://www.fananinyasa.blogspot.com/. ambayo itakuwa ikizungumzia mambo mbalimbali isipokuwa kuhusu nyasa. Katika blog hiyo kutakuwa na makala zake zinazotoka katika magazeti mbalimbali ya Bongo kama MwanaHalisi, Fahamu, Tazama na KwanzaJamii.

Kwa mujibu wa mzee wa Nyasa ni kwamba ameona ni wakati bora zaidi kufanya hivyo ili kuendeleza kipaji chake cha uandishi wa makala. Hapo ndipo utakapoweza kumfahamu zaidi Markus Honorius badala ya yule Markus Mpangala wa Lundunyasa. Inawezeakana usielewe lakini jina kamili la huyu bwana ni MARKUS DAUDI HONORIUS MPANGALA.

Kwani anaita blogu hiyo FANANINYASA? i FANANI= ni msimuliaji, NYASA= ni kwao mwambao wa ziwa nyasa katika kijiji cha Lundu. kwahiyo ni msimulizi kutoka nyasa. Naamini wanablogu watamwunga mkono, lakini lundunyasa itabaki kama ilivyo ila itazingatia sana mambo ya nyasa na RUVUMAnI hayo tu

Markus Daudi Honorius Mpangala
Maliwa Avenue-Monesteri,
Lundu, Mbinga Magharibi
Ruvuma.

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MAMA

Mama leo ni siku yako ya kuzaliwa. Twakupenda mama yetu , na twajua kimwili haupo nasi na twaamini kiroho upo nasi. Leo ningekuwa Ruhuwiko ningekuja Mkurumo kushinda nawe. Ama ungekuwa bado u nasi kimwili ningekupigia simu na kukupongeza kwa siku hii ya kuzaliwa na halafu tungecheka kama tulivyokuwa tukicheka. Tunakukumbuka sana na pia tunakutamani sana.

Baada ya kusikiliza mziki huu nikakawa nimeguswa sana. Nikeona si mbaya kama nikiweka hapa kwani najua wote tuna ujumbe mmoja. HONGERA SANA MAMA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA LEO UNATIMIZA MIAKA 57. HONGERA MAMA NAJUA UNANISIKIA.

Ngoja kwa pamoja tusikilize ujumbe huu

Thursday, October 1, 2009

KAZI YA UALIMU: TAALUMA MUHIMU ILIYODHARAULIWA

Mwalimu akiwa darasani anafundisha

Katika maisha yangu nimeishi na walimu sana . Kwa hiyo nimekuwa nikijiuliza miaka yote hii mingi. Na nimekuwa nikipatwa na uchungu sana nionapo watu/serikali jinsi inavyoiona kazi ya Ualimu kama isiyo na maana. Kila nikijaribu kufikiri, kazi zote hapa duniani naona hakuna kazi ngumu kama UALIMU.

Fikiria mtoto aanzapo shule hajui kuandika, kusoma wala kutamka a, e, i, o, u. Lakini mwalimu anahenya kwa kila njia na baada ya muda mtoto anaweza kusoma kuandika kutamka silabi zote bila shida kama mtoto si mgumu kuelewa. Na hii sio walimu wa shule ya msingi tu ni kuanzia chekea (vidudu) kule ndio kuna kazi kubwa zaidi.

Kwa nini walimu wanadharauliwa na pia mishahara yao ni midogo sana. Kwa kweli inatia huruma. Mshahara wa kima cha chini Tanzania hivi sasa ni laki moja kwa kweli hii ni halali?

Ni juzi tu nimesikia ya kwamba idadi ya wanaoomba kusoma ualimu hapa sweden inapungua kwa kiwango kikubwa sana. Sijui huko tuendako kutakuwa na walimu. Na pia kuna kupunguzwa walimu katika kila shule watapunguzwa walimu 14. Sasa mbaya zaidi wanawapunguza walimu vijana na wazee wanaendelea kufundisha .

Awali nilidhani matatizo ya Waalimu labda ni kwa nchi za Africa pekee, lakini nilipokuja hapa nchini Sweden, ndio nikajua kuwa hata hapa matatiozo ni yale yale, yaani yanafanana kwa kiasi cha kikubwa sana. Kwa hapa Sweden walimu wanateseka sana na pia hawaheshimiwi kabisa. Wanafunzi wana dharau sana wanawaona waalimu kama ni watani wao, wanajibizana nao, na wakijaribu kuwaelimisha jambo ni wabishi ajabu, na kuwaadhibu kwa viboko hapa nchini Sweden ni makosa. Hapa hakuna viboko kabisa kwa hiyo kiboko ni maneno tu. Tena maneno yaenyewe inabidi yawe mazuri na ya unyenyekevu. Na kama Mwalimu akijaribu tu kupandisha sauti kumkaripia mtoto anaweza akachukuliwa hatua kali za kinidhamu na anaweza hata kupoteza kazi yake.

Kuhusu swala la mshahara:- Kima cha chini cha mshahara wa mwalimu hapa nchini Sweden ni 3,600,000TSh, kwa pesa ya hapa ni 20,000SEK. Kiasi hicho cha mshahara kwa huko nyumbani Tanzania unaweza kuona ni kiasi kikubwa sana, lakini ukilinganisha na maisha ya hapa ni pesa ndogo sana na usipokuwa makini unaweza kushindwa kumudu baadhi ya ghrama za maisha. Hebu angalia mchanganuo wa makato ya huo mchahara pamoja na matumizi ya lazima, kodi kwa ujumla anahitaji kulipa 1,200,000TSH. Baada ya hapo zinabaki 2,400,000TSH. Chakula, bili n.k ni kama 10,000SEK = 1,800,000TSH. Baada ya hapo zinazobaki kabisa ni kama 600,000TSH. Kwa kiwango cha gharama za maisha ya hapa Sweden, bado pesa hiyo ni ndogo sana.

Kwa kweli waalimu wanayo kazi kubwa, lakini mapato madogo wakati kazi ya ualimu ni nzito na ndio mwanzo wa watu kujua kusoma na kuandika. Bado najiuliza, hivi kwa nini waalimu wanadharauliwa kwa kazi hii ngumu ya kuelimisha.?