Monday, September 30, 2013
JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TISA INATUKUMBUSHA AFRIKA....TANZAN IA NA MALIASILI YAKE...MBUGA!!!
Nawatakieni wote mwanzo mwema wa wiki hii. Binasi nina furaha isiyo kifani leo kwani rafiki yangu mpendwa tumeongea leo..tulikuwa tumepoteana miezi kadhaa. AHSANTE MUNGU KWA HILI.
Friday, September 27, 2013
LEO NAPENDA NIWAPELEKE MPAKA NYUMBANI KWETU LITUMBAND´YOSI ..HAPA NI SHULE YA MSINGI AMBAYO MDADA MIMI NIMEWAHI KUSOMA ...
SHULE YA MSINGI LITUMBAND´YOSI
Leo nimekumbuka sana nyumbani yaani kule alikozaliwa baba yangu ndiko kwa mimi ni nyumbani kwangu....Nikakumbuka shuleni hapa jinsi tulivyokuwa tukikutana shule nne kwa mashindano ya Kililupa..ikiwa na mana shule ya msingi Kingoli, Litumband´yosi, Luhagara na Paradiso. Ilikuwa ni michezo ya kata. Najua wengi mliosoma shule hizi nayi mtakumbuka jinsi ilivyokuwa....Nawatakieni wote Mwanzo mwema wa mwisho wa wikiThursday, September 26, 2013
NIMELAZIMIKA KUVUNA NYANYA ZANGU KWA AJILI YA BARIDI KUWAHI MAPEMA KULIKO MATARAJIO YANGU....
Hizi ni nyanya zangu ambazo zilikuwa bado kuiva kama mnavyoona ...nimeamka leo asubuhi nimeshikwa na butwaa nyasi zote zilikuwa nyeupe theruji kabisa kitu ambacho zikutarajia kwa haraka hivi. Kwa hiyo imenibidi kuzivuna kabla hazijaharibika sana na kuzihifadhi. Vipi SIJUI kwa kweli..Je nikizihifadhi kwenye boxi zitaiva? Maana hapa ni nusu ya tulizokula....
Hahahaaa:-) na nikaamua nivune tu na vitunguu vilivyobakia ...mkulima wa ajabu anaanza kula kabla hajavuna na sasa vimebaki sita (6) tu....KARIBUNI KUNISAIDIA KULA NYANYA HIZO!!!

Wednesday, September 25, 2013
MSIFIKIRI NIMEPOTEA NIPO ILA MAJUKUMU YANAFANYA NIADIMIKE
....Nitarudi muda si mrefu kuwa nanyi, tena labda kesho tu......nawatakieni wote kila la kheri panapo majaliwa tutaonana kesho. Kapulya
Monday, September 23, 2013
SIMTAKI......UAMUZI MZITO!!!
Leo nimeamaka nikiwa nikiwaza habari ambayo niliwahi kusoma.....Ilikuwa saa 11 jioni. Msichana mmoja kwa jina la Veronika alikuwa akitoka shuleni kwake. Alikuwa kidato cha nne. Alikuwa anaelekea kwenye shule ya Sekondari ya wavulana. Ilimbidi amwone Robert, rafiki yake wa kiume. Veronika alikuwa akifikiri moyoni: "Sina budi kumwona Robert leo. Siwezi kusubiri tena"
Wakati huo huo huo wavulani walikuwa wakitoka shuleni pia. Punde si punde alimwona Robert akitoka katika kikundi cha wavulana wengine akimji. Alikuwa akitabasamu lakini Veronika aliweza kuona kwamba Robert alikuwa na mshangao pia kumwona yeye pale. Kwa kawaida walikuwa wanakutana kwenye stendi ya basi. Na maongezi yaliendelea hivi:-
ROBERT: Habari za jioni Veronika? Nina furahi kukuona .
VERONIKA: Sijambo, Robert ....ah.....Ninataka kuzungumza nawe. Je? kuna mahali pa faragha shuleni kwako- mahali ambapo tunaweza kukaaa na kuzungumza bila mtu kutubugudha?
Robert alimtazama kwa fadhaa kidogo lakini hakumuuliza zaidi.
ROBERT: Ndiyo, nadhani tunaweza kwenda kule maktaba. Leo ni ijumaa na ni mwanzo wa pumziko la wiki, hatuna masomo. Nina hakika hapatakuwa na mtu.
Veronika alimfuata bila kusema kitu. Waliketi mwishoni kabisa mwa chumba cha maktaba wakimpa kisogo mfanya kazi wa makataba ambaye alikuwa akishughulika na kadi za vitabu.
ROBERT: Kuna matatizo gani Veronika? Mbona unaonekana kuwa na wasiwasi na huzuni?
Veronika alimtazama Robert, halafu aliinamisha kichwa .
ROBERT: Veronika kuna nini? huna budi kuniambia unajua mimi ni rafiki yako. Unahofu nini? labda umeshindwa mrihani wako wa katikati ya muhula?
Veronika: Hapana Robert. Ni kitu kikubwa kuliko hicho.... Ni ...nina mimba.
ROBERT: Nini? Una uhakika?
Robert alishikwa na bumbuwazi. Mawazo mengi yalipita ghafla akilini mwake.
VERONIKA: Ndiyo, nina hakika. Lakini simtaki. Robert, simtaki mtoto huyu. Wazazi wangu wakisikia juu ya jambo hili hawatanipokea tena nyumbani kwetu. Pia itakuwa ni mwisho wa masomo yangu. Unajua, mwaka kesho ningeanza masomo ya uuguzi.
ROBERT: Najua.....Utafanya nini sasa? Ninaona njia moja tu: Ondelea mbali "kitu" hicho.
Veronika alifikiri:"kitu" hicho ni mtoto. Moyo wake ulikuwa unamwambia kuwa alichokuwa anapanga sasa ni jambo baya sana. Lakini Veronika hakustahimili ile aibu wala wajibu wa tendo lake. Sasa alikuwa amekata shauri.
VERONIKA: Ninajua nitafanya nini. Nitakwenda kwa rafiki yangu Sarah. Yeye ni muuguzi kule hospitalini. Nitamwomba anipatie dawa ya kuondoa mimba, nina hakika atanisaidia. Hakuna mtu mwingine atakayejua. Hapo maisha yataendelea tena kama mwanzo.
Maneno haya ya mwisho Veronika aliyasema kwa sauti ya kunongóneza. Robert alikuwa ameshika kichwa chake kwa mikono yake miwili naye hakuthubutu kumtazama Veronika. Yeye pia alitambua kuwa anahusika lakini alifikiri: "Kwa kweli, hakuna njia nyingine, au sivyo? Hakujua. Lakini Veronika alikuwa amekwisha amua tayari. Basi, alimuuliza tu....
ROBERT: Utakwenda kumwona rafiki yako lini?
VERONIKA: Kesho......
Inasikitisha kweli kuona jinsi hali hii inavyorudiwa rudiwa mara nyingi siku hizi. Katika namna zoto za maisha kutoa mimba kumekuwa ni jambo la kawaida, jambo linalotokea mara kwa mara. Magazetini huandika kinaganaga jinsi watoto wanavyookotwa kwenye mapipa ya takataka, katika vyoo vya uma, n.k. Kutoa mimba kunaonekana kama njia ya kuondoa kitu kisichotakiwa ; njia ya kusahau kitu ambacho kisingelikuwa kimetokea.....ITAENDELEA......Habari hii nimeipata katika kitabu cha NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA...

Sunday, September 22, 2013
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!
Au pia tumsikiliza dada Jennifer Mgendi na wimbo huu Jaribu langu!!
NAWATAKIENI JUMAPINI NJEMA NA YENYE AMANI PIA UPENDO KWA WOTE NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZITAWALE NYUMBANI MWETU/MWENU AU MWAKO...
Friday, September 20, 2013
MNAKUMBUKA NILIWAHI KUWAAMBIA NIMEPANDA DODOKI ? HAPA NI MAENDELEO YAKE!!!!!
Hicho chungu cha bluu ndio mmea wa dodoki/madodoki mwenyewe umekuwa na umetambaa mpaka kwenye paa ya varanda...sasa leo nimegundua -----
Mmea huo umeanza kutoa maua na pia dodoki zimeanza kujitokeza hakika nimefurahi sana. Ila sasa najiuliza nitaumewka wapi maana kaubaridi kameanza na mmea huu unataka joto ....maana mwisho wako
...ndo dodoki linakuwa hivi hapa tayari lishakomaa na kukauka tayari kwa kujisugulia mwilini. Hili nilinunu Songea Sokoni mwaka huu...Kweli hili hapo juu karibu na ua litakuwa kama hili?...Mwenye ushauri naomba tafadhali!! Nawatakieni jioni yenye upendo na amani.

TUIANZE IJUMAA/MWISHO WA JUMA NA ZILIPENDWA...
Hakika vya zamani ni vizuri na vinadumu hizi tulikuwa tukizisikia tangu tupo migongoni wa mama zetu .....Nafurahi zimetunzwa na leo watoto wetu wanaweza kusikiliza...IJUMAA NJEMA KWA WOTE...
Wednesday, September 18, 2013
NILIKUWA NATEGEMEA KULA HAYA MABOGA LEO KUMBE....HAYALIWI .....
Mavuno ya maboga..Nimepata manne na leo nilipanga iwe siku ya kuyala nilitaka kutengeneza supu, kuchemsha na futari. Lakini wifi yangu kaniambia hayaliwi eti ni chakula cha nguruwe tu na yeye ndiye alinipa mbegu. Sasa hapa najiuliza kama nguruwe anakula na kupona kwanini binadamu asile...Kuyatunza kwote nilikofanya yaani ni kazi ya cheka bure kweli???,,Na ndo nikaamua niwaulize ndugu zanguni je ni kweli?...Maana majani yake yana mibamiba zikukuchoma zinawasha na majani ni mapana kuliko ile mboga ya maboga ya Njombe na ile ya kawaida...Au sijui ni mabuyu/ yale ya kutekea maji au kunywea maji yaani kata?...Duh kaaaazi kwelikweli hapa sasa nimekwama inabidi nianza upya kuwaza cha kula:-(.
Tuesday, September 17, 2013
UJUMBE /SWALI WA/LA LEO!!!
Kama huwezi kujisamehe mwenyewe na uliyoyafanya, utawezaje kuwasamehe wengine?
NAWATAKIENI WOTE JUMANNE NJEMA SANA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA DAIMA!!!Kapulya!

Friday, September 13, 2013
MDADA KAPULYA SI MTU WA KUTULIA ..MSIMU WA BUSTANI UNAKARIBIA KWISHA NA SASA WAJA MSIMU KUCHUMA UYOGA NAYE NI MPENZI SANA WA KAZI HII KWA HIYO LEO ALIKWENDA MSTUNI NA HAPA NI MATOKEO YAKE....
Kuchuma uyoga ni kitu ambacho nakipenda sana , unakuwa na wakati mzuri wa kutafakari, pia mazoezi nahalafu unapata mboga ..Mboga hii mimi nimeipata bure leo mstuni lakini kama ningekwenda kuinunua dukani kwa kilo ni kama kwa kila shilinga 23000/= . Nami nilipata lita kama tano hivi. Sasa kazi nyingine unaporudi nyumbani ni kuusafisha na ndio hapo nafanya kutoa mchanga na takataka nyingine,,,,
Baada ya masaa matatu uyoga tayari umetolewa takataka zote na upo safi kwa kuliwa.....
...Uyoga upo kwenye plain pan tayari kwa kuandaliwa kwa ajili ya mlo wa jioni......
.....baada ya dakika tano umepungua kiasi hiki na maji mengi yamejitokeza ..naendelea kukausha maji...
---Maji yamekakamia na hapa sasa ni kuweka chumvi, sukari kiduchu kwa ajili ya ladha..na pilipili manga kidogo na kikubwa zaidi siagi kama kijiko kimoja cha mezani unakaanga kwa dakika kumi....
...baada ya hapo unaweka krimu ya maziwa na kama huna krimu basi weka unga wa ngano kijiko kimoja cha mezani na maziwa kikombe cha chai,,,,
Na mwisho mlo ukapatikana hivi:- Wali, kuku, uyoga uloungwa kama nilivyosema hapo juu ikiwa na nyanya kutoka bustanini kwetu, tango na majani ya ruccula. Na hivi ndivyo ilivyoisha IJUMAA YA KAPULYA na mpishi ni YEYE MWENYEWE KAPULYA:-) TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA !!

IJUMAA YA LEO NIMEFIKA HADI IRINGA NA NIMEONA NIWAONYESHE KILE NILICHOKIONA NA KUKIFURAHIA:- NGOMA YA ASILI YA WAHEHE/WABENA KARIBUNI!!!
NAPENDA KUWATAKIEWNI WOTE IJUMAA NJEMA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA. Kachiki upu nawe mtani wangu Fadhy na wengine wote jiungeni nasi najua kaka S na dada mkuu msaidizi mnakumbuka kitu hapa...
Wednesday, September 11, 2013
KATIKA MAISHA NI VIZURI KUWAFARIJI MWENYE MATATIZO
Huu ni ushauri wangu mimi kwa wewe uliye na rafiki aliye na matatizo:-
1) Kama rafiki yako ana matatizo usiogope kumwuuliza hali yake kwa ujumla hata kama hali yake inaonekana si nzuri. Kama una matatizo halafu watu/marafiki wanakuuliza U HALI GANI utajisikia amani yaani kuna watu ambao wanakujali haupo peke yako.
Wakati mwingine kunatokea mambo ambayo si kweli na watu wanafikiri kuwa tayari yule mwenye matatizo amepata msaada mtu wa kuongea naye, wakati kumbe wewe upo peke yako kwa hiyo kuuliza ni muhimu sana.
2) Piga simu au nenda ili kujua mpatwa matatizo ana hali gani. Pia pika chakula, nenda kwake na mle pamoja. Wakati matatizo yanapotokea, inakuwa ngumu kuelezea vitu ulivyozoea kufanya kila siku. Kama una watoto inakuwa ngumu zaidi kuwatunza wakati upo kwenye matatizo/majonzi.
3) Onyesha upendo wako, bila kuonekana ni usumbufu kwa mpatwa matatizo, uwe nusu nusu. Usizidishe au usipunguze. HAPO NDIPO UTAWEZA. ......Huu ni mtazamo na ushauri wangu ...PAMOJA DAIMA,.

Monday, September 9, 2013
PALE INAPOFIKIA MSIMU WA BUSTANI KUVUNA/KWISHAKWISHA KWANI MSIMU WA BARIDI UNAKARIBIA SASA
Hapa ni maboga yanakaribiwa kuwa makubwa na tayari kwa kuliwa..kwa uzowefu wangu inabidi yawe na rangi ya njano kidogo ili kujua yamekoma ..ila sijui ni kweli naomba ushauri wenu....
Hapa ni mboga ya maboga mnaona inakaribia kufa/ kwisha ila nimekula sana na akiba nimeweka kwa hiyo karibuni sana .
Nyaya ndo bado, zinaendelea kuiva kila siku ila nasikitika sina sehemu ya kuzihifadhi hapo baridi itakapozidi
Mchicha nao umechokachoka na pia umeanza kuchanua na hapo ndipo nitakapopata mbegu za mwakani ila sijui kama zitawahi kukauka...Je naweza kuzitoa kabla ya kukauka na kuhifadhi sehemu ..akina bwana shamba na wataalamu naomba ushauri....
Na hapa ni ile figiri niliyowaambia nitapanda nyingine imekuwa kufikia hapa. Ni kwamba natumia ujanja wa kufunika na kitambaa fulani chembesi sana ili wale viwavi jeshi wasile na naona inakuwa vizuri. Kwa figiri huwa inavumilia sana baridi maana hizi mbegu nimepata Njombe na baridi ya Njombe ni sawa na hapa mwanzono mwanzoni....
Kapulya si mpenzi wa kulima bustani za mboga tu ni mpenzi wa bustani wa maua na maua ya kupanda kwenye makopo...Ua hili huwa linanikumbusha shule nyingi za msingi na secondary nyumbani Tanzania.
Hapa pia ni ua ambalo nimelitunza na limenipita hadi urefu mimi mwenyewe ..mnaona kazi hiyo...hapa huwa nakaa na kutafakari mengiiiii nikiliangalia hili ua.
HAYA NAWATAKIENI WOTE JUMATATU IWE NJEMA NA PIA WOTE MNAPENDWA...KAPULYA WENU

Sunday, September 8, 2013
NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI WOTE!!
Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda, kuniongoza, kunifanya nipate chakula, na kuniepesha na yasiyo mema. Nakutumaini wewe Mungu wangu , eh Mungu, wewe ni mwamba imara katika maisha yangu ...... Pia napenda kuwaombea familia, ndugu, wazazi/walezi, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzangu pia hata madui zangu. Mwenyezi Mungu na atushushie wote baraka na upendo pia amani ...AMINA. . NA UJUMBE WA LEO NI:- SISI SOTE NI NDUGU,WATOTO WA BABA MMOJA.
Friday, September 6, 2013
NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA ......SEHEMU FUALANI NDANI YA AFRIKA...
NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMA WA JUMA TUWE NA AMANI NA KILA LA KHERI KWA KILA KITU TUKIFANYACHO...NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA....Sisi sote ni ndugu na ni watoto wa baba mmoja ....Kapulya
Wednesday, September 4, 2013
LEO TUANGALIA JIOGRAFI,HISTORIA YA MJI WETU WA SONGEA!!!
Leo tuangalia mji wa SONGEA:-
Songea ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabika kuwa 131,336. Kuna barabara ya lami kutoka Songea kupitia Njombe hadi barabara kuu ya Dar es Salaam - Mbeya. Barabara ya kwenda pwani kupitia Tunduru na Masasi ni mbaya mara nyingi haipitiki wakati wa vua haswa..ila sasa iko mbioni kutengenezwa...
JIOGRAFIA KIDOGO:-
Mji wa Songea uko kimo cha M 1210 juu ya UB katika nchi ya Ungoni kwenye nyanda za juu za kaskazini za Tanzania. Chanzo cha mtu Ruvuma kipo karibu na mji.
HISTORIA:-
Jina Songea ni kumbukumbu ya chifu Songea wa Wangoni aliyekuwa na ikulu yake hapo wakati wa kuenea kwa wa ukoloni wa Ujerumani akauwawa na Wajerumani wakati wa vita ya majimaji.
Mji wa Songea (iliandikwa Ssongea wakati ule) ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani. Ukakua kuwa makao makuu ya utawala wa mkoa wa Songea wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Mazinginra ya mji yaliathiriwa vibaya na vita ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.
Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.....HII NI HISTORIA/GEOGRAFIA YA MJI WA SONGEA...

Tuesday, September 3, 2013
TUSISAHAU METHELI ZETU ZA KISWAHILI....!!!!!
1. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
2. Yote yangáayo usidhani ni dhahabu.
3. Ungelijua alacho nyuki, usingelionja asali.
4. Radhi ni bora kuliko mali.
5. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune.
NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA WOTE NA KAMA UNA METHALI PIA ONGEZEA:-)

Sunday, September 1, 2013
NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA 22 YA MWAKA C IWE NJEMA !!
Mdada katoka kanisani hapa
Sala ya leo kwa ajili ya kuwaombea watu wote:
Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana
yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,
mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.

NA TUSISAHAU KUWAOMBEA JT. YUSTO, INGRID, JN GREGORI MKUU , SOFIA
JO ..ROSALIA, IRMGARD, AL.. ROMULO, ROSWITA...IJ ...MAGNUS, ALEX, JS YIDITH.
TUPO PAMOJA. AMINA
.
Subscribe to:
Posts (Atom)