Showing posts with label ushirikiano. Show all posts
Showing posts with label ushirikiano. Show all posts

Thursday, February 9, 2017

BLOGG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA HII PICHA KUWA PICHA YA WIKI....

Hakuna kupoteza muda hapa...nimeipenda hii safi sana UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU....AU MNABISHA?

Friday, April 12, 2013

LEO TULIKUWA TUKIMSINDIKIZA DADA YETU MPENDWA MARIANA KATIKA SAFARI YAKE/MAKAO YAKE YA MILELE....

Kama nilivyowataarifu hapa basi leo imekuwa siku ya mwisho kumsindikiza dada yetu, Mama yetu na rafiki yet mpendwa Mariana katika makao yake ya milele..................................................................


HAPA NDIPO ATAKAPOLALA DADA MARIANA
 PAMOJA NA MWANAE MANUELA
Siku ya leo imekuwa siku ndefu na ya masikitiko kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na imekuwa siku ya kujifunza mengi kwangu, kutoka kwa da´mkubwa Mariana kwa kweli. Ama kweli wote watendao mema huwa wanatutangulia kwanza. Katika maisha yangu hapa nimewahi kwenda  kwenya misiba/mazishi mingi/mengi sana lakini huu leo hapana. Watu walifurika kuliko kawaida kiasi kwamba nikajiona nipo kwangu Afrika. Na kanisa lilikuwa halitoshi kabisa. Kweli ukitenda mema utarudishiwa hapa hapa duniani. Watu walifumuka pande zote. Au niseme hivi kwa kifupi dada huyu hakuna neno la kutosheleza maelezo yake kwa kweli,,,,alijali sana wengine na mpaka kujisahau mwenyewe. NITAKUKUMBUKA DAIMA. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA

Wednesday, December 7, 2011

TAARIFA ZA MSIBA WA BABU WA BLOGA WENZETU KAKA BARAKA CHIBIRITI HUKU NYUMBANI TANZANIA!!

Picha ya Babu Blezi Chibiriti, akiwa na mwanae wa mwisho mpendwa wake Fabiani Chibiriti


Kwa habari zaidi basi soma hapa. Babu yetu ustarehe kwa amani.

Friday, December 2, 2011

TUWE PAMOJA NA KAKA Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) KWA MAOMBI YA MSIBA WA MAMA MZAZI HUKO NYUMBANI TANZANIA!!

Kaka Mrope pole sana kwa msiba wa mama yetu mzazi kwani naamini mama yako ni mama yetu.Katika pita pita zangu nimekutana na habari hii ya kusikitisha.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
TAARIFA YA MZIBA
Napenda kuwataarifu ndugu zangu na marafiki popote mlipo kuwa nimepatwa na msiba wa mama yangu mzazi Shamsa binti Hassan aliyefariki huko nyumbani Tanzania leo tarehe 2/12/2012. Habari za kisomo na dua zitawajia baadae. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...Kwa pole napatikana 301 222 7739.... nahitaji maombi yenu.Wenu, Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) http://tustaarabike.blogspot.com/

Tuesday, March 29, 2011

SHUKRANI ZA DHATI TOKA KWA FAMILIA YA MZEE NGONYANI/K​LAESSON!!!


Familia ya mzee Ngonyani 2008-2009 Ruhuwiko-Songea
Kwa niaba ya wanafamilia jamaa na marafiki wote. napenda kutoa shukrani za dhati kwa kuwa nasi bega kwa bega tangu 23/3/2011 siku ya Jumatano mpaka hivi leo. Kwa kweli ninyi ni NDUGU wa kweli kabisa hamkuwa nyuma hata mara moja. Nilipopata tu habari hii nikajikakamua ili kuwahabarisha. Hazikupita sekunde baada ya kuweka tangazo mara nikaona maoni yananza kutiririka. Nikawa mchovu nikaenda kulala, kuamka asubuhi naangalia nakuta Mawazoni nako tangazo lipo. Dakika hazipiti mara naona tangazo jingine kwa mdogo wangu kwa mama mwingine Vukani naye ameweka na pia kashikwa na mshangao wa kutoweka kwa ndugu yetu mpendwa Asifiwe. Mara nasikia simu yangu ya kiganjani inaita napokea nasikia sauti ambayo sijawahi kusikia sio mwingine tena bali ni yeye mwenyewe Mwanamke wa shoka. Dada huyu amekuwa akinipigia simu kila siku kutujulia hali. Na pia bila kusahau tumekuwa tukitumiwa barua pepe nyingi nyingi mno pia ujumbe wa simu ya kiganjani. AHSANTENI wote na mwenyezi mungu awazidishia mara dufu kwa wema wenu. Hakika kwa msaada/ushirikiano wenu wa kueneza habari na wengi wakiwemo wanafamilia kuweza kupata habari kwa njia hii tunawashukuru sana. Watu wengi wameguswa sana na kifo cha ndugu yetu Asifiwe, sina la kusema zaidi ya AHSANTENI SANA. Kuhusu kumuenzi Asifiwe hakukuishia hapo naye Swahili wa Waswahili akaongeza mchango wake. Habari zikazidi kuenea na watu wakawa wanazidi kutufariji. Kwa kweli hapo ndipo nilipojikuta najisemea, kweli kublog si kublog tu bali ni mahali ambapo hukutanisha watu na kuwa NDUGU. Muda ukapita nikaona Kazi yako ni jina lako naye kaweka tangazo nikapiga magoti na kushukuru jinsi habari zinavyoenea kwa haraka. Hapa bado ni siku ya Alhamisi 24/3/2011 mara nikaona Mwananchi mimi kaandika kitu pia wakiwa wawili zaidi yaani kaka Shabani Kaluse na Chacha o`Wambura. Na hapo hapo nikawa napokea simu, watu wakitupa pole kwa msiba nikajikuta kama nipo hapa nyumbani na watu 500 kumbe hapana. Matangazoyakazidi kuongezek na watu kupata habari kona zote kwani naye Nyahbing worriors hakuwa nyuma. Ijumaa tarehe 25/3/2011 Diwani ya fadhili akasema hapana ni lazima niweka kitu, kwa kweli nasema kama mdogo wangu Koero Mkundi alivyosema kuwa msiba huu si wangu tu ni wa wote ni kweli kabisa. Kufumba na kufumbua barua pepe zikawa nazo zinamiminika kutoka sehemu mbalimbali. Wote mliotuma msione kimya tumezipata pole zenu ila ni kutingwa tu. Mwenyezi Mungu na awe nanyi. Kweli aliyeanzisha kublog na apongezwe sana. Habari ya msiba wa Asifiwe haikuishia hapo kwani Mzee wa Lundu Nyasa naye akaibuka kutoka ziwani. Lakini hata hivyo kama waswahili wasemavyo hakuna kuchelewa naye Mzee wa Changamoto akaona naye ni lazima atoe aliyo nayo moyoni. Halafu napenda kumshukuru BOSI wangu kwa kunipa ruhusu ya kuwa nyumbani kwa nyumbani kwa kipindi hiki kigumu. Bila kuwasahau WAFANYAKAZI WENZANGU ambao wamekuwa wakipiga simu na kunipa pole. Kwa kweli zimekuwa siku za machungu, pigo pia tumeachiwa pengo ambalo halitazibika kamwe. Tarehe 26/3/2011 ndio ilikuwa siku ya mazishi niliendelea kupokea simu kutoka sehemu mbalimbali na pia nikiwa nawasiliana na Ruhuwiko. Kwa kifupi mazishi yalifanyika kwa utulivu mkubwa, watu walifurika kama utitiri kiasi kwamba Kanisa la Ruhuwiko likawa ndogo . Kwa niaba ya wanandugu, tunawashukuruni sana wote walioshiriki wakiwa karibu au wakiwa mbali kwa kumsindikiza Asifiwe katika safari yake ya mwisho. AHSANTENI SANA WANABLOG/WASOMAJI WANANDUGU WOTE. TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU WA HALI NA MALI. BILA NINYI SIJUI INGEKUWAJE? PAMOJA DAIMA!!!

Monday, March 28, 2011

Marafiki waliokuja kutufariji siku ya ijumaa!!

Hapa ni marafiki wawaili waliokuja kutufariji siku ya ijumaa wote manjua mimi ni hapo katikati na kulia kwangu ni Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo na kuchoto kwangu ni Dada Asta kutoka Ivory Coast. Hapo walinilazimisha kunywa chai na unywaji wangu wote wa chai hapo nilikuwa hoi kabisa. Wote tunawashukuru kwa kutufariji maana wanaonywsha ushirikiana mzuri. Na jana Jumapili alikuaja Dada mmoja yeye anatokea Njombe ila samahani nilitingwa kuchukua picha yake. Na picha hii hapo juu mpigaji si mwingine tena ni Erik..... nitarudi mtandaoni hivi karibuni nitengamae kwanza. MNAPENDWA WOTE...