Showing posts with label destu na mila. Show all posts
Showing posts with label destu na mila. Show all posts

Tuesday, August 20, 2013

PALE MILA NA DESTURI ZINAPOPISHANA...TUMEMZIKA MAMA IRENE IJUMAA 16/8-2013 TANGU ALIPOTUACHA 3/11/2012!!!

Kama wengi mnakumbuka mwezi Novemba tarehe 3 mwaka jana nilifiwa na mama mkwe wangu ghafla tu kwa kujikumbusha inga hapa. nachotaka kusema hapa ni kwamba ijumaa ya tarehe 16/8 -13 ndiyo tumemzika mama Irene. Sababu kubwa ya kusubiri muda mrefu kiasi hiki ni kwamba:- Kwanza ardhi ilikuwa ni ngumu kuchimba kaburi baridi kali mno..Pili ni kwamba mwili wa mama Irene ulichomwa moto. Hakika hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona utamaduni huu. Kwa hiyo kwenye hicho chombo hapo chini ni masalio ya mwili wa mama Irene

Mwili/majivu ya mama Irene

 Hapa pia na mishumaa imewashwa
Na hap ndiyo safari yake ya mwisho kwenye nyumba ya milele. Walichimba kashimo tu ili kutosheleza hicho chombo kilichokuwa na majivu. Na ni kaburi alilozikwa baba mkwe pia kwa hiyo wote wamezikwa katika kaburi moja..Duh ama kweli tembea uone mengi ila kuchomwa moto..mmmhhh sijui!! UPUMZIKE KWA AMANI MAMA YETU MPENDWA IRENE.

Tuesday, June 18, 2013

NIMEFANYA UTAFITI KATIKA MILA NA DESTURI ZA WANGONI UPANDE WA NDOA NA KUCHUMBIA/KUOA MKE KUZAA...MTOTO WA KIUME NA KIKE!!!!

Kugega mdala= Kuoa mke
Kama wote tujuavyo:- Kijana na msichana wakikua, wanaoa. Kwa wangoni, mtoto wa kuime hata kama akikua na kuoa atakuwa bado anahitajika kwenda vitani. Kipindi hicho yupo vitani inabidi aonyeshe nguvu zake zote. Kijana ambaye hajaenda vitani huitwa "lijaha". Kijana aliyerudi toka vitani huitwa "lidoda". Mwanamkewa kuolewa inabidi awe wa uhakika, anayeweza  kufanya kazi za nyumbani. Inabidi aweze kutafuta kuni, kuchota maji, kutwanga  kupika ugali/chakula, kupika pombe na awe mchangamfu/mcheshi achekaye na watu wote mtaani/kijijini.
Ndoa haifungwi ndani ya ukoo. Kwa wangoni hairuhusiwi ni mwiko kuoa/kuolewa na mke/mume ambaye ana jina moja la ukoo. kama watu wakioana kiukoo, wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali? (vitepulana) wataapishwa. Watu wanaogopa kuoana ndani ya ukoo kwa vile watoto watakaozaa watakufa wote au watapata kifafa au hata waliokufa (mahoka) watakasirika. Watu wenye Kifafa na wenye ukoma ni mwiko  kuoana.
MTENGA
Kwa kingoni cha zamani neno mtenga lilifahamika kama mtu aanyenunua au kuuza vitu. Pia Mtenga ni mtu auzaye mtoto wa kike. Yeye ndiye anayetoa mahali ya mwanzo na mahali yote kwa ukoo wa msichana.
VIPI KUTAFUTA MKE:-
Wenye mtoto wa kiume watakapo kumwoza kijana wao, wazazi wengine wanamtafutia mke, Wazazi wengine wanamwacha kijana wao ajitafutie mke ampendaye. Kama wame/watamwona msichana mzuri watatafuta mtu/ndugu ambaye watamtaka na watamwelekeza nini wanataka. Na huyo anaweza akawa MTENGA wao. Mtenga huyo ataanza kuulizia kisirisiri mambo ya wazazi wa msichana yule na ukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa mtoto wa kuime. kama wazzi wakiona ya kuwa ni msichan huyu atamfaa kijana wao kama mke ,watenga wataenda kwa wazazi wa msichana tena na kutoa taarifa ya posa. Kama wenye binti watakataa, watenga/mtenga itabidi awabembeleze.....Itaendelea

Tuesday, June 4, 2013

MILA NA DESTURI:- NI WAZO LA LEO KUTOKA KWA DIARY YANGU....EBU SOMA HAPA CHINI!!!

Katika pitapita zangu kila siku nakutana na mengi sana katika blog nyingi na hivi karibuni nilikuwa nimepita hapa na nikakutana na WAZO la mwanablog mwenzetu nimelipenda wazo lake nami nikaona si mbaya kama nikaleweka hapa ili kueneza wazo lake.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WAZO LA LEO: Mila na desturi zipo, na tumezikuta kwa wazee wetu, zipo nyingi, na nyingi hatuzijui tena kwa vile huenda hazikuwezekana kutekelezeka. Lakini kuna mambo mengi mazuri tumeyapuuzia, na kwa kufanya hivyo tumejikuta tukipata taabu sana,…nachukia kwa mfano wa kutafuta mchumba, kabla mtu hajaoa au kuolewa, wazee wetu walikuwa wakihakikisha kuwa mke au mume wa kuoa au kuolewa anatafutwa kwa kufanyika uchunguzi wa kina kwenye familia anayotoka…ni ni hekima yake, ni kuwa kwa kumpata mume au mke bora ni kwa ajili ya kizai bora, na matokeo yake ni kuwa na familia bora na hili litaweza kujenga taifa lenye amani, hili tumelipuuza, na matokea yake ndio haya..
Pia wazee wetu walikuwa wakiangalia kuwa huyo anayeolewa au kuoa, hana matatizo yoyote ya kiafya au ya kurithi, au tabia za kishirikina, au tabia zozote mbaya…haya yalikuwepo na ukiyachunguza kwa makini utayaona kuwa yalikuwa na faida zake, lakini huenda haya na mengine mengi hayapo tena tumeyapuuza.
Wazo langu la leo. Zipo mila nzuri, tuzifuate, na kama zipo mila potofu, tuziache, au tuziboreshe ziwe bora zaidi, lakini tusisahau kabisa mila na desturi zetu zenye hekima ndani, na kukimbilia mila na desturi za wenzetu,….kwanini tupuuze mila zetu, ….huo ndio utamaduni wetu na anayeacha utamduni wake ni mtumwa.
NIWATAKIENI JUMANNE NJEMA NA KILA MTAKALOTENDA LIWE NJEMA...UJUMBE TUPENDANE....KAPULYA WENU