Monday, November 29, 2021
NARUDI NYUMBANI:- LAKINI KWA MUDA TU!
NI RAHA ILIOJE KUWENDA NYUMBANI KULA LIKOLO LA NANYUNGU! TUTAONANA SI MUDA MREFU
Tuesday, November 9, 2021
Wednesday, October 6, 2021
Friday, September 3, 2021
UJUMBE WA WIKI HII!
Watu watano wanaostahili muda wako:-
1. Familia
2. Rafiki(bora) wa karibu
3. Mshauri/mlezi wako
4. Wanaohitaji msaada wako
5. Wewe mwenyewe yapaswa:- Ujipende na utumie muda wako kutafakari na kujiboresha.
Saturday, August 21, 2021
Wednesday, August 11, 2021
Wednesday, June 9, 2021
Monday, May 10, 2021
MKE ASIYE NA MUME, AKAMCHUMBIE NANI?
Niolewe na nani mie!
Isingekuwa vigeni, mwanamke kuchumbia
Ningepita mitaani, mume kujitafutia,
Nisimuudhi Manani, ndio nimejizuia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Ndege maingainga, si jambo la kujitakia,
Mume mwema natamani, vipi tajitafutia?
Na mwanamume haini, sitaki kunichumbia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Nimetulia nyumbani, sina mume kunioa,
Wanifuatao ndani, si wachumba wa kuoa,
Hutaka kunirubuni, maasini kunitia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Ndege maingainga, si kosa langu sikia,
Niliolewa zamani na mume mwenye udhia,
Kanitia kilabuni, pombe kumchuuzia
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Mimi nikamuamini, huku machozi nalia,
Mume hii kazi gani, alokataza jalia?
Kheri tukate kuni, mimi nitakuuzia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Akapanda hasirani, na maneno akafyoa:
Mke wee mke gani, dini lini ulijua!
Alipozidisha kani, ndoaye nikajivua.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Wako mabwana wa shani, ningependa kunioa,
Hawamtii shetani, Munguamewaongoa,
Nao wamomashakani, kwa mabibi walooa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Tu wema hatujuani, wake na waume pia,
Twaingia mashakani, kwa wenzi waso murua,
Namlilia Manani, mume mwema kunioa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Nawe muombe, ndoa yenu kutulia,
Tusikuone mwakani, viragoumepania,
Mke na mume nyumbani, mumche Mola Jalia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Shairi hili limetungwa na Sheikh Amri Abedi, nami limenivutia nikaona niliweke hapa ili tujifunze kwa pamoja
Thursday, May 6, 2021
MAHINDI YA KUCHOMA NI BORA KULIKO POP CORN!
Hivi kwa nini tusile mahindi ya kuchoma tuingiapo sinema kama ilivyo utamaduni wetu badala ya kula pop corn?
Friday, April 16, 2021
Thursday, March 25, 2021
TUMALIZE MWEZI HUU WA TATU KWA UJUMBE HUU UFUATAO:-
UHURU WA NCHI NI SAWA NA AFYA YA MWILI/MWILINI.
NAPENDA KUWATAKIENI AFYA NJEMA NA TUUMALIZE MWEZI HUU SALAMA.
PAMOJA DAIMA!
KAPULYA WENU.
Sunday, February 21, 2021
Monday, January 18, 2021
Subscribe to:
Posts (Atom)