Monday, April 30, 2018

NI MLO GANI WEWE UNGEPENDA KULA SIKU YA LEO?....

 Ndizi, nyama, na mbogamboga au
Ugali wa muhogo  nyama ya kuku na dagaa nyasa. haya karibu kuchagua.....

Saturday, April 28, 2018

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA HILI LA MWEZI HUU WA NNE!!


NAWATAKIENI  jioni njema ya Jumamosi pia kwa ujumla mwisho mwema wa juma.

Thursday, April 26, 2018

VAZI LA SKETI ALIPENDALO KAPULYA WENU

Sketi ndefu za heshima nizipendazo mimi Kapulya wenu...hiki ni kitenge aina ya dashiki

Tuesday, April 24, 2018

Tuesday, April 17, 2018

VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU

 UUgali kwa dagaa zilipikwa na bamia bila kusahau pilipili....
 Dagaa na mboga mboga kwa ugali mmmhh
 Njegele kwa nazi  yaani utamu mno
Na hsoa ni samaki ilipikwa jwa ustadi :-)

Monday, April 16, 2018

JUMATATU HII TUANZENA PICHA HII...ULANZI

Hii ni picha ya wiki sijawahi kuona unywaji huu wa ulanzi moja kwa moja kwenye mbeta. Duh! kaaazi kwelikweli..JUMATATU NJEMA NDUGU ZANGU PAMOJA DAIMA. PANAPO MAJALIWA.


Sunday, April 15, 2018

UJUMBE WA JUMAPILI YA LEO..MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KILA JAMBO

Usiwe na hofu kwa kuwa binadamu kukuacha katika udhaifu ulio nao kwa sababu yeye sio Mungu, na pesa sio kila kitu katika maisha, maisha hayajakamilika kwa mtu yeyote.

Kuna  mwenye nyumba lakini hana gari, kuna mwenye gari na hana watoto, kuna mwenye pesa hana afya, na kuna mwenye vyote lakini hana AMANI wala FURAHA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO

Saturday, April 14, 2018

KUMBUKUMBU:- USISAHAU ULIKOTOKA KWANI NDIYO MSINGI WA MAISHA


Hapa ni kwetu MAHENGE SONGEA MAMA, MIMI NA BABA 
NA ha pa ni kaka yangu mdogo XVERY  ilikuwa mwaka jana  mwezi wa kumi na mbili kwa kweli ilikuwa ni furaha sana kuweza kuonana

Tuesday, April 10, 2018

VYAKULA VYA USWAHILINI VINAVYOSAHAULIKA

Naanza kuwaza hili jambo iweje tusahau vyakula kama hivi vilivyotukuza, au ndo kama vile tunavyopenda mavazi ya kigeni na sasa ipo kwenye vyakula pia?

Monday, April 9, 2018

HARUSI NA VAZI LA KITAMADUNI KATIKA BAADHI YA NCHI BARANI AFRIKA....!

 Vazi la kitamaduni/asili nchini KENYA NA NIGERIA


Vazi la kitamaduni/asili nchi UGANDA

 Vazi la kitamaduni/asili nchini AFRIKA YA KUSINI/KWA ZULU
 Vazi la harusi la kitamaduni/asili Nchini IVORY COAST
 Vazi la kitamaduni/asili Nchini GHANA

Vazi la harusi la kitamaduni/asili Na hapa ni nchini CONGO
SWALI:- Je? TANZANIA KAMA NCHI HATUNA VAZI LA KITAMADUNI KWENYE HARUSI?

Saturday, April 7, 2018

KUMBUKUMBU...VIAZI VITAMU

Leo  katika kytafuta mahitaji nimekutana na viazi vitamu/mbatata nimenunua viwili, mihogo  2 na ndizi mbanga/mzuzu mbili. Kwa hiyo huu utakuwa mlo wa leo ikiwa kachumbali pembeni. ...mmmhhh utamu.

Thursday, April 5, 2018

WAREMBO WA WIKI...TUIGE MFANO WA NDUGU ZETU WAMASAI KWA JINSI WANAVYOTHAMINI MILA NA TAMADUNI

Inapendeza sana kuona bado kuna makabila/kabila wanadumisha/heshimu utamaduni wao. Nawatakieni kila la kheri kwa yote. PAMOJA DAIMA!

Tuesday, April 3, 2018

PICHA YA WIKI...KULA PAMOJA....UJAMAA KATIKA JAMII

Nimependa  hii picha nakumbuka jinsi nilivyokuwa nakula na ndugu zangu....

Sunday, April 1, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI PASAKA NJEMA NA YENYE AMANI NA BARAKA TELE...BWANA AMEFUFUKA !

TUMSIFU YESU KRISTU !

LEO NI SIKU KUBWA SANA KWETU WAKRISTO NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA KWANI BWANA WETU YESU KRISTO AMEFUFUKA KWELI KWELI AMESHINDA MAUTI YA MSALABA ALELUYAAAAA!!!

BASI SOTE TUIMARIKE KATIKA IMANI KWA KUFUFUKA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO KWANI AMESHINDA MAUTI YA MSALABA, TUJIKUMBUSHE KWA PICHA NZURI NA ZENYE UJUMBE SAFI KWAKO,JIRANI  NA RAFIKI YAKO.

http://jumuiyabmm.blogspot.com/2014/04/bwana-amefufuka.html
KABURI AMBALO BWANA YESU ALIZIKWA LI WAZI KWELI MKOMBOZI AMEFUFUKA ALELUYA.

http://jumuiyabmm.blogspot.com/2014/04/bwana-amefufuka.html
BWANA YESU ANATOKA KABURINI NI USHINDIMKUBWA SANA KWETU. AMINI KWAMBA YESU KRISTO AMESHINDA MAUTI NAWE
UTAKUWA HURU MOYONI MWAKO

http://jumuiyabmm.blogspot.com/2014/04/bwana-amefufuka.html
BWANA YESU MFUFUKA AJIZIHIRISHA KWA WANAFUNZI WAKE, AMINI KWAMBA YESU KRISTO YU HAI NAWE UTAPATA UHAI MOYONI MWAKO.

http://jumuiyabmm.blogspot.com/2014/04/bwana-amefufuka.html
EE! BWANA YESU KWA UFUFUKO WAKO NIFANYE NIWE CHACHU YA MABADILIKO KATIKA JAMII YANGU NA KATIKA FAMILIA YANGU. AMINA
http://jumuiyabmm.blogspot.com/2014/04/bwana-amefufuka.html
EE!BWANA YESU KRISTO WEWE NDIO ALFA NA OMEGA, NAOMBA BWANA UNIKUMBUKE KATIKA UFALME WAKO ILI NIWEZE SIKU MOJA
KUJUMUIKA NA WATATIFU NA MALAIKA MBIGUNI. AMINA