Saturday, August 20, 2022
TUMAZE WIKI NA UJUMBE HUU!
NIMETUMIWA HUU UJUMBE NIMEONA NISIWE MCHOYO WA ELIMU:-
Nyoka uliyembeba kwenye mzigo wa kuni kutoka shambani anaweza kukuumia nyumbani wakati unatua mzigo. Siyo kila unayemsaidia lazima akusaidie, wengine inabidi wakuumize ili ujifunze. Kuna watu wanajifunza vizuri baada ya kuumizwa. Kwa hiyo katika maisha tunahitaji watu wote; wazuri na wabaya. Wazuri watakupa furaha, wabaya watakupa uzoefu ndiyo maana imeandikwa mpende adui yako, ila angalia asikuue, maana ukifa hutojifunza kitu!
Imeandikwa na Mwl. Denis Mpagaze.
Subscribe to:
Posts (Atom)