Sunday, June 28, 2015

Friday, June 26, 2015

MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA

Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)

Thursday, June 25, 2015

NGOJA LEO TUANGALIE MAENDELEO YA BUSTANI YETU

 HAPA NI FIGIRI
NA HAPA NI MCHICHA.
Mwaka huu bustani yetu maendeleo yanaenda polepole sana kutokana na hali ya hewa si nzuri sana ila waswahili husema polepole ndio mwendo, na haraka haraka haina baraka.

Monday, June 22, 2015

HAYA JAMANI NI WIKI NA JUMATATU NYINGINE....TUTEMBELEE SONGEA KWETU ....

Ndo kwanza kunakucha .....na Jua hilo lachomoza...Basi niwatakieni wote jumatatu njema najua wengi mko mzigoni...Binafsi nitapotea kidogokidogo kuwa na famalia.Ila nipo:-)

Thursday, June 18, 2015

Wednesday, June 17, 2015

LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO

Kwa upendo jaribu kumpa taarifa ya ua hili  jirani, rafiki na ndugu zako ili wawe makini kwa ua hili. Basi ngoja mimi Kapulya niwatakieni siku njema  na tutaonana tena panapo majaliwa. Jumatano njema!!

Monday, June 15, 2015

TUANZE JUMATATU NA VAZI HILI ...MWENZENU NIMETOKEO KULIPENDA MNO:-) SARESARE MAUA ASIYEJUA KUCHAGU KABILA YAKE NZEGU-------

 Hapa ni dada edna 
Na hapa ni dada Nuru ....halafu usisahau kuandalia hizo ndala  yaani nimelipenda sana hili vazi .
JUMATATU NJEMA

Saturday, June 13, 2015

TUANZE JUMAMOSI HII KWA KIFUNGUA KINYWA HIKI HAPA CHAI KWA MIHOGO...KARIBUNI!!

 Mihogo ya kuchemsha  na hii chai hapa chini basi siku itakuwa njemaaaa. Karibuni tujumuike
Kwa wale waliozaliwa miaka ya uhuru watakubaliana na mimi kuwa vyombo hivi vilikuwa vya heshima sebuleni, kwenye kabati, halafu unakunywa chai kwa adabu maana yake kikombe cha moto, chai ya moto basi hapo chai inatelemka polepole...

Tuesday, June 9, 2015

NDUGU ZETU WANGONI HAPO KALE

 Familia ya kingoni ilikuwa ikionekana hivi hapo kale
Amejiandaa tayari kwa kujikinga kwa vita, Ngao  na mkiku 
Wavulana wa kingoni katika kucheza ngoma
Kwangu ni kumbukumbu nzuri sana  katika picha hizi Tusisahau ya kale ndugu zangu.

 

Monday, June 8, 2015

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI:- SINENE NI KITOWEO HASA MAARUFU SANA HUKO BUKOBA.....

Nimekuwa najiuliza utamu wa senene ni kama kumbikumbi au? Kama ni hivyo basi sina budi kusema ni watamu.....Pia nimesikia hapa baadaye vyakula kama hivyo vitakuwa vya thamani sana duniani kwoote.JUMATATU IWE NJEMA SANA KWAWOTE!!

Saturday, June 6, 2015

UJUMBE WA LEO KUTOKA KWA KAPULYA WENU!!

Usiumizwe na mtu ambaye haumizwi kwa ajili yako. Tambua maisha ni mafupi kama umeme. Kuwa na furaha na acha kuwa mnyonge.
JUMAMOSI NJEMA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!!

Wednesday, June 3, 2015

TUTOKE MANISPAA YA SONGEA NA TUTEMBELEE JIJI LA ROCK CITY (MWANZA)

Leo nimeona tutembelee jiji la Rock City Mwanza....inawezekana baadhi ya nyumba babu yangu marehemu alijenga maa alikuwa akiishi hapa na alikuwa muhunzi/mjengaji mzuri sana......Kapulya

Tuesday, June 2, 2015

MAISHA YA NDOA!!

Sijui nahitaji miwani au? maana naona hawa walitakiwa kuwa shule..Duh kuanza maisha ya ndo mapema hivi....

Monday, June 1, 2015

TUANZE MWEZI HUU WA SITA NA KUTEMBELEA MJI WA SONGEA-----

 
SOKONI SONGEA
 

 Songea yetu hapa
Napenda kuwasalimu wote mtakaopita hapa na pia kuwakaribisha nyumbani Songea/Manispaa ya Songea. Karibu sana.....NAWATAKIENI MWANZA MWEMA WA MWEZI HUU WA SITA....PANAPO MAJALIWA TUTAONANA SASA NAENDA BUSTANINI:-) Kapulya wenu