Friday, May 31, 2013

NIMEONA TUMALIZE MWEZI KWA VITENDAWILI VIFUATAVYO:- KITENDAWILIIIIII.....

1.Kuku wangu kataga mibani.....
2. Nina watoto wangu ambao daima wanafukuzana lakini hawakamatani.
3. Ninapompiga mwanangu watu hucheza
4. Mwenye kuitwa amefika lakini mjumbe bado hajarudi.
5. Bibi mweupe ametupwa mibani.
HAYA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA !!!!!

Thursday, May 30, 2013

UKIFIKA MKOA WA RUVUMA USIKOSE KUTEMBELEA ZIWA NYASA....USISAHAU ULIKOZALIWA!!!!

 Hapa ni ziwa NYASA ebu angalia linavyomeremeta ....karibuni sana
Pia hutaindoka bila kula kama vile picha hii inavyotuonyesha ni DAGAA ambao huwezi kuwapata sehemu nyingine  na ndio maana wanaitwa DAGAA NYASA.......
Na samaki pia utapata ...Nakumbuka jina lake ni "MAGEGE"  kwa ugali wa muhogo weweeeee!!. TUONANE TENA WAKATI MWINGINE.Kapulya

Wednesday, May 29, 2013

WATU 8 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 11 MAJERUHI AJALI YA GARI - NAMTUMBO !!!!

 

Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga

Watu nane wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiriaKwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma DeusdeditNsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe 26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku katika kijiji cha Hanga eneo la bombambili mkoa wa Ruvuma,chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa.Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA,Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.Kamanda wa Polisi amesema gari hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8) na majeruhi kumi na moja (11) ambaowote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Kutokana na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria. Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja ambapo. CHANZO:- DEMASHO

Tuesday, May 28, 2013

TUSISAHAU HADITHI ZETU:- HARUSI YA MASHAKA!!!

Hii ni hadithi ya wanaume wawili. Kazi yao kubwa ilikuwa kulima, pia walikuwa wawindaji wazuri mno.  Wote wawili walikuwa wameoa, na wote walikuwa wambeya. Walikuwa hutaka kujua kila wanachofanya wake zao. Wote walitambua maneno ya zamani: "WANAWAKE SI WATU KAMILI"
Siku moja hawa wanaume walipokwenda kuwinda pamoja, walianza kuizungumza ile methali. Hapo hapa mmoja kati yao alimuambia rafiki yake kuwa yeye angependa kumjaribu mkewe.
Alimuua njiwa na kumkata vipande. Baadaye akaweka vile vipande vya nyama ya huyo njiwa, vilokuwa vikitoka damu, mguuni kwake, na akachukua kitambaa na kuufunga mguu wake, hapo ilionesha kama kaumia mguu, hasa ilivyokuwa damu ikitokeza kwenye hicho kitambaa mguuni kwake.
Walipokaribia nyumbani, alimuomba rafiki yake ambebe mgongoni. Hapo ilioonyesha kama mtu aliyeumia sana.
Baada ya wiki moja hivi, kidonda chake kilikuwa bado kikitisha , na kilikuwa kikinuka kupita kiasi. Huyu bwana alijifanya kuwa hawezi kusimama kabisa. Mkewe alipata kazi zaidi kutokana  na hali ya mumewe. Hili lilikuwa tatizo kubwa kwa mkewe, na aliamua kumkimbia mumewe na kurejea kwa wazee wake. Kabla ya kuondoka alimuomba rafiki yake mumewe amuangalie mumewe. Alipoondoka tu marafiki walikwenda kwenye mto. Hapo mgonjwa akaoga na kuosha nguo zake zilizokuwa chafu.
Mkewe aliondoka siku nyingi. Baada ya muda alisikia kuwa mumewe kapona tena. Hapo alirejea haraka kwa mumewe.
Baada ya mikasa hii yule rafiki mtu naye akataka kujua vipi tabia ya mkewe. Siku moja alijifanya mgonjwa sana, na siku nyingi zilizofuata alikataa kula. Siku moja alimuomba mkewe amtengenezee chakula kizuri, halafu akamwambia ampatie asali kidogo.
Mkewe alifanya kama alivyoomrishwa. Chakula kilipokwisha tu huyu bwana alijifanya kuwa kazimia. Baadaye alijifanya kuwa kufa.. Wakati mkewe akishughulika kujua lililotokea, aliwaza nini la kufanya. "Sijui niite msaada, au sijui nile kwanza?" aliamua kula kwanza.
Wakati alipokuwa akila alikumbuka asali ambayo alisahau kumpa mumewe. Asali ilikuwa kwenye chupa iliyokuwa juu ya kitanda. Alijaribu kuiteremsha  chupa, lakini hakuweza kuifikia.
Hapo ilimbidi amkanyage mumewe mgongoni ili kuifikia hiyo chupa. Alipomaliza tu kula alitumia njia hiyo hiyo kuirejesha hiyo chupa. Baadaye kidogo aliosha sahani na hapo ndio akaanza kulia na kuwaita watu. Watu kijijini walikuja, na kati ya hao alikuwa rafiki yake mpenzi. Rafiki yake alianza hapo hapo matayarisho ya maziko. Ghafla maiti ikapiga chafya: "Aaccha!!" Watu walimkimbilia maiti na kumsaidia. Baadaye watu wote waliondoka wakiwa na furaha.

Hadithi  hii inatufundisha kuwa ikiwa mtu anataka kujua kila kitu cha mwenzako, utavunjika moyo bure....Je? wewe umejifunza kitu hapa? Ni hadithi kutoka kitabu kiitwacho HADITHI NA VISA KUTOKA TANZANIA..TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA!!!!

Sunday, May 26, 2013

NA HAPA NI BAADHI YA ZAWADI NILIPONGEZWA KWA SIKU HII YA AKINA MAMA/MORS DAG!!

 Kutoka kushoto ni kikombo cha chai ambacho kina chunjio na mfuniko wake si mnajua nilivyo mpenzi wa chai, hicho cha maji ya bahari ni flip cover kwa ajili ya simu yangu, ya tatu ni sceen protertor, nilipata na bahati nasibu /TRISS, ila bahati mbaya sijapata bahati nasibu.. NA MWISHO hicho mkionacho cha bluu ni kwa ajili ya kuhifadhi simu yangu nikimbiapo maana huwa napenda kusikiliza miziki......haikuishia hapo nikaandalia...
....keki na ni dada Camilla ndiyo aliyetengeneza keki hii maalumu kwa ajili ya mama---inaitwa rabarberkaka/keki ya rhubarb...karibuni bado ipo......

LEO NI SIKU YA AKIMNA MAMA (MORS DAG)


Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mama yetu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mama yetu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka/omba.( kwa niaba ya mama)
Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mama yangu. NAWAPENDA AKINA MAMA WOTE DUNIANI.NA TUTAFIKA TU.

Saturday, May 25, 2013

TUSISAHAU NGOMA ZETU ZA ASILI ..NGOMA YA MGANDA HAPA KARIBUNI


 
Hay moja pili tatu uhuuuuuuuu, uhhhhh sikiliza hizo ngoma wangoni hao aaaaah eeeh yaani hapa nipo hoi kabisa...JUMAMOSI NJEMA JAMANI....

Friday, May 24, 2013

MHASHAMU ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA SONGEA DKT NORBERT WENDELIN MTEGA ASEMA AHSANTE JIMBO KUU LA SONGEA

Na, Stephano Mango, Songea
JUMATANO Mei 15, mwaka 2013 ni siku ya historia kubwa na ilioyo dhahiri kwa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea na kwa Waamini wote wa Yesu Kristo na wote wenye mapenzi mema
Ni siku pekee ambayo haikutarajiwa na Wateule, Watakatifu na Wanakanisa pale Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Dkt Norbert Wendelin Mtega alipoamua kuwatangazia Taifa la Mungu kustaafu ( Kujiudhuru) nafasi yake hiyo
Aliamua kuwatangazia uamuzi wake huo Viongozi mbalimbali wa Kanisa Majira ya saa saba Mchana Hanga Monasteri iliyopo Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma nje kidogo ya Wilaya ya Songea, siku ya Jumatano Mei 15, 2013
“…kwa kuzingatia hali yangu ya afya , kwa kuzingatia jinsi nilivyoonja utendaji wangu unavyoonyesha dalili za kuchoka na pengine kuzorota nikiwa katika mwaka wangu wa 28 wa Uaskofu kwa hiari yangu kabisa niliamua kumuandikia barua Baba Mtakatifu ili aniruhusu kustaafu kabla ya kufikia umri wa sheria na kanuni za kustaafu rasmi” alisema Mtega
Alisema kuwa nafurahi kwa kuwa Baba Mtakatifu leo amenijibu na kunikubalia ombi langu na dakika hii mbele yenu natua jukumu lote la Uongozi juu ya Jimbo Kuu la Songea
Kwa hiari yangu na kwa kuashiriwa na hali ya afya yangu na jinsi kazi inavyonielemea kupita uwezo wangu wa awali, nafanya hivyo kwa ajili ya ustawi wa Taifa la Mungu, na hasa Kanisa lililoko Songea kwa hiyo mimi staki niwe kikwazo na hoja ya Jimbo kuzorota katika siku za mbele
Alisema kuwa kuanzia sasa Msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Songea katika kipindi ambacho ambaye ameteuliwa na Baba Mtakatifu ni Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
Ni msimamizi kwa kuwa ataliongoza Jimbo kuu la Songea katika kipindi ambacho Baba Mtakatifu anapitia mchakato wake wa kumteua na kumtuma rasmi Askofu Mkuu mwingine wa Songea. Endelea kusoma zaidi hapa

MAISHA YA NDOA:- MKE NA MUME!!

Nipo kazini mara nasikia simu yangu ya mkononi ujumbe ukiingia, nachukua kuangalia ni nani na nini..nakutana na ujumbe huu na maagizo :- Kuwa  "wape wanandoa wote unaowafahamu ujumbe huu. Mungu na  awatie nguvu!! Ameeeen....!!" Na kwa vile najua wengi ninaowafahamu wanapita hapa nikaona itakuwa njia nzuri kuweka hapa...na ujumbe wenyewe ni kama ifutavyo:-
"Ukiona mko vizuri kwenye ndoa, Usimsifu mumeo/mkeo, Endelea kumtukuza Mungu na kuweka maombi ya akiba. Usitoke bila KUMWOMBEA mkeo/mumeo.
Jifunze pia kumwelewa mwenzako na kutokuuona udhaifu wake kama sababu ya wewe kumfanyia mabaya. Zungumza naye, mtie moyo, mshauri katika usiyoyapenda, mweleze uliyonayo.
Ondoa maswali nafsini mwako. Pata majibu sahihi kutoka kwake. KUMBUKA NI NYAKATI ZA MWISHO. Taasisi ya shetani isiyotaka ichanue ni NDOA. Ikiharibika familia nayo inaharibika. TAFAKARI"....IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMWA WA MWISHO WA JUMA!!!

Thursday, May 23, 2013

UJUMBE/FIKRA WA/ZA LEO!!!

Katika dunia huwezi kuishi maisha bora kama una akili/mawazo hasi/finyu.
NAWATAKIENI WOTE SIKU NA KAZI NJEMA!!!

Tuesday, May 21, 2013

Wanafunzi waliokatishwa masomo kwa mimba wafunguka



Mmoja wa wanafunzi alyepata mimba akiwa kidato cha tatu

Mada hii imenigusa sana,,,,nimekuwa muda mrefu nikulalamika sana kuhusu hili yaaani kwanini wasichana waachishwe shule na sio wavukana pia. na kwanini wasichana wasipate muda wa kusoma baaada ya kupata watoto. ..soma hapa  china...mada hii nimeiipata http://maendeleonivita.blogspot.se/ soma mwenyewe!!!!
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WANAFUNZI wengi wanaosoma katika shule za sekondari wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanakatishwa masomo yao wanapofikia kidato cha pili na cha tatu baada ya kupata mimba na kuolewa wakiwa shuleni.
Hali hiyo inatokana na historia ya wakazi wa wilaya hiyo ambao ni kabila la wayao kutokuwa na mwamko katika elimu hasa kutokana na kutoa kipaumbele kwa desturi na mila za kabila hilo ambazo zinatoa fursa zaidi katika mila potofu za unyago,msondo na jando kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hali ambayo inaathiri suala zima la elimu.
Takwimu ambazo zimetolewa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho zinaonyesha kuwa mwaka 2012 wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari mwaka huu walikuwa ni 2788 hata hivyo hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu ni wanafunzi 1710 tu ndiyo walioripoti hali ambayo inakwamisha maendeleo ya elimu.
Flavian Nchimbi kaimu afisa elimu msingi wilaya ya Tunduru anasema tatizo la mimba katika shule za msingi zimepungua ukilinganisha na miaka mitatu nyuma kulikuwa na mimba karibu 250 ambapo takwimu za mwaka jana zinaonyesha kuwa katika shule za msingi zililipotiwa mimba 16 na kwamba kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu imeripotiwa mimba moja tu.
Hata hivyo afisa elimu sekondari wilaya ya Tunduru Ally Mtamila amekiri tatizo la mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuwa ni kubwa ambapo wanafunzi wa kike wanakatishwa masomo kwa mimba au kuolewa.
Sarah Michael(15) mkazi wa Tunduru alikuwa anasoma katika shule ya sekondari Makita ambapo alipewa ujauzito akiwa kidato cha tatu na mwanaume ambaye alitoroka mara baada ya tukio hilo hali ambayo ilimfanya aishi kwa shida hadi alipojifungua salama mtoto wake wa kiume.
“Baada ya kupata ujauzito niliacha masomo wazazi walinipokea licha ya kupata misukosuko mingi hasa kutoka kwa baba yangu mzazi,nimejifungua naendelea kumlea mwanangu katika mazingira magumu sana kwa kweli nakumbuka shule mwaka huu ningekuwa namaliza kidato cha nne’’,alisema.
Sarah alisema anapenda sana kusoma lakini wazazi wake hawana uwezo wa kumsomesha hivi sasa hivyo endapo atampata mtu wa kumsomesha anaweza kuendelea na masomo ya sekondari na kwamba kitendo cha kupata mimba na kukatisha masomo yake kimetoa fundisho kubwa kwake hivyo hawezi kurudia makosa ambayo yameharibu ndoto za maisha yake.
Hata hivyo anasema baba yake ni mwajiriwa wa serikali anafanya kazi ya uaskari magereza wilayani Mbinga ambaye kitendo cha yeye kukatishwa masomo kilimchukiza na alitaka mtuhumiwa kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,hata hivyo wazazi wa pande zote mbili waliyamaliza na kufuta kesi.
“Hivi sasa baada ya mwanangu kukua nimemwomba baba anisomesha ili niweze kuendelea na masomo,lakini baba bado ana hasira amekataa na kusema ningoje kwanza nijifunze maisha kwa kuwa mimi niliacha shule na kukimbilia mambo yaliosababisha kupata mimba naendelea kumuomba radhi baba kwamba sitarudia tena nikipata nafasi ya kusoma’’,alisema kwa huruma.
Salima Hamad(15) mkazi wa Tunduru anasema alikatishwa masomo yake baada ya kupata mimba akiwa kidato cha tatu mwaka 2012 na kwamba wazazi wake walichukizwa na kitendo hicho ,walifungua kesi ya mwanaume aliyempa mimba,alikamatwa na kutiwa ndani hata hivyo mwanaume huyo ametorokea nchini Msumbuji hadi leo.
“Wazazi walinisakama pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji,nilitamani kutoa mimba lakini nilipiga moyo konde,nilivumilia kulea mimba katika mazingira magumu kwa kuwa wazazi wangu ni masikini hadi nikajifungua salama kwa kufanyiwa upasuaji mtoto wa kike,natamani kusoma lakini sina uwezo’’,alisisitiza.
Salima anasema wazazi wake wamekataa kumsomesha na kudai kuwa hawana uwezo wa kumpeleka tena shule na hivi sasa anaishi kwa kujitazamia na kuuguza kidonda ambacho kimetokana na kujifungua kwa upasuaji.
Hemed Ally mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya msingi Frank Weston wilayani Tunduru anasema katika mafunzo ya msondo na unyago wanafunzi wa kike wanaelezwa faida za kuishi na mume lakini hawafundishwi madhara ambayo wanaweza kupata kwa kushiriki katika ndoa wakiwa wadogo hali hiyo ndiyo inawahamasisha wanafunzi kujiingiza kwenye ngono na kushawishika kuolewa na kupata mimba wakiwa wanafunzi.
Rehema Sara mwanafunzi wa kidato cha nne sekondari ya Mgomba anasema mila za unyago na msondo zimesababisha wanafunzi wengi wa kike katika shule hiyo kuacha masomo kwa kupata mimba au kuolewa ambapo hivi sasa katika darasa lao waliofanikiwa kufika kidato cha nne ni wanafunzi 106 tu kati ya wanafunzi zaidi ya 230 walioanza nao kidato cha kwanza mwaka 2010.
Sarah mkombozi wa kidato cha nne sekondari ya Mgomba ambaye alifanyiwa ngoma ya unyago na msondo akiwa darasa la tatu amekiri moja ya mambo ambayo wanafundishwa katika msondo na unyago ni kufanya mapenzi na watu wazima na kwamba kukataa kufanya hivyo ni kuvunja mila na desturi za wayao’’,alidai mwanafunzi huyo.
“wenzangu wengi ambao nilikuwa nao shule ya msingi na wengine ilitakiwa niwe nao sekondari wameacha masomo kwa kuwa wana watoto baada ya kupata mimba na wengine wameolewa na kuachika hivyo wanaangaika na maisha’’,alisisitiza.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho amekiri mila na desturi za kabila la wayao zinachangia wilaya hiyo kuwa duni kielimu hata hivyo amesema tayari serikali imeunda kikosi kazi cha kuonana na viongozi wa mila, makungwi na manyakanga kuwaelimisha juu ya utoaji wa elimu kwa watoto wa kike kupenda masomo tofauti na sasa ambapo kundi hilo limekuwa likifundishwa kukabiliana na maisha ya ndoa hali iliyosababisha kuwepo kwa matukio mengi ya ndoa za utotoni wakiwa shuleni.
“Mila na desturi za kabila la wayao kuwafanyia unyago wanafunzi ndiyo chanzo kikuu cha tatizo hili,sisi kama serikali ili kukabiliana na tatizo hili tumefanya vikao na viongozi wasiokuwa rasmi lakini wanakubalika katika jamii wakiwemo makungwi, mangariba, masultani,mamwenye,mashehe na maimamu kwa kuzingatia tumejadili kwa pamoja tatizo hili”,anasisitiza.
Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wasichana 8000 kila mwaka huacha shule kutokana na ujauzito. Kati yao 3,000 ni wanafunzi wa shule za msingi.
Kila siku, wanawake 24 hufariki dunia kutokana na mimba au wakati wa kujifungua. Wanawake watano mpaka sita wanaofariki kati ya hao ni watoto wadogo, watoto hao hufariki dunia kwa kuwa miili yao haijakomaa vya kutosha kwa ajili ya kujifungua.
Naibu mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Mohamed Safieldin anasema mbali na athari hizo, pia virusi vya ukimwi (VVU), vinavyosambaa kwa kasi kwa wasichana hao. Tanzania kuna watoto yatima milioni 1.3 walioathirika kwa ukimwi.

Monday, May 20, 2013

PALE INAPOKUWA EMBE MOJA KUGAWANA WATU WANNE....

 Leo tumetamani kweli EMBE ..lakini bei yake mmmh, embe moja shilingi 2300.. Basi tukaishia kununua moja ili angalao kupunguza hamu ya embe....
...na mwisho wake vikatokea vipande vinne..kila mtu akapunguza hamu ...iliishia kwenye ulimi tu hata shingoni haikufika..mweeeeeh maisha haya kaaaaziii kwelikweli..Nakumbuka januari nilikula embe mpaka kuziacha na pia kutupa sasa....mmmmhhh.

TUANZE JUMATATU HII KWA KUTEMBEEA MAENEO YA SOKO KUU LA SONGEA,,,HAPA ILIKUWA MWEZI WA KWANZA 2013....KARIBU!!!

 Hapa ni baadhi ya duka maalumu kwa kanga tu..tukiwa katika msako wa kununua kanga..si umeona zilivyo nyingi. Tulipata shida sana kuchagua. Hili ni baadhi ya kitu dhaifu kwangu..kuchagua.....
 Ndani ya soko kuu ...hapa ni sehemu ya kupata mchele
Huwezi kununua mchele tu Nyanya, Vitunguu na mapochopocho mengine ni lazima pia..

Sunday, May 19, 2013

JUMAPILI NJEMA ..UKIPATA MUDA BASI NAKUOMBA SIKILIZA WIMBO HUU MAANA NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA LEO...!!!


JUMAPILI NJEMA SANA KWA YEYOTE ATAYEPIATA HAPA UPENDO NA AMANI ITAWALE KWENU..MNAPENDWA WOTE AMINAAA...!!

Friday, May 17, 2013

TUSISAHAU USEMI/SEMI WETU/ZETU..LEO TUANGALIA HUU UFUATAO......!!!

Dunia/Ulimwengu ni kama kitabu, na wao waisosafiri, wanasoma ukuraza mmoja tu.
NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA.TUKUMBUKANE:-)

Thursday, May 16, 2013

MAANDALIZI YA BUSTANI ZA MBOGA NA MAUA YAMEANZA...ANGALIEANI WENYEWE...KARIBUNI TUJUMUIKE!!!!

 Hapa ni baadhi ya matu ya bustani yangu ...maandalizi yameanza..leo mnaona udongo tu hapa baada ya wiki mtaona mimea....
 Katika maisha inabidi uwe mtundu hapa nilikwisha andaa baadhi ya miche kama vile NYANYA na Miche ya mboga ZA MABOGA,,ujanja eeeehhh
Mdada/kapulya hapendi shughuli za bustani za mboga tu ni mpenzi sana wa bustani sana wa bustani za maua kama mnavyoona hapa na mawe pia....kwa hiyo msione nipo kimya nipo ...daima pamoja...anayejisikia kuja kusaidia anakaribishwa..majembe yapo mengi tu:-)

Tuesday, May 14, 2013

WANANDOA NA KAULI HIZI: HATA VIKOMBE KABATINI HUGONGANA, ITAKUWA SIE?

Je unadhani au kuamini kwamba kuna ndoa ambazo wanandoa wake hawagombani kabisa? Kama unaamini hivyo, basi unajidanganya na labda unaishi katika dunia ya peke yako.
Ni jambo lenye ukweli wa kutosha kabisa kwamba wanandoa wote duniani hutokea kugombana, lakini kugombana huko hutokana na migongano au mizozo ya muda tu ambayo huweza kutatuliwa na pande mbili kama wakiamua kufanya hivyo.
Wewe unayesoma hapa, napenda kukuambia ukweli kwamba usiogope migogoro ya ndoa, kwani hicho ni kitu ambacho kamwe huwezi kukiepuka. Kuna msemo mmoja unatumika sana huko nyumbani usemao, " hata vikombe kabatini hugongana itakuwa wana ndoa?" Hii ina maana gani, ina maana kwamba haiwezekani watu kuishi pamoja halafu msiwe mnatofautiana, na kama ukiona hivyo, jua kwamba hiyo ndoa si salama kwani siku yoyote bomu litapasuka na madhara yake yatakuwa ni makubwa kuliko kawaida.
Kuna watu ambao hata kama wamekosewa na wenzi wao hunyamaza kimya na kumeza hasira zao, wengine huogopa kuwakabili wenzi wao na kuzungumzia jambo linalowakera kwa kuhofia kuonekana kama wana kasoro au ghubu. Jambo hili ni hatari sana.
Kumkabili mwenzi wako na kumwambia hisia zako kama amekukosea au amekwenda kinyume na matarajio yako ni jambao la maana sana katika kudumisha uhusiano. Lakini naomba nitahadharishe kwamba, ni vyema kufanya hivyo bila kumshusha, kubeza au kusimanga kwani hiyo sio dalili nzuri ya upendo.
Inashauriwa kwamba wanandoa au wapenzi wanapokwaruzana inabidi wajadili tofauti zao bila kusigishana, kila mmoja akitaka kuwa mshindi, hiyo haitasaidia kuimarisha ndoa bali itaongeza tatizo. Ni vyema upande unaohusika na tatizo, uwajibike na kuomba radhi kwa ustawi wa ndoa, huo ndio ukomavu.

Kutojadili mgogoro kwa wanandoa na kuupatia ufumbuzi wa tatizo huwafanya wandoa kuwa mbali kihisia, na athari zake ni kuwakuta wanandoa wakiwa wageni wa kila mmoja kwa mwenzake, yaani hakuna mawasiliano, kila mtu na lwake.
Jambo la msingi kwa wanandoa ni kujadili tofauti zao pindi linapojitokeza jambo linalomkera mmoja wa wanandoa, kwani hakuna jambo linaloweza kujitatua lenyewe bila kutatuliwa na wandoa husika. Kuacha jambo lolote bila kulitafutia suluhu ni sawa na kutega bomu, ambapo siku likilipuka madhara yake ni makubwa sana.
Unaweza kukuta mwanandoa anakereka na mambo madogo madogo ya mwenzi wake lakini hasemi, ingawa yanamkera kupita kiasi akitegemea huyo mwenzi wake atajua na kuacha, thubutu…..inapotokea siku yeye amekosa jambo dogo tu na huyo mwenzi wake akamsema, basi atatumia fursa hiyo kuanza kujibu mapigo kwa kueleza yale yanayomkera kutoka kwa mwenzi wake, na hapo itakuwa kila mtu anavutia kwake kama mwamba ngoma………na aamini nawaambia kuwa kamwe hawezi kupatikana mshindi katika jambo hilo, kwani mjadala huo unaweza kutoka nje ya mada kila mmoja akijitahidi kutafuta makosa ya mwenzi wake hata yale yaliyotokea wakati wa uchumba wenu ili mradi vurugu tupu.
Inatakiwa wanandoa wajadili kila jambo linalojitokeza hadi kulipatia suluhu, vinginevyo ni kuichimbia ndoa yenu kaburi la mapema. Wakati mwingine unaweza kukuta mwanamke analalamika juu ya kutoridhishwa kwake na matumizi ya mumewe, na hapo mume naye ataanza kukumbusha juu ya matumizi yasiyo ya lazima yaliyofanywa na mke huko nyuma. Mke naye hataridhika atakumbushia jambo lingine na lingine hadi hata mada iliyokuwa ikijadiliwa inasahaulika.
Jambo lingine ni kujumuisha mambo, matumizi ya maneno kama, mara nyingi, kila wakati au mara kwa mara si mazuri sana. Unaweza kukuta mtu mwenzi wake amekosea jambo halafu mwenzie anamwambia “Kila mara huwa unafanya hivi” au mara nyingi huwa unafanya hivyo…..Hii ni hatari kwa ustawi wa wanandoa, kwani kwa kujumuisha ni sawa na kumwambia mwenzi wako kuwa kila mara yeye ndiye mkosaji.
Kwa haya niliyoyaeleza hapa sina maana kwamba huu ndio muarobaini pekee wa kuimarisha mahusiano kwa wanandoa, bali ni moja ya mambo muhimu kati ya mengi ambayo yakizingatiwa na wanandoa wote basi ndoa yao itakuwa imara Tujadili pamoja………..

Sunday, May 12, 2013

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE ...BARAKA NA UPENDO VITAWALE KATIKA NYUMBA ZENU

Napenda kuwatakia jumapili njema wote mtakaopita hapa maisha na mafanikio ...naomba wote tusali sala hii...
Salamu Maria, umejaa neema.
Bwana yu nawe
umebarikiwa kuliko wanawake wote,
na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.
JUMAPILI NJEMA SANA KWA WOTE....

Saturday, May 11, 2013

PICHA YA WIKI..MAMA NISHUCHE NATAKA KUCHEZA...

Inaonekana mtoto hataki kubebwa au sijui kaona kitu fulani anataka akachukua??? Au wenzangu mwasemaje? ...mmmmhhh nimetamani mchicha na chaina hiyo ngoja nami nianze kulima bustani yangu...JUMAMOSI NJEMA..

Friday, May 10, 2013

UMETOKA MKOA UPI HAPA?

1. Dar es salaam - Utapeli
2. Arusha - Heka heka
3. Mbeya - Matukio
4. Tanga - Majini
5. Dodoma - Ombaomba
6. Mwanza - Fujo
7. Kagera - Misifa
8. Rukwa - Uchawi
9. Kilimanjaro - Ujanja
10. Mara - Ukatili
11. Kigoma - Ubishi
12. mtwara - Umaskini
13. Ruvuma - Ugoni
14. Singida - Upole
15. Tabora – Majungu
16. Shinyanga - Miujiza
17. Morogoro = Starehe

18. Iringa - Ukorofi
19.Zanzibar ???
 20.Pemba ??
NAWATAKIENI MWANZA MWEMA WA MWISHO WA JUMA...

Wednesday, May 8, 2013

UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!

Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hawezi kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu ambaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mno amekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendesha gari lako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni mchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako . Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!! SIKU NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA.

Monday, May 6, 2013

MTU NA MAZINGIRA...LEO NI USAFI WA NJE....

 Leo tulikuwa katika usafi wa nje..Tulikuwa tumekata miti kama unavyoona hilo lundo hilo. Sheria ni kwamba hakuna kuchoma moto ni lazima kutupa sehemu maalumu...kazi inaendelea.....
 Hapa tumejaza mkokoteni mzima na kufunga kamba kabisa kelekea huko tunakotupa taka----
Na hapa ndiyo sehemu maalumu ya kutupa kwenye haya makontena na halafu mashine yanasaga saga....lakini ni matawi matawi tu.....Hivi ndivyo ilivyoanza JUMATATU YANGU...na sasa ngoja nikapalilie na kutoa majani kwenye maua yangu...Muwe na JUMATATU/MWANZO MWEMA WA JUMA.

Sunday, May 5, 2013

JUMAPILI NJEMA KWA UJUMBE HUU....BABA SHIKAMOO!!!


Ni jumapili ya kwanza ya mwezi huu wa tano..baraka, upendo na amani zitawale katika nyumba zenu. TUPO PAMOJA

Saturday, May 4, 2013

AINA ZA UFUJAJI..HII NI MOJA YA AINA YA UFUJAJI,,UFUJAJI WA KIROHO...

Ni pale ambapo mpenzi anatumia dini au imani ya mwenzake kumwendesha. Kuna wakati anabaini kwamba, kwenye imani ya mpenzi wake kuna kipengele anachoweza kukitumia kumkandamiza mwenzake, ambapo hukitumia.
Kwa mfano, kama imani ya mwenzake inasema mwanamke amtii mumewe, kipengele hicho kitapindwepindwa na mpenzi hadi mfujwaji akubali anayotaka mfujaji, kupitia kipengee hicho.
Lakini pia kumzuia mpenzi kuchiriki kwenye ibada au maombi au huduma yoyote ya imani yake. Kuzuia huku kunaweza kuwa ni kwa moja kwa moja au kwa mbinu za kulaghai na kukashfu. Mara nyingi hata hivyo, kashfa, matusi , kebehi na matumizi ya nguvu hutumika katika sula hili.
Kuna wakati watoto hulazimishwa kufuata imani ambayo mzazi mmoja haitaki na ambayo pengine haikuwa imani ya yeyote kati ya wapenzi wawili. Mpenzi mmoja kabadili  dini wakiwa tayari kwenye ndoa, halafu analazimisha watoto kufuata hiyo dini yake mpya, bila makubaliano na mwenzake ambaye yeye hajabadili dini.
Kuna mkazi mmoja wa Magomeni Mwembechai ambaye aliwahi kuja kwangu, akilalamika kuhusu ndoa yake na mumewe. Alisema, mumewe ameingia kwenye imani mpya. Mume huyo hurejea nyumbani usiku saa tano au sita. anapofika hapo nyumbani huanza kuimba kwa kelele akitukuza imani yake na Mungu.
Mume huyo huwaamsha watoto na kuwataka waimbe usiku huo wa saa tano au sita, akimtaka mke wake naye kujiunga nao. Mke yule aliniambia kwamba, anapojaribu kukataa au kuwatetea watoto kwamba, inabidi walale kwaajili ya kuwahi shule kesho yake, mume huyo humtukana kwa kumwita, ibilisi, mpottevu, mtu wa mataifa, mlaanifu mwenye mapepo wachafu wa ujeuri na kashfa za mataifa, mlaanifu mwenye mapepo wachafu wa ujeuri na kashfa za matusi ya nguoni.
Hii ni aina ya udhalilishaji kupitia dini au imani, ambao ni udhalilishaji wa kiroho. Imani inatumika kutoka maumivu kwa mwingine,
INATOKA KATIKA KITABU CHA MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA....

Friday, May 3, 2013

HUU NI MLO WANGU WA JANA JIONI ..KAZI YA MIKONO YANGU!!!

Hapa chakula ndo kinatoka tu kwenye oven...ni lasagne,,nyama ya kusaga, aina ya pasta, chizi na maziwa..dakika 30 kwenye oven.
 
 
Na hapa ni sahani ya Kapulya ..bila kusahau saladi na kinywaji ni maji

Thursday, May 2, 2013

WANAWAKE NA MIGOROLI ..HAWA NI WAMTINDO/WAREMBO WA WIKI HII...JE UNAWAFAHAMU?

Wanawake/wadada hawa wanaonekana kupenda sana kuvaa mgoroli ..umegundua kitu hapa ni kwamba wote wameachia mkono wa upande mmoja..:-)
Halafu unajua kitu kingine huyo wa juu katabasamu lakini huyu wa chini au mwenye kijani anaonekana yupo mbali kweli kifkra...Unajua ni kitu gani kingine wadada/wanawake hawa wanapenda kufanya?...Karibuni ....

Wednesday, May 1, 2013

SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ..MEI MOSI!!!

Mwenzenu nina swali hapa:- Hivi Wafanyakazi ni akina nani? Wakulima akina nani?...Na wafanyabiashara ni nani?.Maana katika akili yangu naona kila kitu ufanyacho na kutoka jasho ni kazi. Naomba tujadili kwa pamoja hapa...JUMATANO YA MEI MOSI IWE NJEMA.....KAPULYA