Thursday, November 30, 2017
TUUMALIZE MWEZI HUU NA KIPANDE HIKI CHA URAFIKI MWISHO WA MWEZI...
NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA MWEZI NA AFYA NJEMA KUUPOKEA MWEZI MPYA...
Tuesday, November 28, 2017
Monday, November 27, 2017
TUMALIZE JUMATATU YA MWEZI HUU WA KUMI NA MOJA KWA MTINDO HUU....UREMBO WA ASILI
Heleni ....ambazo ni kazi za mikono ya watu kwa ubunifu safi kabisa
Na hapa ni pia ubunifu mzuri kabisa wa viatu/sandosi.
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII NA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMATATU NJEMA SANA NA OMBI LANGU NI KWAMBA TUDUMISHE UTAMADNI WETU....Kapulya wenu...!
Thursday, November 23, 2017
NDUGU ZANGU:- TUTAFARI KWA PAMOJA MALEZI YA WATOTO WETU
Ukimkosoa sana mtoto na kumkaripia mara nyingi unampunguzia ujasiri na uwezo wa kujitegemea awapo mtu mzima.
Msaidie kwa upole, muelekeze, mtie moyo, akikosea mweleze jinsi Mungu anavyoumia kwa kosa alilolitenda.
Usimwambie kuwa hana jema hata moja hasa akiwa binti, maana siku moja kuna vijana wataona jema lake na watamwambia kisha ataweka USIKIVU Wake kwao.
Muombee mwanao/wanao, Mfundishe/wafundishe kuomba mwenyewe/wenyewe Bwana atamsaidia/wasaidia.
Hii ni pamoja kumchapa mtoto viboko, ni kumwongezea usugu tu
Wednesday, November 22, 2017
MSIMU WA BARIDI ....THERUJI YA KWANZA KUANGUKA KUONA NYASI TENA MPAKA MWEZI WA NNE:-(
Leo huku nje ni kimbembe thuriji imeanza kuanguka juzi, lakini leo ndo kwanza inazidi na upepo juu....Ni taarifa tu kwa ufupi. Nawatakieni siku njema.
Monday, November 20, 2017
NI WIKI NYINGINE NA JUMATATU NYINGINE...TUANZE WIKI NA PICHA HII YA KITAMADUNI KABISA
Wanawake wakitwanga nimekumbuka mbali sana nilikuwa nikipata shida sana kutwanga watatu au wanne....:-)
Sunday, November 19, 2017
Wednesday, November 15, 2017
Tuesday, November 14, 2017
NIMEKUMBUKA MKAO HUU NA PIA KUJUMUIKA NA KULA KWA PAMOJA
Nimekumbuka miaka hile ya mwaka -47 wakati watu tulikuwa tunakaa kwa pamoja na kula tena sahani moja. Siku hizi ni marachache sana kuona hii. Kwa kweli inanisikitisha
Friday, November 10, 2017
NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA
Binafsi nafurahia taswira hii ya Moshi...ebu angalia Mlima wetu Kilimanjaro unavyoonekana....MWISHO MWEMA WA WIKI.
Wednesday, November 8, 2017
Tuesday, November 7, 2017
LEO NIMEKUMBUKA ZILIPENDWA
Hakika nisikilizipo miziki aina hii nakuwa na furaha ya pekee maana mtu waweza kusikiliza na kujifunza kitu ...JUMANNE NJEMA WAPENDWA WA ZILIPENDWA.
Monday, November 6, 2017
JUMATATU HII YA KWANZA YA MWEZI HUU TUANZE NA UASILI...MAVAZI YA ASILI
Tubadilike sasa, tuthamini utamaduni wetu, tuachane na hisia za kimwili, turudi katika utamaduni wetu wa asili ya mwafrika, tukumbuke mavazi yetu ya asili kama ilivyo pichani ili tudumishe mila na desturi zetu
Wednesday, November 1, 2017
NASHANGAA MARA HII TUNAANZE MWEZI MPYA NAMI NIMEONA TUANZE MWEZI HUU KIHIVI...
Mdada anashanga utadhani anatoka usingizini ...lakini hapo ni kwamba anashanga kumbe leo ni mwezi mpya....natumaini wenzangu hajashangaa kama mimi Kapulya....
PANAPO MAJALIWA...
Subscribe to:
Posts (Atom)