Wednesday, September 30, 2009

HÖST/AUTUMN = MAJIRA YA BARIDI YA KUPUKUTIKA MAJANI BRRRRRRR!!!!

Hapa ni leo mchana kama saa nane hivi

Nadhani mnaona vazi la leo ni tafaouti na picha nyingine kwani sasa baridi imeanza leo asubuhi iliwa -0.4C. Waliofika Njombe, Iringa Makambako na pia Mbeya wanajua. Mmmmh kazi inaanza sasa kaziiiii kwelikweli, maana mtu unavaa nguo na mwisho unaonekana kama una kilo elfu kumi. Haya ngoja niache.

Tuesday, September 29, 2009

KWA NINI KWENYE KUFUMANIA, MWANAMKE HUBEBA LAWAMA NYINGI UKILINGANISHA NA MWANAUME.?

Hivi karibuni niliweka habari ya diwani mmoja huko mkoani Songea kufuamaniwa akifanya mapenzi na mke wa Shekhe, habari ambayo niliidesa katika mtandao wa Jamii Forum.

Sio dhamira yangu kulizungumzia tukio hili kwa undani zaidi, lakini kinachonifanya nilizungumzia tukio hilo ni kutokana na jinsi jamii inavyolitazama swala zima la fumanizi.

Je ni haki kweli mume kulipwa fidia pale anapomfunia mkewe? Hilo ndio swali ambalo nimejiuliza mara baada ya kusoma ile habari, na baada ya kulipwa ile faini, ni nini kitaendelea? Je mwanamke yule ataendelea na ndoa yake au ndio itakuwa ni mwisho wa ile ndoa? Na je kama ni mwanamke kamfumania mumewe, anayo haki kweli ya kudai fidia kwa yule mwanamke aliyemfumania?

Tunasoma katika Biblia takatifu kitabu cha Yohana Mtakatifu 8:2-1,1 Pale wale waandishi na mafarisayo waliompeleka yule mwanamke kumshitaki kwa Yesu kuwa amezini, tuliona jinsi Yesu alivyowaambia wale washitaki. Aliwaambia, na asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe kumpiga mwanamke huyu……….wale washitaki walikimbia baada ya kushitakiwa na dhamira zao.
Bila shaka Bwana Yesu alifahamu kabisa kuwa yule mwanamke hakupaswa kuwa pale peke yake. Mnamleta huyu kwangu, je mwanaume aliyezini naye yuko wapi? Kitendo cha kuzini ni lazima kifanywe na watu wawili wenye jinsia tofauti, yaani mwanaume na mwanamke, sasa inakuwaje aletwe huyu mwanamke peke yake?

Kuna ukweli ulio dhahiri kwamba wanaume wengi huwachukulia wapenzi au wake zao kama mali zao, ambazo ni wao tu wanaotakiwa kuzimiliki. Yaani wanawachukulia wanawake kama viumbe dhaifu wasio na uwezo wa kuwa na maamuzi yao wenyewe kama wanadamu.

Kwa mfano ukisoma vyombo vya habari vya nyumbani Tanzania, mauaji mengi yanayotokana na fumanizi, wanawake ndio wanaouwawa zaidi ukilinganisha na wanaume. Lakini kama ukilinganisha kati ya wanaume na wanawake, itakuwa wanaoongoza kwa kutoka nje ya ndoa ni wanaume tena kwa kiwango cha juu hasa.

Kama ingekuwa wanawake nao wanawauwa waume zao pindi wanapowafumania basi wanaume wangeuwawa sana. Inashangaza sana kuona kwamba linapotokea fumanizi mwanamke ndio wa kwanza kubebeshwa lawama badala ya kulaumiwa wote, kwani pale anayeonekana kutia aibu ni mwanamke lakini mwanaume ataonekana ni kijogoo, na jamii haitamzungumzia kama atakavyozungumziwa mwanamke.

Unaweza kukuta mwanaume kufumania ujumbe wa simu ya mapenzi kwenye simu ya mkewe au mpenzi wake ikatosha kabisa kumuua mwanamke huyo. Huo ni ujumbe wa simu, je akimfumania wazi wazi akizini, ni nini kitatokea, bila shaka mnaweza kutabiri kitakachotokea.

Sio kwamba nawatetea sana wanawake, la hasha, ni kweli kwamba wanawake wamekuwa wakiwafumnia sana wanaume tena kwa kiwango cha kutosha, lakini kuuwa ni nadra sana.

Na ndio maana narejea lile tukio la Diwani wa Songea kutozwa faini baada ya kufumaniwa na mke wa Shekhe lina uhalali kweli?

Tutafakari kwa pamoja

Monday, September 28, 2009

HONGERA KWA SIKU HII MUHIMU:- HAPPY BIRTHDAY KAKA SHABANI KALUSE

Miaka inazidi kusonga mbele!!

Kuna msemo usemao " nikikutumia ua litasinyaa, kadi itachakaa, msg utafuta kwa hiyo nimeona nikuombee itafaa zaidi Mungu akupe kheri na akujalie maisha marefu wewe na pia familia yako". Nakutakia siku hii iwe njema kwako. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA SHABANI.

Saturday, September 26, 2009

MBALI NAWE

Nimelipenda hili shairi na nimeona si vibaya kama tukirudia tena kusoma kwani kila mtu kuna mtu ampendaye ambaye yupo mbali na pia katika blog zetu wote tuna nia moja ya kuelimishana.

Jua linapochomoza, kila siku asubuhi,
Hunifanya kukuwaza, unipae kufurahi,
Maneno nayokweleza, ni ukweli si kebehi,
Kuishi mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Wewe u sehemu yangu, nuru yangu maishani,
Nilopewa na Mungu, niwe nayo duniani,
Nitayaonja machungu, kama 'tanipiga chini,
Kuishi mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Daima uwapo mbali, hata ni kwa siku moja,
Nitakesha mi' silali, nikeshe nikikungoja,
Tukae sote wawili, tufurahi kwa pamoja,
Kuwa mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Huhisi nina adhabu, napokuwa mbali nawe,
Maisha kuniadhibu, hadi nichanganyikiwe,
Wewe nd'o wangu muhibu, sina tena mwinginewe,
Kuishi mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Nakuwa mi' na upweke, nazo karaha moyoni,
Nayo maji yasishuke, niyanywapo mdomoni,
Yanifanya nita'bike, nijawe nayo huzuni,
Kuwa mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Nakosa mie furaha, nakumbwa nao unyonge,
Maisha yawa karaha, kunifanya nisiringe,
Wala sifanyi mzaha, nisemayo 'siyapinge,
Kuishi mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Sogea kwangu karibu, e pambo la wangu moyo,
Pendo 'silolihesabu, amini niyasemayo,
Ya moyo wangu dhahabu, unipaye pasi choyo,
Kuishi mbali na wewe, ni kitu nisokipenda.

Shairi kutoka http://fadhilimshairi.blogspot.com/

Friday, September 25, 2009

NA IJUMAA YA LEO TWENDEN KWA WENZETU WASAMBAA NA WIMBO MDUMANGE(WABWANGA)

Na Wasambaa, Wabondei, Wazigua na Wadigo

Haya Viva afrika, na wengine wote wanao elewa nini kinasemwa/imbwa muwe na furaha ijumaa ya leo . Pia naomba mniambie wanasema nini kwani nimeambua neno moja tu ila nimependa mapigo ya mziki. IJUMAA NJEMA KWA WOTE!!!!

Thursday, September 24, 2009

DIWANI AFUMANIWA NA MKE WA SHEIKH USIKU WA MANANE


DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa. Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.


Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.
Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.


Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi watoe taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.
Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.


Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.
Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.
Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.


Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.
Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.

Habari hii inatoka Jamii Forum imeandikwa na Joyce Joliga, Songea

Tuesday, September 22, 2009

WANAUME NA KAULI HIZI: 'HUYO SIO WA KUOA, NI WA KUCHEZEA TU'

Bila shaka wewe msomaji unayesoma hapa utakubaliana na mimi kuwa umeshawahi kuzisikia kauli hizi kutoka kwa wanaume pale anapozungumziwa mwanamke mzuri kwa sura na umbo.

Kwa kawaida vipimo vya uzuri wa mwanamke kwa wanaume vimegawanyika. Wanaume wengi hupima uzuri wa mwanamke kwa sura au umbo, lakini linapokuja swala la kuoa, suala la tabia na mwenendo hupewa nafasi kubwa.

Na ndio maana wakati mwingine unaweza kushangaa kukuta mwanaume ambaye ni hodari wa kuchagua wanawake wazuri, lakini ukija kumuona mke aliyemuoa, utakuta ni mbaya kwa sura na umbo, lakini kwa upande mwingine utakuta mke huyo ni mzuri katika maeneo mengine kama vile, tabia nzuri,upendo, wema, na anayemudu malezi ya watoto katika familia.

Sifa nyingine ni zile za kumkubali mwingine kirahisi, kuwa tayari kusaidia yanapojitokeza matatizo katika familia, mpenda amani na kumfanya mume wake aone kuwa hakukosea kumchagua yeye kuwa mke wake. Kwa kifupi wanawake wa aina hii hata kama wangekuwa ni wabaya kwa sura na umbo bado wako kwenye nafasi ya kuonekana kuwa ni wazuri, na huolewa kirahisi zaidi.

Wanawake wazuri kwa sura na umbo ambao tabia na mienendo yao hairidhishi wako kwenye nafasi kubwa ya kuishi bila kuolewa, na kwa bahati mbaya zaidi wanawake wengi wanaohesabika kuwa ni wazuri, tabia na mienendo yao ni ya kutilia mashaka. Wanaume wengi huvutiwa na wanawake hao kujenga uhusiano nao hasa wa kimwili tu na si vinginevyo, na ndio maana wanawake wazuri kwa sura na umbo wanalo soko kubwa sana kwa wanaume, lakini huishia kuchezewa zaidi kuliko kuolewa.

Wanaume nao kwa upande wao wamejenga dhana kwamba wanawake wazuri sana sio wa kuoa na hivyo kuwaogopa. Wanaamini kwamba wanawake wazuri sana ni wasumbufu, kitu ambacho kina ukweli kwa kiasi fulani. Wanaume wanaamini kwamba wanawake wazuri sana kwa sura na umbo huwasababishia waume zao maradhi ya moyo,shinikizo la damu na wakati mwingine hata kuwafanya kupata matatizo fulani ya kiakili, na hiyo inatokana na waume hao kuwa katika mashaka ya wake zao kuchukuliwa na wanaume wengine wakati wowote kutokana na uzuri wao. Hata hivyo wanawake wazuri nao huwaendesha waume zao wakijua kuwa ni wazuri na soko lao liko juu na waume zao nao huwanyenyekea wakihofia kuachwa.

Na ndio maana usishangae kuona kuwa wale wanawake ambao watu wamekuwa wakiamini kuwa ndio wabaya kwa sura au umbo lakini tabia na mienendo yao ni mizuri ndio wanaoolewa na hata ndoa zao zinadumu, tofauti na za wale wanaoonekana kuwa ni wazuri sana kwa sura na umbo na ambao tabia na mienendo yao si mizuri, ndoa zao hazina umri mrefu.

Monday, September 21, 2009

JE? UNAONA NINI KATIKA PICHA HIZI? SIJUI MAPACHA HAWA?:-)

Sijui huyo ni dada wa wapi?


Na huyu pia sijui ni nani ila kuna kitu hawa watu wanafanana au?


Sunday, September 20, 2009

NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA KWA UJUMBE HUU!!!!!

Furaha:- Inakuja wakati kazi zetu na maneno yetu yanapokuwa na faida(fadhila) kwa wewe binafsi na pia kwa wengine.

Amani:- Kuleta amani kwa kila mtu, inabidi kupambana ili kuweka amani yako ya maisha yake pia.

Ushujaa:- Kutokuwepo na woga au kukata tamaa, isipokua ni uwezo wa kushinda.Utulivu:- Ni amani inayokuja wakati nguvu zipo ndani ya upatanifu wa kirafiki upo sawasawa.

Upendo/Mapenzi:- Ni msukumo ambao tumepewa, mapenzi ni pumzi ya maisha juu ya moyo na yanaleta madaha/uzuri ndani ya roho.Bila kusahau ya kwamba upendo una mamlaka , enzi, amri na nguvu hapa duniani.

Busara:- Elimu, kipaji/uwezo wa kuelewa/kuhisi kitu haraka na uzoefu wa mchanganyiko wa kuelekezana na kufikiri jambo/tendo.

Saturday, September 19, 2009

U-MODO WA SIKU MOJA = RAHA JIPE MWENYEWE NA PIA JIPENDE MWENYEWE KWANZA

Hapa vipi tena?
Leo saa sita mchana.

Mawazo mpaka nywele zawasha

Hapa ndo mawazo yamezidi kiasi kwamba nimekuwa kama nyani.
JUMAMOSI NJEMA KWA WAOTE NA POPOTE MLIPO.


Thursday, September 17, 2009

HATUA SITA ZA KUSAIDIA KUDHIBITI MIMBA SHULENI

MAANDALIZI ya safari yangu kwa ajili ya kumpeleka mtoto wa dada yangu kujiunga na masomo ya sekondari Morogoro yalikwenda vizuri na asubuhi yake nilijona mtu mwenye bahati.

Tulifika mapema kwenye kituo kikuu cha mabasi, Ubungo na tulipokuwa tunaelekea kwenye basi moja ambalo tulitaka kukata tiketi, tuliwaona wasichana kadhaa walioonekana kuwa ni wanafunzi, ni kweli nao walikuwa wanakwenda katika shule hiyo. Alikuwepo mwanamume mmoja aliyevalia vizuri ambaye alijitambulisha kuwa mwalimu wa shule hiyo.
Mwalimu huyo, ambaye alikuwa na vitambulisho vya kazi aliwaambia wazazi waliokuwa wanawasindikiza watoto wao wasisumbuke kwani yeye ametumwa kwa ajili hiyo. Hivyo, wazazi, walezi na sisi wengine tuliotumwa tulimkabidhi mwalimu huyo watoto nasi tukarudi nyumbani.

Kwa haiba aliyokuwa nayo mwalimu yule, kwa umri wake na hata upole alioonyesha, alivyokuwa anazungumza taratibu na alivyotuaminishia usalama, haraka tulinong’onezana kuwa ni mlokole. Niliporudi nyumbani asubuhi ile niliwachekesha wazazi wake kwamba 'nimekbidhi binti yao kwa mwalimu mlokole'.
Hilo lilikuwa kosa kubwa. Utaratibu ule ulikuwa tofauti na fikra zake moyoni, alikuwa mbwa mwitu. Mwalimu huyo ambaye, nahifadhi jina lake, ndiye alikuja kutupa pigo kubwa kwa kumkatisha masomo binti yetu baada ya kumpa ujauzito. Tumefungua kesi kortini.

Pamoja na kuchukua hatua hizo, tumekuwa tukijiuliza nini ki kifanyike ili, siyo tu kwa sisi kupata haki kutokana na binti yetu kupewa ujauzito na mwalimu anayepaswa kuwa mlezi wake, bali pia kuwadhibiti walimu wengine wa kiume wenye tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike na kuwapa mimba.
Hii ni kwa sababu tuliokumbwa na kero siyo sisi tu bali wazazi wengi, na kumekuwa na malalamiko kila kona unayopita, kuhusu wanafunzi wa kike kukatishwa masomo baada ya kugundulika wamepata ujauzito shuleni.
Japokuwa baadhi ya wasichana hupewa mimba shuleni na wanafunzi wenzao wa kiume, watu wa mitaani pamoja na wafanyakazi, ukweli ni kwamba wengi wao hukatishwa masomo kwa kupewa mimba na walimu wao.
Taarifa mbalimbali na uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi, walimu wanahusika kwa kiasi kikubwa. Walimu hao huwapata wanafunzi kwa urahisi kwa vishawishi kadha wa kadhaa vikiwemo vya kuongezewa alama, kupewa maswali ya ziada (twisheni) na kupangiwa kazi nyepesi.

Kuna ukweli pia kwamba baadhi ya wasichana hupata ujauzito kutokana na kutokuwa na maadili mazuri, papara au ulibukeni wa maisha lakini wengine hulazimika kujenga mahusiano ya kimapenzi na walimu wao kwa kufundishwa masomo ya ziada ili wafaulu mitihani yake.
Kwa mfano, hivi karibuni, tulisikia katika baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa mwalimu mkuu wa shule moja iliyoko Kusini mwa Tanzania amepandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kumpa mimba mwanafunzi wake.

Katika tukio kama hili, kwa hali ya kawaida unaweza usiamini wala kupata picha inakuwaje, lakini ndiyo hali halisi ya maisha yalivyo katika ulimwengu wa sasa. Kama mzazi wa kiume anaweza kujenga uhusiano wa kimapenzi na mtoto aliyemzaa sembuse mwalimu?.
Ukichunguza kwa makini utagundua chanzo cha tatizo hili ni tamaa ya walimu na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za maadili kazini. Walimu hupaswa kuwa walinzi wa wanafunzi na waongoza maadili kinyume cha hivyo ni utovu wa nidhamu.

Mapendekezo yangu.

Kwanza wazazi wote wenye wanafunzi wa kike wahakikishe wanafungua kesi dhidi ya wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Endapo binti atadai hajui, kwa lengo la kumficha mhusika, basi binti huyo ashitakiwe binafsi.

Pili, wazazi tusikubali vishawishi vya wavulana au walimu au watu wengine weyote walihusika kwamba wasishtakiwe ila waachiwe wawatunze mabinti na ujauzito walionao. Imebainika hufanya hivyo kwa muda tu, baada ya miezi michache huwapa talaka na huo unakuwa mwisho wao.

Tatu, napendekeza serikali iweke uzito kwa upande wa walimu kwamba watakaobainika kuhusishwa tu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi waachishwe kazi. Nina uhakika hakuna anayependa kuachishwa kazi hivyo wataachana na tamaa yao kwa wanafunzi.
Hatua hizo zinaweza kuchangia kupunguza kuwepo kwa matukio kama haya na walimu watajitahidi kuishi juu ya tuhuma za kimapenzi.

Nne, uwepo utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike kila mara na kuwapa ushauri nasaha kwamba wajifunze na wazoee kusema "hapana" wanapofuatwa na walimu wao kimapenzi.

Tano, iko haja ya kuweka sheria kuzuia wanafunzi kufika kwa walimu kama hawana uhusiano wa kidugu. Shule za seminari na zinazoendeshwa na masista zimeweza, kwa nini ishindikane katika shule za serikali?

Sita ni kwamba chanzo kingine cha matukio ya mamba ni kushiriki starehe. Wazazi wawazuie watoto wao; wavulana kwa wasichana kujiingiza kupita kiasi kwenye burudani kwani ni nchimbuko kubwa la maasi ya maadili na mwishowe kupeana mimba.

Hii ilitoka mwananchi la tarehe 23/6/2009 na mwandishi Elizabeth Suleyman.

MZIKI NI MOJA YA MAISHA NGOJA TUMSIKILIZA DADA LADY JAY DEE- NATAMANI KUWA MALAIKA



Dada Jay Dee hata mimi natamani kuwa malaika tu nimeupenda kweli wimbo huu mpaka nimeona niuweka hapa. Ahsante sana. Nadhani siku moja tutakuwa ru malaika.

Wednesday, September 16, 2009

WANAFUNZI WA KIKE WAPATAO MIMBA KABLA YA KUMALIZA SHULE WARUHUSIWA KUFANYA MTIHANI

Nimezoea sana kusikiliza habari za BBC, kwa hiyo wakati nasikiliza habari hii, nikaona sio mbaya kama nikiiweka hapa kibarazani kwangu ili wengi msome na tuweze kujadiliana.

Idadi ya wanafunzi wa kike wanaoacha shule kwa sababu ya mimba isiotarajiwa inazidi kupanda

IDADI ya wasichana wanaokatisha masomo yao na kuacha shule wilayani Kericho, kwa sababu ya kupachikwa mimba wasiotarajia imewashangaza maafisa wa Elimu na wadau wengine.

Katika kisa ambacho kimezua mjadala mkubwa juu ya Elimu na mimba miongoni mwa wanafunzi wa kike, imeibuka kuwa toka kwa idadi ya wasichana 25 waliojiunga katika kidato cha kwanza katika shule moja katika eneo hilo, 24 waliacha shule baada ya kutwikwa mimba.

Katika makala ya wiki hii tunahoji nini kinachopelekea hali kama hii ya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi???? Mwalimu mkuu alizungumzia umbali wa shule kuoka kwa makao ya wanafunzi ambao wanalazimika kupitia katika misitu ya chai jambo amabalo linawaweka katika hatari ya mahusiano ya kimapenzi na hata ubakaji.

Mwalimu huyo mkuu alisema ni jambo la kushangaza sana. Aliongezea kuwa idadi ya waichana katika shule hio sasa ni ishirini pekee. Wengi wa wasichana waliokuwa wakifanya vyema katika masomo wameacha shule baada ya wanafunzi wenzao na baadhi ya wafanyakazi katika mashamba ya chai kuwatwika mimba.

Elimu ya watoto wa kike inaendelea kuwa ndoto isioweza kutimika katika eneo hili la Afrika. Wasichana wengi wanadanganywa na wanaume na kujitosa katika tabia na mahusiano ya kingono yanayopelekea mimba isiotarajiwa. Jambo ambalo huwafanya wasichana hawa kuacha shule na kuanza maisha ya uzazi wakiwa wao wenyewe bado wachanga.

Wengine wanakumbwa na vizingiti vya kitamaduni kama vile tohara ya wanawake, ndoa za mapema, kazi za nyumbani, magonjwa na umasikini. Kumekuwa na mjadala iwapo kuratibishwa kwa masomo ya afya ya uzazi katika silabasi za shule kutaksaidia kudhibiti mimba isiotarajiwa na magonjwa ya zinaa miongoni mwa wanafunzi.

Inchini Tanzania serikali, kwa mara ya kwanza, imewaruhusu wale waliopata mimba wakiwa shuleni kufanya mitihani. Hapo awali wanafunzi waja wazito walikuwa wakikatazwa kufanya hivyo.

Je, nini mchango wako kuhusu yote haya??????

Habari zaidi sikiliza hapa katika kipengele cha kimasomaso. http://www.bbc.co.uk/swahili/

Tuesday, September 15, 2009

HEBU TWENDE NA TUANGALIE AFRIKA LEO!!!!!

ZANA ZETU + KUMBUKUMBU+ UTAMADUNI WETU

1. Ni nyengo ya akina baba. 2. Ni nyengo ya akina mama. 3. Ni upanga na 4 . Ni ujembe hizi zana ni kutoka Ubenani, maana kule mke na mune wote wanafyeke kwa hiyo kila mtu lazima awe na nyengo yake. Ukiangalia vizuri utaona kuna tofauti kati ya nyengo ya baba na mama.
1. Mkuki. 2. Inainekana kama ni fimbo lakini ni kisu . 3. ni kisu kidogo na 4. ni aina ya panga hivi vifaa vinatumika sana umasaini.

Monday, September 14, 2009

UJUMBE WA LEO:- JINSI YA KUCHEZA NA MANENO (KISWAHILI)

Dar es Salaam = Lala salama
Afrika nzima = Wazimana
Tanga = Wanatanga tanga
Wakenya = Wanakenyana
Tanzania = Wanazamia
Naiorobi = Wanaibiana
Arusha = Wanarusharushana
Wasukuma = Wanasukumana
Mombasa = Wanatongozana
Uganda = Wanagandana
Kisumu = wanakisiana

Sunday, September 13, 2009

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA MLO HUU MTAMU WA NDIZI.


VIPIMO

Ndizi Mbivu 6
Nazi Kikopo 1
Sukari Vijiko 3 vya chakula
Hiliki Kijiko 1

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1) Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
2) Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
3) Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
4) Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
5) Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Huu ni mlo wangu wa leo karibuni.

KIDOKEZO:

Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.

Saturday, September 12, 2009

HADITHI YA DOA JEUPE

Nadhani wengi tumewahi kuisikia hadithi hii kama hujawahi basi soma hapa na ufurahi au usikitike.

Hapo zamani, alikuwwepo mfalme ambaye hakupenda kabisa watoto wa kike. Akamwonya vikali mkewe kuwa akizaa mtoto wakike, atamuua.

Mke wake alijaribu kumsihi kuhusu swala hilo, kwa kumueleza kwamba watoto, wawe wa kike au wa kiume ni riziki ya Mungu. Vile vile mtoto wa kike, atamsaidia sana mama yake kwa mambo mengi, hasa shughulu za kika siku za nyumbani. Lakini, yote aliyozungumza mkewe, ilikuwa kama kuzungumza na kiziwi.

Wakati huo, mke wa mfalme, alikuwa na mimba, na siku zilikuwa zimewadia kuzaa. Mfalme, akasisitiza kuwa huyo mtoto ambaye yu njiani kuzaliwa ataishi iwapo atakuwa wa kiume. Mkewe akazaa mtoto, mtoto wa kike. Mfalme bila huruma akamuua yule mtoto.

Mkewe akabeba mimba tena, mara ya pili, vile vile akazaa mtoto wa kike. Mambo yakawa yale yale, mtoto akauliwa.

Mimba ya tatu, mfalme alikuwa safarini. Safari hiyo, ilichukua muda mrefu sana. Huku nyuma mkewe akajifungua mtoto wa kike tena. Kwa kuhofia mumewe kumuua yule mtoto, akaamua afanye kila aliwezalo yule mtoto aishi, kwa maana mumewe alikiwa hayupo. Alimchukua porini asijue la kufanya, akahangaika huku na huku. Hatimaye njiani, akajigonga na jiwe. Jiwe hilo halikuwa la kawaida, lakini yeye hakufahamu. Ghafla, baada ya kujikwatua kwnye ilele jiwe, mbele yake alisimama bibi kizee. Akamuuliza zote mkw wa mfalme kama ana matatizo. Bila kusita, yule mke wa mfalme akamueleza yote yaliyotokea kwa mimba zake za awali na akamueleza pia, alikusudia kumfanya nini huyu mtoto wa tatu aliyekuwa mikononi mwake. Isipokuwa hakufahamu afanye nini, na nani atamsaidia.

Baada ya yule bibi kizee kusikia hayo, akaamua kumsaidia mke wa mfalme, akamwambia:”Nitakusaidia, unaweza kuniachia mimi mtoto huyu. Nitamtunza, lakini ni lazima tupeane ahadi. Utakuwa unakuja kumuangalia wakati mume wako yupo safarini. Hata kama hatosafiri kwa muda mrefu, subiri mpaka asafiri, ni lazima uweke hiyo ahadi. Ikiwa mtoto wako ataugua, nitakuja kwenye ndoto zako. Kwa sababu ya doa jeupe kwenye goti lake, tutamwita Doa Jeupe.”

Wakakubaliana na kuwekeana ahadi. Mtoto akachukuliwa na bbi kizee, mke wa mfalme akaanza rahaa safari ya kurudi nyumbani. Njiani akawaza kwa furaha:- “Hatimaye, nimepata mtoto ambaye ataishi. Niliamini kuwa nitakufa bila ya furaha kama hiyo!”

Mfalme, baada ya siku kadhaa, alirejea toka safarini, kitu cha kwanza, akamwuuliza mkewe kuhusu hali yake. Mkewe akajibu: “Nilizaa mtoto ulipokuwa safarini, lakini aliktoka kabla ya wakati wake kwa hiyo hakuishi nikamzika.” Mfalme akampa pole mkewe kwa masikitiko ya kupoteza mtoto.

Wiki, miezi ikapita mkwewe akaomba sana mume wake asafiri tena, ili akamwone mtoto wake anaendelea vipi. Lakini mfalme, hakusafiri.

Siku moja, mfalme akachukua bundiuki yake akamuaga mkewa kwamba anakwenda mawindoni, siku nzima. Hata hivyo mkewe asingeweza kufanya lolote maana ulikuwa ni muda mfupi kwake. Mfalme akajitayarisha na kuondoka. Njianai kuelekea mawindoni, mfalme akakutana na Doa Jeupe. Kwa uzuri wake alivyoumbika, ingawa alikuwa bado msichana mdogo,mfalme akamfuata alipokuwa akielekea, mpaka kufika kwenye nyumba ya yule bibi kizee na akamwona Doa Jeupe anaingia ndani Akabisha hodi, hapo nyumbani kwa bibi kizee. Mfalme akamwuuliza bibi kizee:- “Huyu mtoto wa nani?” Akajibu: “ Huyu mtoto ni wangu wa kuzaa mwenyewe!” Mfalme akauliza tena: “Anaitwa nani?” “Doa Jeupe;” akajibu bibi kizee. Mfalme akajaribu sana kuzungumza na yule msichana, lakini Doa Jeupe akabaki akimwangalia bila kusema lolote! Mfalme mwishowe akasema : “nataka kumwoa huyu mtoto wako!” Bibi kizaa kwa heshima, akajibu: “ Unavyotaka mtukufu.”

Aliporejea nyumbani, akamweleza mkewe kwamba amekutana na msichana mzuri asiye mfano na angependelea kumwoa akifikia umri wa kuolewe.

Huku nyuma bibi kizee alipata ndoto usiku ule. Ndoto hiyo ilimuonyesha nyumba yake mwenyewe. Nje ya nyumba barazani, aliona alama za mihuu ambayo alifanana na ya mfalme. Kutokana na ndoto hiyo. Akafahamu kwamba mfalme atarudi tena kwa sababu ya Doa Jeupe.
Kwa hiyo akamwambia Doa Jeupe asubuhi yake: “Mwanangu, mimi nina safari ndogo nitakapokuwa sipo, na yule mfalme akija, usimruhusu ndani ya nyumba. Na ukikutana naye nje, usishawishike kumfuata!” Doa Jeupe, akaahidi atafanya alivyoelezwa. Asubuhi, bibi kizee akaondoka. Baadaye kidogo, mfalme akaja muangalia aliyetegemea kuwa mkewe wa maisha ya baadaye. Alibisha hodi, lakini hakuna aliyefungua. Ikabidi aondoke bila mafanikio yo yote. Hayo, yalitokea mara nyingi na ukafika wakati mfalme akakata tamaa kbisa. Hivyo akachukua uamuzi wa kutafuta msichana mwingine, awe mkewe wa pili. Haikuchukua muda akaoa mke wapili. Akamwelezea kuwa :- “Nimekuoa wewe , kwa sababu sikuweza kumpata Doa Jeupe!”

Mkewe mfalme wa pili, kazi yake ilikuwa mkata kuni. Katika mojawapo ya safari mwituni kufuata kuni, alikutana na msichana mzuri sana. Aliporudi nyumbani, akamweleza mume wake kwamba amemwona msichana aliyemzungumza. Mfalme kusikia hivyo, akapata ari na hamu kubwa ya kwenda kumtafuta tena Doa Jeupe. Kweli alipofika ile sehemu mkewe alipomuona, alikuta nyayo za miguu ya Doa Jeupe,zikielekea nyumbani kwa bibi kizee. Akaenda moja kwa moja mpaka mlangoni akabisha hodi. Hakuna aliyemfungulia. Kwa masikitiko, akarudi kwake. Akajaribu tene na tena, mambo hayakubadilika.

Bibi kizee akaanza kuingiwa na wasiwasi, kwa hivyo akamfuata mke wa kwanza wa mfalme. Akameleza nini mumewe anachotaka kufanya kuhusu Doa Jeupe. Mamaye Doa Jeupe, alishtuka sana aliposikia hayo: “Haiwezekani”! alisema. Wakaja na wazo zuri pamoja kwamba yeye bibi kizee na Doa Jeupe wahamie porini zaidi. Wakafanya hivyo siku hiyohiyo.

Mfalme akakata tamaa kabisa, hasa baada ya Doa Jeupe na bibi kizee kuhama walipokuwa wakiishi zamani. Kwa sababu hiyo, Doa Jeupe na bibi kizee waliishi kwa amani miaka mingi bila kubughudhiwa.

Doa Jeupe, akawa msichana mzuri wa ajabu. Siku moja , bibi kizee, ilibidi asafiri kwenda kuangalia ukoo wake. Hivyo akamuacha Doa Jeupe peke yake pale nyumbani. Nyumba yao mpya, ilikuwa karibu sana na mto. Ambapo ndipo walipokuwa wakioga, kufua na kuchota maji. Doa Jeupe, siku hiyo akaenda kuoga peke yake. Wakati huo huo mfalme alikuwa katika moja ya safari zake. Njiani ilimlazimu avuke mto huo huo ambao Doa Jeupe alikuwa akiutumia. Dakika chache baada ya Doa Jeupe kumaliza kuoga na kurudi nyumbani, mfalme naye, akafika sehemu ile ile. Wakati akisubiri mtumbwa wa kumvusha alikaa juu ya jiwe, miguuni kwake, aliona unywele umejisokota katika mguu mmoja wapo . Alishangaa sana maana hajawahi maishani mwake kuona unywele mzuri kama huo. Akaamuru waja wapo wafanyakazi wake wamtafute mwenye unywele huo.

Haikuwa kazi rahisi. Waliendelea kufanya hivyo kwa siku nyingi. Hatimaye wakampata msichana mwenye unywele ule, ambaye alikuwa ni Doa Jeupe! Alipokuwa akioga, unywele ulitoka. Wakamlete mbele ya mfalme. Afurahi kupita kiasi kumuona amekuwa msichana mzuri aliyeumbika vizuri ajabu. Hatimaye, mfalme akafikiri, kuwa amampata msichana ambaye atakuwa mke wa tatu. Hakuwa na hamu ya kuishi na wake zake wawili.

Bibi kizee kupata habari hizo, akafunga safari kurudi kuja kumtaharisha Doa Jeupe asimwoe yule mfalme ambaye ni babake! Akamweleza ukweli wa mkasa wote toka mwanzo mpaka mwisho. Akasisitiza kwa kumwambia; “Usisahau kuwa, mfalme anataka kukuoa kwa sababu wewe ni mwanamke.

Alipomaliza kusema hayo, bibi kizee akaondoka tena: Doa Jeupe alipata uchungu baada ya kuambiwa ukweli wa visa vya baba yake. Mfalme akarudi kumwomba Doa Jeupe amwoe. Doa Jeupe akamjibu: “Usisahau kuwa, mimi ni mwanamke, kama unavyofahamu wanawake hawana faida. Hufahamu kama wanawake ni hatari? Wanaweza kukuua?
Mfalme akahamaki: “Nani kakuambia upuuzi huo?”
Doa akamwambia: “Babu zangu ndio walioniambia, wewe uliyesafiri karibu ulimwengu wote, umeshawahi kuona mwanamke mzuri kama mimi? Nataka nikueleze kuwa, mimi nimetumwa hapa duniani kuangalia mazuri na mabaya niko tofauti na wanawake wengine!”

Mfalme hakuweza kuelewa lo lote. Akabaki akimuangalia tu. Doa Jeupe akaendelea: “Sikia! Mimi ni Doa Jeupe, yule ambaye miaka mingi iliyopita, ulimwona kama msichana mdogo. Ukasema akikua ungependelea kumwoa. Mimi ni binti wa mke wako wa kwanza. Wewe ambaye uliwaua dada zangu wawili wa kwanza na wa pili mara baada ya kuzaliwa, na kusema kuwa hawana faida kwako, unataka kunioa?

Lazima ufahamu kwamba mimi naishi dunuani leo, kwa sababu mama alinizaa ulipokuwa safarini, kuhofia kwamba na mimi yangenikuta yaliyowatokea dada zangu, akanificha kwa bibi kizee. Hivyo, siwezi kuoana na baba yangu!”

Mfalme akakataa kata kata, kuamini aliyokuwa akisikia akauliza ; “ Unaweza kunihakikishia vipi, kuwa wewe ndio yule msichana niliyemuona miaka mingi iliyopita?” Doa Jeupe alkamwambia : “Muulize mke wako wa kwanza ambaye ni mama yangu naye, atahakikisha!”
Mkewe mfalme akaitwa na akaeleza yote yaliyotokea wakati mumewe yuko safarini. Mfalme akamwuuliza; “Ni kweli kwamba ulizaa mtoto wa kike ukamficha nisimwone?” Mkewe akakubali. Mfalme akaendelea kusema: “Unaweza kunihakikishia kuwa msichana mzuri hivi, ni binti yako?” Mkewe akasema: “Nilimwita Doa Jeupe, sababu alizaliwa na kovu jeupe kwenye goti lake!”

Kila mmoja akawa akimwangalia Doa Jeupe ambaye alikuwa akionyesha lile doa kwenye goti lake! Huo, ulikuwa ushahidi wa kutosha! Mama na mtoto kwa furaha ilioje, wakaangukiana na kukumbatiana, wakimwacha mfalme amejaa aibu tele.

HADITHI HII INAWAKUMBUSHA AKINA BABA WENYE UROHO WA WANAWAKE WA WENZAO, KWAMBA WANAWAKE WAMEZALIWA KAMA WASICHANA WADOGO. HIVYO WASITAMANI VYA WENZAO, VYAO WAKAVICHUKIA.
Hadithi kutoka kwenye kitabu cha HADITHI na via kutoka Tanzania.

Friday, September 11, 2009

MICHEZO NI MOJA YA MAISHA HAPA NI HUKO HACHIOJI TOKYO

Hapa ni Mtanzania mwenzetu aliyekuwa kwenye mashindano ya karate huko Hachioji Tokyo Japani. Akipokea cheti.

Hapa akina dogo wakiwatoana jasho.

picha ya tatu akina dada nao hawapo nyuma .

Thursday, September 10, 2009

USICHOKE

Maisha ni kama vita, usichoke kupigana,
Hata kama ukigota, endelea kupambana,
Bado muda wa kutweta, bado ni mapema sana,
Usichoke mwanakwetu.

Nenda shule ukasome, uongeze maarifa,
Ukiwa huko jitume, uliinue taifa,
Nenda kakazane shime, utajipatia sifa,
Usichoke mwanakwetu.

Amka wahi kazini, ili uongeze tija,
Ujuzi wako kichwani, taifa linaungoja,
Ujitume ofisini, na wenzako kwa pamoja,
Usichoke mwanakwetu.

Pigana pasi kuchoka, yapiganie maisha,
Jitihada zako weka, ustawi kufanikisha,
Kwa dhamira ya hakika, malengo kufanikisha,
Usichoke mwanakwetu.

Mwiko kukata tamaa, bado ni ndefu safari,
Kurudi nyuma kataa, pambana nazo hatari,
Tumia kila wasaa, maisha kutafakari,
Usichoke mwanakwetu.

Usifanye masikhara, maisha hayendi hivyo,
Kwa hiyo kuwa imara, vile iwezekanavyo,
Nawe utazidi ng'ara, namna itakiwavyo,
Usichoke mwanakwetu.

Kwa idhini ya Usichoke
Maisha ni kama vita, usichoke kupigana,
Hata kama ukigota, endelea kupambana,
Bado muda wa kutweta, bado ni mapema sana,
Usichoke mwanakwetu.

Nenda shule ukasome, uongeze maarifa,
Ukiwa huko jitume, uliinue taifa,
Nenda kakazane shime, utajipatia sifa,
Usichoke mwanakwetu.

Amka wahi kazini, ili uongeze tija,
Ujuzi wako kichwani, taifa linaungoja,
Ujitume ofisini, na wenzako kwa pamoja,
Usichoke mwanakwetu.

Pigana pasi kuchoka, yapiganie maisha,
Jitihada zako weka, ustawi kufanikisha,
Kwa dhamira ya hakika, malengo kufanikisha,
Usichoke mwanakwetu.

Mwiko kukata tamaa, bado ni ndefu safari,
Kurudi nyuma kataa, pambana nazo hatari,
Tumia kila wasaa, maisha kutafakari,
Usichoke mwanakwetu.

Usifanye masikhara, maisha hayendi hivyo,
Kwa hiyo kuwa imara, vile iwezekanavyo,
Nawe utazidi ng'ara, namna itakiwavyo,
Usichoke mwanakwetu.

Shairi hili linatoka kwa http://fadhilimshairi.blogspot.com/ nimeona sio mbaya kama likisambaa ili wengi wasome ni ujumbe mzuri.

LEO NI MAZISHI YA BABY D

Ndiyo tunakubali kuwa Mungu alitoa na Mungu anachukua lakini inapokuja kwa mtoto huwa inaumiza kidogo nahasa mtoto huyo hata hajaishi kama inavyotakiwa. Na pengine hata hajabebwa na waliompenda. Mtoto D amekuwa katika dunia hii kwa muda wa siku 18 tu. Naomba wote tuchukua angalao dakika na tumwombe mtoto D. Mama, baba, wajomba, shangazi na ndugu wote watakuwa wanakukumbuka kila siku, ustarehe kwa amani peponi. Amina. Zaidi soma hapa. http://changamotoyetu.blogspot.com/ mada aliyoandika jumapili 6/9 na mada yenye kichwa cha habari Rest in peace baby D.

Wednesday, September 9, 2009

HAPA VIPI SASA JAMANI? NAONA KAMA...AU?

Je? hii ni kawaida na haki? Kaaazi kwelikweli!!!!

Tuesday, September 8, 2009

UZOEFU WANGU KATIKA MAISHA AMBAO SITAUSAHAU

Kuna mambo mengi katika maisha ambayo kama wanaadamu tunakuwa tumeyapitia, hayo yote ndio huyafanya maisha haya tunayoishi yawe na maana. Miongoni mwa mambo au masaibu tuliyokutana nayo yapo ya kufurahisha na ya kuhuzunisha na mengine yenye kukera na kutia kinyaa, lakini yote ni maisha na yalikuwa ni lazima yatokee ili kujifunza jambo fulani.

Lakini hata hivyo si rahisi kusahau kila jambo ulilokumbana nalo katika maisha hasa kama lilikuwa ni la kuumiza kihisia, lakini kuna wengine wanasahau upesi na wengine si rahisi kusahau. Kwa mfano kwa upande wangu mimi kuna jambo moja, ambalo mimi SITALISAHAU. Nakumbuka nilikuwa na miaka 10 wakati huo. Baba na mama walikwenda hospital Litembo iliyoko katika wilaya ya Mbinga, mkoani Songea. Mimi na kaka zangu tulibaki kwa baba mkubwa.

Huyu baba mkubwa alikuwa na watoto wa kike 6 na mwanae mkubwa wa kike aliitwa Maria. Siku moja jumapili Nilimwomba dada Maria kanga kwani mimi nilikuwa sina, lakini hakunipa ALININYIMA na kuniuliza kwa nini baba yangu ambaye ni mwalimu asininnunulie. Kwani wakati ule nilikuwa mtoto wa kike peke yangu. Nayeye katika hali ya kinisimanga aliniambia "wewe uko peke yako mtoto wa kike inakuwaje wazazi wako wanashindwa hata kukununulia kanga" .(Mwana mdala nga veve vishindwa kukugulila nyula). Aliongea kwa Kingoni. Siku ile nililia sana, mpaka sasa nalikumbuka vizuri tukio lile na mpaka leo roho inaniuma sana kila nikikumbuka maneno yale.

Sikujua kama binadamu wanaweza kuwa wakatili kiasi hiki, na hasa ukizingatia yeye alikuwa dada yangu. Naomba nikiri kuwa tangu tangu siku ile sijawahi kuwasiliana naye, ingawa sina ukakika kama atakuwa analikumbuka tukio hilo. Kwani waswahili wanasema mtendaji hakumbuki ila mtendewa ndiye anayekumbuka.

Mimi kama walivyo binadamu wengine ninao udhaifu wangu, na udhaifu huo si mwingine bali ni kutomudu kufanya kazi ngumu tangu utototni mwangu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kule kingoli maisha yalikuwa magumu sana kwangu, kwani kulima mpunga na pia karanga na mihogo ilikuwa ni shughuli ambayo ilikuwa inanipa shida sana, ilikuwa kila tukienda shambani, mimi nilikuwa wa mwisho kumaliza ngwe yangu kule shambani.

Mazao ambayo tulikuwa tunalima sana ni karanga na mpunga tangu asubuhi mpaka mchana. Halafu kule kingoli tulikuwa tunakula sana ugali wa muhogo na kwa kuwa sisi tulihamia kule, tulikuwa hatuna shamba la mihogo. Kwa maana hiyo ilibidi tununue, ndugu yangu huko tulikokuwa tukinunulia hiyo mihogo kulikuwa ni mbali, yaani tunatembea mpaka miguu inauma. Tulikuwa tunachimba, kumenya kabisa ili uzito upungue.

Baada ya hapo tunarudi na mzigo kichwani na jua linawakia utosini. tukifika nyumbani na kutua mzigo, kuna kazi ya kuandaa chakula cha mchana. Tukishamaliza kula tunapumzika kidogo kisha tunaanza kazi ya kuchotelea maji ya kulowekea ile mihogo. Kwani kulikuwa hakuna maji ya bomba, tulikuwa tunachota kisimani. Jamani kweli maisha ni safari ndefu.

Kusema kweli kila nikikumbuka maisha niliyopitia kule kijijini kwetu, kuna wakati ninalia na kuna wakati huwa ninacheka sana. Kwa simulizi hii sio kwamba nilikuwa namlaumu dada yangu mkubwa kwa kitendo chake cha kunisimangia kanga yake, kwani ilikuwa ni hiyari yake kunipa au kutonipa, kilichoniuma ni yale masimango, hata hivyo simlaumu kwani kuna jambo nilijifunza, kutokana na kitendo chake kile.

Kama kuna mtu yeyote ambaye ataumizwa na simulizi hii basi anisamehe, kwani sio nia yangu kumuumiza mtu bali nilitaka kusimulia uzoefu wangu juu ya maisha haya tunayoishi, kwamba, kumfanyia mtu wema ni sawa na kuweka akiba ambayo inakufaa kesho..

Monday, September 7, 2009

KUSAIDIA KAZI ZA NYUMBANI + RUHUWIKO -SONGEA 2009

Namsaidia mama kuchambua maharage hapa ilikuwa mwaka huu 2009. Ruhuwiko.
Na mimi namsaidia mama kufua nguo hapa ilikuwa mwaka huu 2009. Ruhuwiko.





WANAUME WA KITANZANIA

WASAMBAA
Ana mke mmoja,
ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mkewe.

WACHAGA
ana mke mmoja,
Ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mpezi wake.

WANGONI
Ana mke mmoja,
Ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mfanyakazi wa nyumba.

WASUKUMA
Ana wake wawili,
Ana wapenzi wawili,
Anampenda zaidi dada ya mke wake.

Coateriana/waZanzibar
Ana wake wanne,
Hana mpenzi,
Ana mpenda zaidi mke yule mpya.

WAJALUO
Ana wake wanne,
Ana wapenzi wanne,
Ampendaye zaidi ni mke wa jirani.

WANYAMWEZI
Ana mke mmoja, wake wawili,wake watatu,
Ana wapenzi kadhaa,
Ampendaye zaidi ni muhudumu wa baa/mgahawa.

WAKURYA
Mke mmoja,
wapenzi wengi,
Anawapiga wote.

WAMASAI
wake wawili,
mpenzi mmoja,
Ampendaye zaidi ni ngómbe wake.

WASOMALI
Wake wanne,
Hana mpenzi,
Anachokipenda zaidi ni miraa.

Sunday, September 6, 2009

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU:- JUMAPILI NJEMA

Furaha na tabasamu ni tiba ya maradhi yanayomsonga mwanadamu. Aidha, furaha huonyesha uhai.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

Saturday, September 5, 2009

GEOGRAFIA YA LEO, TWENDENI PAMOJA NAMI KATIKA MKOA WA IRINGA:- WABENA


Mkoa a Iringa
Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Njombe. Mwaka 2001 idadi ya Wabena ilikadiriwa kuwa 670,000 [1].

Lugha yao ni Kibena. Kutokana na tahariri ya Dr. Kilemile (2009), Kibena ni lugha tajiri sana kwa maneno na ni pana sana ikiwa na lahaja kuu tano: Ki-Kilavwugi (Maeneo ya Ilembula); Kisovi (Kuanzia Lusisi hadi Makambako), Kimaswamu (Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu), Ki-Lupembe (Lupembe)na Kimavemba (Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi ambayo si ya Maswamu).

Lugha ni moja tu; tofauti ni ndogondogo, zikitokana na matamshi, mfano kukaza "dz", kwa lahaja zote isipokuwa Kikilavwugi ambacho ingawa inaandikwa "dzi" inatamkwa kama "dji" umuhudji; na Kilupembe inaandikwa "dzi" lakini watumiaji wanatamka kama "chi" umuhuchi, achile - amekuja, wakati "adjile" (Kikilawugi)... Wengine wote wanakaza adzile, umuhudzi. Tofauti nyingine ni ya kutumia k na h. Mfano: Kamwene/ Hamwene, Kangi?hangi, ukukulima/uhulima n.k.

Suala lingine ni tofauti ya baadhi ya maneno mfano: Asubuhi: Lwamilawu/palukela; Kuketi: kwikala/hwikala/ kutama; Chuma mboga: hukova/kukova imboga na huyava/kuyava imboga; Zizi la Ng'ombe: Ligoma na livaga; nyumbani: hukaye na hunyumba; habari za kazi: mwidaliha na madzengo nk.

Kamusi inatakiwa kujumuisha maneno yote yanayohitilafiana na kudokeza yanakotumika. Maana kamusi ni kihenge cha lugha. Hivyo kuita kamusi yale maneno machache ya Kibena aliyoorodhesha Dr. Joshua ni dhihaka kwa lugha hii ambayo ni tajiri mno kwa misamiati.

Kwa mfano neno kupiga tu lina maneno zaidi ya 100 yakionyesha huyo aliyepigwa amepigwa wapi na ku-suggest hali yake baada ya kupigwa. Pia huashiria hali ya mpigaji. Mfano: (tumia) "k" au "h" kutokana na eneo unalotoka: hutova(general) lakini: hupafula (kiganja), hupefula (nyuma ya kiganja), hututa, hukinya, hung'ilula; hung'alula, hutununa, huwindula, hupwinda, hupana,hulibinga, hufidula, hutadisa, hugong'ola, huniabula, hukinya, huhudugula, huniesa n.k. Habari kutoka sw.wikipedia.org.

Friday, September 4, 2009

ENZI HIZO....MWAKA 1947 WAKATI WA UJANA WANGUUUUUU!!!!


Leo nimeikumbuka picha hii wakati naishi kule Lundo- Nyasa kila siku kumenya mihogo si mnajua ugali wa mihogo na samaki kila siku. IJUMAA NJEMA JAMANI.

Thursday, September 3, 2009

MADAWA YA KULEVYA NA UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KATIKA MAISHA

Duniani wote tunapenda sana kijisikia vizuri. Tunataka kujisikia kuwa na raha, wenye nguvu na sio kuwa na wasiwasi. Hivyo wengi wetu tunaanza kufikiria kuwa dawa za kulevya, pombe na sigara zitatupa raha. Angalia sana! usidanganyike! kutumia vitu hivyo ili kupata furaha bali ni kuhatarisha maisha kwani unaweza kujikuta umeingia ulevini. Kujinasua kwenye hali hiyo itakuwa kasheshe kwelikweli (si lelemama) inahitaji moyo na pia kujizatiti.

Halafu nimefanya utafiti kidogo kupita katika mashule nimeona ni asilimia kubwa wavutao sigara ni wasichana yaani hapa nazungumzia watoto wa shule za misingi. Na ukizingatia watoto hao si zaidi ya miaka 16. Yaani ni watoto wadogo pia wanakunywa pombe. Sijui watakapofikia mia 30 maisha yao yatakuwa ya aina gani. Nimejaribu kujiuliza wanapata nini katika kufanya hivi lakini sijapata jibu naomba tujadili pamoja ndugu zanguni.

Leo nimejisikia kuandika kwa kiswidi pia ili nao wafurahi:

LIVSSTILS HOT:-

Tobak är gift för kroppenRökning är extremt skadlig och ökar risken för cancer, sjukdomar i luftvägarna, hjärt-kärlsjukdomar, typ 2- diabetes, magsår, benskörhet, nedsatt fruktsamhet och dålig sårläkning. Tobaksrök innehåller över 4000 olika ämne, varav många är giftiga - till exempel koloxid och nikotin - medan en del är tjärämnen och andra partiklar som sätter sig i luftvägarna.

Alkohol ger organskadorAlkohol i en mängd överstigande 15ml ren alkohol per dag är skadlig för bukspottkörtel, tarm, lever samt nervcellerna i hjärnan och andra ställen i kroppen. Organskadorna kan leda till dåligt upptag av vitaminer och mineraler, viliket i sig påverkar hälsan negativt. Alkoholens skadeverkningar beror på att det är ett lösningsmedel som irriterar cellerna och belastar leve.

Wednesday, September 2, 2009

HII MLIWAHI KUISIKIA? - MKE NA MUMEWE

Kulikuwa na njemba moja imeowa ,tatizo la njemba huyo ni kukojoa kitandani kila siku ,hatimae mke ustaarabu na uvumilivu ukamshinda ,na siku moja akaamua kumkoromea mumewe kuwa ,kazi ya kufua mashuka na kuanika godoro kila siku itamshinda na anaona aibu maana majirabu wameanza kuhoji mbona kila siku kunafuliwa mashuka na kama haitoshi hata yeye mikono imeanza kuota masuguru na kuchunika kwa tindikali ya kojo lake.

Sasa akamuweka kiti moto mumewe na kumwambia kuwa leo ni siku ya mwisho na ikiwa usiku wa leo atakojoa kitandani basi itakuwa ndio mwisho wa wao kuwa mke na mume kila mtu atashika njia yake na kwa ufupi ndio atakuwa ameachika.

Kwa kweli siku ile njema yule alipata mtihani mkubwa sana na aliona hatima ya ndoa yao inafikia mwisho au ipo ukingoni kabisa.

Kwa bahati usingizi ukawachukua ilipofika alfajiri ,yule mke kitu cha kwanza alianza kupapasa kuona kama kuna kojo limetapakaa kwenye kitanda ,hakuona kitu na kufikiri kuwa mkwala aliomchimbia mumewe umefanya kazi ,dah kuja kutahamaki anasikia harufu ya mavi na kuona kila kukicha ile harufu inazidi kunukia ndani ya chumba chao ,kutahamaki kumbe mumewe siku ile hakukojoa amekunya.

Yule mke akili ikamzunguluka na kuona ya leo ni mpya tena ya aina yake ,ikabidi atulie na kumwita mumewe kwa upole kabisa kabisa huku akionekana mwenye kumshangaa na siejua la kufanya ,haya mume wangu embu nieleze hii ya leo ni ipi maana mtu mzima wewe sasa unaniletea miujiza ?

Yule njemba akamwambia mkewe ,kwanza akataka msamaha na kumwambia kila alalapo inapofika usiku wa manane humjia mtu usingizini na kumuamrisha akojoe kitandani au sivyo atamuua ,ila usiku wa kuamkia leo alipokuja kuja nikampa ile issue na mkataba wako ,hata hivyo haikuwa salama akaniamrisha nifanye kitendo mbadala ,ninye au sivyo atanitoa roho ,nikaona bora ya hivyo kuliko kutolewa roho ,nisamehe mke wangu sio lengo langu ila ni maswaibu ambayo yapo nje ya uwezo wangu ,yule mke kusikia hivyo aliangua kilio haijulikani kwa nini.
Habari hii nimeipata Jamii forum.

Inafanana:-

Nilipokuwa naisoma habari hii nikakumbuka habari moja ambayo inayofanana na moja ambayo niliishuhudia, walikuwa ma jirani zangu wakati naishi Matetereka - Madaba. Mumewe alikuwa kikojozi na akawa anasingizia watoto ndio wanaokojoa. Ndani mlikuwa hamkaliki kwani halafu ilikuwa kali mno. Na hali ya kule Ubenani kulikuwa na ubaridi kila wakati kwa hiyo ilikuwa ni vigumu kukausha godoro na mashuka/mablanketi kila siku. Nikaona sio mbaya nikiweka hapa ili tujadili . Karibuni.

Tuesday, September 1, 2009

KILA MTU ANA MILA+ DESTURI PIA UTAMADUNI WAKE

Hapa ni wanawake wakiwa katika pozi ni huko Papua New Guninea.
Na hapa ni wanaume wa huko huko Papua N ew Guninea nao wakiwa kwenye pozi bila wasiwasi.