Monday, August 31, 2015

NIMEKUMBUKA NILIPOKUWA DARASA LA KWANZA NA PILI TULIKUWA TUKIIMBA SANA NYIMBO MOJAWAPO NI HII:- KWAHERI BABA NA MAMA!!!

1. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kusoma huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuandika huko shuleni pamoja na mwalimu.
 
2. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuhesabu huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuchora huko shuleni pamoja na mwalimu.
 
3. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuimba huko shuleni pamoja na mwalimu.
Twaimba sote pamoja pamoja na mwalimu.
JE? NA WEWE NDUGU YANGU KUNA WIMBO UNAUKUMBUKA AMBAO ULÖIKUWA UKIIMBA KILA SIKU?....Kapulya:-) Panapo majaliwa tuonane mwezi ujao!!
 

Sunday, August 30, 2015

BLOGG TA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA IMALIZE JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI KWA WIMBO HUU AHSANTE MUNGU!!


Nawatakieni wote jumapili njema sana na upendo pia baraka za Mungu zitawale ndani ya nyumba zetu pia mioyo yetu....Kapulya wenu!!

Thursday, August 27, 2015

JINSI MALEZI YETU YA UTOTONI YANAVYOWEZA KUATHIRI NDOA ZETU

Habari za leo ndugu zanguni leo nimeamka nikiwa na fikra nyingi sana juu ya jambo hili la malezi yetu ya utotoni yanvyoweza kuathiri ndoa...Naanza na mfano huu:-  Patrick na Maria  ni mke na mume, kila mmoja amelelewa malezi tofauti.
Patrick alisema  tangu nakua au napata akili, nilizoea kumuona baba akirudi nyumbani muda wowote anaotaka na sijawahi kusikia ugomvi wowote toka kwa mama kuhusu kuchelewa huko.
Kwenye akili yangu, nikaamini kwamba, kumbe mwanamme anaweza kurudi muda wowote nyumbani hata kama ni usiku wa manane. Pia niliwahi kumsikia mzee mmoja akimwambia mzee mwenzake ambaye alikuwa anaomba amruhusu aondoke ili awahi nyumbani.... alimwambia hivi.... wewe ni mwanamme bwana, unawahi nyumbani kufanya nini? Au unaenda kupika? Maneno haya yalimuumiza sana mzee yule na mwisho aliamua kubaki wakaendelea kunywa pombe yao taratibu huku akimshukuru kwa ushauri wake mzuri.
Maneno haya yakazidi kumfanya Patrick aamini kwamba kumbe mwanamme hapaswi kurudi mapema nyumbani, alianza kuwaza na kujisemea kimoyomoyo,  na mimi  nikioa nitakuwa nafanya hivyohivyo kwani huo ndio uanaume.
Kwa upande wa pili, Maria  mke wangu kakulia kwenye familia ya mzee Mapunda ambayo baba alikuwa anarudi mapema sana nyumbani, na binti Maria  akaamini kwamba kumbe mwanamme anapaswa awahi kurudi nyumbani. Hajawahi kusikia ugomvi wowote kutoka kwa baba na mama yake.
Watu hawa wawili ambao wamekulia malezi tofauti wakaoana, wakawa mke na mume.
Siku za mwanzo bwana Patrick  alikuwa anawahi kurudi nyumbani kama ilivyo ada ya mapenzi mapya. Ndoa ilikuwa na furaha kubwa sana
Baada ya miezi miwili kupita, mume akaanza kuchelewa kurudi nyumbani kitendohiki  kilimuumiza sana bi Maria , akahisi mume wake kapata mchepuko ( mwanamke wa nje), ugomvi ukachukua mkondo wake, bi Maria akaanza kumnyima unyumba mume wake, akatumia tendo kama silaha ya kumwathibu mumewe, furaha iliyokuwepo kwenye ndoa hii ikayeyuka ghafla, paradiso iliyokuwepo ndani ya ndoa hii ikageuka na kuwa jehanamu, ikabaki historia, ikawa asubuhi ikawa jioni, maisha yakaendelea.
Mume akazidisha kuchelewa, hamu ya mapenzi ikampanda, akaamua kutafuta mwanamke wa pembeni ili apozee hamu zake.
Siku moja wanandoa hawa wakaamua kwenda kupata ushauri kwa mtaalamu wa masuala ya ndoa. Baada ya kuwasikiliza akawaeleza kwa kina namna jinsi malezi yao utotoni yalivyopelekea kuharibu ndoa yao. Akawapa mtihani wachague, wafuate malezi ya mke au mume? Kwa kuwa mume alikuwa akimpenda sana mkewe akashauri wafuate malezi ya mke ya yeye kuwahi nyumbani mapema.
Huwezi amini sasa hivi ndoa ya bi Maria na bwana Patrick ina amani na furaha maradufu ukilinganisha na wakati wanaoana.
Hebu na wewe jiulize kwenye ndoa yako, kwa nini huelewani na mwenzi wako?

Tuesday, August 25, 2015

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HUU UWE UJUMBE WA LEO!!

KATIKA MAISHA NI BUSARA KUJITATULIA MATATIZO YAKO!
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!

Monday, August 24, 2015

KARIBUNI TUJUMUIKE: UNAKUMBUKA ENZI HIZOOO UTOTONI HASA KWENYE MSOSI???

Chakula tayari ni watu wanakosekana kuushambulia msosi huu mtamu...Mimi hapo hizo dagaa ndo natamani kwelikweli-------Kapulya !

Saturday, August 22, 2015

PICHA YA WIKI: AMA KWELI UKITAKA KUPENDEZA LAZIMA MAUMIVU YAWE.....

Huu ni ubunifu mpya ambao mimi sijawahi kuusikia wala kuutumia. Je wewe umewahi? Basi nikutakieni mwisho wa juma mwema. Panapo majaliwa tutaonana tena. Kapulya wenu:-)

Wednesday, August 19, 2015

HILI NI CHAGUA LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO :- PICHA YA WIKI!!

Pamona na kusema YOTE NJAA:- Lakini pia ndio ujasiriamali hapa anaonekana kama vile kweli yote ni njaa lakini kesho mna kesho kutwa atakuwa mtu mwingine. Ndivyo inavyotakiwa, kupata MAFANIKIO taratibu na sio kuamka tu na kupata.

Monday, August 17, 2015

KUMBUKUMBU:- LEO NI MIAKA KUMI NA MOJA (11) KAMILI TANGU MAMA YETU ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

MAMA! ANAWEZA KUCHUKUA  NAFASI ZA WENGINE LAKINI NAFASI YAKE HAIWEZI KUCHUKULIWA NA YEYOTE YULE
 
KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka kumi na moja  sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana, sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

Friday, August 14, 2015

Wednesday, August 12, 2015

MAISHA NA JAMII:- ZITAMBUE SIFA SITA ZA MSINGI ZA MWANAMKE ALIYE MKE BORA!

Mithali 14:1 "Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake,bali aliye mpumbavu
huibomoa kwa mikono yake."

Kuna mithali isemayo "MAJUTO NI MJUKUU", ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na
kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo
mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu
aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa zamwanamke mwenye hekima pia soma mithali 31:10-31.

-Hufumbua kinywachake kwa hekima, na sheria ya wema katika ulimi wake huwashauri wengine kwa ukarimu mithali (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi / ukali,maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na wanamke ni kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni mbaya.

-Hufanya kazi kwa moyo na huamka alfajiri na mapema.Kuna wanawake ambao ni wavivu
kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana
kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaibu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya
kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haitachelewa mwanaume kulipa fadhili kwa wema
anaotendewa.

-Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake.
Kuna wanawake ambao ni wachafu/ usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala
ni stoo ya nepi za mkojo na nguo chafu,wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti
mwanamke awe msafi muda wote, Wanaume wote wanapenda usafi,marashi hata ya mchina
yasikose,mwanamke hakikisha "Reception" inakuwa safi na kuwa katika hali ya kumfanya mume
ajisikie kujipumzisha kwa raha mustarehe.

-Jali na timiza mahitaji ya NDOA kwa mume wako.
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa
swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki

nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI”  utafikiri ni askari anaendavitani. Wanaume
ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungwa, Fanya makosa
yote lakiniusijefanya  ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa,  hilo ni kosa la
jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za
Mungu.

-Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho famiia itafurahi.
wanawake wengi hasa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaumewengi wanaishia kula
hotelini au kwa mama ntilie, kama umetokabara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga nazi kwa chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, Wanaume wanapenda chakula  chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.

-Mwamini mume wako, wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa
mashoga au ndugu zako.

Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo”.
CHANZO: GAZETI LA MWENGE TOLEO LA JANUARI 2015

Monday, August 10, 2015

TUANZA JUMA HILI NA PICHA HII:- UTALII UNA CHANGAMOTO ZAKE .....

Sasa hapa kweli atapona huyu maana Mbuni ni myama/ndge ambaye anakimbia sana kuliko wanyama/ndege wote duniani...MMMhhhhh hapa kazi kwelikweli...Kapulya

Saturday, August 8, 2015

UJUMBE WA LEO

Ilikuwa ni majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo mzee mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 aliingia katika
hospitali moja ili kusafisha kidonda chake cha mguuni.
Mzee akaanza kwa kuomba afanyiwe haraka kwa kuwa alikuwa na appointiment
ya muhimu sana ifikapo saa tatu kamili ya asubuhi hivyo afanyiwe msaada wa
huduma ya haraka.
Daktari mmoja akaguswa na mzee yule baada ya kuona kila mara akiingalia saa yake na kutikisa kichwa cha kukatishwa tamaa na kuamua kumhudumia kwani alijua ingechukua zaidi ya saa kabla ya
mzee kuhudumiwa kutokana na idadi
kubwa ya watu kwa kuwa yeye hakuwa na
mgonjwa wa kumhudumia wakati huo.
Baada ya uchunguzi wa kidonda chake
kikaonyesha kuwa kimepona na daktari
akaanza kukifungua akishirikiana na nesi
kukisafisha. Wakiwa wanaendelea kukisafisha
kidonda daktari na mzee wakaanza mazungumzo na daktari akamuuliza kama mzee alikuwa na apolintiment na daktari mwingine kwa jinsi alivyokuwa na haraka.
Mzee akajibu hapana, ila natakiwa kuwahi kwenda kunywa chai na mke wangu
ambaye amelazwa kwenye kituo cha kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya ubongo .
Mzee akaendelea kumwambia daktari
kuwa mkewe amelazwa pale kwa zaidi ya
miaka miwili akitibiwa maradhi hayo na hana kumbukumbu kabisa
 Daktari akauliza sasa kama kapoteza kumbukumbu atakumbuka kama umechelewa?

Mzee akamjibu daktari kuwa mke wangu hajawahi kukumbuka kuwa mimi ni nani au nini kinaendelea kwa zaidi ya miaka hiyo miwili.
Kwa mshangao daktari akamuuliza, "Na umekuwa ukiendelea kwenda kunywa
naye chai kwa miaka yote hiyo kila siku asubuhi hata kama amekusahau wewe ni
nani?"
Mzee alitabasamu na kuushika mkono wa
daktari na kumwambia "hanifahamu tena
mimi, ila mimi bado namfahamu ni nani
kwangu na umuhimu wake kwangu"
Daktari alifuta machozi huku akimtazama
mzee yule akiondoka kulekea kwa mkewe
kunywa chai kabla ya saa tatu kamili.
Daktari alijishika mikono yake kichwani na kusema, "Hii ndio aina ya mapenzi
ninayoyataka katika maisha yangu"
Upendo wa kweli hauko kwenye mwonekano wa mtu au mapenzi. Mapenzi
ya kweli ni kukubaliana na hali zote zilizopo, zitakazotokea na ambazo
hazitatokea pia.
Kama umeguswa na kisa hiki tafadhali
CHANZO:- NIMETUMIWA NA RAFIKI

Thursday, August 6, 2015

UJUMBE WA JIONI YA LEO TOKA KWANGU KUJA KWENU

Maisha  ni mtihani Mkubwa na tofauti. Watu wengi huwa wanafeli kwa sababu wanajaribu kuiga maisha ya wengine, bila kujua ya kwamba kila mmoja ana swali lake tofauti.