Tuesday, December 20, 2022

UJUMBE WA JIONI YA LEO

Binadamu hataki kuwa alivyo. Isipokuwa anafikiri angekuwa binadamu wa aina gani! NAWATAKIENI JIONI YENYE AMANI NA FURAHA!

Saturday, August 20, 2022

TUMAZE WIKI NA UJUMBE HUU!

NIMETUMIWA HUU UJUMBE NIMEONA NISIWE MCHOYO WA ELIMU:- Nyoka uliyembeba kwenye mzigo wa kuni kutoka shambani anaweza kukuumia nyumbani wakati unatua mzigo. Siyo kila unayemsaidia lazima akusaidie, wengine inabidi wakuumize ili ujifunze. Kuna watu wanajifunza vizuri baada ya kuumizwa. Kwa hiyo katika maisha tunahitaji watu wote; wazuri na wabaya. Wazuri watakupa furaha, wabaya watakupa uzoefu ndiyo maana imeandikwa mpende adui yako, ila angalia asikuue, maana ukifa hutojifunza kitu! Imeandikwa na Mwl. Denis Mpagaze.

HAYA NDIYO MATOKEO: UTAKULA ULICHOPANDA NA HII NDIYO KAZI YA MIKONO YANGU

TUNAKULA NYANYA ZETU MPAKA KUSAZA....

Monday, April 25, 2022

NAPENDA KUWATAKIENI MWANZO MWEMA WA WIKI NDUGU ZANGU!

NIMEYAPENDA HAYA MAZINGIRA KWA KWELI YAONEKANA NI SEHEMU NZURI NA YA UTULIVU.

Thursday, April 14, 2022

TANZIA:_ NIMEFIWA NA MAMA YANGU MDOGO HUKO MBEYA LEO MCHANA

Mama tulikupendda sana ila Baba wa Mbinguni kakupenda zaidi. Pumzika kwa amani mama yangu

Wednesday, January 26, 2022