Showing posts with label maisha ya ndoa. Show all posts
Showing posts with label maisha ya ndoa. Show all posts

Tuesday, June 2, 2015

MAISHA YA NDOA!!

Sijui nahitaji miwani au? maana naona hawa walitakiwa kuwa shule..Duh kuanza maisha ya ndo mapema hivi....

Monday, October 6, 2014

TUANZA WIKI NA PICHA HII:-MAPENDO!

Kuna wakati mtu ukipenda hakuna awezaye kusema kitu ..maana kupenda ni kupenda. Nawatakieni wote jumatatu njema.

Wednesday, July 2, 2014

PALE INAPOTOKEA KUPEANA HABARI KUNAPOKOSEKANA NA PALE PANAPOKUWEPO KUPEANA HABARI KWA WANANDOA....

MAISHA YA NDOA YA YOSEFU NA PAULINA...
Walikuwa katika hali ya uchumba kwa mwaka mzima sasa. Kwa muda wa miezi sita walikuwa wakionana karibu kila siku. Lakini baada ya hapa, Yosefu aliondoka kwenda kutafuta kazi nzuri. Mwanzoni alimwandikia barua Paulina mara kwa mara. Lakini muda kidogo, barua zilianza kupungua na zile alizopata Paulina hazikuwa na maneno ambayo alitazamia yawemo. Yusefu aliongelea machache sana kuhusu maisha ya mjini, na alisema kidogo tu kuhusu kazi yake mpya na rafiki zake wa huko.
Paulina alianza kupatwa na wasiwasi, kwa kweli wasiwasi mwingi. Lakini hakumwambia Yosefu. Mwanzoni alikuwa anamwandikia juu ya yale mambo aliyopenda na Yosefu ni mzima na angelikuja kumwona hivi karibuni. Lakini mara aliacha kutaja mambo haya. Aliongea tu juu ya mambo ya kijijini na matukio yaliyotukia hivi karubuni katika parokia yao. Zaidi kuhusu mwenyewe hakusema tena.
Kadri miezi ilivyopita ndivyo moyo wake ulivyozidi kujawa na uchungu na bumbuwazi. Angewezaje kuzungumza juu ya mambo yake binfsi kama Yosefu alikuwa hatilii maanani mambo haya? Bada ya miezi sita Yosefu alirudi nyumbani kwa likizo la majuma matatu. Alishangazwa na hata kushtuka kuona jinsi Paulina alivyokuwa hamjali.






























Wazo na swali kutoka kwa Kapulya wenu:- "Na ndio maana kupeana habari ni muhimu kwani mwenzio hawezi kujua wewe unawaza nini na wewe huwezi kujua wenzio anawaza nini.
Na sasa hata  Yosefu anausikitikia mwenendo wa Paulina. Je? watafanya nini?...unfikiri ikiwa wataongelea waziwazi juu ya tatizo lao mapenzi yao yaweza kufufuka?  "  Halafu leo ni tarehe ambayo nilifunga pingu za maisha na baba watoto:-)

CHANZO :- KITABU NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA

Monday, April 28, 2014

KUFUJWA KWENYE NDOA NI NINI?

Ni wiki nyingine na Jumatatu nyingine tena ya mwisho kwa mwizi huu wa nne! Nimeamka nikiwa na mawazo mawazo basi nikachukua kitabu hiki na kusoma. Kitabu chenyewe kinaitwa MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA. Kilichoandikwa na Munga Tahenan... nikafananisha na wimbo ule wa Remmy Ongala usemao nilidhani nimepata kumbe nimepatikana.... bahati mbaya sijaupata wimbo wenyewe....Habari yenyewe inasomeka hivi:- Karibuni tujadili pamoja.

Ifuatayo ni habari ya mwanamke ambaye aliwahi kuja kwangu kwa ushauri kuhusu ndoa yake: Mama Kotilda Mkataha aliolewa mwaka 1980 na mume msomi aliyekuwa na wadhifa mkubwa kwenye taasisi moja ya fedha ya serikali.

Ndoa hii ilifungwa kwa sababu, Kotlida hakuwa na njia, lakini anasema, tangu wakiwa kwenye uchumba, alikuwa tayari na wasiwasi kama ndoa yao ingekuwa ni ya amani. Anasema, wakati bado wachumba, huyo bwana aliwahi kumpiga kibao kwenye kituo cha UDA kwa kosa la kuchelewa kufika kituoni kama walivyokuwa wamekubaliana.
Ndoa ilikuwa ni ya mateso makubwa hata kabla haijafungwa. Mwezi mmoja baada ya ndoa, Mume alimachisha mkewe kazi kwa kwenda kufanya fujo ofisini kwa bosi wake kwa madai kuwa bosi huyo alikuwa na uhusiano na mkewe. Kotlida alianza kuishi kwa mashrti. Hakuna kutoka, hata kwenda kwa jirani bila kuomba ruhusu na kutoa maelezo marefu kwa nini aende huko.
Kusimangwa, kukosolewa, kuitwa mjinga na mbumbumbu, ikaanza kuwa sehemu ya maisha ya mama huyu, Hali iliendelea hivi na Kotlida akawa anajiambia, kuna siku hali itabadilika. Lakini. kwa bahati mbaya, hali haikubadilika. Wakati anakuja kwangu, alikuwa ameshaanza kuamini kwamba, huenda ni kweli alikuwa anastahili kutendewa vile na mumewe.
Huku ndiko tunakoita kufujwa. Mpenzi mmoja anapomuumiza mwingine kwa kauli zake au limwili, mara kwa mara, tunasema hapo kuna kufujana.
Mpenzi mmoja anapokuwa na mamlaka aliyojipa dhidi ya uhuru na haki ya mwenzake, tunasema hapo imekuwa kufujana. Mara nyingi, wanaofuja ni wanaume. Miongoni mwa matatizo ya ndoa ambayo mtu hashauriwi kuendelea kuyavumulia ni kufujwa. Ndani ya kufujwa kuna maumivu makubwa ya hisia na mwili.
Ni vizuri hata hivyo, nikasema kwamba, neno kufuja ni jinsi ya kuelezea hali hii, ambapo mtu mwingine angeweza kuita matesa katika ndoa, kuonewa katika ndoa au kutumia istilahi yoyote.

Swali langu:- Kwanini alipoona mambo yanazidi hakuondoka?

Tuesday, March 11, 2014

MAISHA YA NDOA:- KWA NINI NIMEMWOA?

LEO NIMEAMKIA KUSOMA SOMA KATIKA MOJA YA HABARI NILIZOSOMA NI HII NIKAONA NIWASHIRIKISHE PIA. NI KUTOKA KATIKA KITABU:- NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA. KARIBUNI......
Vincent na Regina walikuwa wa kabila moja. Na walikuwa wamesoma shule moja. Vincent alikuwa amemaliza darasa la 5 lakini ilimbidi kuacha kwa sababu hakuwa na mtu wa kumlipia karo/ada za shule. Regina naye alipaswwa kuachia darasa la 3. Wazazi wake, kama vile wazazi wa Vincent, walikuwa wakulima. Lakini kwa sababu ya uhaba wa mvua kwa miaka kadhaa iliyoopita, wazazi wake walipaswa kuhamia mahali pabaya pasipokuwa na shule karibu.
Vincent alijiunga na baba yake shambani. Regina, baada ya miaka kadhaa alikwenda kufanya kazi kwa wazungu fulani katika mji wa karibu. Alikuwa yaya. Waajiri wake walikuwa wakarimu kwake na mara nyingi walimpa vitu vingi vizuri. Kila wiki alipokea mshahara wake lakini mara nyingi zaidi yeye aliutumia mara tu alipoupokea.
Siku ya soko kila wiki, Vincent alizoea kwenda mjini na bidhaa za kuuza. Lakini kila mara alihakikisha kwamba amemwona Regina kabla ya kurudi nyumbani. Bila shaka siku nyingine Regina alipaswa kufanya hiki  na kile, hivyo hakuweza kuondoka na kufika sokoni. Siku hizo, Vincent alirudi nyumbani akisemasema manenoo yasiyosikika, hivyo mara nyingi wazazi wake walijiuliza ikiwa Vincent ni mgonjwa?
Mwishowe, Vincent na Regina walioana. Vincent alikuwa amejenga nyumba mpya nzuri kwa ajili yao wawili. Mwanzoni kila kitu kilionekana chema kabisa. Ni kweli kwamba mara kwa mara Vincent alikuwa na wasiwasi juu ya Regina. Alijua kwamba Regina alikuwa amejifunza mitindo ya kigeni kwa wale wazungu katika nyumba ile kubwa. Basi, alijisemea kwamba baada ya muda Regina atayasahau kabisa hayo yote na kuwa mmoja wao tena.
Lakini Regina hakuweza kusahau. Alikumbuka vyakula vizuri, sahani na vikombe vizuri, viti n.k. Yeye hatakuwa kamwe na nyumba ya namna hiyo. Polepole alianza kubadili mwenendo wake kwa Vincent. Alikuwa mkimya kabisa, lakini pengine ukimya wake ulibadilika hata ukamfanya afadhaike na kukasirika kwa sababu ya jambo alilosema au alilofanya Vincent.
Kadiri alivyokasirika zaidi, ndivyo alivyojitahidi kumpendeza zaidi. Hakusema chochote aliporudi nyumbani toka shambani akiwa amechoka na kusikia njaa na kukuta chakula hakijawa tayari. Alikumbuka vema aibu aliyopata siku ile ambayo baba na mama waliwatembelea, na Regina akagoma kuwapikia chakula. Usiku, walipokuwa wameondoka, alimpiga Regina, ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kufanya hivyo.
Toka siku hiyo mambo yalizidi kuwa mabaya. Regina aliishi katika nyumba kwa ukimya wa kitoto. Alimjibu Vincent kwa kuguna kila alipomwuliza swali. Hata mara nyingine alikataa kulala na Vincent mpaka naye aahidi kumtendea tendo fulani. Vincent maskini! Hakujua la kufanya. Mara nyingi sana alijisemea: "Maisha ya mjini yamemharibu, kabla yake hakuwa hivi". Alisema kwa sauti ndogo:- "Kwa nini nimemwoa?
Alizidi kutumaini kwamba Regina atabadilika. Miaka ilivyopita Mungu aliwajalia watoto wawili, mvulana na msichana. Hizi zilikuwa ndizo siku njema, wakati kila kitu kilipoonekana kinakwenda sawa tena. Regina alionekana kuwa mtu ambaye Vincent amemtumaini kuwa naye. Lakini jambo fulani likitokea basi, Regina alikuwa anabadilika upesi. Alikuwa anakataa kufagia nyumba, au kupika chakula au hata kuwatunza watoto kwa ujumla.
Wakati kama huu, Vincent alikuwa anajiuliza tena na tena:- "Kwa nini nimemwoa?
Je? hapa wa kumlaumu ni nani na wa kumsikitikia ni nani?
KILA LA KHERI...PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!!

Wednesday, February 5, 2014

INAHUZUNISHA LAKINI KUNA FUNDISHO KUU KWA WOTE!!

Katika mizunguko yako nimekutana na habari hii ambayo ni kusikitisha lakini pia ni kumpa mtu mafunzo mazuri sana. Ungana nami ….

---------------------------------------------------------------------------------------



Ndugu zangu wapendwa!
Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote. “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha ana umizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake. Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauté ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu Sali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu?. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa Jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali, kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwaMary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu! Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande. Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu. Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika nakuwa jambo la hakika zaidi. Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary. Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali Kabila nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa
kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwatatizo kwangu,nilikubali mango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu. Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana nakupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba. Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya utur aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mkewangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe!Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi. Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi. Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... Mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mkewangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono Wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia Mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka. Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu nakumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua....nikapanda ngazi. Mary alifungua mango nikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu
sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mkewangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu nakuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kilo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu Kuba usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani. Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao Mungu awabariki na awe nanyi nyote mliosoma nakujifunza hapa
NAWATAKIENI JUMATANO NJEMA SANA…

Wednesday, January 15, 2014

WANAWAKE NA HISIA ZA USALITI: ZIJUE DALILI ZAKE!!

Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!) Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibuna kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsiatakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengi wafaidike na ELIMU hii.

Thursday, November 28, 2013

MAISHA YA NDOA:- NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI/MFANYAKAZI MWENZANGU!!!!

AKIWA MAWAZONI
Habari za leo Yasinta, ni siku nyingi hatujaonana. U- hali gani? Vipi familia ni wazima wa afya?  Nikamjibu, salama tu na familia wote wazima. Sijui wewe na familia yako? Akaguna...mmmhhh! Sina uhakika, sijisikii vizuri niko katika mawazo mengi. Sijisikii raha kabisa kuwa na mume wangu. Lakini ni ajabu kwa kuwa huwa hawi nyumbani muda wote. Anafanyia kazi zake mbali kidogo anaweza akawa hayupo nasi wiki moja au mbili. Kwa hiyo ilibidi nimfurahie/tufurahiane arudipo lakini ni kinyume. Yasinta, mimi bado kijana..38 na yeye 35, nipo njia panda, sifurahii maisha niliyo nayo. Pia mwenzangu naye haonyeshi kama ananijali.  Nifanye nini? Nisaidie?
Duh! Hapo Kapulya akabaki hoi maana ushauri wangu.....si wa kiataalamu wa mambo ya ndoa. Nikakumbuka Maisha na Mafanikio, kuwa nikiweka hapa kwa pamoja tutaweza kumsaidia rafiki yangu. Na ndio maana nawaombeni tujadili kwa pamoja.  Kwani kesho laweza kukupata wewe au mimi au yule n.k. Nawatakieni kila la kheri na mjadala mwema. SIKU IWE NJEMA......Kapulya

Wednesday, August 28, 2013

PALE WAZAZI WANAPOWACHAGULIA WOTOTO/MABINTI ZAO WACHUMBA!!!

Habari za jioni ndugu zanguni....Hivi karibuni nimetumiwa email kutoka kwa msomaji wa maisha na mafanikio kutoka huko nyumbani Tanzania ikiwa na ujumbe huu na kuniomba kama naweza niuweka hapa kibarazani ...karibu tujadili kwa pamoja
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuna mdada mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wasomi sana. Amemaliza chuo hapa mlimani. Wakati alipokuwa chuoni alibahatika kupata mchumba ambaye walikubaliana kuoana. Na walikuwa katika maelewano mazuri katika uchumba waoi.

Baada ya uchumba huo kuendelea, aliamua kumpeleka kwa wazazi wake na kuwafahamusha kuwa mimi nimepata mtu ambaye naona atanifaa katika maisha yangu. Baada ya kuwafahamisha jambo hili, mama dada huyo alikubaliana na wazo lake la kutaka kuolewa na huyo mchumba wake lakini upande wa baba yake kulikuwa na shaka. Huyo binti alikuwa karibu sana na baba yake na aligundua kuwa baba yake hataki kukubaliana na wazo lake. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mvulani yule kuondoka, binti alimfuata baba na kuzungumza naye na akasema kwa jinsi nilivyomwona huyo mvulana hakufai. Binti akamwambia si vizuri kumhukumu mtu kwa kumwangalia tu. Mimi nimekuwa naye muda mrefu namfahamu vizuri sina shaka naye. Baba yake bado hakukubalina na hilo lakini upande wa mama yake hakukuwa na shida.

Uchumba uliendelea na yule mvulana akasema inaonyesha baba yako hataki kabisha, lakini nitaumia sana endapo kama bado ataendelea na msimamo wake huo. Ni mtu ambaye nimekuzoea, tumeheshimiana sana. Yule binti akamwambia kila kitu kinawezekana na itawezekana tu.

Siku moja yule binti akiwa katika mizunguko yake ya hapa na pale akiwa mjini, alikutana na kaka mmoja akiwa katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa na mwonekano mzuri sana, lakini cha kushangaza yule kaka baada ya kumwona binti yule aliduwaa. Baada ya kuduwaa kwa kipindi aliamua kumfuata binti na kumsalimia na kumuuliza kila kitu, na baadaye walianza kuwasiliana mawasiliano ya kawaida kabisa lakini mwanajeshi huyo alikuwa na mawazo tofauti, na ndipo siku moja akamweleza kuwa angetamani siku moja awe mke wake. Yule binti akamwambia hapana, mimi tayari nina mtu wangu na tunaheshimiana sana, akamwambia sawa. Kwa vile  ni watu marafiki alimrudisha mpaka kwao, kumbe lengo lake yule kijana ni kutaka kujua binti anaishi wapi.
Na ndipo siku hiyo yule kijana aliamua kwenda peke yake nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kukutana na baba yake (Baba wa binti). Na ndipo alipozumza ukweli wa kile alichokiona na lengo lake ni lipi. Na mzee aliweza kumdadisi kijana na kumweleza kila kitu. Kwa  wakati huo yule binti pamoja na mama yake walikuwa hawapo na binti aliporudi akamweleza akaelezwa na baba yake kuwa kuna kijana mmoja alikua yuko hivi na hivi akanieleza kila kitu, nadhani huyo ndiye atakayekufaa. Binti akamwambia hapana, wewe ndiye umemwona na mimi itabidi nimwone. Baadaye yule mjeshi akaja wakazungumza.

Baada ya mazungumzo marefu ya hapa na pale yule kijana mjeshi aliamua kuondoka, na kwa kuwa binti hakutaka kukorofishana na baba yake aliamua kukubaliana na mawazo yake na baadaye wakamwita tena kijana huyo mjeshi. Baadaye taratabu zote za kuoana na mjeshi huyo zikafanyika, kisha binti huyo alienda kwa mchumba wake wa kwanza na kumweleza yote yaliyotokea na kumrishia pete ya uchumba waliyovishana hapao awali. Kijana huyo alisikitika sana kwa uamuzi aliouchukua lakini hakuwa na jinsi aliamua kufuata shinikizo la baba yake. Hatimaye baadaye yule binti aliolewa na mwanajeshi na ndoa ilifungwa kanisani.

Baada ya ndoa tu kinachotokea sasa hivi ni kwamba kosa kidogo tu anaambulia kipigo ambacho hajawahi kukipata, kiasi kwamba inampelekea kumkumbuka yule wa kwanza ambaye walikuwa wakiongea naye kwa utaratibu kabisa.

Ndipo baadaye binti (ambaye sasa ni mke wa mwanajeshi) akamtafuta yule mchumba wake wa kwanza na kumweleza kila kilichotokea. Lakini kijana huyo alijaribu kumweleza namna ya kufanya ili waendelee kuishi vizuri na mume wake na kuzidi kumwombea ili waishi vizuri.

Kwa wakati huu kijana huyo bado hajaoa na anamweleza binti itachukua muda mrefu kwa sababu kwanza itabidi nikusahau wewe pili nikae chini nitulie tatu nijianze upya hivyo itachukua muda sana.
Kikubwa zaidi ni kuwa binti huyo amekubali kuolewa na mwanajeshi kwa shinikizo la baba yake, lakini kinachoendelea ni kwamba kosa dogo tu anaambulia kipigo kisicho cha kawaida na kinachomuuma zaidi zaidi huyo dada ni kuwa siku moja walipotoka NJE walienda sehemu ile ile ambayo walikuwa wakienda na mvulana yule wa kwanza na hivyo hii humuuma zaidi.
Sasa dada huyu anaomba mawazo, ushauri na maoni afanyeje???

Thursday, August 22, 2013

SWALI LA WIKI LILILOPENDWA NA KAPULYA...MKE AU MUME NI NANI KWAKO?

Jana jioni/usiku nikiwa kazini nilipata wasaa wa kusikiliza redio ya http://ebonyfm.com  au pia waweza kuingia http://www.radiostationstz.co na kisha bofya EBONY FM (radio ya 6 toka juu. Basi jana kulikuwa na mada- swali moja nzuri sana na kidogo ya kuchanganya...lilisema hivi:- Mke wako ni mke, rafiki au ndugu? na vivyo hivyo kwa Mume je? ni mumeo, rfikiyo au nduguyo?.....Niliipenda sana mada hii ila bahati mbaya nilishindwa kuchangia na nimeona niiweke hapa maisha na mafanikio na tuweze kujadili kwa pamoja.....KARIBUNI SANA

Monday, July 15, 2013

KWA NINI WANAUME WANASHINDWA KULING'AMUA HILI?

Kuna wakati niliwahi kueleza juu ya wanaume kudhani kuwa kuwanunulia wake au wapenzi wao kila kitu kwa maana ya nyumba nzuri, magari ya kifahari na mavazi ya thamani, inatosha kupeleka ujumbe kwa mke au mpenzi wake kuwa anapendwa. Nilieleza kwa kirefu sana juu ya dhana hiyo jinsi isivyo sahihi na niliweka bayana kuwa, wanawake ni viumbe wanaohitaji kusikilizwa kuliko kitu kingine, bila shaka mlio wengi mnakumbuka makala hiyo.

Kwa asili wanaume wanapenda sana kuwasikia wake au wapenzi wao wakikiri kuwa wanawapenda na kufurahia tabia zao nzuri wema walio nao, vipaji walivyo navyo na sifa nyingine lukuki. Wanaume wanapopewa sifa za aina hii na wake au wapenzi wao hufurahia na kupata nguvu na kuona kwamba wana thamani kubwa mbele ya wake au wapenzi wao, kinyume na hivyo wanaume hukerwa na kutowajali wake zao.

Pamoja na kuoneshwa upendo lakini hata hivyo hiyo haitoshi kuwafanya wanaume wawapende na kuwajali wake au wapenzi wao. Kuna wakati mwanaume anakuwa na kazi nyingi sana na anatumia muda mwingi kwenye kujisomea au kuangalia Luninga, hata pale mke au mpenzi wake anaponyesha kwamba anahitaji kuwa naye kwa muda fulani. Kuna wakati pia mwanaume anajali zaidi kazi zake kuliko mambo mengine ambayo mkewe anayataka na kuyaona ya maana.

Naamini wengi mtakuwa ni mashahidi wa kauli hizi, “Yaani niache kazi zangu nikae kukusikiliza wewe na upuuzi wako, subiri nikipata muda tutaongea mambo hayo” kauli hizi ni sumu kali sana katika uhusiano, na huchangia kwa kiasi kikubwa ndoa na mahusiano ya wapenzi wengi kuporomoka.

Ni kweli kuwa kuna wakati mwanaume anaweza kuwa bize na shughuli zake,lakini pale mke au mpenzi wake anapohitaji ukaribu na yeye ni wajibu wake kuonesha kujali.
Kama mwanamke anahitaji kufanya jambo fulani ambalo inabidi mwanaume amsaidie, lakini inapotokea mwanaume kuonyesha kwamba hajali sana juu ya jambo hilo bila kujali kama yuko bize au hayuko bize, mwanamke huhisi kutothaminiwa na hiyo humuumiza sana kihisia. Lakini kama mwanaume ataonesha kujali hisia za mkewe na kumsikiliza kwa makini hata kama hatatoa ushirikiano hiyo tu inatosha kumridhisha mke au mpenzi kuhisi kuwa anapendwa na anasikilizwa.

Lakini utakuta wanaume wengi hawajali utashi wa kihisia wa wake zao na huamini kwamba wanawake wanachohitaji ni kupewa fedha au mali na kuhakikishiwa maisha ya kifahari basi.
Ukweli ni kwamba wanawake wanahitaji sana kusikilizwa hisia zao na kupewa nafasi pekee na mume au mpenzi wake pale anapohitaji nafasi hiyo ya kusikilizwa. Kumuonesha mwanamke kwamba hana thamani na hana nafasi ya kusikilizwa na badala yake kazi na kusoma, au kuangalia luninga kukaonekana ndio kuna thamani kuliko yeye ni kosa kubwa.

Ni jambo la msingi sana kwa wanaume kulifahamu hili kwa ustawi wa ndoa au mahusiano yao na wake au wapenzi wao, kwani wanawake wanahitaji nafasi kutoka kwa wanaume au wapenzi wao zaidi ya kitu kingine, maana hayo mengine yatakuja kujazia tu

Thursday, September 27, 2012

JINSI YA KUPEANA HABARI KATIKA NDOA ZETU!!!

Tunayo methali isemayo:- "Kisima kikinyauka ndipo tu tunapojua thamani ya maji". Ndivyo ilivyo mara nyingi. Wakati kitu fulani kinapokosekana ndipo tunajua umuhimu wake. Tunapokuwa na afya njema, hatumshukuru Mungu kwa kutujalia afya nzuri na mwili wenye nguvu. Tukipatwa na maradhi ndiyo tunatambua kuwa afya njema ni kitu chenye thamani kubwa. Hali kadhalika, tunashindwa kuwashukuru rafiki zetu kwa ajili ya wema wao kwetu, lakini tukijikuta katika hali ya upweke na huzuni, ndipo twatambua jinsi urafiki ulivyo na thamani sana kwetu.
Ndivyo ilivyo kuhusu kupeana habari. Mara nyingi natambua uhuhimu wa kuongea na mwenzangu wakati ambapo tunakuwa tunakosa kuongea pamoja kwa muda fulani. Ndipo tunatambua kile kinachokosekana, tunaona kila kinachotutenganisha. Hapa tunajaribu kuona jinsi hali inavyokuwa wakati ambapo huna uhusiano mwema katika kupeana habari, na pia mambo gani ya kuhuzunisha hutokea wakati uhusiano unapokuwa si mzuri katika kupeana habari au kutopeana habari kabisa kati ya watu wawili.

Ebu tuangalie mfano huu:- John na maria waliishi katika ndoa kwa muda wa miaka miwili. Walipendana lakinai hakuna aliyemwambia mwenzake juu ya jambo hili. Waliamini ya kwamba kwa kawaida watu wawili waliooana wanapendana, sivyo? Lakini Maria alikuwa na mashaka na Joha. Wakati walikwenda kwenye sherehe au sikukuu fulani, John aliwasifu rafiki zake Maria jinsi walivyokwatua na kuvaa malidadi na jinsi walivyosuka nywele zao. Hata mara moja hakumsifia mkewe au kusema neno lolote la namna hiyo. Maria hakuthubutu kumwambia John juu ya jambo hili. Alizidi kukaa kimya. Siku moja, John alimwuliza Maria, Una nini Maria? Unaonekana huna furaha wakati wote, Hakuna kitu chochote, bali nimechoka tu siku hizi, alijibu Maria.
Kumbe, Maria alikuwa anasema uwongo. Alijua kwamba alikuwa hasemi Ukweli. Lakini John hakujua. Baada ya miezi mitatu kulizuka ugomvi kati ya John na Maria kuhusu fedha, na ndipo ukweli ukaonekana. Kwa kweli Maria hakugombana kwa ajili ya fedha hata kidogo ilikuwa tu ni kisingizio kilichotafutwa ili kuanzisha maneno makali. Sababu ya kweli ilikuwa kwamba Maria alihisi kwamba John alikuwa hampendi tena bali mapendo yake yalielekea kwa wanawake wengine. Kitu kidogo; yaani, kuacha kumsifia na kumwonea fahari mkewe ampendaye kweli, sasa kimekuwa kitu kikubwa, yaani Maria amekuwa na mashaka juu ya mapendo ya mumewe kwake. Kupeana habari kati yao kumekosekana na kitendo hiki kikikomaa, mambo madogo hugeuka kuwa makubwa.
chanzo: KITABU CHA NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ujumbe wangu ni kwamba katika ndoa tuwa na MAWASILIANO NI MUHIMU SANA.

Tuesday, September 25, 2012

MAISHA:- EBU CHUKUA MUDA NA USOME HABARI HII....MAISHA YA NDOA /TALAKA AU ???

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio . Nikachukua muda na kusoma kwa kweli lazima niseme habari hii imenisikitisha pia nimejifunza jambo nasikutaka kuwa mchoyo kwa vile aliyenitumia hajawa mchoyo kwangu tunagawana elimu huu ndio msingi. Na ndio nimeona niweke hapa kibarazani ili wengi tujifunze maisha yalilivyo. KARIBUNI MUUNGANE NAMI.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.
Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.
Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.
Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Jane alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.
Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.
Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.
Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Jane alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.
Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….
Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao
Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa.

Tuesday, September 4, 2012

UJUMBE WANGU:-KUTHUBUTU KUONYESHA MAPENZI/UPENDO NDIYO NGUZO YA MAHUSIANO BORA!!

Kuthubutu kuonyesha upendo wako sio tu maneno mazuri, na sio tu upendo wa matendo au maua na chokleti. Ni kuonyeshana heshima, uaminifu na imani. Pia kuonyesha wepesi wa kuona huruma wakati mwenzako anapokuwa na msongo/matatizo. Kuwa msaidizi mwema na mwenye kusema ukweli.
Kuthubutu kuonyuesha masikitiko yako. Sio kila wakati kujifanya mwenye nguvu(mvumilivu).
Tukumbuke kukaa pamoja  na kupeana mawazo ya maisha..ikibidi kuwa watoto ndani yetu.
Tuwe sisi kwa dadika chache. Dakika chache za furaha., dakika chache za huzuni.Tufanye siku iwe ya sherehe.Tushirikiane katika raha na taabu maishani. Tujipe uaminifu. Tukaribiane na ili kuwa pamoja.

Thursday, August 16, 2012

HII KALI NAONA IWE PICHA YA MWAKA:- MWANAUME AFUNGA NDOA KANISANI NA WANAWAKE WATATU KWA SIKU MOJA!!!

Sijawahi kuona wala kusikia tukio kama hili kaaazi kwelikweli..na tena ni mpya. Mwanamke mmoja tu kazi kwelikweli je watatu na tena kwa mpigo. Nimeshindwa kuvumilia kushangaa peke yangu nimeona niwashirikishe na wenzangu.  

Thursday, August 9, 2012

Raymond Mkandawile na Bibie Janeth Manongi tulifunga pingu za maisha!!!


Hello ndugu,mimi ni mdau na mmiliki wa mtandao wa mkandawilejr.blogspot.com
tafadhali naomba niwekee taswira hizi za siku ya harusi yangu.
Hapo juu ni taswira mbalimbali za siku hiyo ya kihistoria ya tarehe 4/08/2012ambapo mimi Raymond Mkandawile na Bibie Janeth Manongi tulifunga pingu za maisha  huko jijini mbeya katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Sinai na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Teku uliyopo maeneo ya Block T.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushirikiano wenu.
Mr. Raymond Mkandawile
BA (HON) in Business Studies
University of Wales Institute of Cardiff(UK)
Mob; +255656-561-314
Email; raymonds19@yahoo.com
Website;http://www.mkandawilejr.com




Maharusi wakiteta jambo baada ya kunganishwa na kuwa mwili mmoja

Bwana na bibi Harusi wakiwa nanyuso za furaha...
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuwatakieni maisha mema ya NDOA na pia kuwakaribisheni katika maisha haya ya Ndoa. Ambayo yanahitaji UVIMILIVU NA USIKIVU PIA MAWASILIANO. MAISHA MEMA/HONGERENI SANA.



Wednesday, March 7, 2012

Nikanusurika kwenda jela, lakini kikaja kisirani kingine…………

Ni JUMATANO TENA NA NI KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO LEO NIMEKUTANA NA HABARI HII NIMEIPENDA NIMEONA NIWASHIRIKISHE. Nimeipata hapa
------------------------------------------------------------------------------------------------
Ilikuwa ni mwaka 1994 wakati nilipoingia kwenye kasheshe kubwa ambayo nusura tu inipeleke jela. Nikiwa ndio nina mwaka wa pili tangu kuanza kazi, nilimpachika binti mmoja mimba. Alikuwa ni binti wa shule akisoma darasa la sita wakati ule. Mwili wake ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba, ungeambiwa yuko kidato cha nne usingebisha, lakini alikuwa bado mdogo kwa umri.Baada ya kumpachika mimba, mjombake ambaye ndiye aliyekuwa akiishi naye, alilifungia kibwebwe suala lile, akitaka nipelekwe mahakamani. Ndugu zangu na jamaa zangu walijitahidi kwa kadiri walivyoweza kuzuia jambo lile kufikishwa mahakamani. Mjomba wa binti alikubali, lakini kwa sharti la mimi kumwoa mpwa wake, mara moja. Nilikubali haraka kufanya hivyo, kwani nilishauona mlango wa Segerea ukiwa wazi mbele yangu. Nilimwoa binti yule kwa ndoa ya ‘mkeka.’ Wazazi wake hawakuwepo, kwani wanaishi Songea vijijini.Mwezi huo huo nililazimika kwenda mkoani Mbeya kikazi, ambapo nilitakiwa kuishi kwa miezi mitatu kwa ajili ya kazi ya mkataba ambayo kampuni yetu iliipata. Nilipokuwa Mbeya, nilipata mwanamke ambaye alionekana kuwa na adabu zile za kijijini kabisa. Huyu nilimpata hospitalini, ambako nilienda kutibiwa Malaria, wiki ya tatu tangu kufika pale Mbeya.Sijui tulizoeana vipi, lakini alikuja kuwa rafiki yangu. Alikuwa ni mwenyeji wa Mkoani Ruvuma na pale Mbeya alikuwa amekuja kumuuguza kaka yake, ambaye alilazwa hospitali ya rufaa Mbeya. Nilimpenda kwa kweli, hasa nidhamu yake na hekima. Kiumri alinizidi miaka minne. Mimi nilikuwa na miaka 29 wakati huo na yeye 33. Lakini kwa kutazama, mtu angedhani mimi ndiye nilikuwa mkubwa. Niliishi naye kama mke wangu, hadi miezi mitatu ikaisha, nilirudi Dar nikimwacha bado anauguza mgonjwa wake. Wiki mbili baadae tangu nirudi Dar tuliletewa taarifa kwamba baba wa mke wangu amefariki dunia. Tuliamua kusafiri kwenda kwenye mazishi Songea, wakati huo mimba ya mke wangu ilikuwa imetimiza miezi sita. Tuliondoka mimi, yeye, na ndugu zake wawili na ndugu yangu mmoja. Tulifika kijijini kwao jioni, ambapo tulikuta mazishi yakiendelea, tulienda makaburini tukimwacha mke wangu nyumbani kutokana na hali yake. Tulipofika makaburini ilikuwa ndiyo zamu ya kuweka mashada ya maua kaburini.Ilikuwa kama ndoton Fulani, kwani nilimwona yule hawara yangu wa Mbeya akiweka shada la maua na alitajwa kama mke wa marehemu. Nilihisi kama nataka kupoteza fahamu. Nilijikaza, ingawa nilikuwa natoka sana jasho. Baada ya mazishi tulirudi nyumbani, ambapo ilibidi nitambulishwe kwa mzazi wa mke wangu na ndugu zake. Nilitambulishwa kwanza kwa mama mkwe ambaye kule Mbeya alikuwa ni hawara yangu. Kila mmoja kati yetu alijikaza ili isifahamike kinachoendelea. Lakini, hiyo haikudumu, kwani bomu likalipuka sawia. Mama mkwe wangu alilazimika kusema kwa wazazi wake, ati akiogopa mkosi utokanao na jambo kama hilo. Ilibidi siku ya nne baada ya msiba tufanyiwe tambiko la kiasili kuondoa laana. Nataka nikwambie katika maisha yangu sijawahi kukabiliwa na mtihani mgumu kama ule. Ninaye bado mke wangu na tumesahau yaliyopita. Mama mkwe hajawahi kuja kwetu, ingawa sisi tunaenda na kukaa siku chache kwake, kila mwaka.TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA!!!!!

Wednesday, February 22, 2012

NI NINI KINAFANYA MAISHA YAWE NA FURAHA?

NI JUMATANO NA NI KILE KIPENGELE CHA MARUDIO MBALIMBALI LEO NI MARUDIO YA November 25, 2008 NDANI YA MAISHA NA MAFANIKIO.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha ya yako/yangu kuwa na furaha kama hatutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yetu. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je? ume/tumesha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo haya.

Mpenzi msomaji katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tulio wengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi muhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha thamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tulio wengi tumekuwa tukililia au kujionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuolewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.

Kuna misemo isemayo kwamba:- mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamume anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mume; poleni sana wanawake tumepotea, badili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.

Na kwa upande mwingine, Mwanamume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegemea kuwa hatabadilika; Mungu ndiye ajuaye kuwa mwanadamu ni kigeugeu, sasa atutendee nini ndipo tulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwa sababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha ni magumu ndani ya ndoa, na wengine umaskini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.

Swali linakuja je? unafikiri kukamatana ugoni na kuonyeshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatua matatizo katika jamii kama watu hawatatumia njia ya kuiweka wazi mioyo yao kwa kile wanachokipenda na kukitamani?

Ni changamoto kwamba kweli tulichokiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli humpendi mwenzako sema tangu mwanzo liwe wazi tusitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ana nafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.

Maisha ya ndoa ni kuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida, kwa furaha na amani bila majuto.

Wednesday, November 16, 2011

WAMALAWI NA NDOA ZA VIBINTI!

Ni JUMATANO NA NI KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDUI YA MADA/MAKALA NA MTUKIO MBALIMBALI. LEO NIMEPITA KUPEKUA KWA MDOGO WANGU WA HIARI AMBAYE KWA SASA SIJUI YUPO WAPI SI MWINGINE TENA BALI NI KOERO BINTI WA MKUNDI.BONYEZA HAPA.


Mmoja wa wa waathirika wa ndoa hizo



Binti huyu naye ni miongoni mwa waathirika wa ndoa hizi za vibinti


Huyu sio babu na mjukuu wake bali ni mtu na mkewe


“Baba yangu wa kambo aliniamuru niache shule ili niolewe na mzee wa umri wa miaka 77, kwa madai kuwa umri wangu ni mkubwa ukilinganisha na darasa ninalosoma, kwani wakati huo ndio nilikuwa niko darasa la nne. Nilimkatalia na kumweleza wazi kuwa ningependa kuendelea na masomo”. Hivyo ndivyo alivyoanza simulizi yake binti huyu Balita Simpokolwe.



lakini hata hivyo kukataa kwake hakukuweza kumsaidia.



Kwani baba yake alianza kumtuma sokoni kuchukua fedha kwa mtu mmoja mzee hivi, ambaye alikuwa hamfahamu, ambapo alikuwa akipewa kiasi cha kati ya dola 5 mpaka 10, kiasi ambacho alitakiwa anunulie chakula na kiasi kinachobaki alikuwa kumpa baba yake huyo wa kambo.



Balita anakiri kwamba hakuweza kuhisi jambo lolole kuhusiana na zile pesa alizokuwa akipewa na yule mzee kwa kuwa aliamini kuwa yule alikuwa ni rafiki wa karibu wa baba yake wa kambo. Lakini wiki tatu baadae tangu awe anakwenda kuchukua fedha kwa mzee yule, alishangaa kumuona akija nyumbani kwao na jembe dogo la kulimia bustani. ( kwa mila za watu waishio Malawi Kaskazini hususan katika wilaya ya Nsanje jembe dogo la kulimia bustani inatumika kama ishara ya mahari)



“Nilishtuka sana, baada ya baba yangu wa kambo kunitaka nipokee jembe lile la bustani kutoka kwa yule mzee. (Kwa mila zao, binti kupokea jembe kutoka kwa mwanaume ni ishara kuwa amekubali kuolewa na mume huyo). Lakini huku nikiwa imechanganyikiwa, nilikataa kupokea jembe lile.”



Hata hivyo mama yake aliungana naye kupinga binti huyo kuolewa kwa kuwa bado alikuwa ni mdogo, “baba yangu wa kambo alikuja juu akidai kuwa atampa talaka mama yangu iwapo atapinga mimi kuolewa na mzee huyo, na cha kusikitisha zaidi alidai kuwa haiwezekani nisiolewe na mzee huyo kwa kuwa tumeshakula fedha zake.” Alisema binti huyo kwa masikitiko.



Hivyo alilazimishwa kuolewa na mzee huyo, lakini baada ya wiki mbili tangu aolewe kikundi kimoja cha kutetea unyanyasaji wa wanawake na watoto kiitwacho Chitipa Women’s Forum kilimuokoa kutoka katika ndoa hiyo baada ya kuwashwishi wazazi wa binti huyo wamrejeshe shuleni.



Belita Simpokolwe, sasa anaishi na mmoja wa baba zake wadogo, amefurahi sana baada ya kurejea shule kuendelea na masomo yake. Tukio hili ambalo lilimpata Belita Disemba mwaka 2008 lilimuacha akiwa na amesathirika kisaikolojia.



Kwa mujibu wa mwalimu anayemfundisha alikiri kuwa kuna wakati alikuwa anashindwa kuzingatia masomo yake pale kumbukumbu za tukio lile la kutolewa shuleni na kuozeshwa kwa nguvu linapomjia, lakini binti huyo ambaye alikuwa na miaka 13 wakati huo akiozeshwa, amemudu kuendelea na masomo yake ambapo anataka kutimiza ndoto zake za kuwa muuguzi hapo atakapomaliza masomo.



“Kinachoniuma ni kwamba nimekuwa ni muathirika wa ndoa ya utotoni baada ya wale niliowaamini kuwa watanitunza na kunilinda kunitoa kafara kiasi cha kutaka nisitimize ndoto yangu” alisema binti huyo aliyekuwa akisoma shule ya msingi Kawale kaskazini mwa Malawi, akiwa yuko darasa la sita wakati huo.



Belita ni mmoja kati ya mabinti walioathiriwa na mila marufu kama Kupimbira, ambapo mabinti hulazimishwa kuacha shule na kuozeshwa kwa wazee ili kujipatia mahari, na hii hufanyika bila hata ya binti kufahamishwa.



Wakati mwingine wazazi hulazimika kuwaozesha mabinti zao ili kulipa madeni.



Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na tasisi ya Chipita Women’s Forum inaonyesha kwamba ,taktibani asilimia 17 ya mabinti huachishwa shule na kuozeshwa kwa wazee, huku wengine wakilazimika kuacha shule wenyewe kutokana na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na waalimu wa kiume na wanaume wakware wenye uchu wa kufanya mapenzi na vibinti.



Akizungumzia mila zinazotumika kuwakandamiza watoto wa kike na kuwakatisha shule Mwenyekiti wa Chipita Women’s Forum, Bi Ruth Mbale alizitaja mila kama ‘Kupimbira’, ambapo mabinti hulazimishwa kuacha shule na kuozeshwa kwa wazee ili kujipatia mahari, ‘Nhlanzi’ ambapo familia ya mke huozesha binti mwingine kwa mume wa binti yao kama zawadi kutokana na kuitendea wema familia husika, ‘Kulowa kufa’ mwanamke aliyefiwa na mume kuingiliwa kimwili na mwanaume mwingine ili kuondoa mkosi wa vifo kijijini, kwa kawaida shughuli hiyo hufanywa na mwanamume maalum wa kufanya shughuli hiyo. Mila hii pia inasemekana inafanyika hapa nchini hususana wilayani Ukerewe ambapo hujulikana kama ‘Kusomboka’, hii kwa hapa nchini hufanywa na wanaume na wanawake. Bi Mbale pia aliitaja mila ya ‘Fisi’ ambapo mume ambaye hana nguvu za kiume anamkodisha mwanume wa nje ili amuingilie mkewe kwa ajili ya kumpa ujauzito, lengo kuu ni kujipatia watoto.



Bi Mbale alikiri kupata ugumu katika kupiga vita mila hizi kutokana na usiri mkubwa uliokuwepo katika jamii hiyo ya watu waishio Kaskazini mwa Malawi.



Akizungumzia idadi ya mabinti waliiokolewa na taasisi yao tangu walipoanza kampeni ya kuwaokoa wanafunzi walioozwa kabla ya kumaliza masomo, Bi Mbale alisema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa mabinti 40 waliokuwa na umri kati ya miaka 7 hadi 16 ambapo walirejeshwa shule na kuendelea na masomo.



Alisema kuwa, ingawa inakuwa ni vigumu kwa mabinti hao kurejea katika hali yao ya kawaida kabla hawajaolewa lakini huwapa ushauri nasaha hadi warejee kwenye hali zao za kawaida na kuendelea na masomo yao.


Habari hii nimeitoa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ukiwemo mtandao wa inteneti.

Monday, May 2, 2011

NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?

Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu.
Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile.
Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…......
Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo.
Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani.
Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish.
Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye.
Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni?
Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala .
Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu.
Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali.
Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake?
Ushauri tafadhali...........