Sunday, June 28, 2015
Friday, June 26, 2015
MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA
Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)
Thursday, June 25, 2015
NGOJA LEO TUANGALIE MAENDELEO YA BUSTANI YETU
HAPA NI FIGIRI
NA HAPA NI MCHICHA.
Mwaka huu bustani yetu maendeleo yanaenda polepole sana kutokana na hali ya hewa si nzuri sana ila waswahili husema polepole ndio mwendo, na haraka haraka haina baraka.
Monday, June 22, 2015
HAYA JAMANI NI WIKI NA JUMATATU NYINGINE....TUTEMBELEE SONGEA KWETU ....
Ndo kwanza kunakucha .....na Jua hilo lachomoza...Basi niwatakieni wote jumatatu njema najua wengi mko mzigoni...Binafsi nitapotea kidogokidogo kuwa na famalia.Ila nipo:-)
Thursday, June 18, 2015
TUMALIZE WIKI KWA MTINDO HUU ,,,,,,,,SIKILIZA WIMBO HUU UPATAPO WASAA
Nakutakieni IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA WIKI!
Wednesday, June 17, 2015
LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO
Kwa upendo jaribu kumpa taarifa ya ua hili jirani, rafiki na ndugu zako ili wawe makini kwa ua hili. Basi ngoja mimi Kapulya niwatakieni siku njema na tutaonana tena panapo majaliwa. Jumatano njema!!
Monday, June 15, 2015
TUANZE JUMATATU NA VAZI HILI ...MWENZENU NIMETOKEO KULIPENDA MNO:-) SARESARE MAUA ASIYEJUA KUCHAGU KABILA YAKE NZEGU-------
Hapa ni dada edna
Na hapa ni dada Nuru ....halafu usisahau kuandalia hizo ndala yaani nimelipenda sana hili vazi . JUMATATU NJEMA
Saturday, June 13, 2015
TUANZE JUMAMOSI HII KWA KIFUNGUA KINYWA HIKI HAPA CHAI KWA MIHOGO...KARIBUNI!!
Mihogo ya kuchemsha na hii chai hapa chini basi siku itakuwa njemaaaa. Karibuni tujumuike
Kwa wale waliozaliwa miaka ya uhuru watakubaliana na mimi kuwa vyombo hivi vilikuwa vya heshima sebuleni, kwenye kabati, halafu unakunywa chai kwa adabu maana yake kikombe cha moto, chai ya moto basi hapo chai inatelemka polepole...Tuesday, June 9, 2015
NDUGU ZETU WANGONI HAPO KALE
Familia ya kingoni ilikuwa ikionekana hivi hapo kale
Amejiandaa tayari kwa kujikinga kwa vita, Ngao na mkiku
Wavulana wa kingoni katika kucheza ngoma
Kwangu ni kumbukumbu nzuri sana katika picha hizi Tusisahau ya kale ndugu zangu.
Monday, June 8, 2015
TUANZE JUMATATU HII KIHIVI:- SINENE NI KITOWEO HASA MAARUFU SANA HUKO BUKOBA.....
Nimekuwa najiuliza utamu wa senene ni kama kumbikumbi au? Kama ni hivyo basi sina budi kusema ni watamu.....Pia nimesikia hapa baadaye vyakula kama hivyo vitakuwa vya thamani sana duniani kwoote.JUMATATU IWE NJEMA SANA KWAWOTE!!
Sunday, June 7, 2015
NI JUMAPILI YA KWANZA KWA MWEZI HUU NA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUTEMBELEE PAROKIA YA BOMBAMBILI JIMBO LA SONGEA
NEEMA, UPENDO NA FURAHA VITAWALE NDANI YA NYUMBA ZETU NA PIA KATIKA MIOYO YETU. AMINA!!
Saturday, June 6, 2015
UJUMBE WA LEO KUTOKA KWA KAPULYA WENU!!
Usiumizwe na mtu ambaye haumizwi kwa ajili yako. Tambua maisha ni mafupi kama umeme. Kuwa na furaha na acha kuwa mnyonge.
JUMAMOSI NJEMA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!!
JUMAMOSI NJEMA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!!
Wednesday, June 3, 2015
TUTOKE MANISPAA YA SONGEA NA TUTEMBELEE JIJI LA ROCK CITY (MWANZA)
Leo nimeona tutembelee jiji la Rock City Mwanza....inawezekana baadhi ya nyumba babu yangu marehemu alijenga maa alikuwa akiishi hapa na alikuwa muhunzi/mjengaji mzuri sana......Kapulya
Tuesday, June 2, 2015
MAISHA YA NDOA!!
Sijui nahitaji miwani au? maana naona hawa walitakiwa kuwa shule..Duh kuanza maisha ya ndo mapema hivi....
Monday, June 1, 2015
TUANZE MWEZI HUU WA SITA NA KUTEMBELEA MJI WA SONGEA-----
SOKONI SONGEA
Songea yetu hapa
Napenda kuwasalimu wote mtakaopita hapa na pia kuwakaribisha nyumbani Songea/Manispaa ya Songea. Karibu sana.....NAWATAKIENI MWANZA MWEMA WA MWEZI HUU WA SITA....PANAPO MAJALIWA TUTAONANA SASA NAENDA BUSTANINI:-) Kapulya wenu