Tuesday, September 29, 2015

SALAMU ZA MAKABILA YETU TANZANIA

 


Wasomaji wapendwa wa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO, nimejaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini Tanzania. Kama tujuavyo ni kwamba kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini. Nami nimeamua kuangalia zaidi salaam, hasa za asubuhi, kutokana na utafiti wangu pia kwa msaada wa marafiki nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumika katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:

KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi
KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi
KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi
KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi
KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi
KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi
KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi
KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi
KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi
KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi
KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi
KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi
KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi
KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi
KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi
KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi
KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi
KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi
KIMATENGO: Ja kujumuka = Habari za asubuhi
KIKURYA:  Agha nyinkyo = Habari za asubuhi
KIPOGORO: Za mandawila = Habari za asubuhi
Hayo ni baadhi tu ya makabila machache katika mengi yaliyomo nchini kwetu, unaweza ongezea salaam za makabila unayofaham wewe ndugu yangu

42 comments:

Baraka Chibiriti said...

Kigogo - Mbukwenyi.

Ki nyambwa - Wanzukowenyu

ray njau said...

Kichaga cha Vunjo:
----------------
Asubuhi:
---------------
Salamu kwa wakubwa:
--------------------
1.Kamtsa mbe -Baba
2.Kamtsa mae-mama
3.Kamtsa awaye-kaka/dada
--------------------------
Mchana/alasiri,adhuru,jioni na usiku
----------------------------------
Otsinda mbe,mae na awaye.

ray njau said...

Shimbonyi shya nyu:Habari zenu
Kamtsa-Habari za asubuhi
Otsinda-Umeshindaje

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Braka! Ahsante kwa mchango wako...
Kaka Ray! Nawe ushukuruwe kwa mchango wako ulioutoa kwa kabila ya kichaga

ray njau said...

Maisha na mafanikio ni kisima cha maarifa na mwenye kiu ya maarifa na ujuzi anakaribishwa.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wanyasa Mwauka bwanji?
Wanyaturu Amocha wa?
Wnayambo Weimukota?
Waha Mwaraye?

Unknown said...

Kipare salaam ya mchana na jioni ikoje

Fanya uchunguzi wa kabila la wahangaza na hisitoria yao.

Asante sana.

CLAUD said...

Mnisaidie wadau kusema asante kwa lugha za makabila tofauti tofauti.

Unknown said...

Mwadila siyo salamu ya asubuhi,bali ni salamu ya mchana na usiku kwa sisi wasukuma.

Ng'wangaluka ndio salamu ya asubuhi kwa sisi wasukuma na wanyamwezi.

Tr John said...

Kihaya: Mwalailota

Bakari Mohamedi said...

Kimatumbi msaada kwa anaejus

Anonymous said...

Wambaje sio kikunguja na maana yake sio Habari ya asubuhi.
Wambaje ni kipemba na maana yake unasema je? Unajibu sijambo au Sina usemi.
Na Habari ya asubuhi inakua Habari ya unju. Kipemba
Unguja Kuna lahaja tofauti kimakunduchi na kitumbatu na unguja mjini ni kiswahili hakuna kiluga ni Habari ya asubuhi.
Ila maamuzi ya zanzibar ni assalam alaykum mda wote unguja na pemba.

Unknown said...

Kweli kabisa. Hiyo ni salamu kwa Wabena.
Kikinga - Mapembelo

Unknown said...

Kiirak- lawo matle,habari ya asubuhi

Unknown said...

Wazaramo tunaandika wapi jamani?

Unknown said...

Nimependa salamu hiz

Unknown said...

wabondei nao vp??

Unknown said...

Wamakonde ncheme nchicheme

Bonemaro said...

Asheee-kimasai
Wabejha-kisukuma
Naas-kiiraq,kimbulu

Bonemaro said...

Saitake

Unknown said...

Yakindaaae _ za asubuhi

Nuru muhammad said...

Mie mpaka leo sijui salamu yetu

Nuru muhammad said...

Wazaramo jamani

Anonymous said...

Taja kabila

Anonymous said...

Asanter kwa.
Umeshindaje kwa kiiraq

Anonymous said...

tusaidie kizaramo jamani

Anonymous said...

Jaman nawashukulu sana

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kuona ndugu zangu mpo, ni furaha pia kuona na kujua makabila mengine yasemavyo....karibuni kuendelea . Nitajitahidi kufanya uchunguzi jinsi makabila yetu mbalimbali tusemavyo AHSANTE

Anonymous said...

Wambaje....? wapemba wanatumia neno hili kama kuuliza mtu uhali gani? Hapo utajibu sijambo au nabesa. Pia nabesa unaweza ukamuuliza mtu swali "wabesa" na akakujibu nabesa au sijambo.

Anonymous said...

Shemej leo

Anonymous said...

Kimanyema tafadhal

Anonymous said...

Kirangi

Anonymous said...

Jamtondo ,mwatumbwire,jole muvukire,kirangi salam ya asubuhi

Anonymous said...

Kijita je? Na kijaluo

dastan40 said...

Wapare mchana washindadhe au wekithikija au

dastan40 said...

Kipare wanawake Navahache wanaume Nahavome

Anonymous said...

Napenda hizo salamu kwa kaka/dada; baada ya salamu kwa waheshimiwa « Mbe na Mae », wale « awaye » inakuwa kama « awaye yote » - otsinda awaye yote yule, yeyote uliye baki😂!

Anonymous said...

Sahihisho : Wasukuma husalimiana kama Wanyamwezi tu - mwangaluka asubuhi na mwadila jioni ; tofauti ni accent tu, ya Wanyamwezi ikiwa softer & melodious kuliko ya Wasukuma 😊

Anonymous said...

Kimanda anejua salamu ?

Kimki said...

Kiluguru

MAISHA YA UJANA said...

Mwaongelamo bwacha masika


Oyaole engima mabere

Anonymous said...

hermes outlet
bape clothing
ggdb outlet