Tuesday, September 29, 2015

SALAMU ZA MAKABILA YETU TANZANIA

 


Wasomaji wapendwa wa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO, nimejaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini Tanzania. Kama tujuavyo ni kwamba kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini. Nami nimeamua kuangalia zaidi salaam, hasa za asubuhi, kutokana na utafiti wangu pia kwa msaada wa marafiki nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumika katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:

KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi
KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi
KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi
KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi
KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi
KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi
KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi
KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi
KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi
KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi
KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi
KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi
KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi
KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi
KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi
KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi
KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi
KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi
KIMATENGO: Ja kujumuka = Habari za asubuhi
KIKURYA:  Agha nyinkyo = Habari za asubuhi
KIPOGORO: Za mandawila = Habari za asubuhi
Hayo ni baadhi tu ya makabila machache katika mengi yaliyomo nchini kwetu, unaweza ongezea salaam za makabila unayofaham wewe ndugu yangu

42 comments:

  1. Kigogo - Mbukwenyi.

    Ki nyambwa - Wanzukowenyu

    ReplyDelete
  2. Kichaga cha Vunjo:
    ----------------
    Asubuhi:
    ---------------
    Salamu kwa wakubwa:
    --------------------
    1.Kamtsa mbe -Baba
    2.Kamtsa mae-mama
    3.Kamtsa awaye-kaka/dada
    --------------------------
    Mchana/alasiri,adhuru,jioni na usiku
    ----------------------------------
    Otsinda mbe,mae na awaye.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Napenda hizo salamu kwa kaka/dada; baada ya salamu kwa waheshimiwa « Mbe na Mae », wale « awaye » inakuwa kama « awaye yote » - otsinda awaye yote yule, yeyote uliye baki😂!

      Delete
    2. Sahihisho : Wasukuma husalimiana kama Wanyamwezi tu - mwangaluka asubuhi na mwadila jioni ; tofauti ni accent tu, ya Wanyamwezi ikiwa softer & melodious kuliko ya Wasukuma 😊

      Delete
  3. Shimbonyi shya nyu:Habari zenu
    Kamtsa-Habari za asubuhi
    Otsinda-Umeshindaje

    ReplyDelete
  4. Kaka Braka! Ahsante kwa mchango wako...
    Kaka Ray! Nawe ushukuruwe kwa mchango wako ulioutoa kwa kabila ya kichaga

    ReplyDelete
  5. Maisha na mafanikio ni kisima cha maarifa na mwenye kiu ya maarifa na ujuzi anakaribishwa.

    ReplyDelete
  6. Wanyasa Mwauka bwanji?
    Wanyaturu Amocha wa?
    Wnayambo Weimukota?
    Waha Mwaraye?

    ReplyDelete
  7. Kipare salaam ya mchana na jioni ikoje

    Fanya uchunguzi wa kabila la wahangaza na hisitoria yao.

    Asante sana.

    ReplyDelete
  8. Mnisaidie wadau kusema asante kwa lugha za makabila tofauti tofauti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asheee-kimasai
      Wabejha-kisukuma
      Naas-kiiraq,kimbulu

      Delete
    2. Kipare wanawake Navahache wanaume Nahavome

      Delete
  9. Mwadila siyo salamu ya asubuhi,bali ni salamu ya mchana na usiku kwa sisi wasukuma.

    Ng'wangaluka ndio salamu ya asubuhi kwa sisi wasukuma na wanyamwezi.

    ReplyDelete
  10. Kihaya: Mwalailota

    ReplyDelete
  11. Wambaje sio kikunguja na maana yake sio Habari ya asubuhi.
    Wambaje ni kipemba na maana yake unasema je? Unajibu sijambo au Sina usemi.
    Na Habari ya asubuhi inakua Habari ya unju. Kipemba
    Unguja Kuna lahaja tofauti kimakunduchi na kitumbatu na unguja mjini ni kiswahili hakuna kiluga ni Habari ya asubuhi.
    Ila maamuzi ya zanzibar ni assalam alaykum mda wote unguja na pemba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wambaje....? wapemba wanatumia neno hili kama kuuliza mtu uhali gani? Hapo utajibu sijambo au nabesa. Pia nabesa unaweza ukamuuliza mtu swali "wabesa" na akakujibu nabesa au sijambo.

      Delete
  12. Kweli kabisa. Hiyo ni salamu kwa Wabena.
    Kikinga - Mapembelo

    ReplyDelete
  13. Kiirak- lawo matle,habari ya asubuhi

    ReplyDelete
  14. Wazaramo tunaandika wapi jamani?

    ReplyDelete
  15. Jaman nawashukulu sana

    ReplyDelete
  16. Ni furaha ilioje kuona ndugu zangu mpo, ni furaha pia kuona na kujua makabila mengine yasemavyo....karibuni kuendelea . Nitajitahidi kufanya uchunguzi jinsi makabila yetu mbalimbali tusemavyo AHSANTE

    ReplyDelete
  17. Replies
    1. Jamtondo ,mwatumbwire,jole muvukire,kirangi salam ya asubuhi

      Delete
  18. Kijita je? Na kijaluo

    ReplyDelete
  19. Kimanda anejua salamu ?

    ReplyDelete