Tuesday, August 25, 2015

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HUU UWE UJUMBE WA LEO!!

KATIKA MAISHA NI BUSARA KUJITATULIA MATATIZO YAKO!
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!

Monday, August 24, 2015

KARIBUNI TUJUMUIKE: UNAKUMBUKA ENZI HIZOOO UTOTONI HASA KWENYE MSOSI???

Chakula tayari ni watu wanakosekana kuushambulia msosi huu mtamu...Mimi hapo hizo dagaa ndo natamani kwelikweli-------Kapulya !

Saturday, August 22, 2015

PICHA YA WIKI: AMA KWELI UKITAKA KUPENDEZA LAZIMA MAUMIVU YAWE.....

Huu ni ubunifu mpya ambao mimi sijawahi kuusikia wala kuutumia. Je wewe umewahi? Basi nikutakieni mwisho wa juma mwema. Panapo majaliwa tutaonana tena. Kapulya wenu:-)

Wednesday, August 19, 2015

HILI NI CHAGUA LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO :- PICHA YA WIKI!!

Pamona na kusema YOTE NJAA:- Lakini pia ndio ujasiriamali hapa anaonekana kama vile kweli yote ni njaa lakini kesho mna kesho kutwa atakuwa mtu mwingine. Ndivyo inavyotakiwa, kupata MAFANIKIO taratibu na sio kuamka tu na kupata.

Monday, August 17, 2015

KUMBUKUMBU:- LEO NI MIAKA KUMI NA MOJA (11) KAMILI TANGU MAMA YETU ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

MAMA! ANAWEZA KUCHUKUA  NAFASI ZA WENGINE LAKINI NAFASI YAKE HAIWEZI KUCHUKULIWA NA YEYOTE YULE
 
KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka kumi na moja  sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana, sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

Friday, August 14, 2015

Wednesday, August 12, 2015

MAISHA NA JAMII:- ZITAMBUE SIFA SITA ZA MSINGI ZA MWANAMKE ALIYE MKE BORA!

Mithali 14:1 "Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake,bali aliye mpumbavu
huibomoa kwa mikono yake."

Kuna mithali isemayo "MAJUTO NI MJUKUU", ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na
kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo
mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu
aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa zamwanamke mwenye hekima pia soma mithali 31:10-31.

-Hufumbua kinywachake kwa hekima, na sheria ya wema katika ulimi wake huwashauri wengine kwa ukarimu mithali (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi / ukali,maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na wanamke ni kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni mbaya.

-Hufanya kazi kwa moyo na huamka alfajiri na mapema.Kuna wanawake ambao ni wavivu
kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana
kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaibu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya
kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haitachelewa mwanaume kulipa fadhili kwa wema
anaotendewa.

-Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake.
Kuna wanawake ambao ni wachafu/ usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala
ni stoo ya nepi za mkojo na nguo chafu,wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti
mwanamke awe msafi muda wote, Wanaume wote wanapenda usafi,marashi hata ya mchina
yasikose,mwanamke hakikisha "Reception" inakuwa safi na kuwa katika hali ya kumfanya mume
ajisikie kujipumzisha kwa raha mustarehe.

-Jali na timiza mahitaji ya NDOA kwa mume wako.
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa
swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki

nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI”  utafikiri ni askari anaendavitani. Wanaume
ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungwa, Fanya makosa
yote lakiniusijefanya  ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa,  hilo ni kosa la
jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za
Mungu.

-Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho famiia itafurahi.
wanawake wengi hasa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaumewengi wanaishia kula
hotelini au kwa mama ntilie, kama umetokabara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga nazi kwa chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, Wanaume wanapenda chakula  chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.

-Mwamini mume wako, wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa
mashoga au ndugu zako.

Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo”.
CHANZO: GAZETI LA MWENGE TOLEO LA JANUARI 2015

Monday, August 10, 2015

TUANZA JUMA HILI NA PICHA HII:- UTALII UNA CHANGAMOTO ZAKE .....

Sasa hapa kweli atapona huyu maana Mbuni ni myama/ndge ambaye anakimbia sana kuliko wanyama/ndege wote duniani...MMMhhhhh hapa kazi kwelikweli...Kapulya

Saturday, August 8, 2015

UJUMBE WA LEO

Ilikuwa ni majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo mzee mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 aliingia katika
hospitali moja ili kusafisha kidonda chake cha mguuni.
Mzee akaanza kwa kuomba afanyiwe haraka kwa kuwa alikuwa na appointiment
ya muhimu sana ifikapo saa tatu kamili ya asubuhi hivyo afanyiwe msaada wa
huduma ya haraka.
Daktari mmoja akaguswa na mzee yule baada ya kuona kila mara akiingalia saa yake na kutikisa kichwa cha kukatishwa tamaa na kuamua kumhudumia kwani alijua ingechukua zaidi ya saa kabla ya
mzee kuhudumiwa kutokana na idadi
kubwa ya watu kwa kuwa yeye hakuwa na
mgonjwa wa kumhudumia wakati huo.
Baada ya uchunguzi wa kidonda chake
kikaonyesha kuwa kimepona na daktari
akaanza kukifungua akishirikiana na nesi
kukisafisha. Wakiwa wanaendelea kukisafisha
kidonda daktari na mzee wakaanza mazungumzo na daktari akamuuliza kama mzee alikuwa na apolintiment na daktari mwingine kwa jinsi alivyokuwa na haraka.
Mzee akajibu hapana, ila natakiwa kuwahi kwenda kunywa chai na mke wangu
ambaye amelazwa kwenye kituo cha kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya ubongo .
Mzee akaendelea kumwambia daktari
kuwa mkewe amelazwa pale kwa zaidi ya
miaka miwili akitibiwa maradhi hayo na hana kumbukumbu kabisa
 Daktari akauliza sasa kama kapoteza kumbukumbu atakumbuka kama umechelewa?

Mzee akamjibu daktari kuwa mke wangu hajawahi kukumbuka kuwa mimi ni nani au nini kinaendelea kwa zaidi ya miaka hiyo miwili.
Kwa mshangao daktari akamuuliza, "Na umekuwa ukiendelea kwenda kunywa
naye chai kwa miaka yote hiyo kila siku asubuhi hata kama amekusahau wewe ni
nani?"
Mzee alitabasamu na kuushika mkono wa
daktari na kumwambia "hanifahamu tena
mimi, ila mimi bado namfahamu ni nani
kwangu na umuhimu wake kwangu"
Daktari alifuta machozi huku akimtazama
mzee yule akiondoka kulekea kwa mkewe
kunywa chai kabla ya saa tatu kamili.
Daktari alijishika mikono yake kichwani na kusema, "Hii ndio aina ya mapenzi
ninayoyataka katika maisha yangu"
Upendo wa kweli hauko kwenye mwonekano wa mtu au mapenzi. Mapenzi
ya kweli ni kukubaliana na hali zote zilizopo, zitakazotokea na ambazo
hazitatokea pia.
Kama umeguswa na kisa hiki tafadhali
CHANZO:- NIMETUMIWA NA RAFIKI

Thursday, August 6, 2015

UJUMBE WA JIONI YA LEO TOKA KWANGU KUJA KWENU

Maisha  ni mtihani Mkubwa na tofauti. Watu wengi huwa wanafeli kwa sababu wanajaribu kuiga maisha ya wengine, bila kujua ya kwamba kila mmoja ana swali lake tofauti.

Thursday, July 30, 2015

NGUO ZA ASILI NA UREMBO WINGINE KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA!

 MAASAI/TANZANIA/KENYA
 ZULU/AFRIKA YA KUSINI
 ETHIOPIA
UGANDA
Nimependezwa/napendezwa kuona baadhi ya nchi na makabia wanaendeleza mavazi yetu ya asili....Ngoja nami nitafuta vazi la asili la kingoni:-)

Tuesday, July 28, 2015

BUSTANI YETU NA MAENDELEO YAKE:- MAVUNO YA MARA YA PILI

Ni Mchicha mboga Maboga na Figiri  nimechuma na nimechemsha na kuweka akiba si mnajua akiba haiozi...Hii ndi kazi ya mikono yangu, mtoto wa mkuli ni mkulima:-) Ila msiogope  sijahifadhi yote karibuni tujumuike.

Monday, July 27, 2015

SAFARI YETU YA TANZANIA NA ZANZIBAR TULIPATA BAHATI YA KUNUNUA PICHA HIZI ZA TINGATINGA UTAMADUNI WETU:-)

 TWIGA HUYU
Na hapa ni aina ya wanyama wote walioko Afrika/Tanzania...WANAZIITA PICHA ZA TINGATINGA.....TAYARI ZIMEKWISHA BANDIKWA UKUTANI.

Sunday, July 26, 2015

HILI NI CHAGUA LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA WIKI:- JUMAPILI NJEMA KWA WOTE

Sasa hapa sijui tusema ni  kumpendeza Jogoo au? Unafikiri Jogoo anapenda kuvaa hivyo kweli?...Haya Niwatakieni JUMAPILI NJEMA SANA! AMANI NA UPENDO VITAWALE KATIKA FAMILIA ZETU.

Wednesday, July 22, 2015

KANGA NA MISENO /MAANDISHI YAKE.....

Hivi kweli MAPENZI ni pesa? Mmmmhhh ningeomba tujadili pamoja hapa inawezekana mimi nimeelewa vibaya....Kapulya wenu:-)

Tuesday, July 21, 2015

MAWAZO MAKUBWA YA KUFIKIRISHA .....

Mvulana mmoja maskini alikuwa akiangalia gari la bwana mmoja ambaye alikuwa tajiri, tajiri alimchukua yule mvulani na kumwendesha katika lile gari. Mvulani  akasema una gari nzuri sana. Je? hili gari si ghali sana? Tajiri akamjibu, ndiyo ni ghali sana ila mimi nilipewa na kaka yangu kama zawadi.
Mvulana akawa anafikiri. Tajiri akamuuliza unawaza nini? Ebu ngoja, nawe unataka kuwa na gari kama hili eehh? Mvulana akamjibu HAPANA....NATAKA KUWA KAMA KAKAYAKO!!!

Saturday, July 18, 2015

BUSTANI YETU NA MAENDELEO YAKE...KAZI YA MIKONO YANGU

 Hapa ni MCHICHA upo katika hali nzuri kidogo
 Na hapa ni mboga MABOGA sisi wanguni tunasemana LIKOLO LA NANYUNGU/PITIKU:-)
Na hapa mnaona ndo mara ya kwanza kuchuma hiyo mboga ya Maboga na mchicha na pembeni mnaona ni pilipili. Kwa hiyo kwa jioni ya leo ni kujichana tu. KARIBUNI TUJUMUIKE NDUGU ZANGU:-) ni mimi Kapulya wenu.

Friday, July 17, 2015

SWALI/WAZO LA LEO!

Kama kungekuwepo na ndoto za kununua, je? Ni ndoto gani wewe ungenunua?

Tuesday, July 14, 2015

MSIONA KUADIMIKA NIPO....TUPO PAMOJA

Ningependa kuwanongóneza kuwa nipo likizo. Ila nitajitahidi kuwa nanyi pia kinamna ili tusisauliana..ila mmmhhh kuwasahau ndugu si rahisi...WOTE MNAPENDWA NA TUPO PAMOJA. UTAMADUNI/KIMASAI:-)UDUMU MILELE

Saturday, July 11, 2015

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA UWE MWEMA..

Hili ni vazi langu la leo au mwenekano wangu wa leo na napenda kuwatakia wote JUMAMOSI NJEMA AU MWISHO WA JUMA MWEMA. KAPULYA.

Tuesday, July 7, 2015

NGOMA YA ASILI YA MGANDA KATIKA MKOA WA RUVUMA!!

Ngoma ya asili ya Mganda ilinogesha katika ufunguzi wa stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma Julai 19,2014, stendi hiyo ilifunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiwa Mkoani Ruvuma katika ziara ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo.

Sunday, July 5, 2015

UNAKUMBUKA HII? :-) MAHINDI YA KUKAANGA

Mahindi ya kukaanga:- hapa sasa iwe hii siku kunanyesha mvua basi  ndo utaona utamu wa mahindi ya kukaanga kwa mtindo huu....JUMAPILI NJEMA WANDUGU.

Sunday, June 28, 2015

Friday, June 26, 2015

MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA

Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)