Thursday, June 26, 2014

HIVI NDIVYO YALIVYOKUWA MAPISHI NA MLO WA LEO JION AU SASA HIVI.....

 Ndizi  mzuzu, viazi vitamu. mihogo
 Natanguliza samahani yangu ....hapa ni nyama ya kiti moto
 Ikifuatiwa na kachumbali ambayi ni nyanya, kitunguu, kabichi, limau na pilipili kwa mbaliii bila kusahau chumvi:-)
...na hivi ndinyo ilivyoonekama sahani yangu ...ooh nilisahau kulikuwa na uyoga pia...ila chakula bado kingi kwa hiyo karibuni sana. BASI WALE WENYE JIONI  WAWE NA JIONI NJEMA NA MCHANA WAWE NA MCHANA MWEMA PIA ASUBUHI BASI IWE ASUBUHI NJEMA.  PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA......KAPULYA

12 comments:

Mbele said...

Vyakula vinavutia sana. Upikaji wako sio mchezo. Sidhani kama kuna sababu ya kuomba samahani kwa ajili ya hii kitimoto. Watu sehemu mbali mbali duniani hula vitu vya kila aina, kuanzia senene, hadi kuku, hadi konokono. Waombe samahani kwa nani na kwa nini?

Mimi ni mteja wa kitimoto, likungu, kumbikumbi, na kadhalika. Nina uhuru na haki kamili ya kula vitu hivyo.

Kuna wengine hawali nyama; ni "vegetarians." Siwaombi radhi ninapokula nyama. Sitegemei waniombe radhi wanapokula mboga.

Anonymous said...

Leo ni leo, asemae keshio ni mwongo! Chakulaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Hongera dada kwa mapishi safi kabisa. Ila tu changu naomba unipostie cha kwangu. Jioni njema.

Yasinta Ngonyani said...

Pro. Mbele...shikamoo kwanza za afya. Upo sahihi sikuhitaji kutanguliza msamaha jwa wasikula kitimoto/nguruwe...ila niliona tu nifanya hivyo.

Usiye na jina...kipo njiani chaja wala usikonde.!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta msosi umekwenda shule, unatia shauku na hamu ya ula sema hiyo kitu, kiti-fire.
Wengine tunaogopa mifuta isitupeleke kuzimu mapema. Hata hivyo umekosa kitu kimoja swaaafi yaani lager kama si kasachu. Vinginevyo msosi unashawishi. Una rangi zote muhimu na adhimu Wallahi.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango...toa mafuta yote au nunua filet haina mafuta....nashukuru kwa kuona umepsta shauku ya kula
......hicho kasachu ni nini?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta hayo mafuta hayatoki ukiachia mbali ukweli kuwa kitu yenyewe haramuni.Kasachu ni kanywaji hasa ukivuka mpaka ukaelekea kwenye kaya ya Joyce Banda.

Yasinta Ngonyani said...

Umejaribu? ...ni raha ilioge

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Astaghafilullahi nshasema hii kitu haramuni. Tuache maana mwezi mtukufu ushawadia.

Yasinta Ngonyani said...

KWANI NAWE NI HIVYO?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hapana dada sema huwa si mlaji wa viti wala makochi moto kwa sababu binafsi. Huwa nafunga wakati wa kwenda kulala na kufungua asubuhi kwa kifungua kinywa niamkapo.

Yasinta Ngonyani said...

Haya kakangu nimekuelewa...

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur