Nimekaaa hapa na mawazo tele , nikawa nakumbuka Songea Mahenge hapa ndipo nilipoanza kujitegemea. Na ndiyo nimeona nitoe shukrani zangu za dhati kwa wazazi /walezi wangu. Mama Nachihauli na baba Nyoni ahsanteni sana. Kwa yote mliyonifunza katika maisha na leo najua ni vipi kuishi na watu. MUNGU AZIDI KUWAZIDISHIA MEMA.......Hapa ni mwaka jana 2011 miezi kama hii.
Halafu hapa ni mama yangu wa hiari, baada ya kutoka Songea nikawa naishi Matetereka/Madaba na huko nikakutana na mama huyu. Mama Mgaya. Hakika sina maelezo zaidi ya kumshukuru kwa kunilea kama vile nilikuwa binti yake. Na bado ananilea mpaka leo AHSANTE MAMA kwa yote. MWENYEZI MUNGU NA AKUZIDISHIE UPENDO ULIO NAO Hapa pia ni mwaka jana ni NJOMBE KIHESA.NINAWAPENDA NA NITAWAPENDA MILELE KWA YOTE MLIYONIFUNZA NA MNAYONIFUNZA.
6 comments:
Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako kwa sababu tu amezeeka.Nunua kweli wala usiiuze—hekima na nidhamu na uelewaji.Baba ya mtu mwadilifu hakika atakuwa na shangwe; na mtu anayekuwa baba ya mwenye hekima atamshangilia pia. Baba yako na mama yako watashangilia, naye mama aliyekuzaa atakuwa na shangwe.
Shukrani ni neno lenye herufi chache sana, lakini lina uzito mkubwa mnoooooooo, kumbukumbu nzuri na uzidi kuwakumbuka daima
Kaka Ray hakuna ulichokosea...yote uliyonena na sawa kabisa..Kuishi na wawazi ambao si wazazi wako haswa kuna changamoto zake. Pia kuishi maisha na bibi, babu, nk nako kuna changamoto zake mtu unakomaa mapema kimaisha.
Ester! Ni kweli. Kuwasahau hawa itakuwa siku ya mwisho wa uhai wangu ...ni watu MUHIMU SANA kwangu.
Ni neno jema kumshukuru Mungu na wazazi/walezi. Zaidi kuzidi kuwaombea heri na baraka
umenikumbusha mahenge, nawaona hao Wazee (Baba na Mama Nyoni, aka Kapole) ambao uko nao ktk picha, majirani wa Wazee wangu pale mahenge. safi sana!
Kaka Mathew! Yaani hata kama umeshawashukuru ana kwa ana inabidi uwashukuru tena na pia kama ulivyosema kuwaombea.
Usiye na jina kumbe ulikuwa jirani wangu.?...
Post a Comment