Saturday, December 19, 2009

NARUDI NYUMBANI NA REMMY ONGALA:- Nakwenda kula likolo la nanyungu



Jamani mwenzeni baada ya kazi leo nimefika nyumbani na nikajikuta tu mara moja namsikiliza Dr. Remmy Ongala na mara ukaja wimbo huu NARUDI NYUMBANI.Nusura nilia alipoimba nakwenda kula likolo la nanyungu duh! roho iliniuma kweli. Halafu anasema narudi Songea.... NIMEKUMBUKA KWELI NYUMBANI ndio nikaona niuweka hapa huu wimbo na wengine labda watatamani kama mimi. JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI !!!!

5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yasinta likolo na nanyungu ndo chakula gani maana jinsi ulivyokimezea mate mmh..., Halafu unalifahamu LIZOMBE?

Anonymous said...

likolo la nanyungu na ugali wa mayau uumm sio mchezo,,jamani hapa namaanisha ugali wa muhogo na mboga ya maboga(linanyungu) hapo imetulia umenikumbusha mbali dada nangonyani.

Yasinta Ngonyani said...

Da Mija nadhani jibu umelipata:- Ni kweli LIKOLO LA NANYUNGU ni kingoni na maana yake na mboga ya mabogo na sasa si unajua ni msimu wake basi weeeh! Na ndi dada nalifahamu sana tu LIZOMBE je unataka nikuchezee?

Usiye na jina asante kwa ufafanuzi. Nashukuru kama tupo wengi tunaokumbuka kunyumba. halafu ukosewi chimbondi mwenga kunyumba nga kunyumba,

Anonymous said...

''Chimbondi'' duuh hapo nimecheka kweli. Kama sikosei chimbondi ni karanga za kuungia mboga. ''Nihuka lepi mpaka nimale ugimbi''

Anonymous said...

hermes outlet
cheap jordans
goyard
supreme
off white jordan 1
kyrie 7 shoes
golden goose outlet
hermes outlet
bapesta shoes
off white shoes