Thursday, December 18, 2008

JINSI YA KUPEANA HABARI KATIKA MAISHA YA NDOA

Leo nimeona kichwa kinataka kuongelea mambo mengine na pia vidole vyangu vilikuwa vinawasha sana yaani kutaka kuandika kidogo:- Hivi nimeona tuangalie kidogo jinsi ya kupeana habari katika maisha ya ndoa:-


Je?, umewahi kuamka usingizini asubuhi moja, na kubaki umejinyosha kitandani, ukisikiliza sauti mbalimbali kutoka nje? Huenda bila shaka ulisikia ndege wakiimba. Ikiwa ulisikiliza kwa makini, huenda ulingámua kuwa kila ndege anao mlio wake ambao huitikiwa na ndege mwi ngine wa aina hiyo kwa namna ya pekee. Ikiwa unaishi mjini, bila shaka unapoamka uachukizw na makelele ya magari na makelele mengine mitaani ambapo shughuli nyingi hutendeka. Lakini uendepo shambani au kijijini waweza kusikia tena sauti zote za machweo. Hali kadhalika wawez kusikia wadudu wakiitana katika hali tulivu ya jioni. Kwa hiyo tujue hata ulimwengu wa wanyama kuna kupeana habari.

Kati ya binadamu, kupeana habari ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Ni kitu tunachokihitaji mno. Kwa mfano watoto wanaosoma mbali na kwao hufanyaje? Hukumbuka nyumbani kwa wazazi wao na hupenda kupata habari kutoka nyumbani. Hivyo huandika barua, kwani barua ndiyo njia ya kupeana habari ni nusu ya kuonana.

Je? Wewe huwa unafanyaje upatapo habari njema? Huwezi kunyamaza. Mara unatamani kumwambia mtu fulani ili mfurahi pamoja, unataka kumshirikisha furaha uliyopata.

Katika mada iliyopita kuhusu mapendo nilisema kwamba mapendo hukua na kuendelea. Njia ya kwanza ya kukua kwa mapendo, namna ya kwanza ya kusitawisha upendo ndiyo kupeana habari. Upendo unahitaji kule kupeana habari, na bila kufanya hivi, unakufa. Upendo ukiacha kuongea, basi hauwezi tena kutiririka, hufa.

Tukiangalia neno lenyewe lilivyo katika lugha mbalimbali, twaweza kuelewa kidogo maana yake. Katika nyingi neno la “kupeana habari” ama kuongea pamoja, ama kushirikiana kimawazo, linatafsiriwa ka kusema. KUFANYA UMOJA NA MTU.

Kufanya umoja na mtu


Kupeana habari na mwingine hufanya mtu kuwa na umoja na mtu yule. Kupeana habari ni tofauti na taarifa. Taarifa ni kujulisha kitu au kutoa ujumbe. Kupeana habari kuna mikondo miwili:- kutoa na kupokea mara. Katika kpeana habari uhusiano huzaliwa kati ya watu wawili, kifungo hutengenezw. Kifungo kile kinazidi kuimarika kwa njia ya kuendelea kupeana habari. Kwani ndiyo maana halisi ya kupeana habari. Natoa kitu fulani, napokea kitu kingine. Na ndio msingi wa mapendo.

Kupeana habari ni muhimu sana hivyo hata twaweza kusema kuwa kunalingana na umuhimu wa damu katika mwili. Sote twajua jinsi damu ilivyo ya lazima kwa uhai wa mwili wetu. Kama damu itapata ugonjwa au kudhoofika ni nafsi yetu yote inapata taabu. Vivyo hivyo kama hakuna kupeana habari, hakuna uhusiano na ushirikiano, basi upendo kati ya watu wawili huzidi kuzorota na kudhoofika.

Itaendelea.....!!!

5 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Na hapa ndipo tunapooanisha jina na maudhui. Nasema hivi kutokana na MAISHA tujifunzayo ndani ya MAISHA BLOG.
Wenye la ziada na wanisaidie, lakini kwangu nasema ASANTE

Simon Kitururu said...

Asante kwa hii Dada Yasinta!

Fadhy Mtanga said...

Mi niseme Ahsante sana mno zaidi na zaidi. Kila nikifika humu napata kitu kikubwa cha maisha.
Kazi nzuri.

Anonymous said...

Nimekuja tena yule wa kurekebisha matumizi ya lugha yetu. Pamoja na kwamba mikono ilikuwasha kutaka kuchapa, basi dada ungepunguza kasi ya kuandika, au basi baada ya kuandika ungepitia kidogo. mimi hapo kuna neno moja linanipa kero dada, kwamba ukisoma tena utakuta kuna neno hili hapa "umejinyesha" naona halijakaa mahala pake, maana hiyo shughuli kuifanya kitandani inakuwa hatari kidogo.

du mkorofi mimi,

Ngalilihina.

Anonymous said...

hermes outlet
cheap jordans
goyard
supreme
off white jordan 1
kyrie 7 shoes
golden goose outlet
hermes outlet
bapesta shoes
off white shoes