Friday, October 31, 2008

TUFUNGE MWEZI KWA MICHEZO

Basket, huu ni mchezo wangu ambao naupenda kuliko michezo yote. Na nilipokuwa msichana mdogo nilikuwa naufaidi kweli lakini sasa mmh uzee.

MPIRA WA MIGUU

Hapa ni wachezaji maalufu wa hapa Sweden ni Zlatan Iblahimovic na Henrik Larsson mwaka 2006

SWEDEN NA FINLAND


Natumanini wote mnajua huu mchezo unaitwa ishockey

Thursday, October 30, 2008

KILA MTU ANA NDOTO YAKE KATKA MAISHA

HAPA INAKUJA HADITHI YA JUMA.

Mzee Banzi Kijiwe hujipatia pesa kwa kumlazimisha Juma Kombora kuomba omba mitaani. Wakati mwingine Juma hugoma kuomba mitaani na huwambia Mzee Banzi kuwa anataka kwenda nyumbani kwao Morogoro. Mzee Banzi humpiga sana Juma anapokataa. Juma Kombora ana umri wa miaka kumi tu na pia ni mgeni katika mji wa Zanzibar. Maisha ya Juma ni ya kusikitisha sana na mara nyingi hulala na njaa kwa kuwa Mzee Banzi humwachia pesa kidogo sana.
Juma pamoja na watoto wengine wawili hulala mtaani chini ya usimamizi wa Mzee Banzi. Vijana hawa aliwaleta Mzee Banzi Zanzibar kutoka Morogoro kwa njia ua kuwalaghai wazazi wao.

Juma kabla ya kuja Zanzibar alikuwa anaishi Morogoro na mara nyingi alitumia muda mwingi kuchunga mifugo ya baba yake Mzee Kombora na kucheza mpira wa miguu katika nafasi ya ushambuliaji. Juma alikuwa na ndoto akiwa mkubwa atakuwa mchezaji hodari mwenye uwezo mkubwa wa kupiga chenga za maudhi kama Ronaldo. Lakini siku moja ghafla aliitwa na baba yake na kuambiwa kuwa ataenda Zanzibar na rafiki ya baba yake Mzee Banzi. Mama Juma alifurahi sana siku ya kumuaga Juma maana rafiki wa mume wake, Mzee Banzi, alimpa zawadi mama Juma ya kilo 25 za Maharage na kila 25 za mchele pamoja na vitenge doti mbili. Mzee Banzi na Juma waliondoka Morogoro kwa basi mpaka mjini Dar es Salaam halafu wakapanda boti ya kasi mpaka mjini Zanzibar. Juma alikuwa hajawahi kupanda boti maishani mwake kwa hiyo alifurahi sana kupata nafasi hiyo. Wazazi wa Juma wanaamwamini sana Mzee Banzi na walitegemea atamsaidia Juma kupata kazi nzuri kwenye hoteli za kitalii mjini Zanzibar. Juma hajui wapi atapata msaada amebakiwa na ndoto tu za kuwa huru.

Swali langu:- Kwa nini tunakuwa wapesi kuamini ndugu na marafiki kuwa watatusaidia?.

Wednesday, October 29, 2008

FLAVIANA AKIWA AFRIKA YA KUSINI

Hapa sisemi sana ila angalia tofauti na picha za hapo chini.

UJAUZITO+FURAHA+UASILIA


Yaani hapa anaonyesha kwa nini watu tunapoteza pesa kununua nguo za bei mbaya.Mnajua mara nyingi nimekuwa najiuliza kweli kiumbe hai kitakaaje humu tumboni miezi tisa. Mungu kweli ana miujiza yake. Ila pia akina mama tuna kazi kubwa sana. Ila huu mvao wake nimeupenda.

MAVAZI WAKATI UKIWA MJAMZITO


Hata akina mama wajawazito wanatakiwa kwenda na fashion. Wengi wanafikiei ujauzito ni ugonjwa.

Tuesday, October 28, 2008

JE? HUU NI UUNGWANA KUWADANGANYA WATU HIVI?

Sofia Mhagama mwenye umri wa miaka 16 ameenda Dar es Salaam na Shangazi yake Emilia Soko kutoka katika kijiji cha Mpandangindo mkoani Ruvuma. Sofia ni mtoto watatu kuzaliwa katika familia ya watoto saba. Wazazi wa Sofia hawana kipato cha kutosha kuhudumia familia nzima. Baba yake Sofia, mzee Mhagama ni mzee mashuhuri sana kijijini Mpandangindo. Shangazi yake Sofia aitwaye Emilia Soko alihamia Dar es Salaam kutoka Mpandangindo miaka ya themanini mwanzoni. Tangu Shangazi Emilia alipohamia mjini amekuwa akitembelea kijijini kwao Mpandangindo mara kwa mara. Kila wakati shangazi Emilia alipokuwa anakuja kijijini kuleta zawadi nyingi kutoka mjini pamoja na vitu vingi vya kisasa ambavyo ni shida sana kupatikana kijijini. Kila mtu kijijini aliona kuwa maisha ya Shangazi Emilia yamebadilika sana toka ahamie mjini na kuwa bora zaidi kutokana na vitu na misaada aliyokuwa anawapa wazazi wake kijijini.

Baada ya miaka Shangazi Emilia alitembelea tena kijijini kwao Mpandangindo kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya krismas pamoja na wazazi kama ilivyo kawaida yake alikwenda pia kuwatembalea familia ya mzee Mhagama, baba yake Sofia. Shangazi Emilia alimwelezea mzee Mhagama masikitiko yake juu ya hali ngumu ya maisha ambayo inamkabili mzee Mhagama na familia yake. Emilia alimwambia kaka yake kwamba angependa kujitolea kumsaidia mtoto mmoja wa kike, Sofia. Mama yake Sofia hakuelewa kwa nini Emilia amemchagua Sofia wakati kulikuwa na wadogo zake ambao wangefaidika kielimu maana Sofia alikuwa anasaidia kazi za pale nyumbani. Sofia alikuwa anatambulika sana kwa kipaji cha kuimba kijijini pale. Mama Sofia alihisi kuwa hiyo inaweza kuwa ndio sababu kubwa Emilia kumchagua mwanae Sofia. Mzee Mhagama hupenda sana kumsifia binti yake kwa marafiki zake wakati akiwa anakunywa ulanzi, hupenda kusema "mtoto wangu Sofia ana sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni". Wazazi wa Sofia walikubali kwa shingo upande kumtoa binti yao Sofia maana walikuwa wanampenda sana binti yao.
Sofia kwa sasa anaishi nashangazi yake mjini Dar es Salaam. Shangazi yake aliwaahidi wazazi wa Sofia kwamba akifika mjini, Sofia atapata kazi inayomlipa vizuri na nafasi ya kwenda shule. Kwa bahati nzuri kuna ndugu wengine wa Sofia wanaoishi Dar, kwa hiyo Sofia alijua kuna watu wa kuwategemea wakati wa shida akifika Dar, Sofia hakujua jinsi jiji la Dar lilivyo kuwa ya kwamba ni vigumu kutembea mwenyewe na hata kwenda kuwatafuta ndugu zake ambao wako Dar. Shangazi yake Sofia, naye alivunja ahadi yake: Sofia hakuruhusiwa kwenda shule na amefanywa kuwa mtumishi wa ndani kwa shangazi yake bila malipo. Sofia anafanyishwa kazi masaa mengi na kama akikataa hupigwa na kutishiwa kufukuzwa nyumbani kwa shangazi yake na kuachwa mitaani. Sofia anatamani sana kurudi kwao Mpandangindo kwa familia yake na pia kwenda shule, lakini hawezi.

Swali je? hii ni haki kufanya hivyo?

Monday, October 27, 2008

SIO KUSUKA MIKEKA TU HATA KUKAA SIKU NZIMA KUSUBIRI WATEJA NI MOJA YA KUJITEGEMEA

Sijui kama wenzangu mnaona sawasawa wanauza nini. Ah ngoja niwaambia ni kwenye ndoo ni bamia lita mia nna, kwenye ungo ni uyoga bakuli mia tatu, kwenye ungo mwingine kumbikumbi kikombe mia mbili na halafu karoti fungu mia moja.

SIO BIBI TU HATASISI TUNAWEZA

Kwa nini tumwachia bibi tu hata sisi tunaweza, na sisi watoto tunataka kujifunza pia ili utamaduni wetu wa kiafrika usife.

UTAMADUNI+KUJITEGEMA+ RAHA


Ngoja leo tuangalie utamaduni wetu. Bibi ametulia na anasuka mkeka safi sana

Sunday, October 26, 2008

MAISHA YA ZAMANI NA SASA

Jamani leo nimeamka na nimekumbuka maisha ya miaka ya 1970-1980. Kulikuwa na shule moja kila kijiji, kanisa moja kila kijiji, rais mmoja, pia chama kimoja. Leo Je? Mmh. kila kijiji kina shule zaidi ya kumi, sekondari pia, makanisa ndio usiseme kila upande ugeukao yamejaa. Rais, saw bado mmoja, lakini vyama sio kimoja tena ni 13 au zaidi. Binafsi nimepata kiwewe kwani sijui maisha yepi ni mazuri ya miaka ile au sasa. Je wenzangu mna maoni au?

Saturday, October 25, 2008

CHAKULA+HAMBAGA+KOKA-KOLA ULANZI NA KOMONI


Jamani, wote karibuni tushiriki chakula hiki. Hakika siwezi kumaliza hambaga yote hii. Ila chizi haipo ya kutosha na kwa mnaotumia koka-kola ipo ya kutosha tu. Ulanzi na komoni pia myakaya vipo, na mnaotumia vinywaji vingine mje navyo wenyewe. KARIBUNIIIIII.

BABU ANAITWANGA MBEGE/ POMBE YA NDIZI

Karibuni jamani leo si jumamosi. Angali babu alivyoishikilia hiyo nusu. Karibuni kumsaindia

USAFIRISHAJI WA ULANZI



Hapa tayari ulanzi unatoka kuchokuliwa na sasa ndio unapelekwa kwa wateja. Kuna njia nyingi za kujitafutia maisha na pia ushafirishaji.

Friday, October 24, 2008

KWA AJILI YA WIVU AMEPELEKA CHUPI YA MKEWE IPIMWE DNA

Hiki ni kisa cha Antoni na Ana. Baada ya miaka 18 ya ndoa, Ana hataki tena kufanya tendo la ndoa na Antoni. Na Antoni ameshuhudia kwa macho yake mkewe Ana akipigwa busu na mfanyakazi mwenzake wakati wakiwa wanasubiri basi kwenda kazini. Halafu amekuta picha ya yule mwanamume aliyembusu mkewe kwenye pochi ya Ana.

Kwa hiyo hapo inaonyesha ya kwamba Ana anatoka nje. Na Antoni hayaamini maelezo ya Ana kwa nini hataki kufanya tendo la ndoa naye wala kubuswa. Antoni anasema katika maisha yake hakuweza kuwaza ya kwamba mkewe Ana angeweza kumtendea hivyo. Hakujua kama hangeweza kumwamini mke wake,

Majibu ya DNA yamerudi ni kweli kulikuwa na shahawa kwenye chupi, lakini asilimia 100% zinaonyesha kuwa ni shahawa zake yeye Antoni. Baada ya hapo aliamua kuacha kila kitu na pia kutokuwa na haraka za kupeleka vyupi vya mkewe kwani inaonyesha ulikuwa wivu tu. Kwa hiyo tangu siku ile Antoni na mkwe Ana walikuwa na furaha na amani tena katika ndoa yao.

Ana pia alielewa kwa nini mume wake Antoni aliangaika kupima chupi na kumfikiria vibaya. Antoni anasema sasa anamwamini mkewe katika maelezo kuhusu hisia ambazo alikuwa nazo kwa mfanyakazi mwanzake ya kuwa ilikuwa sio mapenzi.

Antoni anasema, Wakati wa kufanya tendo la ndoa alikuwa na makosa kwani aliamini mke wake anatoka nje. sasa mapenzi yao huwezi kufananisha na miaka yote iliyopita, anasema Anton.
SWALI:- Je? ungekuwa wewe ndio ungefanya kama alivyofanya Antoni?
Na J? ungekuwa wewe ndio Ana ungefanyaje?

Thursday, October 23, 2008

DAR ES SALAAM/NYUMBANI



Habari zenu watu wa Tanzania(Bongo) leo nimekuja kuwatembelea, kutoa jasho kidogo kwani hapa swedeni baridi imeanza sasa. Bahati yangu naweza kuwa Tanzania (Bongo) wakati wa baridi ha ha ha ha haaaaaaaa.

PEMBA -ISLAND


Sio nyasa tu hata hapa pazuri au mnasemaje. Najua Kaka Markus atabisha tu shauri yako utajiju mambo ndiyo hayo tena

LAKE -MANYARA


Kwanza nilifikiri nimefika mbinguni, kwa kweli watanzania inabidi tujivunie sana nchi yetu nzuri.

Wednesday, October 22, 2008

MALARIA NI UGONJWA HATARI

Habari za ziku mbili hizi nilikuwa katika harakati za kuitafuta picha hii. Ngoja tuiangalie kidogo nadhani wote mmegundua ni nini. Hata hivvyo nitawaeleza kidogo.




Hapa ni mnaona jinsi malaria yanavyoharibu chembechembe za damu(blood cell) katika miili yetu. Malaria aina hii yanaitwa malaria malaria. Ilikuwa mwaka 2001 wakati tulipokuwa Tanzania, nilitaka kumpoteza mume wangu kwa homa hii ya malaria. Nina maana vidudu hivi vya malaria mnavyoviona vilikuwa mwilini mwake.

Sunday, October 19, 2008

MAISHA BAADA YA KIFO

Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swalihili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengene wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, baada yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katka nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifa wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.

JAMHURI YA SAHARA MAGHARIBI


Marocco ilijitoa kwenye Umoja wa Nchi Huru za Afrika Mwezi Novemba 1984 baada ya Umoja huo kuitambua rasmi Jamhuri ya Sahara Magharibi kama Nchi Huru.

UMOJA WA NCHI HURU ZA AFRIKA

Umoja wa Nchi huru za Afrika uliundwa tarehe 25 mei 1963 na Nchi Huru 32 huko Addis Ababa. Malengo ya Umoja huu ni kudumisha Umoja wa Udugu baina ya Wanachama wake, Ukoloni katka Afrika na kukuza ushirikiano wa Kimataifa. Baraza la Wakuu wa nchi hizi hukutana kila mwaka kuratibu masuala mbalimbali ya Kisiasa, Kiutamaduni, Afya, Sayansi na Ulinzi. Mpaka mwaka 1987 Umoja huu ulikuwa na Wanachama 50

BENDERA ZA CHAMA CHA SWAPO+CHAMA CHA ANC+CHAMA CHA PAC


Chama cha SWAPO kinachopigania Uhuru wa Namibia, Vyama vya ANC na PAC vinavyopigania haki na kupinga siasa ya ubaguzi wa rangi huko Afrika ya kusini, vinashiriki katka vikao Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kama wasikilizaji

Friday, October 17, 2008

KICHOCHO (Biliharzia) NI UGONJWA HATARI

Ngoja leo tuangalia kidogo magonjwa kwani ndiyo adui mkubwa katika maisha ya binadamu:-

Namna ya uambukikizwaji

Kichocho ni ugonjwa usababishwao na vijidudu ambavyo mtu hupata anapotumia maji yaliyo na vijidudu vya ugonjwa huu hashwa katika nchi za kitropiki. Bilirhazia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Viini vilivyokomaa huishi katika mishipa katika kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa.

Mayai yanapokuta maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi, ambao hupenya konokono hawa wa majini. Katika konokono hawa wa majini viluwiluwi huwa hukua na kuongezeka na kutoka. Viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya kwenye ngozi na wakisha penya huingia hadi kwenye mishipa ya Ini ambapo hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu na haja kubwa.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka mitatu na nusu lakini huweza kuwa zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpaka na kibofu husababisha athari kubwa. Maambukizi yasiyotibiwa husababisha matatizo ya Ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Wakati mwingine mayai huingia katika uti wa mgongo au mara nyingine katika ubongo.

Jinsi ya kujizuia

Inasemekana hakuna chanjo iliyopatikana. Katika nchi ambazo ugonjwa huu upo, inadidi kujitahidi kuepuka maji ambayo si Safi na salama. Usidhani ya kuwa maji yoyote ni safi na salama katika sehemu zenye ugonjwa huu. Kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea, hizi ndizo sehemu za hatari.

Fukwe za bahari na fukwe zilizo na mawimbi si rahisi kuwa na konokono wa majini, hivyo hizi sehemu zinaweza kuwa salama. Viluwiluwi huweza kuishi kwa masaa 48 baada ya kutoka kwa konokono na huweza kusafiri mwendo mrefu, kwa sababu hii maeneo yenye maji katika sehemu zenye ugonjwa huu hayawezi kuwa salama kabisa.
Maziwa katika nchi ya Tanzania na Malawi yana vimelea vya kichocho, lakini fukwe nyingi karibu na mahoteli ya kitalii yana uoto mdogo wa mimea hivyo huwa ni sehemu ambazo si rahisi kupata ugonjwa huu.
Mabwawa ya kuogele ni salama kama yana dawa ya klorini(chlorine) na hakuna konokono wa majini.
Bahari ni salama
Maji ambayo yamatuama kwa siku tatu ni salama endapo hakuna konokono wa majini.Maji ya kuoga yanayochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mito na maziwa yanaweza kusabaisha maambukizi.

Namna ya kujikinga na kichocho

Kama uanapopalilia, vaa mabuti marefu ya mpira. Viluwiluwi hawa hufa haraka mara tu wanapokuwa nje ya maji na hawawezi kuepuka kifo. Nguo na ngozi zenye maji zikikaushwa kwa haraka husaidia kujikinga na maambukizo.

Dalili za maambukizi
Wasafiri wengi walioambukizwa huwa hawaonyeshi dalili yeyote ya ugonjwa huu
Kunakuwa na mwasho katika sehemu alipoingilia kimelea kama “mwasho wa muogeleaji”.Unapata homa baada ya wiki nne baada ya kutumia maji yaliyoambukizwa. Unapatwa na kikohozi kikavu ndiyo dalili ya hatua hii ya maambukizo. Kupungua kwa uzito na kujihisi kuchoka. Damu katika mkojo na haja kubwa kama ugonjwa umekomaa. Na pia kuvimba kwa miguu. Na muda wa kuambukizwa huchukua wiki nne (4) kwa mayai kuonekana katika choo na kuonekana kwenye mkojo. Lakini hata hivyo ikishajua tu umetumia maji yenye vimelea basi inabidi uchunguzi ufanyike miezi mitatu baada ya kutumia.

Tiba ya kichocho
Kichocho hutibiwa na madawa maalumu dhidi ya vimelea hivi ambazo hupatikana katika kliniki na hospitali yoyote ile iliyo karibu na makazi yako. Ni vizuri kupima mara kwa mara unapopatwa na mashaka ya kuambukizwa na kichocho hasa baada ya kutumia maji yenye vimelea vya kichoccho

RAMANI YA TANZANIA NA MBUGA ZAKE


Naipenda nchi yangu, Tanzania ni nchi yenye amani katika Afrika.

SERENGETI NATIONAL PARK


Kuna mtu anaweza kuniambia anaona nini katika picha hii. au niseme ni wanyama gani hao. Hapa picha hii ni mapema alfajiri nimepiga.

TARANGIRE NATIONAL PARK

Angalia tembo wanavyofurahia maisha

MBUGA ZETU


Hapa ni Ruaha National Park

Wednesday, October 15, 2008

KUMBUKUMBU+HISTORIA

Leo nimekumbuka kweli mika ya tisini; wakati nilipokuwa nasoma Songea. Familia yangu walikuwa wanaishi kijiji kimoja kiitwacho Kingoli. Sijui nisemeje ili mnielewe kwani wengine msije mkasema ni kudeka tu. Haya semeni mtakavyo. Yaani nilikuwa natembea toka Kingoli mpaka Peramiho kwa miguu kulikuwa hakuna magari. Pale kijijini kulikuwa na lori moja tu lilikuwa linasafiri kwa wiki mara moja.

Baina ya Kingoli mpaka Peramiho kuna vijiji kama vitano hivi, hivi safari hiyo ilikuwa inachukua siku moja – mbili nilikuwa nalala katika kijiji kimoja kiitwacho Mgazini. Wakati mwingine sikuwa na maji wala chakula, na kama nilikuwa na chakula basi nilikuwa na (CHIMBONDI) = karanga zilizokaangwa na kutwangwa pamoja na chumvi. Au kama ni ule msimu wa maembe basi kuzitwanga kweli embe. Kwani wengine wana maisha ya raha, wengine ya kuteseka, ndugu zangu hivyo ndivyo maisha yalivyo.--

Tuesday, October 14, 2008

MWALIMU ENZI ZA UJANA WAKE

Kuzaliwa ni bahati kufa ni lazima hayo ndio maisha.

NYERERE AKIWA NA MAMA YAKE NA MKEWE


Maisha kweli ni safari ndefu sana. Wengine safari zao zinakuwa ndefu na wengine huwa fupi. Na wengine safari zao huwa za furaha wengine za matatizo.

BABA WA TAIFA AMETUACHA


Hapo ni mwishini mwishoni wa maisha yake

KUMBUKUMBU YA MANENO ALIYOSEMA HAYATI BABA WA TAIFA JULIUS K. NYERERE

"Uongozi unaweza ukwa mzuriau mbaya, au usijali, lakini kama watu wameamka na wanajitambua wenyewe, kutoshirikishwa kwa mawaza na tabia ya jamii hakutaendelea kwa muda mrefu".

NYERERE:- BORA NINGEKUWA MHUBIRI WA DINI KULIKO KUWA RAIS WA NCHI!

Baadhi ya maneno ya hayati Mwalimu, alipofikisha umri wa miaka 50"..Wakati nikiwa Makerere, niligundua kwamba serikali ya nchi yangu ilikuwa ikinilipia kiasi cha paundi 80 kila mwaka kwa ajili ya elimu yangu. Lakini hio haikuwa na maana kubwa sana kwangu, isitoshe paundi 80 ni chembe ndogo tu ya kiasi cha jumnla ya pesa zinazokusanywa na kutoka kwa walipa kodi wa nchi yangu, yaani wa-Afrika. Leo hii, paundi 80 ziimeongezeka thamani yake na kuwa na maana kubwa kwangu. Siyo kwamba ni zawadi muhimu tu na tunu kwangu, lakini pia ni deni ambalo kamwe sitaweza kulilipa.""Sina uhakika kama wengi wetu wamepata kufikiria kwamba wakati paundi 80 zilikuwa zinatyumika kunitunza mimi kule Makerere, hela hizo zingeweza kujenga Zahanati angalau mbili katika kijiji changu au chochote kingine Tanzania."".. Inawezekana kabisa kuwa wananchi walikuwa wanakufa kwa ukosefu wa dawa kwa sababu tu ya kukosa paundi zile 80 zilizokuwa zikilipwa kwa ajili yangu. Kwa hiyo kuwapo kwangu chuoni kuliinyima jamii huduma ya wale wote ambao wangeweza kusomeshwa kwenye shule chini ya miti, na kuwaandaa kina Aggreys na Booker Washingtons, Je nitawezaje kamwe kutolilipa hilo deni kwa jamii yangu hii?.""Jamii inatumia fedha zote hizo kwa ajili yetu kwa sababu inataka tuwe nyenzo za kuiinua jamii hiyo. Kwa hiyo lazima siku zote tubakie chini ya jamii hiyo na kuhimili uzito wote wa wananchi ambao wanahitaji kuinuliwa, na lazima tusaidie kuifanya hiyo kazi ya kuwainua wananchi wasiojiweza"Wakati nikisoma matukio yaliyojiri kuelekea kifo cha Babu (Sokoro) kama tulivyozoea kumuita, machozi yamenidondoka sio tu kwa sababu ya kuondokewa na mtu muhimu kwangu na Taifa, bali pia kwa kukosa nafasi ya kutimiza nadhiri yangu ya kumpa shukrani japo ya ahsante kwa mema aliyonitendea mimi pamoja na mafanikio aliyonitabiria tarehe 2.1.1987. Pia nalia kwa sababu baada ya kuonana naye wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba mwaka 1999, sikumuona tena zaidi ya alipokuwa ndani ya jeneza pale Msasani na Butiama.Lakini nalia zaidi ninapokumbuka kuwa baada ya kifo chake, watu wengi wamikuwa victimized kwa sababu ya misimamo ya kiuadilifu. Wazalendo wamekuwa wakitemewa mate na kupewa majina ya huyo siyo MWENZETU (katika ufisadi) n.k. Waovu katika jamii wamepewa majina ya Huyo mjanja n.k. Nitaendelea......... machozi yamelowanisha Key Board mpaka imestark.

Monday, October 13, 2008

JIKO LA MAFIGA MATATU


Leo nimekumbuka wakati nilipokuwa mdogo kazi za jikoni ndio zilikuwa zangu kuchochea mboga(maharage) kupika ugali nk

MAJI

Maji ni kitu muhimu sana katika maisha ya sisi binadamu. Tena tunahitaji maji safi na salama.

KUJITEGEMEA

Nipo sokoni nauza dagaa lakini tangu asubuhi sijapata hata mteja mmoja. Maisha ya kutafuta pesa kazi kweli


Sunday, October 12, 2008

JE? NI VIGUMU KUISHI BILA NGONO?

Wengi tunajua/pia tunajadili ukimwi na ngono, lakini tunahitaji kukumbuka kuwa sio waTanzania wote ama binadamu wote ni hivyo. Cha muhimu ni kuelewa kuwa ugonjwa huu unaua binadamu, na kwamba, hawa binadamu wanatokea katika kila sekta ya maisha, wanadini, wapagani, wasio na elimu, wenye elimu, wamjini, wanavijiji, nk.
Je? kuna ubaya gani kuwaelimisha wengine kuhusiana na matumizi ya ndomu?

Tukumbuke ya kwamba baada ya Hawa na Adam kula lile tunda baya, sote tulizaliwa madhambini, na tunashawishika kirahisi. Yaani, hata Hawa na Adam , ghafla waligundua ya kuwa wako uchi, nadhani mle bustanini kulikuwa kuzuri na kulikuwa na hewa bora yaani jua lilikuwa haliwachomi, majani hayakuwakata ..walipofukuzwa ndio walilazimika kuvaa nguo kwa sababu ya jua kali, mavumbi, miiba nk. Hakuna aliyewaamrisha kuvaa nguo.

Ngono inashawishiwa maishani kwa mbinu nyingi ambazo ni vipofu tu wasioziona. Katika magazeti, mavazi, sinema, hadithi za waliojaribu, umbea nk. Ni kama vile Hawa na Adamu, walivyoshawishika kula lile tunda hata walivyojua Mungu wao aliwakataza, lakini sisi wengine tuanashawishika kirahisi kula hili tunda liitwalo "ngono". Wote tunajua tukishalionja tunda hata yeyote akikuambia "basi acha" wengi tunacheka ana kushangaa? Hii in kama vile mtoto akishaonja pipi, halafu ategemewe kutotamani pipi mbeleni.

Pipi zitakuwepo duniani kwa miaka mingi, vishawishi vya ngono vitakuwepo duniani kwa miaka mingi... Hii ndio sababu tunahitaji kuelimishwa kuwa pipi si nzuri kiafya. Lakini pia tunahitaji kuelimishwa kuwa wale watakao tamani basi wale nyingina wasisahau kupiga mswaki. Naamaanisha, ujembe wa kuacha ngono uambatane na ujumbe wa kupunguza kufanya ngono na watu wengi NA elimu ya kutumia ndomu.

Saturday, October 11, 2008

LIZOMBE NGOMA YA WANGONI


Oktoba Mosi huwa siku ya wazee. Hapa unaona wazee wakiwa wakiselebuka kwa ngoma ya Lizombe katika Manispaa ya Songea, kwenye bustani ya Manispaa Songea.

UZURI+ MAZINGIRA+ UTULIVU

Hapa ningependa kusimama na kuangalia na wala sichoki maana panapendeza mno.

MILIMA YA URUGURU

Nipo Moro mji usio na maji(Ziwa)

Friday, October 10, 2008

BAADHI YA MANENO YA KISWAHILI NA MAANA YAKE

Leo nimeona nijikumbushe kidogo maneno ya kiswahili kisije kikaniacha. Kama si sahihi naomba msaada:-

Muungwana = Mtu mwenye adabu na desturi njema, Mtu anayekaa na binadamu wenzie kwa uzuri, mtu mwenye utu. Pia unaweza kusema mtu asiye mtumwa au jina la heshima analoitwa mtu.

Mvumilivu = Mtu anayestahamili taabu au mambo mazito (mstahamilivu).

Ngangari = Mtu mwenye msimamo.

Fadhila = Wema, ukarimu, hisani, huruma.

Wema = Ni hali ya matendo mazuri.

Ukarimu= Utoaji vitu au mali kwa kukaribisha watu au kuwasaidia wanaohitaji msaada bila ya malipo. Ni kinyume cha ubahili.

Hisani = Moyo wa kutaka kutenda mazuri kwa ajili ya mwingine.

Huruma = Moyo wa wema; imani, rehema na upole.

1. Imani ni mambo anayokubali mtu kuwa ni ya kweli na anayopaswa kuheshimu hasa katika dini: itikadi. Na pia ni maoni ya moyo yanayomfanya mtu awe na mkabala fulani juu ya jambo au kitu.

2. Rehema ni neema anazopata binadamu kutoka kwa mwenyezi Mungu. Na neema ni hali ya kuweko na uwingi wa nafasi; hali ya kutoweko shida au upungufu wa vitu vya kumuendeshea binadamu maisha; baraka na ustawi. Pia ni jambo jema analopata kiumbe kutokana na uwezo wa mwenyezi Mungu; riziki.

3. Upole ni hali ya kutopenda fujo, hali ya mtu mtulivu na mtaratibu.

Thamini = Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii.

Na mwisho ni Si bitozi = Asiyejisikia.

Thursday, October 9, 2008

TANZANIA +AFRIKA


Hapa sisemi sana semeni ninyi. Naona fahali sana kuwa mtanzania/mwafrika

UREMBO UNATAKA MOYO

Vijana wa kimasai wapo kazini wakiwasuka akina dada. Inasemekana kwamba vijana hao wa kimasai ni wasusi wazuri kipita maelezo. Wengi wanajiuliza kama kuna usalama au?

WANA UREMBO+MITINDO


Sio mwingine tena ni Flaviana Matata na mwenzake Nancy Abraham Sumari

HELENI

Ukivaa ni hizi uwongo mbaya

UASILIA/UZURI

Mwanamke wa kimasai katika utamaduni wao. napenda sana mambo ya asili.

BANGILI


Napenda sana vitu vya asili kuliko vya kisasa.

Wednesday, October 8, 2008

MAISHA NA MAZINGIRA

Leo mwenzenu nimeamka vibaya, Kwani nimekasirika sana. Kisa ni kwamba nimekuwa nimefikiri muda mrefu ni vipi watu wanaweza kufanya hivi. Yaani siku zote hizi nilikuwa nimefungwa kabisa. Leo ndo naamka na nimekasirika mno. Mazingira, nani alisema watu wanaruhusiwa kumiliki maji au niseme nusu ya bahari. Watu wageni wanatoka huko na mihela yao na kuja nchi za wengine na kuamua yeye anamiliki nusu bahari. Kwa mfano Jangwani Seabreeze Resort, mtu anatoka huko Pakistani na kujengelea fensi ile wenye nchi wasiwe huru kwa nini? Na kwa nini wengine wanakubali kulipa pesa nyingi kwa sehemu ambayo Mungu ameifanya ili watu wote wafurahie maisha. Lakini sasa ni wachache tu wanafurahia. Kwa kweli naumia sana kuona wananchi hawana uhuru kwa sababu ya mtu ana pesa na katoka huko PAKISTANI. WATANZANIA TUSIWE HURU KATIKA NCHI YETU. Bado sielewi kwa nini? Je? wenzangu mnaelewa?

UZURI+UPENDO+MAPENZI

Jamani tuache uongo hapa mahali kwa kweli nimepapenda sana. Angalia jinsi palivyo, raha sana.

SASA TUPO KWENYE KIKAO CHETU


Karibuni wote wapenzi wa ulanzi. Tena huu ule ndio ule mkangangafu usiwe na wasiwasi kuna ule mtamu.

MBETA YA ULANZI


Leo nimetembele kijiji changu nilipoishi zamani ni maalufu sana kwa ulanzi hapa ndo wanakinga ulanzi kwenye mbeta.

AKINA MAMA WANAPIKA POMBE ZA KIENYEJI

Kutafuta pesa nako ni kazi na kuna aina mbalimbali za kutafuta pesa kama hapa akina mama wanajiwezesha kwa kupika pombe.

BIA POMBE ZA KIWANDANI


Hapa ni ndovu, serengeti, kilimanjaro, safari, pilsner na tusker

Tuesday, October 7, 2008

MAISHA YA NDOA

Kuna wasichana na wavulana wengi ambao wanaishi maisha ya ndoa bila kuyafurahia maisha kama inavyotakiwa. Kuna wengine wanaolewa/oa bila kufikiri kwa busara. Wanakuwa na haraka/hawapangi kwa utulivu wala makini. Na kuna wengine wengi wanaolewa/oa bila hiari kwa lazima yaani inakuwa ni lazima kufanya hivyo ili wanafamilia/ndugu wafurahi au pengine sio wafurahi isipokuwa kwa kuwatesa. Au kuwaonyesha ni nani anaweza kuyatawala maisha yake.Yaani hii yote inatokana na kuwa na hasira, pia kwa vile hakuna mtu mwingine anayemsaidia msichana au mvulana huyu ni nini aamue. Na baada ya ndioa, miaka inapita na akili zinaongezeka na ndipo anapogundua uamuzi aliouchukua haukuwa wa busara. Basi anaona hakuna maisha tena katika dunia hii. Sasa labda itakuwa tatizo kuamua tena uamuzi wa kuondoka/achana kwani sasa ameshakuwa mama/baba.Kwa hiyo wasichana na wavulana wote msioolewa/oa kaeni chini na tafakarini kwa busara, kweli huyu kijana/msichana ni ndiye mungu aliyenipangia kuishi naye miaka yote? Kweli ni mapenzi au kuna kitu nakikimbilia? Pia jaribuni kuwa wachumba kwa muda mrefu kwani hapo ndio mtaweza kujuana tabia na kuona kama kweli ni mapenzi ya kweli aula.

Jambo jingine ambalo limekuwa likinisumbua sana akili yangu, ni kwamba kwa nini? Wazazi wengi wanapenda sana kuingilia uamuzi wa watoto wao. Nina maama kwa nini mabinti na vijana wasichague wenyewe wenzi wao ambao wataishi nao maisha yao yote. Hivi ni nani ataishi na msichana au mvulana huyo? Wazazi, msichana au mvulana? Nimekuwa nikijiuliza hili swali miaka yote tangu nipate akili. Lakini bado sijapata jibu na bado naona katika jamii nyingi za kiafrika zinaendelea na tabia hiyo. Najue wengi watasema nimesahau utamaduni/mfumo wa maisha ya kiafrika. Eti wazazi wanasema sisi hatumtaki/ hatuutaki kijana/binti/ukoo huu. Na ukijaribu kuwaeleza haya ni maisha yangu na ni mimi ndiye ninayempenda kijana au binti huyo na ndiye nitakayeishi naye. Na hii imewafanya baadhi ya mabinti na vijana kuchukua uamuzi bila kuwaza kwa makini/busara au utulivu. Na matokeo yake yanakuwa hakuna raha katika ndoa, na mwisho huanza kuwaza mawazo mabaya na hata inaweza ikatokea hatari kubwa katika maisha.

Monday, October 6, 2008

NYWELE+UZURI+NDESANJO

Hawa ni wafuasi wa vuguvugu la wapigania uhuru nchini Kenya Maumau. Hizo nywele ni zoa

Ndesanjo akiwa Dakar
Asante kwa picha hizi nzuri kaka Ndesanjo

Friday, October 3, 2008

MAISHA YA KAZI

Ungekuwa wewe unafanya kazi halafu unaona mfanyakazi mwenzako anafanya mambo si mazuri. Yaani kinyume na sheria. Je ungemwita na kumwambia au ungemwacha tu aendelee. Kwa sababu naona kuna watu wengi wanasema/wanatetena fulani yule mmh anatabia mbaya sana au angalia kwanza anategea kweli, hafanyi kitu. Hasa sisi akina dada/mama. Kwa nini usimwite na kumwambia/ongea naye, pengine yeye anaona anafnaya kazi nzuri kabisa. Je wote tupo hivyo

Thursday, October 2, 2008

MBUGA + MLIMA KILIMANJARO NA UZURI WAKE

Hakana wanyama niwapendao kama Twiga angalia jinsi wanavyopendeza shingo ndefu pia miguu yao mirefu. Hapa ni Mbuga za wanyama Ruaha mwaka jana.
Angalia panavyopendeza


Wwamenuia kuungea mlima sijui kama watawez. Kilimanjaro yetu.


Barafu katika mlima Kilimanjaro. Angalia kunavyopendeza huwezi kudhani ni Afrika-Tanzania. raha kweli