Thursday, October 9, 2008

UREMBO UNATAKA MOYO

Vijana wa kimasai wapo kazini wakiwasuka akina dada. Inasemekana kwamba vijana hao wa kimasai ni wasusi wazuri kipita maelezo. Wengi wanajiuliza kama kuna usalama au?

3 comments:

  1. Kazi kwelikweli, wamejipatia ajira.

    ReplyDelete
  2. Yasinta mimi huwa nafikiria masaa mengi yanayotumika katika shughuli hii. Hivi mwanamke hawezi kuwa mrembo bila kuuteketeza muda wote huu kubandika nywele za bandia?

    Mimi naona nywele za waafrika ni nzuri bila hata kuhitaji kuzalisha ajira za aina hii. Nadhani.

    ReplyDelete
  3. Ndiyo kaka mbilinyi hapo tayari wamejipatia ajira.

    Na ndiyo kaka bwaya kweli kabisa nyweli za kiafrika ni nzuri kama zilivyo. Lakini kama ujuavyo sisi binadamu(wanawake ) hatutosheki na kile tulichopewa na muumba wetu.Ni kweli kabisa mwanamke anaweza kuwa mrembo bila kuweka hayo mabandia. kwani mimi sidhani kama urembo/uzuri ni nywele za bandia.

    ReplyDelete