Sunday, October 26, 2008

MAISHA YA ZAMANI NA SASA

Jamani leo nimeamka na nimekumbuka maisha ya miaka ya 1970-1980. Kulikuwa na shule moja kila kijiji, kanisa moja kila kijiji, rais mmoja, pia chama kimoja. Leo Je? Mmh. kila kijiji kina shule zaidi ya kumi, sekondari pia, makanisa ndio usiseme kila upande ugeukao yamejaa. Rais, saw bado mmoja, lakini vyama sio kimoja tena ni 13 au zaidi. Binafsi nimepata kiwewe kwani sijui maisha yepi ni mazuri ya miaka ile au sasa. Je wenzangu mna maoni au?

5 comments:

  1. Binafsi naupenda sana mfumo tulio nao wa sasa ingawa unaweza kuwa na mapungufu yake pia.

    Maana naamini kuongezeka kwa shule ni maana yake pia kuongezeka kwa idadi ya watu kujiunga shule ila HOFU yangu je hiyo idadi inapata kile kinachohitajika? Yaani Elimu BORA au wanapata BORA elimu?

    ReplyDelete
  2. Mimi naona kama kadiri tunavyosonga mbele ndivyo tunavyorudi nyuma.

    ReplyDelete
  3. asanteni edwin na bwaya binafsi naona hakuna kinachoendelea kwa kweli shule nyingi lakini naamini hakuna elimu BORA tunazidi kurudi nyumba kabisa

    ReplyDelete
  4. Na si tu kwamba tunaendelea kwa mwendo kasi hasi, bali kwa spidi ya kufumba macho kabisa.

    ReplyDelete
  5. Je sasa tufanyeje ili macho yetu yafumbuke?

    ReplyDelete