Friday, June 29, 2012

MAISHA:- NIMEGUSWA SANA NA HABARI HII NA NIMEKUMBUKA MENGI, AMA KWELI MAISHA NI CHANGAMOTO KUBWA YA MAISHA!!!


MAMA MJAMZITO AKIPELEKWA HOSPITALI
Ni juzi tu nilikuwa nasikiliza/angalia habari. Mama mmoja mjamzito alipatwa ghafla na maumivu ya tumbo. Na alipotoa taarifa kwa gari la kubeba/kuchukua wagonjwa lilichelewa kuja . Lilikuja baada ya kama nusu saa. mama mjamzito huyo maumivu ya tumbo yakazidi na akawa anatoka damu. Alikuwa na ujauzito wa miezi saba. Kiumbe kilizaliwa kimekufa.....
Na ndiyo nimekuja kukumbuka jinsi wanawake wengi wanavyo poteza maisha kutokana na umbali wa hospitali na usafiri. Nakumbuka wakati tunaishi kijiji cha Kingoli kulikuwa  na gari moja la kijiji, duka moja kanisa moja, shule moja. Sasa hapo mtu uwe mjamzito hakuna nafasi ya kupona kama kunakuwa na shida kama ya huyu mama. Maana kutoka hapo kijijini hospitali ni Peramiho na kufika huko ni siku mbili kweli kuna kupona hapa? Ndo nikawa najiuliza sasa kama unapiga simu na watu wanachelewa kuna kuna maana gani sasa si sawa na kule kwetu Kingoli tu baiskeli au machela.... Ebu tumalizie   kijana Side boy na wimbo huu JIFUNGUE SALAMA...

IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA.!!!

Wednesday, June 27, 2012

KWELI ZILIPENDWA HASWA!!!!

NI KILE KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO YA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUWA HAPA HAPA YAANI NDANI YA BLOG HII KWA KURUDIA NA PICHA HII NILISHAWAHI KUIWEKA  KWA KUKUMBUSHA ANGALIA HAPA KAPULYA. KARIBUNI SANA.....
Kitu kimoja nasikitika sina picha ambayo nilikuwa kabinti kadogo sana. Najiuliza sijui nilionekana vipi lakini sipati jibu. Panapo majaliwa tuonane tena JUMATANO IJAYO....Kaaaazi kweli naipenda zamani/zilipendwa kwa kweli..inaonekana niliupenda huo mpapai au sijui ndo ulikuwa mtindo kusimama kwenye miti..LOL

Tuesday, June 26, 2012

JE HAPA NI ILE NJOO TULE BASI.....AU?

Hata wanyama na ndege nao wana tabia kama BINADAMU...unafikiri hapa JOGOO ANASEMA NINI KWA HUYU KUKU JIKE?

NENO LA LEO!!

Kama vyakula ulavyo sio vizuri kwa mwili wako, basi angalia viwe ni vizuri kwa ajili ya nafsi yako.
SIKU NJEMA KWA WOTE...KAPULYA

Monday, June 25, 2012

Tuanze jumatatu hii kwa kuangalia jinsi watu walivyo:- Malezi ya watoto/Ukatili Kwa Watoto


Watu /binadamu tumeumbwa tofauti , labda pia ni jambo la kumshukuru Mungu. Maana fikiria kama wote tungekuwa wakatitili sijui ingekuwaje? Na kama wote tungekuwa wema sijui ingekuwaje??

Sunday, June 24, 2012

NI JUMAPILI YA MWISHO KATIKA MWEZI HUU NAMI NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA LA KHERI!!!

Tupeni wavu upande wa kulia nanyi mtapata samaki Yn 21:6.
NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA.

Saturday, June 23, 2012

ULANZI, ULANZI UNAPITAAAAA!!!

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA ILA, KUMBUKA POMBE SI MAJI ....HAYA KILA LA KHERI...NIMEJIULIZA MARA NYINGI NI VIPI ULANZI UNANOGA? SIJAPATA JIBU....MMMMHHHH!!!

SARAT​ANI YA UTUMBO MPANA NI HATARI

Habari Wanablog wote, Tatizo hili yaonesha ni kubwa sana, toka nimeweka posti nimepata emails na simu nyingi sana, naomba kwa heshima na taadhima ku-share kwenye blog zenu tukufu ili watu wengi zaidi wape ujumbe huu wa kutia matumaini. Asanteni. Bernard.

Blog: Rwebangira Blog
Post: SARATANI YA UTUMBO MPANA NI HATARI
Link: http://bongopicha.blogspot.com/2012/06/saratani-ya-utumbo-mpana-ni-hatari.html

Friday, June 22, 2012

IJUMAA NJEMA... Mziki Asili Yake Wapi!!!!


Mziki asili yake nini usiniona naimba ukazani ninayo furaha kumbe ninayo huzuni moyoniiii......haya endelea kuimba nawe..
IJUMAA NJEMA SANA NDUGU ZANGUNI!!!

Thursday, June 21, 2012

TUMALIZE SIKU HII KWA KUANGALIA:- UREMBO HUU WA KIASILI!!!

Hakuna kiti  nikipendacho kma hizi bangili ....Ebu angalia kwanza rangi zake zilivyokaa kaa ...Hivi ni waMasai tu ndio wanaoweza kutengeneza vitu hivi. Hakika kama ni wao tu nawapa hongera sana kwa kudumisha utamaduni hii mwanana. Ipo kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutupa mikono pia ubunifu. Bado nasikitika bangili yanmgu ilikataka :-) Je wewe pia ni mdhaifu vya vitu kama hivi vya asili?

Kisa Cha Mmasai Na Mchungaji Wa Kanisa...

Kuna kisa cha Mchungaji wa Kanisa la Kibabtisti aliyefika kijiji cha Wamasai Jumapili moja kuhibiri dini.
·        Mchungaji akawa na nia pia ya kuanzisha kanisa kijijini hapo.
·        Wamasai wakakusanyika kanisani. Baada ya kuhubiri Neno la Mungu kwa saa mbili, Mchungaji akaomba arudi tena kijijini hapo Jumapili inayofuata. 
·        ... Ndipo hapo akasimama Mzee wa Kimasai na kutamka;
Mzee wa Kimasai;
 ·        " E bwana Chungaji sisi iko furahia sana neno yako ya Mungu. Lakini, usije juma la kesho, ni kwa vile kuna ile padri ya Roman imesema inakuja kusema neno ya mungu pia."
Mchungaji: 
·        " Je, inawezekana nikaja Jumapili ya keshokutwa ?"
Mzee wa Kimasai: 
·        " Hapana, Chungaji, Jumapili ya keshokutwa kuna ile Imam ya Msikiti imesema inakuja kutupa mawaidha ya Kiislamu"
Mchungaji: 
 ·        " Sasa nyinyi hamuwezi kuchanganya dini na madhehebu, itabidi mchague!"
Mzee wa Kimasai: 
·        " Aisee Baba Chungaji, wewe iko chungaji na mimi pia ni chungaji. Zile ng'ombe nachunga zinakula majani pamoja. Wake zetu wanashinda na kufanya kasi pamoja. Watoto zetu wanacheza pamoja. Sasa sisi hatutaki hiyo dini inakuja kutagawa hapa"
HABARI HII NIMETUMIWA NA MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO NAMI NIKAONA NI VIZURI KUJUZANA.

ALHAMIS YA LEO TUANGALIE:- MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!

1. Hata kama mtu ni mwerevu, huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda mrefu. Siku moja utagunduliwa, kwa sababu "siku za mwizi ni arobaini" au "habari za uwongo zina ncha saba.
2. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana budi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira.
3. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
4. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni
5. usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu. Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au maskini hachoki, akichoka keshapata.
7.Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
8. Si utu kwende kwa uliyempa zawadi na kumwambia akurudishi zawadi yako
9. wivu hangamiza familia nyingi ulimwenguli
Namba kumi naomba wewe uzaja. Ni kwamba kama nawe una msemo na basi karibu jumuika nami......

Wednesday, June 20, 2012

MAMA NA MWANA!!!!

Mama nisubiri ....picha hii imenikumbusha mbali kweli ....je wewe msomaji umepitia maisha haya??Kama si shughuli hii je ni shughuli gani ulikuwa ukiependa kufanya/saidia?

Chakula cha KIZUNGU ndio chakula gani hicho?-Chakula cha KIAFRIKA ndio chakula gani HICHO?


Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO na leo katika pitapita zangu nimekutana na hii  na nimeona si vibaya tukirudia. Na kama nisemavyo kurudia kitu/somo ndio kujifunza zaidi. Na nilikutembelea na kukutana na hii ni kwa Mtakatifu. KARIBUNI SANA...
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nimestukia kuna katabia ka WAAFRIKA kusifia MAJINA ya vyakula vya KIAFRIKA na kwa WAZUNGU visemekanavyo ni vya KIZUNGU,...
... bila kusahau WAARABU, Wahindi, Wachina ...nk....
....na hii ni bila kukumbuka kuwa labda CHAKULA sio MAJINA wala UTAMU wa CHAKULA,...
.... kama mahitaji ya MWILI ndio yalengwayo.
Swali:
  • Hivi tunakumbuka ni nini MWILI wa BINADAMU yeyote unahitaji -kitu ambacho chaweza kuwa ni zaidi ya kuhusianisha WATU wa ENEO fulani na VYAKULA vyao hata kama sio KIMAJINA hasa ukizingatia labda ni virutubisho tu fulani fulani ndivyo muhimu kwenye hivyo vyakula ndio MUHIMU kuliko lililobobea kimtazamo ambalo ni MAJINA tu na staili za MAPISHI ya kiitwacho ni CHAKULA?
  • Si yasemekana CHURA wakukaanga na UGALI -labda uhitajicho mwilini mwako ni CHURA kwa kuwa ushakunywa uji wa MTAMA asubuhi na wala sio UGALI?
  • Ndio,...
.... labda mambo mengine ni ladha na MAZOEA tu,....
.... kwa kuwa MTU ahitajicho zaidi ni MATEMBELE au tu MATE kipenzi litakalomfanya asile sana asivyohitaji MWILINI!:-(

PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO !!!!

Tuesday, June 19, 2012

JINSI NILIVYOWAZA NINI CHA KUPIKA JIONI YA LEO/NIMETAMANI MBOGA!!!



Nimeiangalia picha hii na kujikuta :-) ebu angalia hayo matembele na naona hapo kwenye hilo kapu kuna zaidi ila nikakaza moyo na kuendelea kuwaza.....

Jioni inaingia nimekaa hapa nawaza nini cha kupika mwanamke mimi...Ghafla natoka nje naangalia bustani . Uwiiiii..bado  bado kabisa. Naingia tena mtandaoni ili kupata mawazo nakutana na picha hii. Kamoyo kanadunda na hamu ya kupa huo mchicha, matembele,chaina ...halafu naangalia akina mama walivyojipanga hapa nami naanza kupata wazo nitawauzia majirani mboga zangu...ujanja eeeh:-)  Picha kutoka kwa Mjengwa.

UJUMBE WA JUMANNE HII !!!NI KAMA IFUATAVYO....!!!!

Katika dunia hii sio wote ambao wanakupenda. Lakini kama unajipenda mwenyewe huna sababu ya kuwa na wasiwasi. Kuwa na furaha.Na kumbuka Mungu anakupenda. KILA LA KHERI WA WOTE!!!

Monday, June 18, 2012

TUENDELEE NA JUMATATU HII KUWA NA YASINTA:- KWA KUWASHUKURU WALEZI HAWA!!!

Nimekaaa hapa na mawazo tele , nikawa nakumbuka Songea Mahenge hapa ndipo nilipoanza kujitegemea. Na ndiyo nimeona nitoe shukrani zangu za dhati kwa wazazi /walezi wangu. Mama Nachihauli na baba Nyoni ahsanteni sana. Kwa yote mliyonifunza katika maisha na leo najua ni vipi kuishi na watu. MUNGU AZIDI KUWAZIDISHIA MEMA.......Hapa ni mwaka jana 2011 miezi kama hii.
Halafu hapa ni mama yangu wa hiari, baada ya kutoka Songea nikawa naishi Matetereka/Madaba na huko nikakutana na mama huyu. Mama Mgaya. Hakika sina maelezo zaidi ya kumshukuru kwa kunilea kama vile nilikuwa binti yake. Na bado ananilea mpaka leo AHSANTE MAMA kwa yote. MWENYEZI MUNGU NA AKUZIDISHIE UPENDO ULIO NAO Hapa pia ni mwaka jana ni NJOMBE KIHESA.
NINAWAPENDA NA NITAWAPENDA MILELE KWA YOTE MLIYONIFUNZA NA MNAYONIFUNZA.

JUMATATU HII TUANZE NA SWALI HILI:- ATLASI KAMA HII BADO ZIPO?

Maana mara nyingi niwapo Peramiho Bookshop huwa nasahau kuangalia na hii nilinunua pale miaka kadhaa iliyopita. Sijui wamebadili mwonekano au? JUMATATU NJEMA!!!!

Saturday, June 16, 2012

PICHA YA WIKI ITAKUWA HII...!!!JUMAMOSI NJEMA KAPULYA!!!!

Najiuliza sijui hapa nilikuwa nasema nini? Naonekana kama mwalimu mkali kweli.Ila nimeipenda hii picha mwenzenu.  Haya ngoja niwatakieni Jumamosi njema  wote mtakaopita hapa...:-)

Friday, June 15, 2012

VYAKULA VYA ASILI NI VITAMU/ HAPA MIMI NIMEFIA KABISA

Hakika ebu angalia hapa ugali tena bongo BONDO, samaki na mboga majani  na matunda/matikiti maji baada ya chakula. Halafu sasa fikiria hapo ugali umelima mahindi/mihogo, ulezi au sijui mtama, mboga umelima mwenyewe bustani, samaki umewavua mwenyewe au tu umetoka kuwanunu wakati tu wavuvi wamerudi. Matikiti maji nayo labda umeyalima mwenyewe ....ashilia mbali viungo. Yaani hakuna kitu kilichokaa kwenye kopo wala nini? Mmmmhhh!! Yamu yamu yamu  ngoja niache ...picha toka kwa kaka Mjengwa.

INAKARIBIA MCHANA NGOJA TU TUANGALIE VYAKULA MBALIMBALI KUTOKA TANZANIA LABDA UNAWEZA KUPATA WAZO NINI KUPIKA MCHANA HUU!!


NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA SANA PIA MWANZO  WA KUANZA MAPUMZIKO UWE SALAMA. Najua wiki hii kwa wengi imekuwa na mikikimikiki mingi maana wengi sasa hasa wanafunzi wanaanza likizo (sommar lov) ...Labda nichukue nafasi hii pia kuwatakia wale wote ambao wapo LIKIZO..

Barua kwako mpenzi wangu

Nipo hapa kazini  na nikaanza kukumbuka shule ya msingi. Jinsi tulivyokuwa tukiandikiana barua za kirafiki. Nakumbuka  kwamba tulikuwa tukimtuma mtu (mshenga/mtenga )hata kama alikuwa rafiki wa kike. baadaye nikakumbuka kuna sehemu nilisoma barua moja nzuri sana oh! ilikuwa ni hapa kwa mtani wangu  mwananchi mimi. hebu soma mwenyewe  ...
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mpenzi wangu,
Nikupendaye kwa dhati kutoka moyoni mwangu,
Nakusalia salamu ya huba iliyoambatana na busu motomoto.
Mpenzi wangu nianze kwa kukushukuru sana kwa barua yako iliyojaa huba ambayo nimeipokea jana mchana nikiwa kazini. Niseme tu nimefurahi sana mpenzi wangu kupata barua yako. Siku zote barua zako huwa tiba mahabuba moyoni mwangu. Kila niusomapo mwandiko wako wa kimahaba huwa napata liwazo la haja moyoni mwangu. Maneno ya kwenye barua yako ni dawa isiyo na kifani ndani ya moyo wangu. Kila mara najikuta moyo wangu unaongeza maradufu upendo juu yako.
Mpenzi wangu, usishangae kuwa nimepata barua jana lakini nimechelewa kukujibu hadi leo ndiyo nimeshika kalamu na karatasi ili nikuandikie ewe malaika wa moyo wangu. Nilipoipata barua yako nilitafakari kwa muda mrefu mno hadi kujikuta nikitokwa na machozi. Hayakuwa machozi ya furaha kama yale yanidondokayo kila wakati nisomapo maneno matamu kutoka kwako ewe mwandani wangu. Maneno ya kwenye barua yako yamenichoma moyoni mwangu mithili ya mkuki wenye ncha kali tena iliyoiva vilivyo kwenye tanuru la moto. Mpenzi wangu, niliyekuchagua mimi mwenyewe kutokana na hisia kali na mapenzi mazito sana niliyonayo moyoni mwangu juu yako, amini bado nakupenda sana.
Mpenzi wangu, nikakiri kwa yakini kuwa nilikuahidi toka miaka mingi sana kuwa pindi nitakapojaaliwa kupata kazi nitakuoa. Nayakumbuka maneno ya ahadi niliyokuwa nikikupa kila mara tulipokuwa tukipata kaupenyo ka kuwa pamoja. Ahadi yangu bado ipo pale pale mpenzi wangu. Moyo wangu, kwa dhati kabisa, bado una dhamira ya dhati ya kukuoa mpenzi wangu nikupendaye kuliko chochote humu duniani, kuliko hata niipendavyo nafsi yangu. Bila wewe mpenzi wangu, dunia hii ina faida gani kwangu?
Mpenzi, nimetokwa machozi kwa sababu ya uzito wa jambo lenyewe. Kwenye barua yako umeandika jinsi unavyokata tamaa kwani sasa ni mwaka moja toka nianze kazi lakini sijatimiza ahadi yangu ya kukuoa. Mpenzi unaona kama nakupotezea muda na unaniomba kama sina haja nawe nikupe nafasi uolewe na mtu mwingine ambaye hata leo hii yupo tayari kuleta posa kwa wazazi wako. Sijui niyaelezeaje maumivu makali ninayoyasikia ndani ya moyo wangu.
Mpenzi wangu, niseme tu ukweli. Ninakupenda mno kuliko hata maana ya neno lenyewe upendo. Ninatamani sana hata sekunde hii hii niwe nimeoana nawe. Lakini, kama nikwambiavyo siku zote, ugumu wa maisha hapa Dar es Salaam hususani kwangu mie mfanyakazi wa kima cha chini ndiyo unaonifanya nikose uthubutu wa kukuoa ewe mpenzi wangu niliyekupa moyo wangu wote, haraka iwezekanavyo kama ambavyo nimekuwa nikikuahidi mara nyingi sana. Mpenzi wangu, moyoni mwangu inaniuma sana maana maisha magumu ninayoyaishi hapa Dar es Salaam kwa kweli yanatishia kwa kiasi kikubwa sana ustawi na uhai wa penzi letu.
Mpenzi wangu, nikwambie nini ili ufahamu kwa kiasi gani akili na moyo wangu vyatamani kwa dhati kabisa kuishi nawe milele yote kadri Mwenyezi Mungu atakavyotujaalia siku za kuishi humu duniani. Nikwambieje ili ufahamu ni namna gani nalitamani pendo hili lidumu humu duniani na baada ya hapo?
Mpenzi, maisha yangu mfanyakazi wa kima cha chini ni magumu mno. Fikiria mpenzi wangu, kamshahara kangu ambako ni kadogo mno, kanapaswa kalipe kodi ya nyumba, umeme, maji, matibabu, gharama za usafiri na mengineyo chungumbovu. Mpenzi wangu huwezi amini kuna wakati huwa nalazimika kutembea kwa miguu kutoka kazini pale Stesheni mjini hadi nilikopanga Mbagala Kizuiani. Huwa inanigharimu masaa karibia mawili nachapa tu mwendo tena wakati mwingine mvua ikininyeeshea mwili mzima. Sijakwambia tu mpenzi wangu, mara zingine huwa nalazimika kushindia mlo mmoja ama pengine nisile kabisa. We acha tu mpenzi wangu.
Mpenzi, natamani ningekuwa na uwezo wa kukufungulia moyo wangu uyaone yaliyo ndani. Natamani mno tena kupita maelezo kuoana nawe. Kinachonikwamisha mpenzi wangu ni ugumu tu wa maisha ninaokabiliana nao hapa mjini. Sikusudii kukuoa ili uteseke. Sikusudii kukuoa ili nikushindishe njaa. Siyakusudii hayo.
Mpenzi wangu, sikusudii kuuweka uhusiano wetu rehani. Mpenzi sina namna niwezayo kuibadili hali halisi kwa sasa zaidi ya kulazimika kufanya kazi kwa bidii ili pengine bosi wangu anione anipandishe cheo ama kunipa nafasi ya kwenda kujiendeleza kielimu. Lakini tatizo kazini kwetu kumejaa majungu mno kiasi kwamba uchapakazi wangu unanifanya nionekane kimbelembele. Kila mtu ananiona nina kiherehere hadi nalazimika kuwa mpole na goigoi kama wafanyakazi wengine. Kwa mtindo huu sijui ni lini nitafanikiwa kimaisha.
Mpenzi, kweli kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu, sitamani wala siombi uniache na kuolewa na mwingine kwa sababu tu ya hali yangu duni. Machozi yananitoka mno kuyaandika maneno haya. Ninakuomba mpenzi wangu univumilie walau kwa mwaka moja mwingine pengine serikali itatufikiria na kuamua kuboresha hali zetu. Chonde chonde mpenzi wangu.
Mpenzi wangu, najaribu kukwepa kuufikiria mtihani mkubwa unaokukabili kwa sasa. Mapenzi ya kweli ama maisha bora. Najaribu tu kupambana na wivu moyoni mwangu. Najaribu kutamani kuvivaa viatu vyako na kuchagua mapenzi ya kweli. Lakini sipungukiwi imani.
Mpenzi wangu, najua nimekuchosha kwa barua ndefu sana ambayo hata hivyo imeshindwa kujibu swali lako la nitakuoa lini. Ninatumai maelezo yangu pamoja na kutojibu moja kwa moja swali lako, angalau yametoa mwelekeo wa jibu.
Mpenzi wangu, natamani kusema mengi sana zaidi ya haya. Najua hata siku moja dau tupu haliendi joshi na maneno matupu hayajengi nyumba. Ninaloweza kukwambia ni kuwa ninakupenda mno, daima ninakuwaza wewe kwa kuwa umetamalaki moyoni mwangu. Wewe ndilo pambo la moyo wangu. Kwa huba na mahaba yajazayo vibaba na vibaba, penzi langu kwako limeshiba.
Nikupendaye daima,
Mpenzi wako.

Thursday, June 14, 2012

HUU KWELI NI UUGWANA? AU AKINA MAMA TUNA MOYO WA KIKATILI HIVI KWELI?


Nimesoma habari hii na kuona picha hii nimepatwa na maumivu yasiyosemekana. Na nikaanza kuwafikiria  watu wanaofanya kila mbinu ili kupata watoto/mtoto halafu wengine wanatupa. Yaani nimeguswa na habari hii si kawaida. Nikaanza kuwa kubeba mimba miezi 9 maumivu yote ya kujifungua halafu anamtupa mtoto. Kama haku/hawataka watoto/mtoto kwa nini kutafuta mtoto? Mbona kuna vizuizi? Malaika kama huyo hana kosa... nashindwa kuendelea kuandika. Soma hapa chini...
----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Wewe na mie tuchunguze vizuri photo hiyo, ni dampo la takataka eneo moja huko Mtwara,lakini ukichunguza sana utaona ni uchafu uliyokuwa pamoja na binadamu,binadamu aliyezaliwa na mwanamke.
Ni kitoto kichanga kilichozaliwa na mama huko Mtwara na kukitupa kwenye lindi la mikusanyiko ya kila aina ya uchafu,Hivyo wimbo wa nani kama mama una maana yoyote kwa akina mama wenye moyo wa ukatili kama huyo? .je ni kitu gani kilicho msibu mama huyo hadi kufikia kufanya kitendo hicho kiovu.( Source Mitandao ya Kijamii ) Picha na habari nimeipatahapa

TUSISAHAU SANAA NA UTAMADUNI..NIMEPENDA SANA VINYAGO HIVI/HIKI!!!


Hii picha/kinyago nakipenda sana ..ila huwa najuuliza kwanini nakipenda? Na pia najiuliza kwa nini mtu aliyetengeneza hakutengeneza na mikono ? Na pia mguu mmoja tu?  Mmmmmhhh !!! Je wewe mwenzangu unafikiri alifikiri nini  mchongaji?

Au kama hivi hapa yaani mikono jamani imepata kipaji ambacho hakiwezi kusimulika. Hapa ni mke ma mume wakiwa wameshika jembe na shoka lakini bahati mbaya shoka la mama lienipotea na umebaki mpini tu. Hii nilipata zawadi kwa rafiki yangu Joyce toka Njombe. AHSANTE JOYCE!!!!!

Wednesday, June 13, 2012

WANAUME KATIKA MAPENZI NI KAMA MASOKWE...!

Ndugu zangu wapendwa leo ni JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA MAMBO /MAKALA,PICHA MBALIMBALI. Nale katika pitapita nimekutana na hii na si kwingine tena ni kwa  kaka yangu wa hiari Kaluse. KARIBUNI!!!!
Katika utafiti uliofanywa na akina Kruger na wenzake kwa wanyama jamii ya Sokwe, ilibainika kwamba kulikuwa na vifo vingi vya Sokwe madume wenye umri wa miaka 13. Hali hii ilitokana na sababu kwamba, kwa kawaida katika umri huo, Sokwe madume huwa wamefikia umri wa kupanda na kufanya mapenzi na hivyo huanza kushindana wenyewe kwa wenyewe wakigombea majike na hata kwa lengo la kudumisha hadhi yao miongoni mwa Sokwe wengine.
Katika hatua hii Sokwe hao hufikia mahali pa kupigana na hata kuuana kwa lengo la kujipatia wapenzi na kudumisha hadhi zao. Hali hii haiko kwa sokwe peke yao, bali hata kwa wanyama wengine pamoja na ndege wa aina mbalimbali.


Hata hivyo, pamoja na ukweli huo binadamu naye hajanusurika hata kidogo na purukushani za aina hiyo. Labda kinachomtofautisha binadamu na wanyama hao ni namna wanavyokabiliana na mashindano hayo. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, hata akichagua njia ya aina gani ili kushindana na binadamu wenzake, bado matokeo ya mwisho yatafanana na yale ya wanyama, yaani kifo.
Imeonekana wazi kwamba binadamu wa kiume ndiye mwenye mwelekeo mkubwa wa kupenda purukushani na kuhatarisha maisha yake. Ingawa binadamu huyu wa kiume au mwanaume hahitaji kupigana mweleka na mwanaume mwenzake ili kumpata mwanamke, lakini harakati zake ni zaidi ya kupigana mweleka.

Hata hivyo katika mazingira mengine, mieleka hupiganwa sana katika sura ya mieleka halisi au katika sura nyingine za ushindani wa kutafuta ushindi katika kumpata mwanamke. Wengi tunajua kuhusu habari za kuuawa kwa wanaume kutokana na vurugu za kugombea wanawake.

Tabia hii ya wanaume ya kuhatarisha maisha si ya leo, bali ni ya tangu kale. Huenda huko nyuma baadhi ya wanaume walitumia silaha kwa lengo la kuwadhulumu ama kuwauwa wanaume wenzao ili hatimaye waweze kuwamiliki wanawake wanaowapenda.
Kwa kawaida, wanaume hushindana wao kwa wao kwa lengo la kumiliki rasilimali na kuhifadhi au kudumisha hadhi na heshima yao ndani ya jamii wanamoishi.


Huu ndio ukweli wenyewe ambao hautofautiani hata chembe na ule wa Sokwe. Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali adimu kama vile fedha na anapoweza kusimika kwa uhakika heshima na hadhi yake, ndani ya jamii iliyomzunguka, mambo hayo humpatia thamani kubwa na kumrahisishia kazi ya kumpata mwanamke anayemtaka.
Au tu tumaliziae na ujumbe huu kutoka kwa CHOX FT ALIKIBA - TUSIGOMBANE

MUNGU AKIPENDA TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO NA RUDIO JINGINE. KWA SASA NASEMA JUMATANO NJEMA!!!

Tuesday, June 12, 2012

JAMANI MNAKUMBUKA HADITHI HII BAADHI YETU TULISOMA TULIPOKUWA DARASA LA TATU :- JOGOO ALIYESEMA




Kumbukumbu ni nzuri jamani leo nawasomea wanangu nao wananisomea ...nimeona niwakumbushe na wenzangu pia si vizuri kuwa mchoyo.

Monday, June 11, 2012

KAPULYA NA BUSTANI YAKE LEO....

Kama wengi mnakumbuka wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na shughuli ya kulima bustani  kwa hiyo  hapa ni mwendolezo au niseme .....


 inaendelea kama muonavyo hapa ni leo na mimea imeanza kuchipua ukiangalia sana utaona
....mdada anaendelea kumwangilia ili mimea ikua kwa haraka  mpiga picha ni dada Camilla...haya tutaendelea kuona mafanikia baada ya wiki tena...JUMATATU NJEMA NA JIONI NJEMA ....

TUANZE JUMATATU HII NA SWALI HILI:-JE NI KWELI?

Nakumbuka nilipokuwa mdogo wakati naishi kule Lundo kulikuwa na sehemu tulikuwa hatupiti. Kisa kulikuwa kunasemekana kuna JOKA kubwa ambali lilikuwa lina vichwa vitatu na pia lilikuwa linauma kichwani tu. Sijui kama ilikuwa kweli au ilikuwa ni njia ya kuwazuia watoto wasiende kule? je Nyoka kama huyu yupo kweli? na anatumia midomo yote kuuma? Katika wadudu/wanyama niwaogopao nyoka ni namba moja , ingawa sijawahi kuumwa na nyoka. Huwa nashangaa nionapo watu wana nyoka ndani ya nyumba  kwa ajili ya kufuga ......sipati jibu kwa nini....

Sunday, June 10, 2012

NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA SANA KWA WIMBO HUU!!


Leo ni Jumapili ya EKARISTI TAKATIFU lakini nimeshindwa kupata wimbo maalumu ila najua huu pia ni mzuri. Basi NIWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI NNJEMA SANA NA MWENYEZI MUNGU  AWASHUSHIE BARAKA ZENYE  UPENDO NDANI YA NYUMBA ZENU PIA KATIKA MIOYO YENU. KAPULYA!!!

Afrika Mvunja Nchi Ni Mwanasiasa, Kiongozi Wa Kidini"- Makala Yangu Gazeti Mwananchi

Na Maggid Mjengwa,

Ndugu zangu,
SWALI ambalo mara nyingi nakutana nalo ni hili; ’Huogopi’? Swali hili linatokana na mambo niandikayo.

Ukweli, kuna Watanzania wengi sana wanaishi kwa hofu.

Ndiyo, hofu zimetawala mioyo ya Watanzania wengi. Ni muhimu na busara kukawapo na mazingira ya wanajamii kutoa fikra zao kwa uhuru, hata kwenye masuala yenye kuhusu imani.

Hatuwezi kuzuia kero na migongano ya kijamii kwa kuikimbia mijadala. Kufanya hiyo ni kuahirisha matatizo, na zaidi kuyalundika. Na siku yakifumuka, athari yake huwa ni kubwa na mbaya zaidi.

Mimi nadhani, kuwa Watanzania wengi hatuna maarifa ya dini. Shule zetu hazina masomo ya dini kwa ujumla wake. Kuna wanaosoma elimu kuhusu maarifa ya Uislamu ( Islamic Knowledge) . Kuna wanaosoma kuhusu maarifa ya Biblia, hivyo Ukristo (Bible knowledge).

Lakini, shuleni hakufundishwi maarifa kuhusu dini kwa ujumla wake, ( Religious Knowledge) Hili ni tatizo, kwamba Wakristo wanapata mafundisho juu ya Ukristo, Waislamu vivyo hivyo. Wahusika wanakosa ufahamu juu ya dini za wengine. Ingelikuwa vyema, kama tangu shule za msingi, watoto wakajifunza juu ya dini mbalimbali za dunia hii.

Na kuna Watanzania wengi ambao hawajui kuwa kuna tofauti ya Uarabu na Uislamu; kwamba si kila Mwarabu ni Mwislamu. Watanzania wengi bado hawajui kuwa kuna dini nyingine za dunia zaidi ya Uislamu na Ukristo hata kama Uislamu na Ukristo ndizo dini kubwa na maarufu hapa duniani.

Na lililo kubwa kabisa; dini zote za dunia zinahimiza uwepo wa amani na upendo miongoni mwa wanadamu. Katika kuishi kwangu sijapata kusikia dini ambayo misingi yake imejengwa katika kuwafanya waumini wake wawachukie na kuwabagua wanadamu wenzao wasio wa imani yao.

Duniani hakuna dini inayohimiza waumini wake kuwatendea maovu wanadamu wenzao wasio wa imani yao. Kuna wanadamu wenye hulka mbaya, ikiwamo kutenda maovu.
Na hao wamo miongoni mwa Wakristo, Waislamu, Wahindu, Wapagani na wengineo. Na kamwe, maovu yakifanywa na wachache si haki kuhukumu wote katika kundi analotoka mtenda maovu.
Na kwa Afrika, mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi na ya kundi dogo badala ya yale ya kitaifa.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.

Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachaga na wao Wazaramo.

Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao. Kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani.
Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania.

Hekima ituongoze katika kutambua, kuwa nchi yetu ina makabila zaidi ya mia na ishirini. Ina waumini wa dini za kimapokeo; Uislamu na Ukristo, ina waumini wa dini za jadi, kuna Wahindu na wengineo. Na kisiasa, nchi yetu ina vyama vingi vya siasa .

Hivyo basi, haiwezekani kwa kabila moja tu kuweza kuongoza nchi hii. Haiwezekani kwa Watanzania wa dini moja tu kuongoza nchi hii. Haiwezekani kwa chama kimoja tu cha siasa kikashika hatamu zote za uongozi na kufanikiwa bila kushirikiana na vyama vingine.

Ndiyo, kilichotusumbua huko nyuma ni kuendekeza ubaguzi wa kisiasa. Ndicho kinachotusumbua sasa. Na kwa vile kuna ombwe ( vacuum) la uwepo wa siasa za upinzani zinazokubaliwa na walio madarakani. Kwamba jamii yetu, na hususan wanaokuwa madarakani, bado hawajakubali kwa moyo wote uwepo wa siasa za upinzani. Kukubali kuwa tofauti za kifikra na kimitazamo ya kisiasa na kiuchumi ni jambo la siha kwa taifa.
Na kama ombwe hili litaendelea kuwapo, nahofu kuwa huko tuendako siasa za ’Chai- Maharage’ zitachukua nafasi zaidi kuziba ombwe hili la siasa za upinzani.
Tunaona leo jinsi wanasiasa wetu wanavyoshindwa kutenganisha dini na siasa katika kazi zao. Tunawaona wakishiriki mikusanyiko ya kidini na kutoa matamko ya kisiasa na hata kupigana vijembe. Ni hatari sana. Nahitimisha.

Mungu Ibariki Tanzania. ( Chanzo: Gazeti Mwananchi, Jumapili) nimetumiwa na kaka Mjengwa
0788 111 765
http://mjengwablog.com/

Saturday, June 9, 2012

AU TU TUMALIZE JIONI YA JUMAMOSI HII KIHIVI:-MAISHA YA NDOA/MARRIAGE!!

 A man and his fiancĂ© were married. It was a large celebration. All of their friends and family came to see the lovely ceremony and to partake of the festivities and celebrations. A wonderful time was had by all. The bride was gorgeous in her white wedding gown and the groom was very dashing in his black tuxedo. Everyone could tell that the love they had for each other was true. A few months later, the wife comes to the husband with a proposal: “I read in a magazine, a while ago, about how we can strengthen our marriage. “She offered. "Each of us will write a list of the things that we find a bit annoying with the other person. Then, we can talk about how we can fix them together and make our lives happier together." The husband agreed. So each of them went to a separate room in the house and thought of the things that annoyed them about the other. They thought about this question for the rest of the day and wrote down what they came up with. The next morning, at the breakfast table, they decided that they would go over their lists. "I'll start, “offered the wife. She took out her list. It had many items on it. Enough to fill 3 pages, in fact. As she started reading the list of the little annoyances, she noticed that tears were starting to appear in her husband’s eyes. "What's wrong? “she asked.” nothing “the husband replied, “keep reading your list." The wife continued to read until she had read all three pages to her husband. She neatly placed her list on the table and folded her hands over top of it. "Now, you read your list and then we'll talk about the things on both of our lists. “She said happily. Quietly the husband started, “I don't have anything on my list. I think that you are perfect the way that you are. I don't want you to change anything for me. You are lovely and wonderful and I wouldn't want to try and change anything about you." The wife, touched by his honesty and the depth of his love for her and his acceptance of her, turned her head and wept. IN LIFE, there are enough times when we are disappointed, depressed and annoyed. We don't really have to go looking for them. We have a wonderful world that is full of beauty, light and promise. Why waste time in this world looking for the bad, disappointing or annoying things when we can look around us, and see the wondrous things before us? I believe that WE ARE THE HAPPIEST when we see and praise the God and try our best to forego the mistakes of others. Nobody's perfect but we can find perfection in them to change the way we see them. It is necessary to understand the difficulties and be a helping hand to each other....THAT BRIGHTENS THE RELATIONSHIP.
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio nami nimeona tusinyimane habari kama hizi.

Friday, June 8, 2012

WATU TUMETOKA MBALI/KUJIFUNZA MAISHA!!!

Picha hii imenipeleka mbali sana. Hakika watu tumetoka mbali na changamoto nyingi tumepitia. Binafsi napenda kuwashukuru wazazi/walezi wangu kwa kunilea, kuniongoza vipi jinsi ya kuishi maisha. Je? wewe pia unakumbuka kazi za utotoni?.......IJUMAA NJEMA TENA!!!

PIGA MOYO KONDE SIKU YAKO INAFUATA/ USICHOKE USIMAME!!!


Mziki/wimbo kila wakati una ujumbe wake maalumu. Kama wimbo huu una ujumbe wake ambao wengi wanaweza kujifunza kitu.
NAWATAKIENI WOTE IJUMMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA....!!!!

Thursday, June 7, 2012

PICHA YA WIKI : - NIMEIPENDA SANA PICHA HII NA NIMEONA IWE WAREMBO WA WIKI!!!JE? UNAJUA NI NANI KATI YA HAWA WAWILI!!!? NALITAKA VAZI HILI

Picha hii nimeipenda sana yaani sana. Kiasi kwamba nimeona iwe picha ya wiki. Kama kichwa cha habari kinavyosema je Unamfahamu mmoja wa wadada hawa warembo?

Wednesday, June 6, 2012

SALAMU NI NUSU YA KUONANA

Au tu kwa vile ni jumatano ya marudio basi ngoje turudie  na hii. nimeipata hapa
Tusalimiane japo kwa maneno machache wakati wowote bila kujali majukumu yetu ndani mikikimikiki ya maisha kwa kuwa kila mmoja anamhitaji mwenzake kwa nyakati tofauti ijapokuwa nyakati nyingine waweza kuhisi kuwa mtu fulani siyo muhimu sana kwako lakini wakati wa uhitaji ndiyo unatambua bila fulani mchakato wa maisha na mafanikio hauwezi kufikia tamati.
Kama wingi wa viungo mwilini kwa kutazama lakini wakati wa mahitaji kila kimoja kwa nafasi yake humtimizia binadamu haja yake.
"Salamu ni daraja la urafiki"
Wasalamu na shukrani;
 

JUMATANO NJEMA!!!

Wanafunzi hawa wanafanyishwa vibarua


Ije jumatano ya KIPENGELE CHETU CHA MARUDIA NDIO LEO NA LEO NIMEONA KWA VILE WIKI ILIYOPITA TULIZUNGUMZIA KIDOGO KUHUSU ELIMU BASI TUENDELEE KIDOGO NA MADA HII YA SHULE NA ELIMU.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ndingine mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakifanyishwa kazi ya kusomba tofali muda wa masomo
LICHA ya serikali kupiga marufuku walimu kuwafanyisha vibarua wanafunzi wakati wa masomo,bado baadhi ya shule hasa katika maeneo ya vijijini,zinaendelea na tabia hiyo hali ambayo inachangia kuzorotesha elimu nchini.
Uongozi wa shule ya msingi Ndingine iliyopo kata ya Ngumbo mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma bado unaendelea kuwafanyisha vibarua wanafunzi licha ya afisa elimu wa wilaya hiyo kupiga marufuku jambo hilo.
Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi katika kijiji cha Ngumbo hivi karibuni ulibaini wanafunzi baadhi wakiondolewa madarasani tena majira ya asubuhi na kwenda kufanyishwa kibarua cha kubeba tofali za kuchoma kutoka kwenye tanuli lililokuwa mtoni hadi mahali ambapo nyumba inajengwa umbali wa kilometa tatu.
Wanafunzi wa darasa la tatu na la sita kutoka shule hiyo walishuhudiwa wakisomba tofali hadi nne kichwani huku wakilalamika kuwa wanafanya kazi ambayo hawanufaiki nayo licha ya kuambulia maumivu kutokana na mzigo na umbali.
Baadhi ya wanafunzi wanasoma darasa la sita walipohojiwa ,walidai kuwa mwalimu amewaambia huo ni mradi wao ambao utawawezesha kupata fedha kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumaliza elimu ya msingi hapo mwakani watakapomaliza darasa la saba.
Hata hivyo wanafunzi wa darasa la tatu walilalamika kuwa wao wamelazimishwa na mwalimu kwa kuwa hawapati chochote na kwamba fedha zote wanachukua walimu,ingawa tofali zinachangia kuchafua sare zao za shule ambazo wakirudi nyumbani inawalamu wazazi kununua sabuni ili kufua nguo zao.
Miongoni mwa wazazi waliohojiwa kuhusiana na watoto wao kuendelea kufanyiwa kazi za vibarua,waliomba serikali ya wilaya kuwachukulia hatua walimu wa kata za Ngumbo na Liwundi kwa kuwa wamezoea kuwafanyisha kazi wanafunzi wao licha ya wazazi na walezi kukataa.
“Sisi wazazi kwenye vikao tulishakubaliana tutachangia shilingi 2000 kila mzazi ,walimu waache tabia ya kuwafanyisha kazi watoto wetu badala yake waendelea na kusoma lakini walimu bado wanaendelea kuwafanyisha kazi mbalimbali wanafunzi kama vile kuchota maji ya walimu,kubeba tofali,kukata matete,kubeba kuni pamoja na kazi nyingine nyingi’’,alisema Martha Nchimbi mkazi wa Mkili.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ndingine Aidan Mbilinyi alipohojiwa kuhusiana na kuwafanyisha kazi za vibarua wanafunzi alidai kuwa katika shule yake wanafunzi hawafanyishwi vibarua badala yake wazazi wanachangia kila mwaka shilingi 2000 kwa ajili ya sherehe za mahafali ya darasa la saba .
Katika kikao cha walimu wakuu wote wa wilaya ya Mbinga ambacho kiliitishwa na idara ya elimu chini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Septemba 23 mwaka huu pamoja na mambo mengine waliazimia kuacha kuwafanyisha vibarua wanafunzi vikiwemo kusomba tofali na kuvuna kahawa.
Afisa elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga David Mkali amekemea tabia ya walimu wakuu kuendelea kuwafanyisha kazi wanafunzi na kusisitiza kuwa kuanzia sasa atachukua hatua za kinidhamu kwa walimu wakuu wote ikiwa ni pamoja na kuwashusha vyeo vyao.
“Maazimio yalipitishwa tangu mwezi Septemba mwaka huu marufuku wanafunzi kufanyishwa vibarua,shule zibuni miradi ya kujitegemea itakayowawezesha kupata fedha,pia walimu kuwapatia wanafunzi maarifa ya kujitegemea kwa mfano kulima bustani baada ya saa za masomo’’,alisisitiza.
Mkali aliyataja mambo ambayo yamechangia kushuka kwa elimu na ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Mbinga kuwa ni pamoja na wanafunzi kufanyishwa vibarua,utoro na ulevi kwa baadhi ya walimu,walimu kutofundisha siku zote 195 zilizopangwa na wizara,walimu wakuu kutofuatilia ufundishaji,ukaguzi wa maandalio na kazi za watoto.
Takwimu zilizokusanywa katika shule 321 katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kuanzia darasa la tatu hadi la saba zinaonesha kuwa wanafunzi 15,128 kati ya 116,966 hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu
Makala hii nimeipata hapa JAMIIFORUM IMEANDIKWA NA  Albano Midelo hapo decemba 13th 2011 pia kwa kuweza kusoma habari nyingi inayofanana na hii ingia hapa. TUKUTANO TENA JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA.
 

Tuesday, June 5, 2012

KWANINI PILIPILI MBUZI INAITWA HIVYO? NA JE KWA NINI HIKI CHOMBO ZA KUKUNIA NAZI PIA CHAITWA MBUZI?

Pilipili mbuzi zikiwa kwenye mti jee unajua kwanini zina itwa Pilipili Mbuzi? ni kwa kuwa zina faa sana kwenye supu ya Nyama ya Mbuzi au?
N ahap ni mbuzi mwenyewe , sioni kama kuna mfanano hapa...
 ...na hapa sasa ni kifaa cha kukunia nazi nacho kinaitwa MBUZI . Mara chache nimesikia wengine wakisema kikunio au je kuna jina jingine ambalo mimi sijawahi kulisikia...naamini kwa pamoja tutafika pahala pazuri. Mchana,jioni au sijui usiku mwema....KAPULYA



Monday, June 4, 2012

WAZO LA JIONI YA LEO:- KUTOKA KWENYE TAIPURETA/typewriter MPAKA KWENYE KOMPYUTA/SIMU!!!

                                  
Leo nimekaa hapa nikawa nafikiri jinsi hali ilivyobadilika kwa haraka toka miaka ya 1990 mpaka leo. Nimekumbuka kazi yangu ya kwanza kama Karani pale Wilima Secondary. Nikiwa nachapa mitihani yote, kwa kutumia mashine/typewriter aina hii, na halafu kuburuza kwenye mashine ya kuburuzia ukitoka hapo nguo zote nyeusi.......Lakini leo
...mambo yamebadilika kweli.  Kuandika/kuburuza huhitaji kuchafuka ...nawaza kwa sauti na natamani leo ndio ingekuwa miaka ile...na hivi karibuni au nisema kwa sasa kila mtu ana simu na kila kitu kinafanyika kwenye simu...kaazi kwelikweli...

AU LABDA TUENDELEE JUMATATU HII KIHIVI NA HUYU DADA MREMBO AMBAYE NI KIKOJOZI....


Ni tatizo ambalo huwezi kulitolea ufafanuzi na pia huwezi kulitegemea linapotokea kwa mtu wa makamo, lakini ni tatizo kubwa na lipo ndani ya jamii zetu zinazotuzunguka, matokeo yaker ni aibu, fedheha na karaha....
Nilipoangalia hii nikakumbuka jirani yangu mmoja  kila ukienda nyumbani kwake kulikuwa na harufu kali kweli ya mkojo. Naye alikuwa anasema ni watoto wanakojoa sana. Kukojoa kitandani inasemekana ni homa lakini wengi wanafikiri wanaokojoa wanafanya makusudi.

KUTOKA SPORTSMAN MPAKA PORTSMAN...

Mimi si mvutaji wa sigara lakini naklumbuka nilipokuwa mdogo kulikuwa na sportsman zaidi na sigara nyingine nilikuwa natumwa kununu hasa mjomba wangu ani mvutaji sana wa sigara. Lakini mwaka jana nilipokuwa nyumbani katika pilikapilika nikaona kuna portsmn pia....ujazo, na kila kitu ni sawa ...mmmhhh labda sijui sigara zenyewe ni tafouti?.....MWANZO MWEMA WA JUMA!!!!

Sunday, June 3, 2012

LEO KIJANA ERIK ANATIMIZA MIAKA 12...HONGERA ERIK!!!

Tarehe kama ya leo 3/6/2000 familia iliongezeka, alizaliwa kijana huyo Erik  na leo hii anatimiza miaka 12. Erik, sisi wazazi, dada, ndugu pia marafiki wote tunakutakia kila la heri katika yote unayofanya. Kama vile masoma, yako, kwa vile unapenda sana michezo kama vile mpira wa miguu, flow boll na michezo mingine basi tunakutakia juhudi snyingi. Erik anasoma darasa la tano kwa sasa karibu ataanza la sita. Mwenyezi Mungu na akubariki uwe mtiiifu, mwenye juhudi kimasoma na mengine yote. DUH! KAMA MCHEZO LEO MIAKA 12. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ERIK.!!!!  

Saturday, June 2, 2012

UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO..MAISHA!!!


Katika maisha inabidi tuwe makini. Maisha yapo kama yalivyo. 
Na kama haturidhiki nayo :- Basi tuchukua uamuzi na kuyabadili.
JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI

Friday, June 1, 2012

IJUMAA HII YA MWEZI MPYA NIMEONA TUANZE HIVI!!!

ONENI UZURI WA AJABU WA UUMBAJI WA MUNGU
Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote. Na kwamba Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu. Bali wafanyao mashauri ya zamani kwao kuna furaha.
 au LABDA TU KAKA SUMA LEE AMALIZIE NA HAKUNAGA

IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA KILA LA KHERI KWA KUUANZA MWEZI MPYA NA PIA    MWISHO WA JUMA UWE MWEMA.!!!!!